text
stringlengths
3
16.2k
UFICHUZI wa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko kwamba mtu aliingia kwenye seli anamozuiliwa katika kituo cha... Na BENSON MATHEKA
Aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Bw Mike Sonko anajuta kwa vitendo alivyofanya akiwa mamlakani; akiepuka kuadhibiwa kwa... Na RICHARD MUNGUTI
KAMA kuna wakati wenye changamoto tele kwa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko ni sasa.
Maji yalizidi unga hata... Na RICHARD MUNGUTI
MASAIBU ya aliyekuwa gavana wa Nairobi, Bw Mike Sonko, yaliongezeka Jumatano ilipofichuka kuwa serikali inapanga... Na RICHARD MUNGUTI
ALIYEKUWA Gavana wa Nairobi, Mike Sonko aliangua kilio kortini Jumatano wakati wa kusikizwa kwa kesi ya ufisadi wa... Na CHARLES WASONGA
WANASIASA na watu ambao majina yao yatawekwa katika orodha ya aibu ya Tume ya Uwiano na Utangamano ya Kitaifa (NCIC)... BENSON MATHEKA na SIMON CIURI
Masaibu ya aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Mike Sonko yaliendelea kuongezeka jana alipozuiliwa rumande baada... Na RICHARD MUNGUTI
MASAIBU ya aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko Mbuvi Gidion Kioko yameongezeka baada ya  kusukumwa ndani hadi... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA SAMMY WAWERU MSANII tajika wa nyimbo Mugithi, Samuel Muchoki maarufu kama Samidoh huenda ametengana na mpenzi wake mwanasiasa Karen Nyamu. Hii ni kutokana na video iliyochipuka ambayo anaskika akisema “nilikuwa kwenye ndoa ya mitara, sasa niko singo”. Samidoh amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Seneta Maalum Karen Nyamu, na wamejaaliwa kupata watoto wawili. Msanii huyo wa nyimbo za Agikuyu, alifichua kuachana na Karen kupitia video ya mbashara ya Tiktok (live) ambapo alikuwa akijibu maswali ya mashabiki wake. Wakati wa mafichuzi hayo, alionekana kuwa kwenye eneo la burudani alikoandamana na msichana ambaye hakuweka wazi endapo ndiye mchumba wake mpya. “Ati hongera kwa kuwa na mpenzi mpya…” Samidoh akasoma mojawapo ya jumbe zilizotumwa na mashabiki wake. Alijibu, “Si wewe pekee ulishushwa madaraka kutoka kiwango cha hadhi hadi dereva wangu…Nilikuwa kwenye ndoa ya mitara ila sasa niko singo”. Mfuasi huyo aliendelea kumdadisi, akitaka kujua iwapo Samidoh anafahamu kuhusu ukurasa wa kimitandao unaohusishwa na mchumba wake – Karen Nyamu Fun Page. Kwa ucheshi, mwimbaji huyo wa kibao tajika cha Kairetu Gakwa (Binti yangu) na Ndiri Mutwe Mwega (Sina kichwa kizuri) alisema kwa sasa anajishughulisha na biashara. “Kwa sasa, ninajishughulisha na masuala biashara. Ikiwa si mradi au biashara, ishi na mama yako,” alielezea. Shabiki wake alimkejeli akitaka kujua aliko nina yake, isijulikane ikiwa alimaanisha mama yake mzazi au mpenzi wake. “Ameoleka na kwa sasa anafurahia fungate (honeymoon),” Samidoh alidokeza. Kidosho aliyeandamana naye alitambua shabiki huyo kama Shabaan, akisema kwamba yeye ni mchochezi. “Wee acha hiyo, unajua Shabaan wewe ni mchochezi sana… (Yuko hapa (akimaanisha Karen Nyamu),” mwanadada huyo alisema. Naye Samidoh aliendelea, “Tunataka Karen, naona hivo ndivo mchango safuni unasema…Naona, lakini sasa yuko online kweli?” Kipusa aliyeandamana naye, alijibu, “Yuko online, mjaribu”. Aidha, shabiki wa Samidoh alitaka Karen Nyamu ajumuishwe kwenye mazungumzo hayo ya mbashara Tiktok. Kilichoshangaza zaidi na kuashiria utengano wa Samidoh na Karen, ni kudai kwamba alimbloki mtandaoni na angeweza kushiriki endapo atamuondoa alikomuweka. “Yuko kwenye orodha ya kublokiwa, sasa hiyo ndio shida. Labda nisitishe mazungumzo haya ya moja kwa moja ili nimuondoa aweze kujumuika nasi,” Samidoh alifafanua. Mahusiano kati ya Samidoh na Karen, ndiyo yalichangia kuachana na mkewe, Edday Nderitu ambaye alihamia Amerika Mei 2023. Edday alikuwa ameonya msanii huyo mapema 2023, akisisitiza kwamba hakuwa tayari kuwa kwenye ndoa ya mitara. Samidoh na Edday wana watoto watatu pamoja. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MAOSI WAKAZI wa mtaa wa Mazembe viungani mwa mji wa Nakuru wamekiri kuhangaishwa na wezi ambao huwaibia na kuwasindikiza hadi nyumbani. Huwawekea ulinzi huo makusudi ili kuhakikisha kwamba wateja wao wanafika nyumbani salama salimini. Kwa kawaida, wahuni wamebuni mbinu mpya ya kutembea na mbwa wakubwa nyakati za usiku, ili kujiwekea ulinzi wa kibinafsi. Owen Shibala mwendeshaji bodaboda kati ya Nakuru mjini na Mazembe, anasema hajui walikotoa ujasiri walio nao kushika doria usiku utadhani ni polisi. Mazembe ni mojawapo ya mitaa ambayo hushuhudia visa vya kihalifu na utumiaji wa mihadarati mara kwa mara. “Ukikutana nao usiku ni lazima usalimishe kila kitu lau sivyo utaona cha mtema kuni. Watakucharaza viboko na kuiba kila kitu cha nguvu,”akasema. Hata hivyo, wanapoiba hujitwika jukuma la kuwasindikiza wakazi, wasije wakakutana na vibaka wengine barabarani. Aidha, wanalia sare za polisi jambo linalowafanya baadhi ya raia kuamini huenda wanashirikiana na maafisa wa polisi. Baadhi yao wanajifanya ni maafisa wa polisi ambao huwa wameshika doria, wakilenga kuhangaisha wapita njia wanaotoka kazini usiku. Agnes Wahome mfanyibiashara mtaani Rhonda anasema huwa wamejihami kwa visu, rungu na wako tayari kupigana. Kulingana na Bi Wahome, hii ni hali ya kawaida siku hizi katika mitaa ya Manyani, Bondeni na Freearea ambapo vijana wengi wamejiingiza kwenye uhalifu. Bi Wahome anasema wahalifu wengi wanajulikana, kwani ni vijana wadogo kutoka mitaa jirani ya Flamingo na Lakeview. Mkazi huyo angependa polisi kushika doria katika maeneo husika ili kuzuia kuzuka kwa magenge hatari yanayohangaisha wenyeji. Hili linajiri siku chache baada ya Taifa Leo Dijitali kufichua visa vya wizi ambapo baadhi ya wezi kutoka kwenye mtaa wa Gioto, Nakuru wamekuwa wakipika chakula katika kila nyumba wanamoingia kuiba. Mtaa wa Bondeni, Kaunti ya Nakuru ambapo wezi huwaibia wakazi na kuwasindikiza mpaka nyumbani. PICHA|RICHARD MAOSI
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L

You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MUNGUTI MASKWOTA wapatao 10,000 wamewasilisha upya kesi katika Mahakama ya Upeo wakiomba ibatilishe uamuzi kwamba wafukuzwe kutoka kwa shamba la ukubwa wa ekari 25,000 wanalong’ang’ania umiliki wake na familia ya mwanasiasa marehemu Mark Too. Maskwota hao wanaodai mababu zao ndio waliotimuliwa kutoka kwa shamba hilo enzi za ukoloni, wanasema walipewa shamba hilo rasmi na aliyekuwa Rais hayati Daniel arap Moi, kisha Kamishna wa Ardhi M Okundu akaratibisha uamuzi huo mwaka 2007. Katika ombi lililowasilishwa na wakili William Arusei chini ya sheria za dharura, kikundi cha maskwota hao–Sirikiwa Squatters Group–kimeomba mahakama ibatilishe uamuzi huo kwa vile ilitegemea ushahidi ambao haukuwa umewasilishwa katika kesi waliyoshtaki katika Mahakama ya kuamua kesi za mashamba (ELC), Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu. Pia wameeleza bayana Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaack Lenaola, na William Ouko walitegemea ushahidi wa Afisa wa Ugavi wa Mashamba R J Simiyu kutoa uamuzi wang’atuke shambani. Maskwota hao wamesema ushahidi wa Bw Simiyu uliowasilishwa mbele majaji hao saba kwa njia ya afidaviti ni mpya na kamwe “haukuwasilishwa mbele ya Jaji Antony Ombwayo aliposikiliza na kuamua kesi hiyo 2017.” Pia wanasema ushahidi huo haukuwasilishwa Mahakama ya Rufaa iliyosikiliza rufaa iliyowasilishwa na kampuni ya Fanikiwa, familia ya marehemu Mark Too, kampuni ya Lonrho Agribusiness (EA) Ltd, na Bw David K Korir. Hivyo basi, maskwota hao wanaeleza mahakama hii ya upeo kwamba ni kinyume cha sheria kutegemea ushahidi mpya kutoa uamuzi wa kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma. “Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu wa Desemba 15, 2023, hauna mashiko kisheria na kamwe hauna nguvu kisheria kuwatimua maskwota hawa kutoka kwa shamba lao,” asema Bw Arusei. Pia maskwota hawa wanadai kwamba badala ya Mahakama ya Juu kujadili masuala ya kikatiba jinsi ilivyo jukumu lake, majaji hao walianza kufafanua na kutafsiri ushahidi wa watu binafsi na kuelezea maana ya ‘skwota’. Mahakama hii imeombwa ikague upya uamuzi iliyotoa kwa vile ilidanganywa na walalamishi na pia kutendewa ujanja. Akinukuu maamuzi ya majaji wastahiki kama vile Lord Dening, Bw Arusei amesema, mahakama ikigundua ilipotoshwa au kudanganywa na upande mmoja, iko na mamlaka na uwezo wa kufutilia mbali uamuzi iliyotoa na kuandika mwingine. Maskwota hao wanaomba Mahakama ya Juu iwarudishe shambani kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Ombwayo na Mahakama ya Rufaa. Vile vile mahakama hiyo imekosolewa kwa kumshambulia hayati Moi katika uamuzi huo pasi kutoa agizo wasimamizi wa mali yake wafike mbele yao kutoa mwanga kuhusu suala la umiliki wa shamba hili lililorudishwa kwa serikali na kampuni iliyokuwa inakuza miti inayotumika katika viwanda vya ngozi. Naibu msajili wa Mahakama ya Juu Nelly Kariuki aliwaamuru maskwota hao wawakabidhi nakala za kesi hii yao mpya wahusika wote kabla ya Januari 31, 2024, kesi itakapotajwa tena kwa maagizo zaidi. Jaji aliyesikiliza kesi hii mpya hakuiratibisha kuwa ya dharura ila aliamuru pande zote ziwasilishe ushahidi katika muda wa siku 14 kuanzia Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti,  baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA BRIAN OCHARO MHUBIRI Paul Nthenge Mackenzie amepatikana na hatia ya kutumia filamu ambazo hazijakaguliwa na kuainishwa, mwanya ambao inadaiwa alitumia kuendeleza mafundisho ya kidini yenye itikadi kali. Hakimu Mkazi wa Malindi Onalo Olga alisema upande wa mashtaka ulithibitisha bila shaka yoyote mashtaka mawili ya kumiliki filamu ambazo hazijaainishwa, na kuendesha studio ya kurekodia filamu bila leseni zaidi ya shaka. “Mshukiwa amepatikana na hatia kwa mashtaka mawili ya kumiliki na kusambaza filamu kwa umma ambazo hazijachunguzwa na kuainishwa na Bodi ya Uainishaji wa Filamu Nchini (KFCB) na kuendesha studio ya kurekodi filamu na kutengeneza filamu bila leseni halali,” alisema hakimu. Hakimu huyo hata hivyo alimuachiliaa huru Mackenzie katika shtaka la kwanza ambapo alishtakiwa kwa kuchochea umma kukiuka sheria. Hapa, serikali ilidai kuwa Mackenzie alichochea watoto dhidi ya kuhudhuria shule na kutumia zaidi filamu hizo kuwachochea watu dhidi ya Wahindu, Wabudha, na Waislamu. “Upande wa mashtaka haujathibitisha shtaka hilo kwa kiwango kinachotakiwa kisheria, hivyo basi mshukiwa ameachiliwa kwa kosa la kwanza la uchochezi wa uvunjaji wa sheria,” alisema hakimu huyo. Mackenzie alikuwa amejitetea kwamba hajawahi kusababisha migogoro kati ya dini kupitia mahubiri yake, ambayo alisema yalilenga ujumbe wa nyakati za mwisho kwa wafuasi wake na wale waliojali kusikiliza. “Yaliyomo katika kanda ya DVD yalikuwa maudhui ya wachungaji na makanisa mbalimbali duniani kote. Nilikuwa na kituo cha runinga cha Kanisa la Good News International Church lakini upande wa mashtaka haukuleta ushahidi kuonyesha kuwa vidio zilizofikishwa mahakamani zilipeperushwa na kituo cha runinga cha Times,” alisema. Mackenzie aliiambia mahakama kuwa anafahamu kuwa jumbe zake za nyakati za mwisho ziko kwenye chaneli ya YouTube inayoitwa Times Tv na kwamba yeye ndiye alizipakia huko ili kuwasilisha mafundisho yake. Hata hivyo, mahakama ilisema kuwa serikali kupitia kwa Kiongozi wa Mashtaka Joseph Mwangi ilithibitisha kesi dhidi ya Mackenzie bila shaka yoyote. Hakimu alibaini kuwa Mackenzie alishindwa kujiondoa kutoka kwa ushahidi wa mashahidi wanne wa upande wa mashtaka na vielelezo vikiwemo kanda za video akitoa mahubiri hayo makali. Pia, mahakama iliona kuwa Mackenzie alikiri kuwa Televisheni ya Times ilikuwa ya kanisa lake, ambapo filamu za DVD zenye mahubiri ya wakati wa mwisho zilipatikana ofisini kwake. Mackenzie angali kizuizini katika gereza la Shimo La Tewa. Anazuiliwa kuhusiana na kesi ya vifo vya mamia ya watu katika msitu wa Shakahola. Anadaiwa kuwapotosha wafuasi wa mafundisho yake ambapo zaidi ya wa 400 waliangamia kupitia mfungo mbaya ambao umeishangaza dunia. Mahakama imemruhusu Mackenzie muda zaidi kuwasilisha jibu la ombi la serikali la kutaka kumweka kizuizini kwa miezi sita zaidi. Hakimu Mwandamizi Mkuu wa Shanzu Yusuf Shikanda wakati huo huo alimruhusu wakili wa Mackenzie, Bw Wycliffe Makasembo kukutana naye (Mackenzie) na mwenzake kupata maelezo ya kuweka kwenye hati ya kiapo ya kujibu ombi la serikali. Bw Shikanda aliagiza washukiwa ambao wanazuiliwa katika magereza ya Kilifi na Malindi wafikishwe katika gereza la Shimo la Tewa wiki ijayo kwa mkutano wa saa moja na wakili wao. Mahakama iliagiza kikao kati ya washukiwa hao na wakili wao kifanywe kabla ya saa sita mchana. Mahakama pia iliagiza Sh103, 000 zilizopatikana kutoka kwa mshukiwa aliyekufa Joseph Buyuka ziwasilishwe kortini mnamo Novemba 20, 2023. Hakimu pia aliagiza kwamba kitambulisho cha mke wa Makenzie, Bi Rhoda Wambua, ambacho kilichukuliwa na serikali, kirudishwe kwake. Serikali imeorodhesha sababu kadhaa kwa nini inataka Mackenzie na wafuasi wake wazuiliwe kwa siku 180 zaidi huku uchunguzi wa kile kilichotokea katika msitu wa Shakahola ukiendelea. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MUNGUTI KESI ya mauaji kinyama ya aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Fedha katika Nairobi Hospital Eric Maigo imechukua mwelekeo mpya baada ya mshukiwa mkuu kubadilisha maungamo yake ya hapo awali kwamba alimuua afisa huyo mnamo Septemba 23, 2023. Anne Adhiambo Ouma almaarufu ‘Nut’ alibadilisha mawazo na kukanusha shtaka dhidi yake aliposhtakiwa mbele ya Mahakama Kuu ya Kibra, mnamo Alhamisi. Mnamo Oktoba 26, 2023, Adhiambo alikiri kwamba alimuua Bw Maigo aliposomewa shtaka mbele ya Jaji Kanyi Kimondo. Kuungama mauaji hayo kuliwashtua wote hata Jaji Kimondo akamiuliza mara tatu: “Unakiri ulimuua Erick Maigo. Unakiri ulimuua Erick Maigo. Kweli unakiri ulimuua Erick Maigo?” Adhiambo alidumisha maungamo yake lakini Jaji huyo akaamuru azuiliwe katika gereza la wanawake la Langata kutafakari maungamo yake. Jaji huyo aliamuru wakati huo kwamba mshtakiwa afikishwe mbele ya Jaji Diana Kavedza jana Novemba 9, 2023, kusomewa shtaka tena. Pia Jaji Kimondo alimtaka wakili Samuel Ayora anayemtetea Adhiambo amshauri kuhusu athari za kukiri shtaka moja kwa moja. Bw Ayora aliyeshtushwa na maungamo hayo aliambia korti “nimepigwa na butwaa Adhiambo anakiri shtaka.” “Nilikuwa nimemshauri lakini ameamua kukiri shtaka. Naomba nipewe muda kuzugumza naye zaidi,” akasema Bw Ayora. Kesi hiyo ilipotajwa mbele ya Jaji Kavedza, Bw Ayora aliomba mahakama imsomee mshtakiwa shtaka upya. “Naomba mshtakiwa asomewe kesi upya. Nimeshauri kuhusu athari za kukiri shtaka,” Bw Ayora alisema. Jaji alimsomea Adhiambo shtaka upya kwamba anadaiwa alimuua Maigo mnamo Septemba 23, 2023, katika mtaa wa Woodley, Nairobi ndipo akajibu,“Si kweli.” Kesi hiyo iliendelea kwa njia ya mtandao. Kiongozi wa mashtaka Allan Mulama alipinga ombi la mshtakiwa kuachiliwa kwa dhamana akisema “atatoroka.” Bw Mulama alisema tabia ya mshtakiwa kuhepa na kujificha kwa zaidi ya mwezi baada ya mauaji hayo “ni ishara kwamba mshtakiwa atachana mbuga na kutokomea kabisa.” Pia mahakama ilifahamishwa mshtakiwa hana pahala maalum pa kuishi jijini Nairobi. Jaji alifahamishwa polisi walimkuta mshtakiwa akiwa amejificha katika mtaa wa mabanda wa Kibra. “Mshtakiwa atatoroka akiachiliwa na polisi hawajui pahala ambapo wanaweza kumpata,” Bw Mulama alimweleza Jaji Kavedza. Pia alisema adhabu kali itakayotolewa dhidi ya mshtakiwa akipatikana na hatia ni “kivutio chake kutoroka akiachiliwa kwa dhamana.” Bw Mulama aliomba mshtakiwa aendelee kuzuiliwa katika gereza la Wanawake la Langata hadi kesi isikilizwe na kuamuliwa. Wakili Ayora aliomba apewe muda zaidi kujibu ombi la DPP. Jaji huyo aliagiza kesi hiyo iendelee Desemba 14, 2023, Bw Ayora atakapoomba korti imwachilie mshtakiwa kwa dhamana. Adhiambo alifikishwa mbele ya hakimu mwandamizi Gilbert Shikwe mnamo Septemba na kuelezwa na Bw Ayora kwamba “afisi ya DPP haijatayarisha cheti cha shtaka na wala haijamkabidhi nakala za mashahidi.” Bw Ayora aliomba mahakama iamuru mshukiwa huyo azuiliwe katika kituo cha polisi cha Kilimani hadi atakaposomewa shtaka kwa njia ya mtandao. Bw Ayora alieleza korti kwamba Adhiambo yuko na umri wa miaka 16. Alitiwa nguvuni Septemba 26, 2023 katika eneo la Olympic, Kibra baada ya Maigo kuuawa kwa kudungwa kisu mara 25. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA NDUBI MOTURI KIONGOZI wa chama cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Economic Freedom Fighters (EFF) Julius Malema amedai hatua ya Rais William Ruto ya kuonyesha mwegemeo kwa Israeli inapokabiliana na kundi la Hamas katika ukanda wa Gaza inakiuka umajumui wa Afrika almaarufu ‘Pan-Africanism’. Bw Malema ambaye amekutana na viongozi vijana katika hoteli ya Serena, amesema Ijumaa kwamba hata ingawa baadhi ya wale wanaomuunga mkono Rais Ruto hawajakubaliana naye kwa kumsuta kuhusu suala hilo la Israel, ni lazima alizungumzie. “Huwezi ukawa wewe ni mwanamajumui halafu unaunga mkono upande unaonyanyasa Wapalestina ambao wametengwa kwa muda mrefu. Lengo la umajumui wetu unajikita kwa kutengwa tangu zamani na yeyote anayedhulumiwa anafaa kuegemea kwa bega letu,” amesema Bw Malema. Amedai Wapalestina wakiwemo wa eneo la ukanda wa Gaza wamenyanyaswa namna ambavyo wapiganiaji wa ukombozi nchini Kenya walivyodhulumiwa wakisaka uhuru. “Rais Ruto akisema anaiunga mkono Israeli, anafanya hivyo kwa msingi gani? Taifa hilo limelipua kambi za wakimbizi na kuwaua watoto na wanawake wajawazito. Mwanasiasa huyo amedai kwamba Waisraeli wameua wamiliki halisi wa vipande vya ardhi katika uwanja wa machafuko na kamwe “hatuwezi tukahurumia watu wa aina hiyo.” Amewataka viongozi vijana kujitolea na kuwaambia wakubwa wa vyama vyao ukweli wa mambo. Aidha, ametaka demokrasia ipaliliwe kwa msingi wa haki katika upigaji kura na utangazaji wa matokeo sahihi ya uchaguzi kuepusha migogoro na machafuko. Amewataka raia wasiuane akisema hata hapa nchini Kenya, endapo kiongozi wa upinzani Raila Odinga aliandikiwa urais, atakuwa tu “hata waibe namna gani.” “Wale wanaotaka niachane na siasa za Kenya, kwamba hii si Afrika Kusini, ninasema hivi… Siasa za Kenya zinanihusu namna ambavyo siasa za Afrika Kusini zinawahusu. Kila kitu kinachoathiri Afrika kinatuathiri sote sisi wanamajumui wa Afrika. Akihutubu katika Chuo Kikuu cha Lukenya katika Kaunti ya Makueni, Bw Malema alisema Rais Ruto si yule wa wakati wa kampeni alipokuwa anaomba kura. “Yale ambayo Rais Ruto alikuwa akisema na yale anayotenda sasa ni vitu viwili tofauti,” alisema mwanasiasa huyo. Alisema hayo wakati wa kuzindua Taasisi ya Umajumui katika chuo kikuu hicho. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA SAMMY KIMATU WASHUKIWA 14 walikamatwa Alhamisi huku zaidi ya katoni 200 za pombe haramu kunaswa katika operesheni kali Njiru, Nairobi. Msako huo ulifanywa na idara mbalimbali za serikali kuu, serikali ya kaunti, idara ya polisi na maafisa wa utawala. Polisi waliongeza kwamba mshukiwa mkuu yuko mafichoni. Akiongea na wanahabari, mkuu wa polisi eneo la Njiru, Bw Lucas Ongaya alisema msako huo uliongozwa na kinara wa utekelezaji katika Mamlaka ya Kudhibiti Vileo na Mihadarati (NACADA) Bw Nicholas Kosgei akishirikiana na naibu kamishna wa Njiru Bi Florence Syokau. Aliongeza kwamba operesheni hiyo ilifanyika katika eneo la Kona Mbaya katika mtaa wa Kayole. Bw Ongaya alisema miongoni mwa vilivyonaswa ilikuwa ni pamoja na pombe ambayo siku zake za matumizi zimepita, na pombe ambayo haikufikia viwango vinavyotakikana kiubora. Pia walifunga baa zilizokuwa zikiendeshwa pasipo na leseni na kuuza pombe saa zisizoruhusiwa kisheria. Katika operesheni kwenye kilabu cha kwanza kinachofahamika kama Spiders Annexe Wines and Spirits, maafisa hao walinasa pia kifurushi cha sigara feki. Aidha, mhudumu wa kike aliyekuwa kazini wakati huo alijifungia ndani ya baa na kukataa kuwafungulia polisi. Iliwalazimu wenye operesheni kutumia nguvu kupata nafasi ya kuingia kilabuni. Lililokera zaidi ni kunaswa kwa kemikali na vifaa vilivyopatikana ndani ya klabu vya kutengeneza mfinyo. “Tulinasa kemikali, vifaa na chupa zilizotumika ambapo hutumiwa tena kujazwa pombe baada ya kutengenezwa katika stoo moja wakati wa operesheni yetu,” Bw Kosgei akaambia wanahabari. Katika msako huo, maafisa hao pia walinasa nembo feki zilizobandikwa chupani za Mamlaka ya Kudhibiti Ushuru Nchini (KRA). Mbali na hayo, vyumba katika majumba tofauti mtaani humo vilivunjwa huku pombe zaidi ikipatikana. Katika baa ya pili kwa jina Spiders Annexe Bar and Restaurant, maafisa hao walitwaa runinga kadhaa kubwa zinazoaminika kuibwa kwingineko na kufichwa katika stoo. Isitoshe, ndani ya kilabu hicho kulipatikana pia mashine kadhaa za kuchezea kamari ambazo serikali ilipiga marufuku wakati wa aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani Dkt Fred Matiang’i wakati huo. Akiongea na wakazi waliofurika kushuhudia tukio hilo, Bi Syokau aliwapongeza wananchi kwa kutoa habari kwa vitengo vya usalama. Kadhalika, aliwaonya dhidi ya kunywa pombe isiyoidhinishwa kuwa salama kwa matumizi ya binadamu. “Chukueni hatua za tahadhari wakati mnatumia vileo kwa sababu hivi ambavyo havijaafikia ubora ulioidhinishwa na serikali kwa manufaa yenu, vinahatarisha maisha yenu,” Bi Syokau akasema. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA RAIS William Ruto amesema Kenya iko kwenye mkondo mzuri wa ukuaji kutokana na utekelezaji wa sera za utawala wake mwaka mmoja baada ya kuingia mamlakani. Akitoa hotuba bungeni mnamo Alhamisi kuhusu Hali ya Taifa, Dkt Ruto alisema mageuzi na mipango ambayo serikali yake inatekeleza katika sekta mbalimbali yameanza kuzaa matunda. “Tulianza kutekeleza ajenda yetu ya ufufuaji wa uchumi kuanzia ngazi za chini katika mazingira yenye changamoto kadha humu nchini na kimataifa. Lakini mipango yetu katika sekta za Kilimo, Afya, Elimu miongoni mwa zingine imeanza kuleta afueni kwa raia,” akasema. Rais Ruto alieleza kuwa serikali yake haswa imewekeza katika sekta ya kilimo kama njia mwafaka ya kudhibiti kupanda kwa gharama ya maisha. “Mpango wa serikali hii wa kupunguza bei ya mbolea kutoka Sh7,000 hadi Sh2,500 kwa gunia moja la kilo 60 sasa umewaweza wakulima kuimarisha uzalishaji wa chakula. Hii ndio maana sasa bei ya unga wa mahindi imeshuka kutoka Sh230 kwa paketi moja ya kilo mbili mwaka 2022 hadi Sh145, kwa kutegemea chapa ya unga ambao utanunua. Na mkebe mmoja wa kilo mbili wa mahindi ile inayojulikana kama gorogoro sasa inauzwa kwa kati ya Sh60 na Sh100,” Rais Ruto akaeleza. Kiongozi wa taifa alisema ni kutokana na hali hiyo ambapo Wakenya wameweza kuongeza uwezo wao wa kuweka akiba. “Kwa mfano, wale ambao wameajiriwa wamefanikiwa kuweka akiba ya Sh6.5 bilioni kila mwezi kupitia hazina ya NSSF, pesa ambazo bila shaka zitawasaidia kujiimarisha kimaisha,” akasema katika kikao hicho cha pamoja cha wabunge na maseneta. Hata hivyo, ongezeko hilo la kiwango uwekaji akiba unatokana na hatua ya serikali ya Rais Ruto ya kuongeza makato kwa hazina hiyo ya uzeeni kutoka Sh200 kila mwezi hadi Sh2,000. Aidha, Rais Ruto alisema serikali yake imepiga jeki wafanyabiashara wadogo kwa mkopo wa gharama nafuu kupitia Hazina ya Hasla. “Kufikia mwezi Oktoba, Hazina ya Hasla imetoa mikopo ya kima cha Sh36.6 bilioni huku wafanyabiashara hao wadogo wakiweka akiba ya Sh2.3 bilioni. Jumla wafanyabishara 7.5 milioni wamechukua mkopo huo zaidi ya mara moja huku kiwango cha ulipaji kikiwa asilimia 75,” akasema. Chini ya mpango wa serikali yake ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu, Rais Ruto alisema jumla ya nyumba 46,792 zimejengwa kufikia sasa. “Na nyumba nyingine 40,000 zitaanza kujengwa hivi karibuni kote nchini. Aidha, tunajenga masoko 400 katika katika mpango unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya kitaifa za serikali za kaunti,” Dkt Ruto akaeleza huku akiongeza mpango huo umezalisha zaidi ya nafasi 50,000 za ajira. Katika sekta ya elimu, Rais alisema serikali yake imejitolea kutekeleza mageuzi yote yaliyopendekezwa na jopo kazi lililoongozwa na Profesa Raphael Munavu. “Tumeajiri jumla ya walimu 56,796, idadi kubwa zaidi kuwahi kuajiriwa kwa wakati moja na Mheshimiwa Omboko Milemba hapa anaweza kuthibitisha hilo. Aidha, tumetoa mafunzo zaidi kwa walimu 8,200 watakaofunza katika kiwango cha sekondari ya msingi (JSS),” Dkt Ruto akaeleza. Aliongeza kuwa mfumo mpya wa ufadhili wa elimu ya juu utawezesha wanafunzi kutoka jamii masikini kupata elimu hiyo sawa na wengine kutoka jamii zenye uwezo. “Vile vile, mpango huu utasaidia kuondoa vyuo vyetu vikuu kutoka lindi la madeni ambayo wakati huu yamefikia kima cha Sh60 bilioni,” Rais Ruto akasema. Katika sekta ya afya, kiongozi wa taifa alisema serikali imeajiri jumla ya wahudumu wa afya katika jamii (CHPs) 100,000. “Wahudumu hao wamepewa vifaa vyote hitajika na watakuwa wakizunguka kote vijijini kutoa ushauri na huduma za afya msingi,” akaeleza. Kuhusu usalama, Rais Ruto alisema serikali yake itaendeleza mipango yake ya kupambana na aina mbalimbali za uhalifu kote nchini. “Tayari juhudi zetu za kupambana na ugaidi, ujangili, na wizi wa mifugo katika maeneo ya Kaskazini mwa Kenya, Kaskazini mwa Bonde la Ufaa na Pwani zimeanza kuzaa matunda,” akasema. Rais alisema serikali yake inatekeleza mpango ambapo vijana wa Huduma ya Kitaifa (NYS) ndio watapewa kipaumbele katika usajili wa maafisa wa vikosi mbalimbali vya polisi na jeshi.Rais Ruto pia alisema kuwa serikali yake imepiga hatua kubwa zaidi katika mpango wake wa kukumbatia mfumo wa kidijitali kuimarisha utoaji huduma. “Kufikia sasa jumla ya huduma 13,000 za serikali zinatolewa kwa mfumo ya kidijitali na kufikia Desemba huduma zote zitatolewa kwa mfumo huo,” akaeleza. Kuhusu mahusiano ya kimataifa, Rais alisema Kenya inashiriki katika michakato ya kuleta amani katika mataifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Sudan. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MARY WANGARI RAIS William Ruto jana alitoa hotuba yake ya kwanza kabisa kuhusu Hali ya Taifa kwenye kikao cha pamoja cha Bunge la Kitaifa na Seneti tangu achukue usukani mbamo Septemba 2022. Wabunge, maseneta, mawaziri na wajumbe mbalimbali waliwasili mapema na kuchukua nafasi zao kabla ya Kiongozi wa Taifa kuwasili huku baadhi wakitumia muda huo kuelezea matarajio yao kwa vyombo vya habari. Msafara wa Rais uliwasili saa nane na dakika ishirini na saba adhuhuri huku Rais akiandamana na mkewe mama Rachel Ruto. Naibu Rais Rigathi Gachagua, Maspika Seneti Moses Wetangula (Bunge la Kitaifa) na Amason (Seneti) walikuwa ngangari kumpokea Rais aliyewasalimu viongozi kabla ya kukagua gwaride la heshima. Wimbo wa Taifa na wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliimbwa. Kinyume na matarajio ya wengi waliotarajia hotuba hiyo iwe ndefu, Rais Ruto alichukua muda wa karibu saa moja tu kuzungumzia hatua muhimu ambazo serikali yake imefanikisha hasa kuhusiana na kulipa madeni, mfumo wa Bottom Up na hazina ya Hasla Fund, afya, kilimo, na elimu hususan mikopo kwa wanafunzi. Hata hivyo, hisia mseto ziliibuka baada ya Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga kukosa kuhudhuria kikao hicho. Licha ya kutengewa kiti kwenye Kitengo cha Spika katikati ya kinara mwenzake wa Azimio, Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka na Waziri wa Ulinzi Kithiki Kindure, Kiongozi wa ODM hakujitokeza. Badala yake, Bw Odinga alichagua kuhudhuria hafla iliyojumuisha vyuo vikuu mbalimbali nchini akiandamana na viongozi wengine wa ODM akiwemo Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino na Gavana wa Siaya James Orengo. Kinyume na Katibu Mkuu wa ODM Ediwn Sifuna aliyetangaza hadharani mwanzoni mitandaoni kwamba angesusia hotuba ya Rais Ruto, Bw Raila hakuashiria chochote kuhusu nia yake ya kuususia. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MARY WANGARI GAVANA wa Kaunti ya Meru Kawira Mwangaza mnamo Jumatano alikabiliwa na wakati mgumu akijitetea mbele ya Seneti kuhusiana na malalamishi yaliyowasilishwa dhidi yake na Bunge la Kaunti ya Meru. Hali ya suitafahamu iligubika Bunge la Seneti baada ya video zilizokusudiwa kutumiwa na kikosi cha mawakili tisa wanaomwakilisha Gavana Kawira, kukumbwa na hitilafu za sauti mwanzoni na kuchelewesha kikao hicho, kilichoingia siku ya pili, kwa karibu saa moja. Ilimlazimu Spika wa Seneti Amason Kingi kuingilia kati na kuwaagiza mafundi wa mitambo kumaliza mushkili huo uliotishia kuvuruga ushahidi wa mmoja kati ya mashahidi wanne wa Bi Kawira. Gavana huyo alitokwa na kijasho huku mawakili wawili wanaowakilisha Bunge la Kaunti ya Meru wakimtaka kufafanua kuhusu madai ya usimamizi mbaya na ufujaji wa pesa za umma, yakiwemo matumizi mabaya ya afisi, kwa kuruhusu jamaa zake kusimamia majukumu ya fedha za kaunti. Kuhusu kauli ya kaende kaende, gavana huyo alikanusha kuwa ilidhamiriwa kuonyesha ukaidi akifafanua kwamba ilimaanisha kuashiria kasi ya kutekeleza ajenda yake ya maendeleo katika Kaunti ya Meru. “Nilitumia kauli ya kaende kaende kabati kabati kwa sababu inaashiria maendeleo. Inamaanisha kuendeleza maendeleo kwa kasi ya juu bila kukatiza,” alifafanua. Kupitia wakili wake Elisha Ongoya, Bi Kawira alipuuzilia mbali madai ya kumtusi na kumdhalilisha naibu gavana wake Isaac Mutuma kwa kutumia maafisa wa ngazi za chini na makundi ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp. Gavana huyo alieleza kuwa si yeye aliyekuwa akiendesha makundi hayo wala hajui jinsi alivyojiunga nayo wala aliyemjumuisha. Aidha, alionekana kumlaumu naibu wake kupitia video iliyomwonyesha Bw Mutuma akiimba nyimbo za kumpinga yeye akiwa na kundi la watu wengine. Katika mojawapo ya video, Mbunge wa Tigania Mashariki Mpuru Aburi anaonekana akitumia maneno machafu na kile kilichofasiriwa kwenye Seneti kuwa vitisho vya dhuluma za kijinsia dhidi ya Bi Mwangaza. Aidha, Gavana Kawira alifafanua kuhusu ziara ya China iliyowajumuisha jamaa zake wanne badala ya maafisa wa afya wa Meru kuhusiana na Kituo cha Matibabu ya Saratani. Kulingana na Bi Kawira, alilazimika kuvunja safari ya kwenda China baada ya kugundua kampuni iliyokuwa imezuru afisi yake ilikuwa kundi la watu waliotaka kufanya biashara na Kaunti ya Meru wala si kutoa ufadhili wa vifaa vya matibabu jinsi walivyoeleza awali. “Kampuni hiyo kwanza ilijihusisha na serikali ya China. Kama kawaida nilituma kikosi changu kilichojumuisha msaidizi wangu, mlinzi na waziri wa afya kwa maandalizi. Lakini walipofika waligundua kampuni hiyo hata haina afisi China. Sikuona haja ya kusafiri na kupoteza wakati kwa ziara kama hiyo,” akajitetea. Diwani wa Nyaki Mashariki, Josphat Kinyua aliyekuwa mmojawapo wa mashahidi wa Bi Kawira, alieleza Seneti jinsi Naibu Gavana alivyotumia vishawishi kuwavutia madiwani kuunga mkono hoja ya kumng’oa mamlakani Gavana wa Meru. Shahidi huyo alisimulia jinsi hafla iliyokusudiwa kupanda miti ilivyogeuzwa ghafla hafla ya wazee wa Njuri Ncheke kuwalisha kiapo madiwani wa Meru ili waunge mkono hoja ya kumfurusha Bi Kawira. “Hafla iliyopangiwa kupanda miti iligeuzwa tambiko la kula kiapo lililofanyika kwenye jukwaa la Meru. Madiwani wapatao 40 walialikwa na wazee wa Njuri Ncheke kula kiapo,” alieleza Kinyua. Akaongeza: “Mzee mmoja wa Njuri Ncheke alisikika akiwaonya madiwani kuhusu adhabu kali na laana endapo wangeghairi baada ya kula kiapo.” Kikao cha Jumatano kilichukua muda mrefu hadi saa ikabadilika na Alhamisi kuingia. Mnamo saa sita na dakika chache usiku huo wa kuamkia Alhamisi, spika Kingi aliwaongoza maseneta kupiga kura, Bunge la Seneti likishindwa kumng’oa ofisini. Kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa Jumanne iliamuliwa baada ya maseneta kusikiliza ushahidi wa madiwani na kumpa nafasi Gavana Mwangaza kujitetea.  Spika Kingi alifafanua kabla ya shughuli ya upigaji kura, akisema maseneta wangepiga kura kwa kila mojawapo ya mashtata dhidi ya Gavana Mwangaza. Maseneta walipiga kura mara saba. Shtaka la kwanza lilikuwa ni ubadhirifu na matumizi mabaya ya rasilimali za kaunti. Maseneta 19 walipiga kura ya kukubaliana na madiwani huku maseneta 28 wakipiga kura ya ‘La’. Shtaka la pili lilikuwa upendeleo wa jamaa na ukiukaji mwingine wa maadili. Maseneta watano waliunga mkono ang’olewe huku 42 wakipinga. Katika shtaka la tatu la kuwadhalilisha viongozi wengine kura ilipigwa ambapo matokeo yalikuwa kwamba watatu walikubaliana na madiwani wa Meru huku 44 wakipinga. Kwenye shtaka la nne, Gavana Mwangaza alimulikwa na madiwani kwa kufanya uteuzi unaokiuka mchakato unaohitajika ambapo katika upigaji kura, maseneta 20 wamekubaliana na madai hayo huku 27 wakipinga. Nalo shtaka la tano likihusu kuidharau mahakama ambapo maseneta watatu wamekubaliana na madiwani lakini wakalemewa na 44 waliopinga. Aidha kiongozi huyo wa Kaunti ya Meru alikabiliwa na shtaka la sita la kuipa barabara jina la mume wake Bw Murega Baichu. Maseneta wanne wamepiga kura ya ‘Ndiyo’ ambapo tena walilemewa na 43 waliopinga. Shtaka la saba na la mwisho lilisema Gavana Mwangaza alidharau Bunge la Kaunti. Shtaka hilo limepata uungwaji mkono kutoka kwa maseneta 10 pekee, tena wakilemewa na 37 waliopinga. “Seneti haijathibitisha kosa lolote hivyo Gavana Kawira Mwangaza anaendelea kuongoza Kaunti ya Meru,” amesema spika Kingi. Ikiwa maseneta wangepitisha hata shtaka moja tu, basi Gavana Mwangaza angebanduliwa ofisini. Sasa cha kusubiriwa ni kuona namna atakavyojinyanyua tena na kutafuta njia ya kushirikiana na madiwani waliopitisha hoja ya kumbandua. Hii imekuwa mara ya pili kwa kesi dhidi ya Gavana Mwangaza kuwasilishwa na kujadiliwa katika Bunge la Seneti. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA WINNIE ATIENO SERIKALI imepiga marufuku wakuu wa shule kuongeza karo ya shule za msingi na za sekondari msingi (JSS). Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu alieleza kuwa karo ya shule za mabweni pia itasalia ilivyo kwa sasa. Akizungumza Jumatano wakati wa ufunguzi rasmi wa kongamano la walimu wakuu wa shule za msingi katika shule ya msingi ya Sheikh Khalifa Bin Zayed jijini Mombasa, Bw Machogu alieleza kuwa serikali haitaongeza karo kwa shule zote kwa sasa. “Serikali ya Rais William Ruto haina lengo la kuongeza karo ya shule za Sekondari msingi na zile za upili . Karo ya shule za mabweni zitasalia kama ilivyopitishwa,” akasema Bw Machogu. Bw Machogu alinukuu kipenge cha 53 cha katiba kinachosema elimu ya msingi ni ya bure na ya lazima. “Yeyote anayefanya hilo atakuwa ameenda kinyume na Katiba yetu. Yeyote ambaye hataki kuwa mkuu wa shule, hatukulazimishi, waweza kujiuzulu. Kuna Wakenya wengi ambao wanataka kupata nafasi hizo na wana uwezo wa kufuata sheria,” akasema. Waziri huyo, alisema wakuu wa shule walikuwa wamekiuka sheria kwa kutoza karo ya Sh200,000 kila mwaka huku wengine wakitoza Sh150,000. “Elimu ilikuwa imekuwa ghali sana kwa Wakenya wengi. Ilikuwa imetengewa waliojaliwa mali na serikali ikasema hapana. Fedha zilizokuwa zikitozwa zilikuwa zikiingia mifukoni mwa watu binafsi,” akasema Bw Machogu. Alihoji kuwa, licha ya serikali kuwa ikijitolea kufadhili ununuzi wa vitabu vya kusoma, taasisi za elimu zilikuwa zikikosa bidhaa hizo muhimu. Alisema kuwa serikali itaendelea kuzisaidia shule na wanafunzi kupitia kutoa mgao wa fedha, sehemu ya jukumu la serikali likiwa kutoa elimu ya hali ya juu, ya bure iliyo lazima kwa kila mtoto. Alieleza kuwa kuanzia manmo 2003. Serikali ilikuwa imetekeleza elimu ya msingi isiyo na malipo. Kwa sasa kila mwanafunzi analipiwa Sh1,420 kwa shule za msingi. Kwa shule za sekondari ya msingi serikali hutoa ufadhili wa kifedha wa Sh15,042 kwa kila mwanafunzi. Wanafunzi wa shule za sekondari hufadhiliwa Sh22,240 kwa kila mwanafunzi. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA LUCY MKANYIKA RIPOTI ya mashirika yasiyo ya kiserikali imemulika kampuni ya Wildlife Works, inayoendesha mradi wa kupunguza kaboni katika Kaunti ya Taita Taveta, kwa ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya wafanyakazi wa kike na jamii ya eneo hilo kwa upana. Ripoti hiyo iliyotolewa na Kituo cha Utafiti wa Mashirika ya Kimataifa (Somo) na Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KHRC), ilionyesha kuwa baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo inayoshirikiana na shirika la Verra katika mradi huo wa Kasigau Corridor REDD+, wamekuwa wakinyanyasa wanawake kimapenzi. Mradi huo ulikusudia kulinda misitu na wanyamapori, kupunguza utoaji wa gesi ukaa, na kutekeleza miradi ya manufaa kwa jamii na hivyo kutoa ajira, elimu, na uwezeshaji wa wanawake. Mradi huo ni mmojawapo wa miradi iliyoidhinishwa kukabiliana na kaboni duniani na umepokea sifa kwa kufanikisha maendeleo endelevu na umeuza kaboni kwa Microsoft, Shell, Benki ya Dunia (WB), na Benki ya Uwekezaji wa Ulaya. Hata hivyo, ripoti hiyo imefichua unyanyasaji wa kijinsia ambao umekithiri katika eneo hilo la mradi la Kasigau. Ripoti hiyo inaonyesha jinsi baadhi ya wafanyakazi wa kiume na walinzi wa wanyamapori (rangers) walivyonyanyasa kingono wafanyakazi wa kike, wanawake na wasichana wa eneo hilo, ili kupewa kazi, kupandishwa vyeo au kuongezwa marupurupu. Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa walioasi walipokea vitisho na ubaguzi hadi kwa familia zao. “Utafiti wetu unaonyesha kuwa unyanyasaji huu umeendelea kwa kipindui cha mwongo mmoja au zaidi,” inasema. Waathiriwa pia walikabiliwa na vikwazo wakati wa kuripoti unyanyasaji huo, kama vile unyanyapaa na kukosa kupata haki. “Wanawake waliokataa unyanyasaji wa kingono waliishi na kufanya kazi kwa uoga, kama mmoja wao alivyosema kwa sababu wanaweza kuachishwa kazi wakati wowote bila sababu za kimsingi,” ripoti hiyo ilisema. Ripoti hiyo ilitoa wito kwa kampuni hiyo ya Wildlife Works, wateja wake, na kampuni ya ukaguzi kushughulikia madai hayo ya waathiriwa na jamii kwa ujumla na kuchukua hatua za kuzuia na kurekebisha ukiukaji wowote zaidi dhidi ya haki za binadamu. Ripoti hiyo pia inaitaka serikali kuwajibika kuhakikisha kuwa haki za watu walioathirika zinaheshimiwa na kulindwa na wahusika wanachukuliwa hatua. Kwa upande wake, shirika la Verra lilisema kuwa limefahamishwa kuhusu tuhuma za unyanyasaji wa kimapenzi katika Mradi wa Kasigau. Katika taarifa yake, Mkurugenzi Mkuu wa Maswala ya Mawasiliano na Utetezi Joel Finkelstein alisema shirika hilo linachukua hatua kwa kuanzisha uchunguzi dhidi ya madai hayo. “Verra ilifahamishwa kuhusu tuhuma za unyanyasaji wa kingono katika Mradi wa Kasigau nchini Kenya. Verra itachukua hatua mara moja,” ilisema taarifa hiyo ya Finkelstein. Alisema mradi huo utasitishwa hadi uchunguzi utakapokamilika. Naye Rais wa Wildlife Works Mike Korchinsky alisema katika taarifa kwamba hatua ilichukuliwa baada ya ripoti ya madai hayo kufichuka. “Wafanyikazi wawili waliotajwa wamesimamishwa kazi na mfanyakazi mwingine angali anachunguzwa huku matokeo ya uchunguzi huo yakisubiriwa,” alisema Korchinsky. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA WIZARA ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) imetoa zawadi ya ‘data bundles’ bila malipo kwa Wakenya watakaonunua simu aina ya smartphone za bei rahisi zilizozinduliwa wiki jana na Rais William. Katibu katika Wizara hiyo Mhandisi John Tanui alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuwatia shime Wakenya kununua simu hizo, moja ikiuzwa kwa bei ya Sh7,499. Azma ya serikali ni kustawisha uchumi wa kidijitali. “Serikali inalenga kuhakikisha kuwa Wakenya wanakumbatia mfumo wa kuendesha shughuli za kiuchumi kidijitali. Kwa kutumia simu hizi, wananchi watapata nafasi kupata zaidi ya huduma 5,000 ambazo wakati huu zinapatikana kupitia mitandao,” akasema Bw Tanui. “Simu hizi zilizozinduliwa juzi na Mheshimiwa Rais Ruto zinagharimu Sh7,499 pekee na wanunuzi wa kwanza kwanza watapewa ‘bundles’ bila malipo,” Bw Tanui akasema Jumatano asubuhi kwenye mahojiano katika kituo cha redio cha Spice FM. Hata hivyo, Katibu huyo wa Wizara hakufichua kiwango cha data ambacho wanunuzi wa kwanza wa simu hiyo watapewa. “Wakati huu uchumi wa kidijitali unakuwa mara 2.5 ya uchumi wa kawaida. Hii ndiyo maana serikali imejitolea kuendeleza uchumi huu kwa kuzindua simu hizi ambazo zitahakikisha kuwa hata Wakenya katika maeneo ya mashambani wanapata huduma za serikali kwa urahisi,” Bw Tanui akakariri. Mnamo Oktoba 30, 2023 Rais Ruto alizindua simu hiyo mpya inayotengenezwa na kampuni ya kampuni ya East Africa Device Assembly Kenya (EADAK) Ltd, iliyoko eneo la Mavoko, Kaunti ya Machakos. Simu hizo chapa Neon 5 ‘Smarta’ na 6 ½ ‘Ultra’  zina uwezo wa kutumia mawimbi ya 4G na zinauzwa katika maduka ya Faiba, maduka ya Safaricom na maduka mengine ambayo huuza simu kote nchini. Aidha, zitauzwa mitandaoni kupitia jukwaa la ‘Masoko online’. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MHARIRI
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini.
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na BENSON MATHEKA
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na MASHIRIKA