text
stringlengths 0
4.5k
|
---|
Heri wenye huzuni,maana watafarijiwa. |
Heri wanaolia,maana watapokea roho ya furaha na kusherehekea. |
Heri wenye huruma,maana watahurumiwa. |
Heri wenye kuleta amani,maana wataitwa watoto wa Mungu. |
Heri wanaoteswa kwa kufanya anavyotaka Mungu,maana ufalme wa Mungu ni wao. |
Heri wale wanaotukanwa na kuteswa na kusemwa uongo mambo ya uovu ya kila aina. Furahini na kushangilia,maana zawadi yenu mbinguni ni kubwa. |
''Ndugu zangu,ninapowatuma,ninyi ni chumvi ya dunia,chumvi yenye ladha ya kuokoa. Lakini kama chumvi ikipoteza ladha yake,itakolezwa na nini?Haifai kwa chochote isipokuwa kutupwa tu na kukanyagwa na watu. |
Ninyi ni mwangaza wa dunia. Mji uliojengwa juu ya mlima hauwezi kufichika,wala watu hawawashi mshumaa na kuufunika kwa debe,ili huuweka juu ya kinara uwaangazie watu wote walio nyumbani. Hivyo hivyo,mwanga wenu uangaze mbele ya watu ili wayaone matendo yenu mema wamsifu Baba yenu aliye mbinguni. |
Nawapeleka ninyi katika dunia kuniwakilisha na kuwa kama mabalozi wa ufalme wa Baba,na mnapokwenda kutangaza habari njema,wekeni imani katika Baba ambaye ninyi ni taarishi wake. Msipinge udhalimu kwa kutumia nguvu,usitumainie nguvu ya mkono wako. Jirani yako akikupiga shavu la kulia,mgeuzie lingine pia. Muwe radhi kuvumilia udhalimu miongoni mwenu, kuliko kwenda kwenye vyombo vya sheria, . Kwa upole na huruma wasaidie wote wenye matatizo na wenye shida. |
'' Baba yangu aliye mbinguni anaangaza jua kwa waovu na wema,pia analeta mvua kwa watenda haki na wasiotenda haki,ninyi ni watoto wa Mungu,na zaidi,ni mabalozi wa ufalme wa Baba yangu. Muwe na huruma,kama ambavyo Mungu ana huruma,na katika siku zijazo katika ufalme mtakuwa wakamilifu milele,kama ambavyo Baba yenu wa mbinguni ni mkamilifu. |
''Mmepewa kamisheni kuokoa watu,siyo kuwahukumu. Mwisho wa maisha yenu ya dunia wote mtategemea huruma;kwa hiyo nawataka wakati wa uhai wenu,muonyeshe huruma kwa ndugu zenu. Msifanye kosa la kutaka kuondoa kibanzi kutoka kwenye jicho la mwingine wakati kuna gogo katika jicho lako. Kwanza ondoa gogo kutoka kwenye jicho lako halafu utaona vizuri na kuweza kuondoa kibanzi kutoka kwenye jicho la mwingine. |
''Uelewe ukweli vizuri,ishi maisha ya haki bila woga,na hivyo mtakuwa mitume wangu na mabalozi wa Baba yangu. Mmesikia ikisemwa,'Kama vipofu wakiongozana,wote watatumbukia ndani ya shimo.' Kama unataka kuwaongoza wengine waingie katika ufalme,wewe mwenyewe lazima uonyeshe hukumu ya haki na hekima nzuri. Usiwape mbwa vitu vitakatifu,na lulu zako usiwatupie nguruwe,au watazikanyaga na kugeuka kukurarua. |
''Nakuonya kuhusu nabii wa uongo ambao watakuja kwako na vazi la kondoo,wakati ndani ni mbwa mwitu wakali. Mtawajua kwa matunda yao. Je watu huchuma zabibu kutoka kwenye miti yenye miba au tini kutoka kwenye mbigili?Hivyo hivyo kila mti mzuri huzaa matunda mazuri,mti mbaya huzaa matunda mabaya. Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya,mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri.Kila mti ambao hauzai matunda mazuri hatimaye utakatwa na kutupwa katika moto. Ili uweze kuingia katika ufalme wa mbinguni ni nia ndio inahesabiwa. Baba yangu anatazama katika mioyo ya watu na kuwahukumu kutokana na nia na malengo yao. |
''Katika ile siku kubwa ya hukumu ya ufalme,wengine wataniambia,'Tulitangaza ujumbe kwa jina lako,kwa jina lako tulifanya kazi nyingi njema'Lakini nitalazimika kuwaambia;'Ondokeni hapa ninyi walimu wa uongo' Lakini yule ambaye anasikiliza haya maagizo na kwa dhati anatimiza kamisheni aliyopewa kuniwakilisha kwa watu kama ambavyo mimi nilivyomwakilisha Baba yangu kwenu,atakaribishwa kwenye utumishi wangu na katika ufalme wa Baba yangu mbinguni.'' |
Mitume walikuwa hawajawahi kumsikia Yesu anaongea namna hii,kwa vile alikuwa anaongea kama vile alikuwa na mamlaka yoye. Walishuka kutoka mlimani,karibu na saa ya machweo,lakini hakuna aliyemuuliza Yesu swali. |
Ujumbe wangu kwa UV-CCM hapo,ujumbe mkubwa ni pale ninaposema wasitumainie nguvu za mikono yao,kama wanafanya kazi halali,watasaidiwa na vyombo vya sheria,ambao naona ni ujumbe mzuri,wakati huu ambapo wanajitayarisha kufanya kampeni za Uchguzi Mkuu. |
VIDEO: Majibu ya Linex kuhusu kuhamia kwenye muziki wa injili – millardayo.com |
VIDEO: Majibu ya Linex kuhusu kuhamia kwenye muziki wa injili |
‘Mwaka huu nitarekodi muziki wangu wa kawaida lakini nitarekodi na nyimbo za injili na hadi sasa ninazo ngoma mbili kwahiyo sifikiri kama ni kitu kibaya kufanya hata muziki wa injili kwa lengo la kumshukuru Mungu‘ –Linex |
MSIBA HARUSINI: Bibi Harusi kafariki saa 11 baada ya kuolewa…kisa? |
BREAKING: Msimamo wa CLOUDS MEDIA baada ya Makonda, Ruge na Wahariri kuongea leo |
Katiba mpya kuzinduliwa Aprili 26, 2014 -- Waziri Mkuu |
Haya, serikali sasa imejicommit na kutaja tarehe rasmi ya kuzinduliwa kwa katiba mpya -- Aprili 26, 2014. Kazi kwetu kuchangamkia mchakato wa katiba na kuweka mambo sawa ili uchaguzi mkuu wa 2015 ulete uhuru kamili kwa Tanzania! |
*TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI* |
kuzinduliwa rasmi Aprili 26, 2014 wakati wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya |
Akifungua Semina Elekezi kwa Wakuu wa Mikoa na wa Wilaya kuhusu mchakato wa |
Katiba Mpya, kwenye ukumbi wa Hoteli ya St. Gasper, alisema hayo ndiyo |
matarajio ya Serikali . |
Ni matarajio ya Serikali kuwa Katiba Mpya itakuwa imekamilika na |
kuzinduliwa ifikapo tarehe 26 Aprili, 2014 katika Maadhimisho ya Miaka 50 ya |
Muswada wa Sheria kuhusu Mapitio ya Marekebisho ya Katiba utawasilisha |
Bungeni mwishoni mwa Mkutano wa Nne wa Bunge unaoendelea hivi sasa au |
mwanzoni mwa Mkutano wa Tano Oktoba mwaka huu. |
Aliwataka Wakuu wa Mikoa na wa Wilaya kutoa ushirikino wa kutosha kwa Tume |
kuhudhuria na kutoa maoni yao. |
Mchakato huo wa kuelekea uundwaji wa Katiba Mpya, umekwishaanza na katika |
hatua ya awali, Serikali imeandaa rasimu ya Muswada wa Sheria ya Mapitio ya |
Marekebisho ya Katiba *(The Constitutional Review Act*) ya Mwaka 2011. |
Waziri Mkuu alisisitiza kuwa hatua ya sasa siyo kutunga Katiba Mpya bali ni |
kuunda Tume ya Kuratibu na Kukusanya Maoni ya Wananchi kuelekea kutungwa kwa |
Katiba Mpya. |
* Ofisi ya Waziri Mkuu,* |
Huu ni usanii tu. Serikali inaogopa maandamano ya CHADEMA. Wametangaza tarehe ya kuzinduliwa katiba mpya ili CHADEMA watulie wasitishe maandamano ya kudai katiba mpya kuanzia sasa 2011 mpaka 2014 ili CCM itawale kwa amani na JK aendelee kutalii ulaya na safari zake za ulaya kila siku. |
By the time inafika April 2014 katiba ikiwa bado ni rahisi kwa serikali kuwadhibiti CHADEMA kwa mwaka mmoja mpaka uchaguzi wa 2015. Hii staili ya kujata tarehe ni danganya toto ili kuleta matumaini hewa wananchi watulie wasidai katiba mpya. Kikwete alisema tangu Desemba 2010 ataunda tume ya maoni ya katiba mpya. Mpaka leo amekaa kimya. |
Hivi kwa nini usiwe na subira kuliko kuwa na mashaka hata pasipostahili? Katiba hii itakuja kwa utashi wa wananchi wote na siyo shinikizo la Chadema kama wewe unavyodhani. |
Tunachotaka ni kuwa uchaguzi mkuu ujao uwe chini ya katiba mpya. |
Mkuu bila kuwashinikiza hawa chama cha magamba wanaweza kabisa kufanya usanii ili uchaguzi ujao ufanyike kwa kutumia hii katiba ambayo imepitwa na wakati. Wanaweza kuongea upupu wowote ule kama ukosefu wa pesa n.k. kama ndio sababu ya kushindwa kuwa na katiba mpya kabla ya uchaguzi wa 2015 |
Je kati ya sasa na huo mwaka 2014 nini na htua gani zitafanyika? |
Mpaka sasa wanachi wengi hawajui nafasi yao na jinsi gani wanataiwa kushiriki kuchangia na kutoa maoni yao katika hii kitu |
Kazi nzuri hii chini ya uratibu wa TISS! Lakini kwa kizazi cha leo jibu kimeling'amua!! |
Tunahitaji katiba kuanzia sasa mpaka uchaguzi ujao itumike hiyo! |
Tunataka tu mfumo mzuri wa uundwaji wa katiba na ushiriki wa watu, katiba si kama sheria nyingine, hakuna sehemu raisi anatia saini kwenye katiba, JK tunamuheshimu, Tanzania yetu atuachie! |
Mtoto huyu ni malaika, anahitaji msaada wetu, na amekataa kwenda Loliondo |
Mtoto Cecilia Edward (14) (pichani), mkazi wa Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani, ambaye kwa sasa anaishi na mlezi wake, Mbagala jijini Dar es Salaam, bado anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo na amekuwa akihudhuria kliniki na hajapata mabadiliko. |
Kwa mujibu wa mlezi huyo, Cecilia anasumbuliwa na ugonjwa huo, hali iliyosababisha tumbo kujaa maji mara kwa mara. |
Imeelezwa na mlezi wake huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwamba tatizo hilo lilimuanza Cecilia baada ya wazazi wake wote kufariki dunia akiwa na umri wa miaka minne. |
Hata hivyo, mlezi wake huyo alisema mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam kuwa hana niya ya kwenda kutibiwa Loliondo kama ilivyoripotiwa na gazeti hili siku za nyuma. |
Sina mpango wa kumpeleka mtoto huyu Loliondo na anaendelea na kliniki, alisema. |
Awali gazeti hili katika toleo namba 687 la Mei 31 liliandika kimakosa kuwa jina lake ni Khadija Ally na kuwa mtoto huyo anaomba msaada wa kwenda kutibiwa Loliondo kwa Babu. |
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza. |
Kwa kweli nimesikitishwa sana na hali ya huyo mdogo wetu. Napendekeza kuwa wapewe taarifa waziri wa afya na ustawi wa jamii, waziri wa jinsia na watoto na mbunge wa jimbo analotoka. Wenye uwezo wa kumfikisha kwa hao waheshimiwa wajitahidi ikiwezekana wote wajulishwe ili mhusika mkuu apatikane kati ya hao waheshimiwa. Pole sana mdogo wangu! |
Akabembeleza kuwa ameelewa matatizo ya wananchi wake. Vyote havikufua dafu kubadilisha mioyo ya Wamisri ambao walijua hakuna kitu kingine walichokitaka toka kwake; si sura yake, si urafiki wake na Marekani, si maneno yake ya kizalendo - hawakutaka chochote zaidi ya yeye kutoka madarakani; pamoja na chama chake! Walimkataa. |
Tumaini lake kwa miaka yote ya utawala wake ni utii wa jeshi ambalo yeye mwenyewe aliwahi kulitumikia. Kwa miaka yote iliyopita jeshi lake limekuwa pamoja naye kumlinda na kumhakikishia usalama wake na mwendelezo wa utawala wake. |
Aliitisha uchaguzi na akashinda, tena kwa kishindo. Alikitambia chama chake kuwa ushindi wao ulikuwa ni ushindi mnono. Walimshangilia. Mtoto wake wa kiume alijipitisha pitisha akionekana kumtetea baba yake na hata kuonekana kuwa ni mrithi mtarajiwa. |
Naam, mwanae alipewa hata uongozi katika chama, tena katika nafasi za juu. Alipopita mwanae aliheshimiwa, watu wazima walinyenyekea mbele yake na wazee walimbusu mikono yake - kwa sababu tu ni mtoto wa Rais. Walimuonesha heshima; kumbe heshima ya wanaokandamizwa. |
Ndugu zangu, kuanguka kwa Hosni Mubarak hakukuja kwa bahati mbaya. Kukataliwa kwa utawala wake na yeye mwenyewe kutupwa katika shimo lisilosamehe la historia kulitokana na msingi aliouweka yeye mwenyewe. Huwezi kuzuia mioyo ya watu kupata uhuru. |
Lakini wananchi wa Misri walipoamua kuikataa serikali yao kwa maandamano jeshi halikuingilia kati. Wengine wanauliza kwanini? Kwanini jeshi halikufanya kile kilichofanywa na Jeshi la China mwaka 1989 pale uwanja wa Tianmen jijini Beijing. |
Kwa wanaotaka kukumbushwa maandamano ya kudai mabadiliko ya kisiasa nchini China yalizimwa kwa nguvu na jeshi la nchi hiyo bila kujali gharama ya maisha ya wananchi wake. Jeshi la China linadaiwa kuua zaidi ya watu 400 kuamkia Juni 4, 1989! Ndio ulikuwa usalama wa watawala wa China. Kwanini jeshi la Misri halikufanya hivyo? |
Kwamba mamlaka ya kutawala yanatoka kwa wananchi. Watu wengi wanafikiri kuwa mamlaka ya kutawala yanatoka kwenye Katiba na hivyo kwao Katiba ndiyo kila kitu. Watatuambia tuheshimu Katiba na ya kuwa Katiba imesema n.k na ni kweli katika mazingira ya kawaida Katiba inatakiwa iwe ndiyo mwamuzi wa mwisho. Wananchi wa Misri walikuwa na Katiba ambayo iliwatumikia kwa miaka kadha wa kadha. |
Alisahau kwamba Katiba inaweza kubadilishwa endapo watu wenye sovereignty wanaamua hivyo. Katika ufalme - ni wafalme na katika jamhuri ni wananchi. Ndiyo maana Mfalme wa Jordan na Mfalme wa Saudia wanaweza wakaamua kufanya kitu kwa matakwa yao bila kuhojiwa na mtu yeyote kwani wao ndio hakimiya - sovereigns. |
Jeshi la Misri ni miongoni mwa majeshi makubwa kabisa duniani na ambalo watendaji wake wengi wamejifunza nadharia za kijeshi za Magharibi ambazo zinayaweka majeshi chini ya watawala wa kiraia. |
Nadharia hizi za kijeshi zinaamini kuwa majeshi yana majukumu ya kulinda uwepo wa nchi, uhuru wa nchi na hakimiya ya nchi yenyewe. Jukumu lao ni tofauti kabisa na la polisi na vyombo vingine vya dola. Jeshi ndilo mlinzi wa mwisho wa uwepo wa nchi au taifa na ndilo mtetezi wa mwisho wa uwepo wa watu kama taifa. |
Hili ni muhimu kuelewa. Wamisri walikuwa hawatishiwi uwepo wao kama taifa au huru wao kama nchi. Kilichokuwa kinatokea ndani ya Misri ni kuwa wananchi wa Misri hawakukubaliana na watawala wao na waliamua kuwapinga wazi na wakatumia haki yao ya mwisho ya kuwaondoa watawala hao. |
Haki hiyo haiondolewi na katiba wala haiondolewi na jeshi. Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kuandika na kusema wananchi wanapopoteza imani na serikali yao na ya kuwa njia zote za kuwashawishi watawala wao wabadilike na kuwa inavyotarajiwa na kupaswa na wananchi hao; basi wananchi wana haki kuchukuka silaha na kuiondoa serikali ile ya kipuuzi. Silaha zinaweza kuwa bunduki au mawe! Wamisri hawakuwa na bunduki isipokuwa sauti zao! |
Matokeo yake, vijana wa Uwanja wa Tahrir, ule uwanja wa ukombozi, uwanja uliotakaswa kwa damu ya Wamisri Wakristu na Waislamu; ule uwanja ambao daima utakumbukwa kuwa ni mahali wananchi wa Misri walisimama na kuweka mguu chini na kuambia utawala wa kifisadi imetosha! |
Jeshi la nchi hiyo liliwaacha wananchi wawe waamuzi wa mwisho. Matokeo yake ndani ya siku 18 za kukosa usingizi, za kulia sana, za kukaa mbali na familia zao wananchi wa Misri waliweza kumlazimisha Hosni Mubarak kuachia ngazi. |
Na hapa ndipo Nyerere wetu anaonekana ni shujaa kati ya wenye kiu ya madaraka. Hata wale wanaosema Nyerere alikuwa dikteta ni lazima waone haya leo hii kwani madikteta hawaachii madaraka kwa furaha na kwenda kulima! Jeshi la Misri lilikaa pembeni ili wananchi wa Misri watumie haki yao ya mwisho ya kubadilisha utawala wao. |
Ndugu zangu, natumaini nasi tumejifunza somo hili la demokrasia. Maana watu wanafikiria demokrasia ni uchaguzi tu! Kwamba tukishakuchagua basi tusubiri miaka mitano kubadilisha serikali. |
Jamani Wamisri walikuwa na uchaguzi miaka mitano iliyopita na walitarajia kuwa na uchaguzi Septemba mwaka huu. Lakini wananchi walisema hawawezi kusubiri miezi tisa. Serikali haiwezi kuwa mbaya hadi miaka mitano ipite. |
Sawa, kuna mambo ambayo serikali inavumiliwa kwa sababu inaonekana kweli inajitahidi, lakini kama kujitahidi huko matokeo yake ni miaka 30 ya vitisho, kuburuzana na kuwapuuza wananchi mwisho wananchi wanafikia kikomo. |
Kama kuna kitu kilitukera wengi mwaka jana ni jinsi jeshi lilipoingilia kati mchakato wa kisiasa kwa matamshi yale ya kutisha wananchi kiasi kwamba maana ya uchaguzi huru haikuwapo tena. |
Ni matumaini yangu jeshi letu litaacha Polisi wafanye kazi zao na liwe kama Jeshi la Wamisri ambalo lilisema wazi kabisa kuwa halitanyanyua silaha zake dhidi ya wananchi wake. |
Yawezekan bado hatujafika hapo. Yawezekana labda baada ya miaka 50 Watanzania wanaweza kufika walipofika wa Misri baada ya miaka thelathini. Na tusiombee kufika huko, na tujitahidi pamoja kama taifa kutofika huko. Tusije kulazimika kuandika Katiba mpya katika mazingira ya machafuko. |
Ninaamini, kati ya mambo ambayo yataamua tunakotaka kwenda ni kuhakikisha kuwa tuna Katiba mpya ifikapo uchaguzi wa 2015. Hili halina mjadala. Watanzania wanataka Katiba Mpya na wanaitaka kabla ya uchaguzi mkuu ujao. |
Vyombo vya dola vikae pembeni, tukiandamana wakae pembeni, tukibishana na kumwagiana maji ya kuwasha na Polisi, Jeshi likae pembeni. Haki ya kutawala inatoka kwa wananchi, na milele inabakia kwa wananchi. Hili ni somo la kukumbukwa. |
Wana bodi, japo tuko kwenye harakati za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge, kuna swali linanitatiza kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar, ambapo majibu yake sahihi, pia yanaweza kuwa ni kiashiria tosha cha mshindi wa urais wa Zanzibar, iwapo uchaguzi utakuwa huru na wa haki. |
Swali hili lahusu ukweli haswa kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964, baada ya kuibuka kwa kitabu kingine kiitwacho 'Kwaheri Ukoloni Zanzibar, Kwaheri Uhuru Zanzibar' kilichoandikwa na Mwanazouni wa Zanzibar, Dr. Harith Ghassany, kama kilivyofanyiwa mapitio na mwandishi Mohamed Said, kwenye gazeti la Al-Nuur la leo. |
Pia mwandishi anamalizia kwa kusema hata mauaji ya Karume, haykutekelezwa na wapinga mapinduzi, bali ni miongoni mwa hao hao wanamapinduzi, baada ya kupishana kauli fulani fulani za uendeshaji wa Zanzibar baada ya Mapinduzi. |
Nimesoma kitabu cha John Okello kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar, yeye anasema yake, vitabu kadhaa vya waandishi wazungu wanasema yao, historia tukuka ya mapinduzi hayo nayo inasema kivyake, hivi hakuna any straight line yoyote kuhusu Mapinduzi hayo, yalipangwa na nani, yalitekelezwaje, nini haswa kilichotokea, nani alifanya nini wapi? na wahanga ni kina nani haswa?. |
kama kuna uwezekano wa kuwekwa tukakipitia si vibaya |
Tukizembea, historia ya kweli ya mapinduzi ya Zanzibar haitajulikana kamwe, ni wajibu wetu kuufahamu ukweli kwa faida ya vizazi vijavyo... |
Kwa tuliozaliwa baada ya mapinduzi ndio tunazidi kuchanganywa zaidi, hatuelewi nani ni nani maana kila siku yanaibuka mapya! Kwa kweli kuna haja ya historia ya mapinduzi kuandikwa upya na sio sasa ambapo kila mtu anasema yake kulingana na namna alivyoathirika na mapinduzi hayo! |
Ndugu yangu usipoteze muda mapinduzi haya yalikuwa mfano wa tamthiliya, jaribu kupitia nchi zilizopitia mapinduzi ya kweli,utaona watu wanavyojivunia asili zao sasa rudi kwa hawa ndugu zetu wa kiunguja asili bora wanayoiona wao ni ya kiaarabu, maana halisi ya mapinduzi hawaijui ndio maana kila kukicha utasikia hadithi mpya za mapinduzi haya, si rahisi kupata ukweli wa haya mapinduzi kwani wahusika wengi walikimbilia kuoa wanawake wa kiarabu baada ya mapinduzi, matokeo yake kutokana na kuwanyenyekea wake wapya wa kiarabu waliweza kupotosha ukweli wa maneno angalia baraza zima (asili) linaloitwa la mapinduzi angalia wake utaona ukweli wa jambo hilo, watu ambao wanaweza kutupa ukweli wa tamthiliya hii wote ni marehemu (Mwl. Nyerere na Karume) (RIP), kwa sasa hivi acha tuchukue maneno yao, hizo hadithi za kina Ghassany waachie wenyewe, hata wewe ukitaka kuandika historia unaweza pesa yako tu, huyu Ghassany ameandika kitabu hicho kwa uchungu wa Zanzibar au ni mwendelezo wa tamthiliya ya kiarabu? Ukweli wa mapinduzi haya utaupata waunguja watakapokuwa na mapinduzi ya kweli ndani ya nafsi zao. |
nyie mnaokwepa kueleza sababu halisi ya mapinduzi mnakwepa kitu gani na kwa maslahi ya nani? leo imezuka hadithi mpya ya warusi kesho sijui itakuwaje. |
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.