text
stringlengths
3
16.2k
ALIYEKUWA Gavana wa Nairobi, Mike Sonko aliangua kilio kortini Jumatano wakati wa kusikizwa kwa kesi ya ufisadi wa... Na CHARLES WASONGA
WANASIASA na watu ambao majina yao yatawekwa katika orodha ya aibu ya Tume ya Uwiano na Utangamano ya Kitaifa (NCIC)... BENSON MATHEKA na SIMON CIURI
Masaibu ya aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Mike Sonko yaliendelea kuongezeka jana alipozuiliwa rumande baada... Na RICHARD MUNGUTI
MASAIBU ya aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko Mbuvi Gidion Kioko yameongezeka baada ya  kusukumwa ndani hadi... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA SAMMY WAWERU MSANII tajika wa nyimbo Mugithi, Samuel Muchoki maarufu kama Samidoh huenda ametengana na mpenzi wake mwanasiasa Karen Nyamu. Hii ni kutokana na video iliyochipuka ambayo anaskika akisema “nilikuwa kwenye ndoa ya mitara, sasa niko singo”. Samidoh amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Seneta Maalum Karen Nyamu, na wamejaaliwa kupata watoto wawili. Msanii huyo wa nyimbo za Agikuyu, alifichua kuachana na Karen kupitia video ya mbashara ya Tiktok (live) ambapo alikuwa akijibu maswali ya mashabiki wake. Wakati wa mafichuzi hayo, alionekana kuwa kwenye eneo la burudani alikoandamana na msichana ambaye hakuweka wazi endapo ndiye mchumba wake mpya. “Ati hongera kwa kuwa na mpenzi mpya…” Samidoh akasoma mojawapo ya jumbe zilizotumwa na mashabiki wake. Alijibu, “Si wewe pekee ulishushwa madaraka kutoka kiwango cha hadhi hadi dereva wangu…Nilikuwa kwenye ndoa ya mitara ila sasa niko singo”. Mfuasi huyo aliendelea kumdadisi, akitaka kujua iwapo Samidoh anafahamu kuhusu ukurasa wa kimitandao unaohusishwa na mchumba wake – Karen Nyamu Fun Page. Kwa ucheshi, mwimbaji huyo wa kibao tajika cha Kairetu Gakwa (Binti yangu) na Ndiri Mutwe Mwega (Sina kichwa kizuri) alisema kwa sasa anajishughulisha na biashara. “Kwa sasa, ninajishughulisha na masuala biashara. Ikiwa si mradi au biashara, ishi na mama yako,” alielezea. Shabiki wake alimkejeli akitaka kujua aliko nina yake, isijulikane ikiwa alimaanisha mama yake mzazi au mpenzi wake. “Ameoleka na kwa sasa anafurahia fungate (honeymoon),” Samidoh alidokeza. Kidosho aliyeandamana naye alitambua shabiki huyo kama Shabaan, akisema kwamba yeye ni mchochezi. “Wee acha hiyo, unajua Shabaan wewe ni mchochezi sana… (Yuko hapa (akimaanisha Karen Nyamu),” mwanadada huyo alisema. Naye Samidoh aliendelea, “Tunataka Karen, naona hivo ndivo mchango safuni unasema…Naona, lakini sasa yuko online kweli?” Kipusa aliyeandamana naye, alijibu, “Yuko online, mjaribu”. Aidha, shabiki wa Samidoh alitaka Karen Nyamu ajumuishwe kwenye mazungumzo hayo ya mbashara Tiktok. Kilichoshangaza zaidi na kuashiria utengano wa Samidoh na Karen, ni kudai kwamba alimbloki mtandaoni na angeweza kushiriki endapo atamuondoa alikomuweka. “Yuko kwenye orodha ya kublokiwa, sasa hiyo ndio shida. Labda nisitishe mazungumzo haya ya moja kwa moja ili nimuondoa aweze kujumuika nasi,” Samidoh alifafanua. Mahusiano kati ya Samidoh na Karen, ndiyo yalichangia kuachana na mkewe, Edday Nderitu ambaye alihamia Amerika Mei 2023. Edday alikuwa ameonya msanii huyo mapema 2023, akisisitiza kwamba hakuwa tayari kuwa kwenye ndoa ya mitara. Samidoh na Edday wana watoto watatu pamoja. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MAOSI WAKAZI wa mtaa wa Mazembe viungani mwa mji wa Nakuru wamekiri kuhangaishwa na wezi ambao huwaibia na kuwasindikiza hadi nyumbani. Huwawekea ulinzi huo makusudi ili kuhakikisha kwamba wateja wao wanafika nyumbani salama salimini. Kwa kawaida, wahuni wamebuni mbinu mpya ya kutembea na mbwa wakubwa nyakati za usiku, ili kujiwekea ulinzi wa kibinafsi. Owen Shibala mwendeshaji bodaboda kati ya Nakuru mjini na Mazembe, anasema hajui walikotoa ujasiri walio nao kushika doria usiku utadhani ni polisi. Mazembe ni mojawapo ya mitaa ambayo hushuhudia visa vya kihalifu na utumiaji wa mihadarati mara kwa mara. “Ukikutana nao usiku ni lazima usalimishe kila kitu lau sivyo utaona cha mtema kuni. Watakucharaza viboko na kuiba kila kitu cha nguvu,”akasema. Hata hivyo, wanapoiba hujitwika jukuma la kuwasindikiza wakazi, wasije wakakutana na vibaka wengine barabarani. Aidha, wanalia sare za polisi jambo linalowafanya baadhi ya raia kuamini huenda wanashirikiana na maafisa wa polisi. Baadhi yao wanajifanya ni maafisa wa polisi ambao huwa wameshika doria, wakilenga kuhangaisha wapita njia wanaotoka kazini usiku. Agnes Wahome mfanyibiashara mtaani Rhonda anasema huwa wamejihami kwa visu, rungu na wako tayari kupigana. Kulingana na Bi Wahome, hii ni hali ya kawaida siku hizi katika mitaa ya Manyani, Bondeni na Freearea ambapo vijana wengi wamejiingiza kwenye uhalifu. Bi Wahome anasema wahalifu wengi wanajulikana, kwani ni vijana wadogo kutoka mitaa jirani ya Flamingo na Lakeview. Mkazi huyo angependa polisi kushika doria katika maeneo husika ili kuzuia kuzuka kwa magenge hatari yanayohangaisha wenyeji. Hili linajiri siku chache baada ya Taifa Leo Dijitali kufichua visa vya wizi ambapo baadhi ya wezi kutoka kwenye mtaa wa Gioto, Nakuru wamekuwa wakipika chakula katika kila nyumba wanamoingia kuiba. Mtaa wa Bondeni, Kaunti ya Nakuru ambapo wezi huwaibia wakazi na kuwasindikiza mpaka nyumbani. PICHA|RICHARD MAOSI
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L

You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MUNGUTI MASKWOTA wapatao 10,000 wamewasilisha upya kesi katika Mahakama ya Upeo wakiomba ibatilishe uamuzi kwamba wafukuzwe kutoka kwa shamba la ukubwa wa ekari 25,000 wanalong’ang’ania umiliki wake na familia ya mwanasiasa marehemu Mark Too. Maskwota hao wanaodai mababu zao ndio waliotimuliwa kutoka kwa shamba hilo enzi za ukoloni, wanasema walipewa shamba hilo rasmi na aliyekuwa Rais hayati Daniel arap Moi, kisha Kamishna wa Ardhi M Okundu akaratibisha uamuzi huo mwaka 2007. Katika ombi lililowasilishwa na wakili William Arusei chini ya sheria za dharura, kikundi cha maskwota hao–Sirikiwa Squatters Group–kimeomba mahakama ibatilishe uamuzi huo kwa vile ilitegemea ushahidi ambao haukuwa umewasilishwa katika kesi waliyoshtaki katika Mahakama ya kuamua kesi za mashamba (ELC), Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu. Pia wameeleza bayana Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaack Lenaola, na William Ouko walitegemea ushahidi wa Afisa wa Ugavi wa Mashamba R J Simiyu kutoa uamuzi wang’atuke shambani. Maskwota hao wamesema ushahidi wa Bw Simiyu uliowasilishwa mbele majaji hao saba kwa njia ya afidaviti ni mpya na kamwe “haukuwasilishwa mbele ya Jaji Antony Ombwayo aliposikiliza na kuamua kesi hiyo 2017.” Pia wanasema ushahidi huo haukuwasilishwa Mahakama ya Rufaa iliyosikiliza rufaa iliyowasilishwa na kampuni ya Fanikiwa, familia ya marehemu Mark Too, kampuni ya Lonrho Agribusiness (EA) Ltd, na Bw David K Korir. Hivyo basi, maskwota hao wanaeleza mahakama hii ya upeo kwamba ni kinyume cha sheria kutegemea ushahidi mpya kutoa uamuzi wa kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma. “Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu wa Desemba 15, 2023, hauna mashiko kisheria na kamwe hauna nguvu kisheria kuwatimua maskwota hawa kutoka kwa shamba lao,” asema Bw Arusei. Pia maskwota hawa wanadai kwamba badala ya Mahakama ya Juu kujadili masuala ya kikatiba jinsi ilivyo jukumu lake, majaji hao walianza kufafanua na kutafsiri ushahidi wa watu binafsi na kuelezea maana ya ‘skwota’. Mahakama hii imeombwa ikague upya uamuzi iliyotoa kwa vile ilidanganywa na walalamishi na pia kutendewa ujanja. Akinukuu maamuzi ya majaji wastahiki kama vile Lord Dening, Bw Arusei amesema, mahakama ikigundua ilipotoshwa au kudanganywa na upande mmoja, iko na mamlaka na uwezo wa kufutilia mbali uamuzi iliyotoa na kuandika mwingine. Maskwota hao wanaomba Mahakama ya Juu iwarudishe shambani kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Ombwayo na Mahakama ya Rufaa. Vile vile mahakama hiyo imekosolewa kwa kumshambulia hayati Moi katika uamuzi huo pasi kutoa agizo wasimamizi wa mali yake wafike mbele yao kutoa mwanga kuhusu suala la umiliki wa shamba hili lililorudishwa kwa serikali na kampuni iliyokuwa inakuza miti inayotumika katika viwanda vya ngozi. Naibu msajili wa Mahakama ya Juu Nelly Kariuki aliwaamuru maskwota hao wawakabidhi nakala za kesi hii yao mpya wahusika wote kabla ya Januari 31, 2024, kesi itakapotajwa tena kwa maagizo zaidi. Jaji aliyesikiliza kesi hii mpya hakuiratibisha kuwa ya dharura ila aliamuru pande zote ziwasilishe ushahidi katika muda wa siku 14 kuanzia Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti,  baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA WALIMU wakuu wa shule tisa za upili na walimu 23 wamesimamishwa kazi kwa madai ya kushiriki udanganyifu katika Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE) unaoendelea kote nchini. Aidha, watahiniwa 46 wamepatikana na hatia hiyo ya kujaribu kutumia njia za mkato kupita mtihani huo ambao utaamua ikiwa watajiunga na vyuo vikuu na vile vya kadri mwaka 2024. Miongoni mwa walimu hao wakuu ni Charles Onyari wa Shule ya Upili ya Nyambaria iliyoko katika Kaunti ya Nyamira, aliyesimamishwa kwa madai ya kupatikana akishiriki uovu huo ilhali alikuwa msimamizi wa kituo cha mtihani. Shule hiyo ya kitaifa, isiyojulikana sana, ilishangaza wengi kwa kuongoza katika matokeo ya KCSE 2022 kwa kupata alama wastani ya 10.60. Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu anasema kuwa visa nyingi vya uovu huo mwaka huu 2023 viliendeshwa kwa njia ya kuingiza vitu visivyohitajika ndani ya vyumba vya kufanyia mitihani, watu kujifanya kuwa watahiniwa na wasimamizi kuwasaidia watahiniwa. “Kufikia sasa tumethibitisha visa vitatu vya watahiniwa kushirikiana, visa viwili vya watu kujaribu kujifanya kuwa watahiniwa na mameneja tisa ambao ni walimu wakuu waliokuwa wakisimamia shule mbalimbali wamesimamishwa kazi. Aidha watahiniwa 46 wametuhumiwa,” waziri Machogu akasema Ijumaa katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Kolanya, iliyoko Teso Kaskazini, Kaunti ya Busia. Shule hiyo ni ya hadhi ya kitaifa. Mwalimu Mkuu mwingine aliyesimamishwa kazi kwa wizi wa mtihani ni Eva Odhiambo wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Sironga, iliyoko Kaunti ya Nyamira. Shule nyingine ambako wizi wa mitihani iliripotiwa ni Shule ya Upili ya Gekomoni na Shule ya Upili ya Wavulana ya St Paul Gekano, zote katika Kaunti ya Nyamira. Katika Kaunti ya Migori, polisi walitibua sakata ya wizi wa mitihani na kuwakamata walimu 23 wanaozuiliwa kuhojiwa. Baadhi ya walimu walikamatwa katika kanisa moja Kaunti ya Migori wakiandaa majibu ya maswali ya mtihani wa Kemia kwa nia ya kupitisha majibu kwa watahiniwa wa Shule ya Upili ya Wasichana ya St Mary’s Mabera. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA KAMPUNI ya kusambaza stima nchini, Kenya Power, imetangaza kuwa maeneo mbalimbali yamegubikwa na giza baada ya usambazaji wa kawi hiyo kukatika. Kwenye taarifa iliyotoa saa mbili na nusu Jumamosi, Novemba 11, 2023, kampuni hiyo ilisema kuwa wahandisi wake wanaendeleza juhudi za kurejesha usambazaji wa stima. “Tunaomba msamaha kwa usumbufu uliosababishiwa wateja wetu. Taarifa kuhusu hatua za kurejeshwa kwa usambazaji wa stima na chanzo cha kupotea kwa kawi hiyo itatolewa baadaye,” ikasema taarifa hiyo. Miongoni mwa maeneo yaliyokumbwa na hitilafu hiyo ni Nairobi, Nakuru, Kisumu, Taita Taveta, Kwale, Eldoret, Laikipia, Samburu, Mombasa, na Murang’a. Maeneo mengine ni Tana River, Vihiga, Kakamega, Bomet, Makueni, Kapenguria, na Baringo miongoni mwa maeneo mengine. Kampuni ya Kenya Power ndio kampuni ya kipekee ya kusambaza stima nchini. Na kiwango kikubwa cha stima huzalishwa na kampuni ya KenGen. Biashara nyingi ambazo hutegemea stima ziliathirika na kupotea kwa stima na hivyo wamiliki kupata hasara. Stima ilianza kupotea kuanzia saa moja na dakika 50 za usiku. Kenya imekuwa ikishuhudia visa kadha vya kupotea kwa stima sehemu zote, kikiwemo kile cha Agosti 26, 2023, ambapo hali hiyo ilidumu kwa zaidi ya saa 20. Kisa cha Agosti kilitanguliwa na kingine cha Machi 2023, ambacho Kenya Power ilidai kilisababisha na hitilafu katika mitambo yake. Mnamo Novemba 2022 na Desemba 2022, maeneo ya Nairobi na Mlima Kenya yaliathirika na kupotea kwa stima. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA DANIEL OGETTA JUMLA ya maafisa 32 wa Polisi wa Utawala (APs) walifanya harusi ya pamoja chini ya ufadhili wa Afisi ya Mke wa Naibu Rais (OSDP). Harusi hiyo ilifanywa Jumamosi katika Chuo cha Mafunzo ya Polisi wa Utawala (APTS) eneo la Embakasi, Nairobi. OSDP ilisimamia na kufadhili maandalizi ya harusi hiyo ya maafisa hao wa usalama ambayo hufanywa kila mwaka chini ya kauli mbiu ya wakfu wa Pasta Dorcas Rigathi ya ‘Ukasisi na Uhubiri na Utunzaji wa Maadili ya Familia’. Bi Rigathi alisema alibuni maoni ya kudhamini harusi ya maafisa wa polisi ili waweze kuhalalisha ndoa zao. “Kwa njia hiyo wake wa maafisa wa polisi wanaweza kuwa salama endapo kwa bahati mbaya waume wao wataaga dunia,” akasema. Kulingana na afisa mmoja katika OSDP, harusi hiyo ilidhaminiwa na afisi hiyo kwa kima cha asilimia 80. Maafisa hao walighiramia mavazi, pete na mahitaji mengine madogo ya sherehe hiyo. “Familia ni asasi muhimu zaidi. Nawahimiza kutopoteza imani na familia zenu. Ndoa hufaulu na ni kitu kizuri,” Bi Rigathi akasema. Akaongeza: “Nafahamu kwamba maafisa wengi hukabiliwa na changamoto nyingi kutokana na aina ya kazi wanayofanya. Nyakati nyingine kazi ya maafisa hawa huwa ngumu na hatari ndiposa wanahitaji familia thabiti.” Bi Rigathi alisema wakfu wake utaendelea kuandaa harusi kwa maafisa wa usalama wanaohitaji. Askofu Simon Mwangi ambaye ni mkurugenzi wa wakfu wa Ukasisi, Uhubiri na Maadili ya Kifamilia katika Afisi ya Bi Rigathi alisema mnamo Juni wakati mipango ya harusi hiyo ya pamoja ilianza, wanandoa 87 walikuwa wamejisajili. Lakini kutokana na sababu mbalimbali baadhi yao walijiondoa. “Tulikuwa na wanandoa 87 waliojisajili. Waliwasilisha maombi kwa msajili wa ndoa ili waidhinishwe kushiriki katika hafla hii,” Askofu Mwangi alieleza. “Lakini wengi wao hawakuweza kuvuka hatua hiyo, kimsingi, kwa sababu wazazi wa wake waliitisha mahari. Na kwa sababu wengi wao hawakuwa wamekutana na wakwe zao kulipa mahari, hawakufika hatua hii. Lakini ni furaha yetu kwamba wanandoa 32 wameweza kufikia hatua hii. Hili ni kundi letu la kwanza,” akaongeza. Mipango ya harusi hiyo ya pamoja ilipoanza, OSDP ilitoa ushauri wa ndoa kwa maafisa 200 wa polisi. Ni baada ya hapo, Askofu Mwangi alisema, ambapo OSDP ilianzisha kampeni ya kusajilia maafisa kwa hiari. “Usajili huo ulikuwa wazi kwa maafisa wote za usalama. Kufikia mwaka ujao, tunataraji kusimamia harusi ya mamia ya maafisa wa polisi kwa sababu wengi wao wameshuhudia ufanisi wa hafla ya leo. Baadhi yao wameanza kujisajili na ninatumai kuwa idadi ya wanaojisajili itaongeza kadri muda unavyosonga,” Askofu Mwangi akasema. Afisa Eric Muturi na mkewe Alice Wairimu, ambao wameishi pamoja kwa miaka mitano ni miongoni mwa wanandoa ambao walihalalisha ndoa Jumamosi. Walikutana kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook mnamo Aprili 2018. Walikutana ana kwa ana baadaye Novemba 2018. Kisha walianza kuchumbiana kupitia mitandaoni. Uhusiano wao uliendelea kuimarika hadi wakaanza kuishi pamoja mnamo 2019. Mabwana Harusi walivalia sare zao rasmi za kikazi na Bi Harusi ambao ni maafisa wa polisi lakini waume zao sio polisi, walipewa ruhusa ya kuvalia mavazi ya harusi. Kasisi aliyesimamia harusi hiyo Cleopha Mophat akawauliza mabwana harusi hivi: “Unakubali kuchukua mwanamke huyu kuwa mke wako halali.” Na wakajibu hivi kwa pamoja: “Ndio ninakubali”. Kasisi Mophat aliuliza swali sawa na hilo kwa Mabibi Harusi, na wakatoa majibu sawa na ya waume wao. Na hapo ndipo wakatambuliwa kama wake na waume rasmi na kihalali kwa mujibu wa sheria. Bi Rigathi alikamilisha hafla hiyo ya kipekee kwa maombi. Baadaye wanandoa wakarushiana mabusu. Umati ulishangilia, maombi yakafanywa na wanandoa hao wakaondoka na kuanza maisha kama watu waliooana kisheria. TAFSIRI: CHARLES WASONGA You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA SERIKALI imetoa tahadhari kuhusu usalama wa nyama ya kuku inayouzwa Nairobi na miji mingine mikuu nchini. Kwenye taarifa, mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Mifugo Obadia Njagi alisema aina nyingi ya nyama aina hiyo inayouzwa katika maduka mengi huwa haijakaguliwa na maafisa wa afya. Kulingana na Bw Njagi, wakati huu kuku huchinjwa katika maboma ya watu badala ya vichinjio maalum namna inavyohitajika kisheria. Aliongeza kuwa usafirishaji wa nyama kutoka maboma ya watu binafsi hadi kwenye maduka unafanywa pasina kanuni za usalama na usafi kuzingatiwa. “Nyama hii hupatikana moja kwa moja kutoka kwa wafugaji wa kuku wa nyama, ambao huwachinja katika vibanda vyao na kuisafirisha hadi kwa hoteli na mikahawa mingine. Nyama hii si salama,” Bw Njagi akasema kwenye barua iliyonakiliwa kwa wakurugenzi wa idara hiyo katika ngazi za kaunti. Maduka yaliyolengwa zaidi ni yale yanayouza vyakula vya mafuta (fast food) katikati mwa jiji la Nairobi na miji mingine nchini. Vichinjio vingi nchini vililaumiwa kwa kutoa nyama ya kuku moja kwa moja kutoka kwa wafugaji kuku. “Hii ni kinyume na Sheria ya Kusimamia Usalama wa Nyama, kifungu cha 356 inayosema kuwa wanyama wa kuliwa sharti wachinjwe katika vichinjio vilivyoidhinishwa na kupewa leseni na ambavyo hukaguliwa na maafisa husika,” akasema. Bw Njagi aliwashauri wakaguzi wa nyama katika kaunti kufuatilia kwa makini mwenendo huo mbaya unaoweka maisha ya Wakenya hatarini. Idara hiyo pia imeonya kuwa wafanyabiashara watakaopatikana na hatia ya kukiuka sheria na mahitaji kuhusu nyama ya kuku watachukuliwa hatua kali. “Maovu kama hayo huwaweka wateja katika hatari ya kununua nyama isiyo salama na yenye vimelea vya kusababisha maradhi,” barua hiyo ikasema. Kwa upande mwingine, Bw Njagi aliwashauri Wakenya kuwa wakini wanaponunua nyama ya kuku kutoka kwa maduka mbalimbali jijini Nairobi na miji mingine nchini, kufuatia ufichuzi unaotilisha shaka usalama wa nyama hiyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA KASSIM ADINASI KIONGOZI wa Azimio la Umoja-One Kenya Raila Odinga ametishia kwamba atabwaga hadharani sakata ya ufisadi akisema ndiyo chanzo cha bei ya mafuta kuendelea kupanda kila uchao. Bw Odinga ambaye alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Awelo amesema kuna bonge la sakaka katika sekta ya mafuta nchini. “Tumefanya uchunguzi wetu na wiki ijayo nitaanika sakata hiyo hapa nchini Kenya. Ufisadi katika sekta hiyo ni mkubwa na unahujumu maendeleo kote nchini,” amesema Bw Odinga. Akaongeza: “Hata (Rais wa Uganda Yoweri) Museveni ameapa kukoma kununua mafuta hapa Kenya kwa sababu ya ufisadi. Alisema hawezi kufadhili ufisadi nchini Kenya na ndiyo sababu anajitoa.” Waziri huyo mkuu wa zamani amedai kwamba serikali ‘inakulia’ Sh30 kwa kila lita ya mafuta yanayouzwa nchini. “Hii inahujumu na kumfinya mwananchi wa kawaida,” amesema. Kiongozi huyo wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) ameitaka serikali ikome kumfinya mwananchi wa kawaida. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA STEPHEN ODUOR POLISI katika eneo la Madogo kaunti ya Tana River wanamzuilia mwanamke mmoja na wasaidizi wake kwa kutia mchanga kwenye pakiti za unga na kuwauzia wateja wasiojua. Fatuma Issa alikamatwa baada ya muuzaji kumshtaki kwa kumuuzia bandali saba za mchanga uliokuwa umetiwa ndani ya mfuko wa unga wa ngano chapa fulani nchini. Wengi hutumia unga wa ngano kupika chapati almaarufu ‘chapo’. Wengine huutumia kupika maandazi na mahamri. Kulingana na ripoti ya polisi, mwanamume kwa jina Edward alikuwa amemtumia mshukiwa mkuu Sh11,900 kwa mifuko minne ya unga, ila akagundua baadaye kuwa mifuko hiyo ilikuwa imejaa mchanga. “Wateja wangu walinijuza saa chache baada ya kuwauzia kuwa bidhaa niliyodhania ilikuwa unga ilikuwa mchanga. Ilinilazimu kufungua pakiti nyingine ndipo nikagundua nilikuwa nimehadaiwa,” akasema Bw Edward. Anaeleza kuwa, hakumpigia simu muuzaji huyo kwa kuhofia kuwa angetoroka punde tu baada ya kujuzwa habari hizo. Wamiliki wengine wawili wa duka pia walitapeliwa, kwani walikuwa wamenunua bandali 15 za unga huo lakini uliojaa changarawe. Polisi walimtafuta mshukiwa na kumpata mafichoni alikokuwa ametorokea na kukodisha chumba eneo la Adele, umbali wa kilomita moja na nusu kutoka Madogo. Aidha alipatikana akitia changarawe ndani ya mifuko ya unga, tayari kufikisha bidhaa sokoni. Naye mshukiwa mwingine ambaye anadaiwa kushirikiana naye amekamatwa. Tony Mokaya alikamatwa akiwa na mifuko 240 ya changarawe ndani ya mfuko wa unga wa ngano. Wawili hao wamezuiliwa katika kituo cha polisi cha Madogo wakisubiri kufikishwa mahakamani Jumanne. Jumatatu, Novemba 13, 2023, ni sikukuu ya kupanda miti, serikali ilitangaza. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

Na XINHUA KHARTOUM, SUDAN MAMIA ya watu wameuawa na wengine kudhulumiwa katika mapigano katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan, kulingana na ripoti zilitolewa na mashirika ya nchi hiyo na yale ya kimataifa. Shirika la Kimataifa kuhusu Uhamiaji (IOM) lilisema kwenye taarifa kwamba karibu watu 700 wameripotiwa kuuawa, 100 kujeruhiwa na wengine 300 haijulikani waliko katika jimbo hilo kufuatia mapigano kati ya wanajeshi wa Sudan (SAF) na wapiganaji wa kundi la Rapid Support Forces (RSF) katika eneo la El Geneina. Nalo Shirika la Kutetea Haki za Kibinadamu la Al-Juzoor linasema watu 1,300 waliuawa na wengine zaidi ya 2,000 wakajeruhiwa katika eneo la Ardamata. Kwa upande mwingine, kundi la kutetea haki ya umma ya West Darfur State Revolutionaries Bloc lilisema kuwa watu 2,000 waliuawa na wengine 3,000 wamejeruhiwa katika vita hivyo vilivyodumu kati ya Jumatatu na Ijumaa wiki hii. Awali, mnamo Alhamisi Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kutoa Usaidizi Sudan (UNITAMS) kilisema kuwa kundi la RSF kutwaa udhibiti wa kambi ya SAF, wapiganaji wanaounga mkono RSF walitekeleza vitendo vya ukiukaji haki katika kitongoji cha Ardamata, eneo la El Geneina. Ripoti zinasema kuwa wapiganaji wa Kiarabu waliuawa raia kadha na kuwajeruhi watu wengine wengi katika jamii ya Masalit. UNITAMS ilielezea hofu kuwa vita hivyo vinasababisha athari kubwa kwa raia na kutoa wito kwa pande hasimu kuzingatia wajibu wao wa kulinda maisha ya raia wakati wa makabiliano hayo. Aidha, ubalozi wa Amerika jijini Khartoum ulitoa taarifa ukielezea hofu yake kuhusu vitendo vya ukiukaji wa haki za kibinadamu vinavyotekelezwa na kundi la RSF na wapiganaji wanaoliunga mkono. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA WINNIE ONYANDO RAIS William Ruto na Naibu wake Rigathi Gachagua wametofautiana kuhusu mvua ya El-Nino iliyotabiriwa kuwa itanyesha nchini. Akihutubia vyombo vya habari katika Harambee House Annex, Nairobi mnamo Ijumaa, Bw Gachagua alisema kuwa mvua inayoshuhudiwa kote nchini ni El-Nino. “Nadhani suala hilo limetatuliwa… mvua inayonyesha ni El-Nino,” akasema Bw Gachagua. Hii ni baada ya Bw Gachagua kumuambia Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa Dkt David Gikungu kuwaomba Wakenya msamaha na kutangaza kuwa nchi inapokea mvua ya El-Nino. “Nataka kueleza kuwa kama ilivyotabiriwa hapo awali, tuna El-Nino katika msimu huu wa mvua fupi 2023 na tunaomba radhi kwa hilo,” Dkt Gikungu alibainisha. Hata hivyo, mnamo Oktoba 22, 2023, Ruto alitangaza kuwa Kenya haitakumbana na El-Nino kama ilivyotabiriwa. Badala yake, alisema kuwa msimu wa Oktoba-Novemba-Desemba utakuwa wa kipindi kifupi cha mvua ambayo haitaleta madhara kwa wakulima. “Hivi majuzi ulisikia kwamba nchi yetu itakabiliwa na El-Nino, lakini Mungu ni nani,” Ruto alisema. Hii inaonyesha wazi kuwa viongozi hao wawili wanawakanganya Wakenya. Hata hivyo, Bw Gachagua amesema kwamba serikali imejipanga kukabiliana na athari za El-Nino. “Tayari tumeanza kusambaza chakula kama vile maharagwe, mahindi, mchele na mafuta ya kupika kwa waathiriwa wa mvua,” Bw Gachagua akasema. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MUNGUTI UCHAGUZI wa viongozi katika makanisa yote ya dhehebu la Africa Inland Church (AIC) ambao ungeanza Novemba 12, 2023, umesimamishwa na Mahakama Kuu. Akipiga breki uchaguzi huo wa makanisa ya AIC, Jaji Lawrence Mugambi alisema wadhifa wa Askofu wa Eneo (ACC) haukutangazwa wazi ilhali Maaskofu wanaohudumu katika nyadhifa hizo wanafaa kuchaguliwa upya. Katika kesi iliyoratibishwa kuwa ya dharura, Jaji Mugambi aliwaamuru walalamishi watano waliowasilisha kesi hiyo wamkabidhi Askofu Mkuu wa AIC Kasisi Abraham Mulwa nakala ya kesi waliyoshtaki pamoja na agizo la kusitisha uchaguzi huo katika muda wa siku tatu. Walalamishi waliowasilisha kesi hiyo ni Kasisi Stephen Melly ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chebisaas District Church Council (DCC), Pasta Dan Saat, Barnabas Sergon, Meshack Rutto, na John Maritim. Jaji Mugambi alifahamishwa endapo uchaguzi huo utaendelea haki haitatendeka kwa vile baadhi ya maaskofu wanaosimamia maeneo-ACC-wamekamilisha vipindi vyao vya kuhudumu lakini wamekwamilia katika nyadhifa hizo. Walalamishi hao wamewashtaki Askofu Mkuu Mulwa, Naibu Askofu Mkuu Kasisi Paul Kirui, Mwekahazina Mkuu Bw Samuel Gichuhi, na Katibu Msimamizi Kasisi John Kitala. Walalamishi walimweleza Jaji Mugambi katika utaratibu wa uchaguzi wadhifa wa Askofu wa Eneo (ACC) haukutangazwa huku wakiomba mahakama iamue kwamba wanaohudumu katika nyadhifa hizo wanastahili kuchaguliwa upya. Walalmishi hao wanadai Kasisi Kitala hakutangaza wazi nyadhifa za maaskofu hao wa maeneo ACC. Mahakama ilielezwa maaskofu hawa wanataka kujishinikiza katika nyadhifa hizo pasi kuchaguliwa. Pia walalamishi hao walimweleza Jaji Mugambi kwamba uchaguzi huo umekumbwa na kasoro tele na “unafaa kusimamishwa hadi pale utaratibu muafaka utakapofuatwa.” Chaguzi za kamati mbali mbali zilikuwa zimeorodheshwa kuendelea kati ya Novemba 12, 2024, hadi Januari 11, 2024, ambapo wanachama wa Baraza Kuu (CCC) la AIC watakapochaguliwa. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA SAMWEL OWINO KENYA imeomba ufadhili wa Sh36 bilioni kutoka jamii ya kimataifa ili kuwatayarisha polisi wake 1,000 watakaoelekea Haiti kwa shughuli za kulinda amani. Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki aliwaambia wabunge kwamba pesa hizo zitatumiwa kutoa mafunzo ya ziada kwa maafisa hao na kununua vifaa watakavyotumia wakiwa Haiti. Ikizingatiwa kuwa mataifa mengine pia yatachangia walinda usalama katika kikosi cha kulinda amani Haiti (HMSSM) gharama ya mpango huo huenda ikawa juu zaidi. Profesa Kindiki aliambia Kamati ya Pamoja ya Wanachama wa Kamati za Usalama katika Bunge la Kitaifa na Seneti kwamba pesa hizo (Sh36 bilioni) pia zitatumika kununua silaha, risasi na vifaa spesheli za kupambana na fujo. “Pesa za kugharamia shughuli hiyo zitatokana na michango kutoka kwa mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa na mashirika husika. Pesa hizo zitawekwa katika hazina maalum,” Profesa Kindiki akaiambia kamati hiyo ambayo inakusanya maoni kutoka kwa umma kuhusu mpango huo wa Kenya kutuma polisi wake kupambana na magenge ya wahalifu nchini Haiti. Angalau mataifa mengine kumi yameonyesha kujitolea kwao kutuma walinda usalama katika nchi hiyo ya Caribean. Lakini ni polisi wa Kenya ndio wataongoza kikosi kizima kutoka mseto wa mataifa ambacho kilipata idhini ya kutekeleza kibarua hicho kutoka kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) mnamo Oktoba 2, mwaka huu. Nchi zingine zitakazoshirikisha walinda usalama katika kikosi hicho ni pamoja na Senegal (350), Burundi (250), Chile, Jamaica, Ecuador, Barbados (200) na Ushelisheli ambayo itatuma maafisa wa usalama 190. Mataifa mengine yaliyoonyesha nia ya kupeleka wanajeshi Haiti ni Mongolia, Uhispania na Bahamas. Amerika imetangaza kuwa itatoa ufadhili wa dola 200 milioni (Sh30.4 bilioni) kwa shughuli hiyo huku Canada ikiahidi kutoa usaidizi wa kiufundi. Waziri Kindiki alisema huenda Kenya itatumia pesa zake kuwaandaa polisi 1,000 watakaokwenda Haiti kisha watarejeshewa pesa hizo na baraza la UNSC. Hatua ya Kenya kukubali kuongoza ujumbe wa kikosi cha walinda usalama watakaotumwa Haiti iliibua pingamizi kali nchini. Mjini Nairobi, wakili amewasilisha kesi mahakama akitaka mahakama kusitisha mchakato huo hadi kesi hiyo itakaposikizwa na kuamuliwa. Hata hivyo, serikali imeendelea na mpango huo ikiwemo kusaka idhini ya bunge kutuma polisi hao. Nchini Haiti, baadhi ya mashirika na vuguvugu zimepinga hatua ya nchi za kigeni kuingilia shughuli za taifa hilo. Tangu 1920s, Haiti ambayo ndio taifa la kwanza la watu weusi duniani kupata uhuru, imeshuhudia hali ambapo mataifa ya kigeni huingilia mizozo yake. Hali ya usalama nchini humo imezoroteshwa na magenge ya wahalifu katika miaka ya hivi karibuni. Hii ni baada ya nchi hiyo kupitia mapinduzi 13 na mauaji ya viongozi wake saba katika miaka ya nyuma. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MHARIRI
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini.
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na BENSON MATHEKA
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na MASHIRIKA
LONDON, Uingereza
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya... Na ELIZABETH MERAB
WANASAYANSI wanachunguza kuhusu mchipuko wa virusi vipya vya corona aina ya Delta, katika nchi za Amerika, Uingereza,... Na MAUREEN ONGALA
MASAIBU ambayo wagonjwa wa Covid-19 hupitia katika kaunti za Pwani, yameanikwa wazi baada ya kifo cha afisa mkuu wa... SIAGO CECE na ANTHONY KITIMO
UFISADI miongoni mwa baadhi ya maafisa wa serikali katika mpaka wa Kenya na Tanzania, umezidi kuwaweka... Na WAANDISHI WETU