text
stringlengths
3
16.2k
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L

You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAKAZI wa mtaa wa Mazembe viungani mwa mji wa Nakuru wamekiri kuhangaishwa na wezi ambao huwaibia na kuwasindikiza hadi nyumbani. Huwawekea ulinzi huo makusudi ili kuhakikisha kwamba wateja wao wanafika nyumbani salama salimini. Kwa kawaida, wahuni wamebuni mbinu mpya ya kutembea na mbwa wakubwa nyakati za usiku, ili kujiwekea ulinzi wa kibinafsi. Owen Shibala mwendeshaji bodaboda kati ya Nakuru mjini na Mazembe, anasema hajui walikotoa ujasiri walio nao kushika doria usiku utadhani ni polisi. Mazembe ni mojawapo ya mitaa ambayo hushuhudia visa vya kihalifu na utumiaji wa mihadarati mara kwa mara. “Ukikutana nao usiku ni lazima usalimishe kila kitu lau sivyo utaona cha mtema kuni. Watakucharaza viboko na kuiba kila kitu cha nguvu,”akasema. Hata hivyo, wanapoiba hujitwika jukuma la kuwasindikiza wakazi, wasije wakakutana na vibaka wengine barabarani. Aidha, wanalia sare za polisi jambo linalowafanya baadhi ya raia kuamini huenda wanashirikiana na maafisa wa polisi. Baadhi yao wanajifanya ni maafisa wa polisi ambao huwa wameshika doria, wakilenga kuhangaisha wapita njia wanaotoka kazini usiku. Agnes Wahome mfanyibiashara mtaani Rhonda anasema huwa wamejihami kwa visu, rungu na wako tayari kupigana. Kulingana na Bi Wahome, hii ni hali ya kawaida siku hizi katika mitaa ya Manyani, Bondeni na Freearea ambapo vijana wengi wamejiingiza kwenye uhalifu. Bi Wahome anasema wahalifu wengi wanajulikana, kwani ni vijana wadogo kutoka mitaa jirani ya Flamingo na Lakeview. Mkazi huyo angependa polisi kushika doria katika maeneo husika ili kuzuia kuzuka kwa magenge hatari yanayohangaisha wenyeji. Hili linajiri siku chache baada ya Taifa Leo Dijitali kufichua visa vya wizi ambapo baadhi ya wezi kutoka kwenye mtaa wa Gioto, Nakuru wamekuwa wakipika chakula katika kila nyumba wanamoingia kuiba. Mtaa wa Bondeni, Kaunti ya Nakuru ambapo wezi huwaibia wakazi na kuwasindikiza mpaka nyumbani. PICHA|RICHARD MAOSI
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MUNGUTI MASKWOTA wapatao 10,000 wamewasilisha upya kesi katika Mahakama ya Upeo wakiomba ibatilishe uamuzi kwamba wafukuzwe kutoka kwa shamba la ukubwa wa ekari 25,000 wanalong’ang’ania umiliki wake na familia ya mwanasiasa marehemu Mark Too. Maskwota hao wanaodai mababu zao ndio waliotimuliwa kutoka kwa shamba hilo enzi za ukoloni, wanasema walipewa shamba hilo rasmi na aliyekuwa Rais hayati Daniel arap Moi, kisha Kamishna wa Ardhi M Okundu akaratibisha uamuzi huo mwaka 2007. Katika ombi lililowasilishwa na wakili William Arusei chini ya sheria za dharura, kikundi cha maskwota hao–Sirikiwa Squatters Group–kimeomba mahakama ibatilishe uamuzi huo kwa vile ilitegemea ushahidi ambao haukuwa umewasilishwa katika kesi waliyoshtaki katika Mahakama ya kuamua kesi za mashamba (ELC), Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu. Pia wameeleza bayana Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaack Lenaola, na William Ouko walitegemea ushahidi wa Afisa wa Ugavi wa Mashamba R J Simiyu kutoa uamuzi wang’atuke shambani. Maskwota hao wamesema ushahidi wa Bw Simiyu uliowasilishwa mbele majaji hao saba kwa njia ya afidaviti ni mpya na kamwe “haukuwasilishwa mbele ya Jaji Antony Ombwayo aliposikiliza na kuamua kesi hiyo 2017.” Pia wanasema ushahidi huo haukuwasilishwa Mahakama ya Rufaa iliyosikiliza rufaa iliyowasilishwa na kampuni ya Fanikiwa, familia ya marehemu Mark Too, kampuni ya Lonrho Agribusiness (EA) Ltd, na Bw David K Korir. Hivyo basi, maskwota hao wanaeleza mahakama hii ya upeo kwamba ni kinyume cha sheria kutegemea ushahidi mpya kutoa uamuzi wa kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma. “Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu wa Desemba 15, 2023, hauna mashiko kisheria na kamwe hauna nguvu kisheria kuwatimua maskwota hawa kutoka kwa shamba lao,” asema Bw Arusei. Pia maskwota hawa wanadai kwamba badala ya Mahakama ya Juu kujadili masuala ya kikatiba jinsi ilivyo jukumu lake, majaji hao walianza kufafanua na kutafsiri ushahidi wa watu binafsi na kuelezea maana ya ‘skwota’. Mahakama hii imeombwa ikague upya uamuzi iliyotoa kwa vile ilidanganywa na walalamishi na pia kutendewa ujanja. Akinukuu maamuzi ya majaji wastahiki kama vile Lord Dening, Bw Arusei amesema, mahakama ikigundua ilipotoshwa au kudanganywa na upande mmoja, iko na mamlaka na uwezo wa kufutilia mbali uamuzi iliyotoa na kuandika mwingine. Maskwota hao wanaomba Mahakama ya Juu iwarudishe shambani kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Ombwayo na Mahakama ya Rufaa. Vile vile mahakama hiyo imekosolewa kwa kumshambulia hayati Moi katika uamuzi huo pasi kutoa agizo wasimamizi wa mali yake wafike mbele yao kutoa mwanga kuhusu suala la umiliki wa shamba hili lililorudishwa kwa serikali na kampuni iliyokuwa inakuza miti inayotumika katika viwanda vya ngozi. Naibu msajili wa Mahakama ya Juu Nelly Kariuki aliwaamuru maskwota hao wawakabidhi nakala za kesi hii yao mpya wahusika wote kabla ya Januari 31, 2024, kesi itakapotajwa tena kwa maagizo zaidi. Jaji aliyesikiliza kesi hii mpya hakuiratibisha kuwa ya dharura ila aliamuru pande zote ziwasilishe ushahidi katika muda wa siku 14 kuanzia Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti,  baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA WAKILI mtatanishi Miguna Miguna amemkosoa Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa kumshambulia mwanasiasa wa upinzani kutoka Afrika Kusini, Julius Malema aliyezuru Kenya juzi. Bw Gachagua alikasirishwa na Bw Malema ambaye ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Afrika Kusini Economic Freedom Fighters (EFF) kwa kumkosoa Rais William Ruto. Malema alichukizwa na kile alichodai ni hatua ya Ruto kuunga mkono Israeli katika vita vyake dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, akisema hiyo haiendelezi falsafa ya utetezi wa Afrika. “Mtetezi wa masilahi ya Waafrika ni yule anayetetea wale wanaokandamizwa. Wapalestina wametengwa na kuuawa kinyama katika ardhi yao kama Mau Mau walivyouawa hapa Kenya. Halafu Ruto anasema anaunga mkono Israeli, anasemaji hivyo?” Malema akauliza Alhamisi wiki iliyopita katika Chuo Kikuu cha Lukenya. Malema alikuwa amezuru Chuo hicho kuzinua Taasisi ya Kutoa Mafunzo Kuhusu Utetezi wa Masilahi ya Waafrika. Kiongozi huyo wa EFF pia alimkosoa Rais Ruto kwa kufeli kutimiza ahadi alizotoa wakati wa kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu wa 2022. Malema alisema matendo ya hivi karibuni na semi zake kabla ya uchaguzi hazilandani, na “ni tofauti kama mchana na usiku”. “Yale ambayo Rais William Ruto alisema wakati wa uchaguzi na yale ambayo anasema sasa ni tofauti,” akaongeza. Lakini Bw Gachagua akiongea Ijumaa akiwa Kilifi alimkaripia Malema akimwonya dhidi ya kuingilia masuala ya ndani ya Kenya. “Kama wewe ni mgeni hapa Kenya fanya mambo yako kisha urudi kwenu. Huyo mtu kutoka Afrika Kusini amekuja hapa na kuleta ujuaji mwingi usio na maana. Mimi nikienda kule kwao huwa sizungumzii mambo yao,” Bw Gachagua akasema. Lakini Bw Miguna alimtaka Bw Gachagua kukubali ukosoaji huu wa Malema hata kama yeye ni mgeni. “Umekosea Rigathi. Mbona Julius Malema asikosoe viongozi wa Kenya ambao anaamini kuwa ni wanafiki? Nani alikuzuia kukosoa viongozi wa Afrika Kusini ulipotembelea huko?” Miguna akauliza kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X (zamani twitter).   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

CHARLES WASONGA, BARNABAS BII, SAMMY KIMATU na WAWERU WAIRIMU MVUA kubwa inayoendelea kunyesha nchini inazidi kusababisha hasara maeneo tofauti, ikiwemo mauti na uharibifu wa miundomisingi. Viongozi kutoka Kaunti ya Mandera sasa wanamtaka Rais William Ruto kutangaza mafuriko yanayoshuhudiwa eneo hilo kama janga la kitaifa huku watu watatu wakisemekana kufa kutokana na hali hiyo. Wakiongozwa na Gavana wa kaunti hiyo Mohamed Adan Khalif na Seneta Ali Roba viongozi hao Jumapili, Novemba 12, 2023 waliitaka Serikali ya kitaifa kupeleka misaada ya chakula, dawa na mahitaji mengine ya kimsingi. Viongozi hao walisema zaidi ya familia 4, 000 zimeathiriwa, usafiri ukikatizwa baada ya barabara kuharibiwa na mafuriko hali ambayo imefanya wakazi kutofikiwa na chakula pamoja na mahitaji mengine ya kimsingi. “Tunataka serikali kusafirisha chakula kwa watu wetu kwa sababu malori ambayo huleta chakula kutoka Nairobi na kaunti zingine za karibu haziwezi kufika katika kaunti ya Mandera,” Gavana Khalif akasema kwenye kikao na wanahabari jijini Nairobi. Walikuwa wameandamana na viongozi kadhaa wa kaunti hiyo wakiwemo wabunge; Abdul Haro (Mandera Kusini), Adan Haji (Mandera Magharibi), Mohamed Abdikeri (Lafey), Hussein Weytan (Mandera Mashariki) na Mbunge Mwakilishi wa Mandera Bi Umulkheir Kassim. Katika kaunti ya Isiolo, familia 800 zinahitaji msaada baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko. Kwingineko, Shirika la Msalaba Mwekundu (KRCS) sasa linaonya kutokea kwa mkurupuko wa magonjwa kutokana na mafuriko yanayoendelea kushuhudiwa nchini. Mafuriko hayo yamesababishwa na mvua kubwa inayonyesha na tayari imeanza kuzua uharibifu na maafa maeneo mbalimbali. Kwa mujibu wa KRCS zaidi ya familia 95, 000 ziko kwenye hatari ya kuathirika na mvua hiyo inayokisiwa ni El Nino huku mkurupuko wa Kolera, Malaria na magonjwa mengine ukihofiwa. Kaskazini mwa Bonde la Ufa, wakazi wa kaunti za Pokot Magharibi, Elgeyo Marakwet, Nandi na Turkana zipo kwenye hatari ya kuhamishwa na mafuriko hayo. “Tunatambua maeneo ambayo yataathirika na El Nino na kuweka mikakati ya kupambana na mkurupuko wa magonjwa mbalimbali hasa za maji,” akasema Esther Chege, Mshirikishi wa KRSC ukanda wa Bonde la Ufa. Katika Kaunti ya Nandi, KRCS imeomba familia zitoke maeneo ambayo hukumbwa na maporomoko ya ardhi hasa Nandi Kaskazini na upande unaopakana na Kakamega. Mnamo 2018, familia 1, 045 zililazimika kuhama makwao eneo la Tinderet na Meteitei kutokana na mafuriko. Kwenye Kaunti ya Elgeyo Marakwet, Kamishina John Korir amesema mamia ya familia zinazoishi maeneo ambayo hukumbwa na mafuriko, zimeshauriwa kuhamia maeneo salama kutokana na El Nino hiyo. Katika Kaunti ya Nairobi, familia kadhaa katika mitaa ya mabanda kaunti ndogo ya Makadara, zilikesha kwenye baridi baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko baadhi ya nyumba katika mitaa ya mabanda ikiwemo Fuata Nyayo, Commercial, Kenya Wine, Kayaba, Crescent, Budalangi, Maasai Village, Kwa Reuben, Kingstone na Lunga –Lunga zikifurika maji.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA SAMWEL OWINO BUNGE linataka majibu kutoka kwa serikali kuhusu masuala nyeti saba inayotaka yaangaziwe kabla ya kuidhinisha mpango wa kuwatuma maafisa 1, 000 wa polisi Haiti. Kamati ya Usalama inayojumuisha Bunge la Kitaifa na Seneti inayoendesha vikao vya kushirikisha umma kuhusu suala hilo ilisema masuala hayo ni sharti yaangaziwe kikamilifu kabla ya polisi wa Kenya kuondoka. Miongoni mwa masuala yaliyotajwa na wanachama wa kamati hiyo yanajumuisha mpango thabiti wa bima kwa maafisa watakaotumwa Haiti, fidia kwa familia zitakazoachwa na maafisa kutokana na kifo au kujeruhiwa kwa maafisa walio tegemeo na kwamba hakuna fedha za umma zitakazotumika kwenye oparesheni hiyo. Aidha, wabunge wanaitaka serikali kufafanua iwapo kutakuwa na mabadiliko ya zamu au ni maafisa hao tu 1, 000 watakaohudumu kwa mwaka mzima na iwapo ipo, ni baada ya muda gani. Wanaitaka pia Wizara kutathmini kupunguza idadi hiyo hadi 500 ili kuepuka kuhujumu usalama nchini. Isitoshe, wabunge wameitisha ripoti ya jopokazi linalojumuisha vikosi mbalimbali kutoka Kenya lililohusika na uchunguzi wa oparesheni hiyo ya Haiti kuhusu ufaafu wake, wakisema ni baada tu ya kupata matokeo ya timu hiyo ndipo wataweza kutoa mapendekezo kuhusu uidhinishaji. Hatua ya Rais William Ruto kutangaza kutuma maafisa hao Haiti kukabiliana na magenge ya wahuni waliokosesha nchi hiyo amani, ilipata pigo baada ya Mahakama Kuu kusimamisha mpango huo Oktoba 2023. Chama cha Thirdway Alliance Kenya (TAK) kinachoongozwa na Dkt Ekuru Aukot kwa ushirikiano na Bw Miruri Waweru, kiliwasilisha keri kortini kupinga mpango wa Dkt Ruto. Baadaye, Waziri wa Usalama wa Ndani, Prof Kithure Kindiki alisema maafisa 1, 000 waliosemekana watatumwa Haiti kudumisha amani, wataruhusiwa kuondoka nchini kupitia idhini ya bunge. Haiti imekuwa ikishuhudia ghasia na machafuko tangu 2021, baada ya Rais wa nchi hiyo Jovenel Moïse kuuawa. Pendekezo la Rais Ruto liliidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Kimataifa, mataifa mawili wanachama wa baraza hilo (China na Urusi) yakikataa kupiga kura kuunga au kukataa. Rais wa Amerika, Joe Biden pia alisifu taifa la Kenya kwa hatua hiyo aliyoitaja kuwa ya “kijasiri”.       You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA SERIKALI imetoa tahadhari kuhusu usalama wa nyama ya kuku inayouzwa Nairobi na miji mingine mikuu nchini. Kwenye barua, mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Mifugo Obadia Njagi alisema nyama nyingi zinazouzwa katika maduka mengi hazijakaguliwa na maafisa wa afya. Kulingana na Bw Njagi, nyakati hizi kuku huchinjwa katika maboma ya watu badala ya vichinjio maalum inavyohitajika kisheria. Aliongeza kuwa usafirishaji nyama inayotolewa kutoka maboma ya watu binafsi na kupelekwa kwenye maduka unakiuka kanuni zilizowekwa za usalama na usafi. “Nyama hii hupatikana moja kwa moja kutoka kwa wafugaji wa kuku wa nyama, ambao huwachinja katika vibanda vyao na kuisafirisha hadi kwa mikahawa na vioski vya kuuza chakula. Nyama hii sio salama,” Njagi akaonya kwenye barua hiyo iliyonakiliwa kwa makurugenzi wa Idara hiyo katika ngazi za kaunti. Maduka yaliyolengwa zaidi ni yale yanayouza vyakula vya kisasa (fast food) katikati mwa jiji la Nairobi na miji mingine nchini. Vichinjio vingi nchini vinalaumiwa kwa kutoa nyama ya kuku moja kwa moja kutoka kwa wafugaji kuku. “Hii ni kinyume na Sheria ya Kusimamia Usalama wa Nyama, Kifungu cha 356 inayosema kuwa wanyama wa kuliwa sharti wachinjwe katika vichinjio vilivyoidhinishwa na kupewa leseni na ambavyo hukaguliwa na maafisa husika,” akasema. Bw Njagi aliwashauri wakaguzi wa nyama katika kaunti kufuatilia kwa makini mwenendo huo mbaya unaoweka maisha ya Wakenya hatarini. Idara hiyo pia imeonya kuwa wafanyabiashara watakaopatikana na hatia ya kukiuka sheria na mahitaji kuhusu nyama ya kuku watachukuliwa hatua kali. “Maovu kama hayo huwaweka wateja katika hatari ya kununua nyama isiyo salama na yenye vimelea vya kusababisha maradhi,” barua hiyo ikasema. Biashara za kuchinja na kuuza nyama za kuku zinazidi kunoga mitaa mingi Nairobi.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA SHABAN MAKOKHA ALIYEKUWA Gavana wa Kakamega, Wycliffe Oparanya ameelezea nia yake kuwania kiti cha urais 2022. Naibu Mwenyekiti huyo wa ODM, alitangaza wikendi kwamba huenda atakuwa debeni iwapo Kiongozi wa chama, Bw Raila Odinga hatashiriki kumenyana na Rais wa sasa, William Ruto katika uchaguzi mkuu huo ujao. Dkt Ruto (Kenya Kwanza) atakuwa akisaka kuhifadhi kiti chake kuhudumu muhula wa pili na wa mwisho. Chama pinzani cha ODM tayari kimeanza mchakato wa kuwasajili wanachama wapya kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027. ODM pia itakuwa ikiandaa uchaguzi wake wa mashinani kuanzia Februari 2023. Bw Oparanya alisema kuwa atawania urais kuwaokoa Wakenya dhidi ya dhuluma za kiuchumi ambazo wanatendewa na utawala wa Kenya Kwanza. “Niko tayari kukabiliana na Rais Ruto 2027 kwa sababu Azimio ina mipango ambayo ingependa kutekeleza. Uongozi wangu na rekodi yangu i wazi na nawahakikishia Wakenya kuwa nitawapa uongozi bora,” akasema. Alikuwa akizungumza katika Shule ya Msingi ya Eshirembe, Butere wakati wa mazishi ya mjombake Jared Oluoch Nandwa mnamo Jumamosi, Novemba 11, 2023. Hatma ya Bw Odinga ikiwa atakuwa debeni 2027, hata hivyo, haijabainika. Muungano wa Azimio umekuwa ukikosoa vikali utawala wa Rais Ruto hasa kwa nyongeza ya mara kwa mara ya ushuru na kodi, hatua ambayo inaendelea Mkenya wa kawaida kwa sababu ya ugumu wa maisha.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA FRANCIS MUREITHI KATIBU Mkuu wa Jubilee, Jeremiah Kioni amedai kwamba eneo la Mlima Kenya halitaunga mkono Urais wa William Ruto mwaka 2027 baada ya kufanya hivyo 2022. Bw Kioni alisema wakazi wa Mlimani sasa wamegundua walifanya kosa kwa kuunga Kenya Kwanza, kwa kuwa ahadi nyingi zilizotolewa bado hazijatimizwa pamoja na gharama ya maisha kuendelea kuwa juu. “Kutokana na hadaa tupu na unafiki ambao naona kwa sasa. Hakuna chochote ambacho kitabadilika chini ya utawala huu,” akasema Bw Kioni. Alikuwa akizungumza Nakuru baada ya kuhudhuria mazishi ya Mama Monica Wangu Wamwere ambaye ni mamake naibu waziri wa zamani na mbunge wa Subukia Koigi Wamwere. “Hatuwezi kuenda mbali kama taifa iwapo unafiki huu utaendelea. Lazima tujali maslahi ya Wakenya wengine. Ukisikia kondoo mzee akipiga chafya kwa uchungu, basi fahamu kuwa anaumwa sana. Hii ni dalili kuwa ni mgonjwa au kuna jambo linalomtatiza,” akasema Bw Kioni. “Iwapo hatutashirikiana kimawazo basi tutaangamia pamoja na hili si jambo la mzaha. Kuna mambo ambayo tumekuwa tukiyafanya vivi hivi na kudhani ni mzaha ilhali ni hatari,” akongeza Katibu Mkuu huyo wa Jubilee. Jubilee, ni chama kilichotawala Kenya kati ya 2013 hadi 2022 chini ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta na ambacho katika uchaguzi mkuu wa 2022 kilikuwa kinaunga mkono Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga (Azimio) kuingia Ikulu. Mbunge huyo wa zamani Ndaragwa alisema kuwa mabadiliko yaliyopendekezwa kupata kitambulisho kipya kwa kulipa Sh1000 na Sh2,000 kwa aliyepoteza, yataumiza Wakenya ambao hawana ajira. “Wengi sasa hawatatuma maombi ya kupata kitambulisho nyingine baada ya kupoteza vyao,” akaonya Bw Kioni. Mwanasiasa huyo pia alilalamikia hatua ya serikali kuongeza ushuru akisema kuwa hata makanisa yameathirika na kodi za juu. “Sote tunapitia changamoto za kiuchumi na hatuwezi kuendelea kuvumilia milele,” akasema.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA WYCLIFFE NYABERI BAADHI ya maseneta wa muungano wa Azimio wamemkashifu vikali Rais William Ruto kwa kutozungumzia suala la gharama ya juu ya maisha wakati wa hotuba yake kwa taifa wiki jana, Alhamisi, Novemba 9, 2023. Wakiongozwa na Okong’o Omogeni wa Nyamira, Stewart Madzayo (Kilifi), Enoch Wambua (Kitui) na Eddy Oketch (Migori), maseneta hao wamemuonya Dkt Ruto kwamba huenda akawa Rais wa kwanza kuhudumu kipindi cha muhula mmoja kwa sababu ya kupuuza kilio cha Wakenya kuhusu kupanda kwa gharama ya maisha. Kulingana nao, Ruto ameonyesha dalili za kukatakataa licha ya maisha kuzidi kuwa magumu hasa kwa sababu ya nyongeza ya ushuru (VAT) inayoongezwa kiholela. Wakizungumza mnamo Jumamosi, Novemba 11 katika Kaunti ya Nyamira, Wadi ya Bonyamatuta, wakati wa harambee kusaidia ujenzi wa Kanisa la Waadventista Wasabato, maseneta hao waliushutumu uongozi wa Kenya Kwanza kwa kuendelea kuwekelea Wakenya mzigo wa kodi za juu, jambo ambalo walisema ni kinyume na ahadi ambazo muungano huo tawala ulitoa ukikampeni 2022. “Hii serikali imetuvunja mioyo. Ruto ametuvunja nyoyo. Ruto amevunja familia zetu. Ruto amevunja watoto wetu. Ruto amevunja ndoto zetu lakini kuna Mungu. Wakati utafika ambapo Mungu atasema sasa ni wakati wa kuvunja moyo wa Ruto na kura zenu mikononi. Atakuwa Rais wa muhula mmoja kwa sababu hajatimiza ahadi zake kwa wapiga kura,” Seneta Oketch alisema. Mwanasiasa huyo mchanga alijutia kwamba wazazi walikuwa na ugumu wa kusomesha wanao, akisema serikali ilikuwa imepunguza mgao wa fedha za kuwafadhili. Kauli yake iliungwa mkono na seneta Madzayo ambaye alibainisha kuwa rais hana njia ya kuwaondoa Wakenya kutoka kwa “udanganyifu” huo. “Rais yuko kwenye rekodi akisema kuwa ni mtu mjinga tu ambaye habadiliki. Umesikia kila mtu nchini analia kwamba gharama ya maisha imegonga paa lakini hutaki kusikiza. Ukiambiwa hata hujibu. Alipokuwa akihutubia taifa, hakuna swali hata moja alilojibu kuhusu jinsi ananuia kuwaondolea Wakenya mzigo wa gharama ya juu ya maisha. Alipuuza tu. Kwake, nchi hii si lolote,” Seneta Madzayo, ambaye pia ni Kiongozi wa Wachache katika Seneti alilalamika. Aliendelea, “Kama kweli wewe ni Rais, kwa nini hutaki kuwasikiliza Wakenya? Mmepoteza mwelekeo lakini fanyeni abautani na muwaache Wakenya wawe na maisha ya heshima,” akasema. Seneta Wambua alieleza kukerwa kwake na notisi ya hivi majuzi kwenye gazeti la serikali iliyoongeza tozo nyingi zaidi, ikiwa ni pamoja na kubadilisha kitambulisho, akitaja hatua hiyo kama njia mpya kukama Wakenya. Notisi hiyo ilisitishwa baadaye na Mahakama Kuu, ikisubiri kuamuliwa kwa kesi iliyofikishwa mahakamani na daktari mmoja Nakuru. “Watu wamebanwa na kushinikizwa hadi kufikia hatua ambayo hawawezi kupumua. Lakini tena hivi karibuni, Farao amesema hata ukifa, tozo zinazotozwa kupata vyeti vya vifo zitaongezwa. Umewadhulumu watu wakiwa hai na tena unawafuata kifoni ili kuwakandamiza zaidi,” Seneta Wambua alishangaa. Mbali na kuelezea kusikitishwa kwake na jinsi serikali ya Kenya Kwanza ilikuwa ikishughulikia suala la gharama ya juu ya maisha, mwenyeji Seneta Omogeni alitoa wito kwa idara ya usalama kushughulikia visa vinavyoongezeka vya ukosefu wa usalama huko Nyamira. Seneta Omogeni alisimulia jinsi visa vya hivi majuzi vya ukosefu wa usalama vimetikisa Nyamira na kuwataka polisi kujitokeza na kuwalinda watu wake. “Ulisikia kesi ya Nyamakoroto kuhusu wanandoa ambao walikuwa wamerejea kutoka Amerika kwa likizo, na kuuawa kikatili. Wiki tatu zilizopita, mlisikia kilichotokea Kieriera huko Keroka. Wahalifu waliingia kwenye nyumba kadha kisha wakashika wenyeji mateka kiasi cha kuwabaka na mabinti mbele ya watoto wao. Tunahitaji kukomeshwa kwa tabia hii mbaya,” Seneta Omogeni alisema. Maseneta hao walitetea shule za Gusii kuhusu visa vya udanganyifu katika mitihani. Wiki iliyopita, Mkuu wa Shule ya Upili ya Nyambaria, shule iliyoongoza katika mtihani wa KCSE 2022 alisimamishwa kazi na Tume ya Kuajiri Walimu Nchini (TSC) baada ya kudaiwa kuhusika katika makosa ya mitihani. Aidha, mwalimu huyo alikuwa mmoja wa mameneja kusimamia vituo vya kusambaza mitihani. Kesi sawia pia ziliripotiwa katika Shule za Sironga na Gekomoni, jambo ambalo lilizua taharuki miongoni mwa viongozi wa Kisii. Maseneta hao walimkashifu Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu wakimwambia anafaa kujitokeza na kutetea shule kutoka jamii yake dhidi ya dhuluma na uonevu wowote.       You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

STEVE OTIENO, MANASE OTSIALO na ANGELINE OCHIENG SIKU chache baada ya Rais William Ruto kudai kuwa mvua ya El Nino haitashuhudiwa nchini, naibu wake Rigathi Gachagua Jumamosi, Novemba 11, 2023 aliitisha kikao na wanahabari ambapo wataalamu wa hali ya anga walikubali kuna El Nino. Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Utabiri wa Hali ya Anga David Gikungu, aliomba msamaha kwa kile ambacho alitaja kama habari za kupotosha kwamba mvua ya msimu huu haitasababisha uharibifu. “Ningependa kusema kuwa, tofauti na utabiri wa awali, tunashuhudia El Nino wakati huu wa msimu wa mvua fupi. Na tunaomba msamaha kwa habari za kupotosha zilizotolewa awali kwa sababu tulikosea,” Dkt Gikungu akasema. “Kuanzia sasa, tujiandae kwa mvua kubwa kutokana na El Nino inayoshuhudiwa wakati huu,” akaongeza. Bw Gachagua alikubaliana na kauli ya Dkt Gikungu kwamba hali inayoshuhudiwa nchini wakati huu, kwa kweli, ni El Nino. Lakini wiki mbili zilizopita, Rais Ruto alisema kuwa alijulishwa na wataalamu wa hali ya anga kwamba El Nino haitashuhudiwa nchini bali “mvua nyingi sehemu mbalimbali na ambayo haitasababisha uharibifu.” “Juzi mlisikia kuwa nchi yetu itashuhudia mvua ya El Nino, lakini Mungu ni nani. Mumesikia wale wataalamu wa hali ya anga wakisema kuwa hakutakuwa na El Nino ila mvua kubwa isiyoleta hasara,” Rais Ruto akasema. Lakini jana, Jumamosi Bw Gachagua aliwaeleza Wakenya kuhusu hatua ambazo serikali inachukua kukabiliana na uharibifu unaosababishwa na mafuriko yanayoshuhudiwa kote nchini. Wakati huu, kaunti 19 zimeathirika zaidi na mvua kubwa inayoendelea kunyesha. Barabara katika kaunti za Wajir, Isiolo, Mandera, Marsabit, Tana River na Garissa zimeharibiwa. Maelfu ya familia zimepoteza makao katika kaunti hizo huku mifugo ikisombwa na maji ya mafuriko na mimea ikiharibiwa. Watu watatu waliripotiwa kufa maji katika eneo la Elwak, kaunti ya Mandera wiki jana. “Familia nyingi zimepoteza makao, haswa Kaskazini mwa Kenya na maeneo yanayopakana na mto Tana. Juhudi zinaendeshwa kunakili idadi ya watu waliopotea, mifugo iliyopotea na mimea iliyoharibiwa. Tutatoa data hii, baada ya maafisa husika kuthibitisha,” Bw Gachagua akaambia wanahabari nje ya afisi yake Jumba la Harambee Annex, Nairobi. Serikali pia inabashiri kuwa mito itavunja kingo zake na hivyo imewashauri Wakenya kuwa waangalifu. Kutokana na mafuriko yanayoshuhudiwa serikali inatumia helikopta kuwasafirisha hadi maeneo salama watu walioathirika na mafuriko. Vyombo hivyo vya usafiri pia vinatumiwa kusambaza chakula cha msaada, kama vile mahindi, mchele, maharagwe na mafuta ya kupikia, kwa familia zilizoathirika. Aidha, helikopta hizo zinatumika kusafirisha karatasi za mtihani wa KCSE katika maeneo ambako barabara zimeharibiwa na mafuriko. Bw Gachagua pia alisema serikali inasambaza jumbe za ushauri na uhamasisho kwa familia zinazoishi katika maeneo tambarare na yale ambayo hushuhudia mikasa ya maporomoko ya ardhi.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MOSES NYAMORI RAIS Mstaafu Uhuru Kenyatta aliaibishwa na kuepukwa na Wazungu kama mgonjwa wa ukoma, punde alipotangazwa kuwa kati ya washukiwa sita katika barua ya Ocampo. Aliyekuwa Mkuu wa Utumishi wa Umma, Francis Muthaura, amefichua dhiki alizopitia Bw Kenyatta kwenye kitabu chake A Moving Horizon, ikiwa ni pamoja na Bw Kenyatta kutengwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron. “Wakati wa mkutano wa kujadili mizozo ya Somalia na Sudan Kusini jijini London, Cameron alikataa kumwalika Rais Kenyatta. Ilibidi Umoja wa Afrika (AU) utishie kususia kikao hicho, ndipo akaalikwa. Hata alipofika London, hakuchangamkiwa inavyostahili kwa kiongozi wa nchi,” anatanguliza Bw Muthaura. Kitabu hicho chenye kurasa 456 kinaeleza jinsi mataifa ya Ulaya yaliungana kutaka kuzima azma ya Bw Kenyatta na aliyekuwa mgombea mwenza William Ruto (Rais wa sasa) kuwania uongozi mwaka 2013. “Walimtumia aliyekuwa mshauri wa masuala ya Afrika John Carson kuwaonya Wakenya kuwa maamuzi huwa na matokeo. Kwamba maamuzi mabaya yangeleta matokeo mabaya. Hii ilikuwa sehemu ya njama kuhakikisha kuwa Bw Kenyatta na mgombea mwenza William Ruto hawaingii Ikulu,” anasema. Pingamizi za uchaguzi Hata wawili hao walipochaguliwa, Bw Muthaura anasema kwenye kitabu chake kuwa, mataifa ya Ulaya yaliendelea kuwatenga. “Uamuzi wao ulionekana wazi kupitia aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Uingereza, William Hague na aliyekuwa Waziri Msaidizi wa Marekani wa masual ya Africa Johnnie Carson,” aeleza. “Wawili hao walisema kuwa uhusiano wa kidiplomasia na washukiwa wa ICC ungefanywa tu katika shughuli muhimu,” akaongeza. Mbali na kuaibishwa na kutengwa, Bw Muthaura anasema, Rais mstaafu Kenyatta alilengwa na mashahidi wa kesi yake ICC. Kwamba kulikuwa na jaribio la mashahidi wawili kuitisha Sh50 milioni. “Walidai kuwa na ushahidi hatari dhidi ya Bw Kenyatta uliomhusisha na kundi la Mungiki. Kwanza waliitisha Sh30 milioni kutoka kwa mawakili wa Bw Kenyatta. Walipofeli, wakaunda nyaraka walizodai kuwa ushahidi na kumfuata Bw Kenyatta mwenyewe, mimi (Muthaura) na aliyekuwa Kamishna wa Polisi Meja Jenerali Mohamed Hussein Ali wakitaka Sh50 milioni,” ameandika Bw Muthaura. Kitabu hicho kinasema afueni kwa Bw Kenyatta na Bw Ruto ilipatikana tu pale mrithi wa Ocampo, Bi Fatou Bensouda, alipotamatisha kesi zao. Mnamo Desemba 2014, Bi Bensouda alieleza mahakama kwamba hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuendelea na kesi za wawili hao. Hata hivyo, aliacha mwanya wa kuwakamata endapo kutatokea ushahidi mpya. Bw Muthaura anaeleza kuwa kwa mara ya kwanza tangu wafunguliwe mashtaka, wawili hao walianza kualikwa na viongozi wa Magharibi.     You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA SAMMY WAWERU MAKACHERO wa Idara ya Upelelezi wa Uhalifu na Jinai (DCI) Jumapili, Novemba 12, 2023 walitia nguvuni wanaume wannne wanaoaminika kuhusika katika wizi wa Sh94 milioni za duka la kijumla la Quickmart wiki iliyopita, zilizokuwa zikisafirishwa benkini na Wells Fargo. Tangazo hilo la DCI limejiri siku chache baada ya kuchapisha mitandaoni picha za washukiwa wawili wakuu ambao ni wafanyakazi wa kampuni hiyo ya uchukuzi. Kupitia taarifa, mshukiwa wa kwanza anayesemekana kusafirisha wahusika wakuu na pesa zilizoibwa kwa kutumia gari, alitiwa nguvuni eneo la Rongai, kiungani mwa Jiji la Nairobi. “Ismael Patrick Gitonga anaaminika kuwa dereva na mshirika aliyefirisha kikosi cha Wells Fargo; Mugetha, Nduiki, na Sh94,918,750 zilizoibiwa kutoka kwenye gari la kampuni hiyo eneo la South C (Nairobi) kwa kutumia gari lake aina ya Toyota Fielder lenye namba ya usajili KBM 751W,” DCI imedokeza. Fedha hizo za Quickmart ziliibwa mnamo Novemba 6, 2023 na makchero kutoka makao makuu ya DCI, Kiambu Road kwa kushirikiana na wenzao wa Nairobi wamekuwa wakiendeleza uchunguzi. Washukiwa wa pili na wa tatu, ndio Michael Matoro Njeru na Samuel Onyango, walitiwa pingu eneo la Njiru ambapo walipatikana wakiwa katika harakati za kukarabati gari lililotumika kusafirisha wahusika wakuu na pesa. Kulingana na DCI, ni baada ya kuwahoji ambapo waliwaelekeza kwa mshukiwa wa nne TRM, mtaani Roysambu. “Mshukiwa wa nne, Martin Nderi Ng’ang’a alikamatwa. Alipeleka makachero kwenye nyumba yake ya kukodi na baada ya msako, Sh9.1 milioni pesa taslimu zilipatikana,” taarifa ya DCI inaendelea kueleza. Udadisi wa maafisa hao pia uliwaelekeza eneo la Karen, msitu ulio karibu na Soko la Gataka ambapo masanduku ya kusafirisha pesa zilizoibwa yalitwaliwa. DCI inaamini kuwa msitu huo ndio ulitumika kugawanya hela, miongoni mwa wahusika hao wa wizi. Huku oparesheni ya uchunguzi ikiendelea, picha zilizochapishwa na DCI kwenye akaunti yake ya Twitter na Facebook, walitwaa mtungi wenye pesa zilizopatikana na vilevile sanduku (suitcase). You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA ALLAN ODHIAMBO WAMILIKI wa majumba ambayo yameunganishiwa umeme sasa wana jukumu la kuhakikisha umeme unaotumiwa, umelipiwa baada ya serikali kusitisha utoaji wa mita nyingi kwa nyumba zinazomilikiwa na mtu mmoja. Kampuni ya Kusambaza Umeme Nchini (KPLC) imechukua hatua hiyo kuhakikisha kuwa inaziba mianya ya kupoteza mapato kupitia umeme kuunganishwa kwa njia haramu. Pia KPLC imetangaza kuwa haitaidhinisha ombi lolote la kugawa mita. “Usimamizi hivi majuzi ulitoa mwongozo mpya kuhusu ombi jipya la kuunganisha mita. Kuanzia sasa, kila ploti inayomilikiwa na mtu mmoja itakuwa na mita moja pekee. Hata akiwa na vyumba kadhaa, bado ataruhusiwa kuwa na mita moja pekee,” akasema Kaimu Meneja wa KPLC kuhusu ustawi wa maendeleo Kennedy Ogalo. Bw Ogalo aliandikia barua mameneja wa kanda mbalimbali kuhusu agizo hilo jipya. “Hii ina maana kuwa maombi mapya ya kupata mita kwa majumba yatahusisha tu mita moja. Mchakato wa kugawa mita haupo na badala yake mita za sasa zitakuwa zikiunganishwa kwa mmiliki wa jumba au majumba,” akasema. Mita iliyogawanywa hupokea umeme kutoka kwa mita kuu ambapo huwawezesha wamiliki wa nyumba kupima kiwango cha umeme ambacho kimetumika. Kwa mujibu wa Bw Ogalo, wamiliki wa majumba watakuwa na jukumu la kulipa gharama ya umeme ambayo imetumika kupitia mita kuu ya KPLC. Mwongozo huo, hata hivyo, unasaza majumba ya bei nafuu yaliyojengwa na serikali na majumba yanayomilikiwa na serikali. Ili kuhakikisha kuwa mwongozo huo mpya unatekelezwa, KPLC imekumbatia mchakato wa kudhibiti mita zote kuanzia wakati wa kutuma maombi, hadi wakati wa kutoa mita yenyewe. Aidha, KPLC inasisitiza kuwa laini moja tu itawekwa kwa kila ombi ili kusambaza umeme kwa majumba ambayo yanamilikiwa na mtu mmoja. “Wakati wa kuchora ramani, eneo ambalo linastahili kuwekewa umeme litatathminiwa kisha mahitaji ya kawi yazingatiwe. Wakati wa kuweka umeme huo, masuala yote ya kimsingi yatazingatiwa hasa mteja na vyeti vya utambulishi vinavyohitajika,” akasema Bw Ogalo. Inadaiwa serikali imekumbatia masharti hayo mapya ya kuunganisha mita kutokana na visa vingi ambapo nyaya za umeme zimekuwa zikiunganishwa kwa njia haramu. KPLC inalenga kuhakikisha kuwa gharama ya umeme inalipwa kwa wakati ili kuongeza mapato yake. “Kumekuwa na mchanganyiko wakati ambapo mtu mmoja ana mita mbalimbali. Hatua hii huleta changamoto zake hasa wakati wa kulipia umeme ambao umetumika na itakuwa rahisi kuhakikisha malipo hayo yanafanyika iwapo itakuwa chini ya mita moja,” ikasema duru kutoka KPLC. Kuunganisha umeme kwa wateja wapya kumekuwa ni changamoto kubwa, kwa sababu ya ukosefu wa mita kutokana na vita visivyokwisha vya tenda. Kampuni hiyo ilifichua kuwa zaidi ya wateja 300, 000 bado wanasubiri kuunganishiwa umeme baada ya mita walizokuwa nazo kuisha.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MHARIRI
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini.
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na BENSON MATHEKA
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na MASHIRIKA
LONDON, Uingereza
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya... Na ELIZABETH MERAB
WANASAYANSI wanachunguza kuhusu mchipuko wa virusi vipya vya corona aina ya Delta, katika nchi za Amerika, Uingereza,... Na MAUREEN ONGALA
MASAIBU ambayo wagonjwa wa Covid-19 hupitia katika kaunti za Pwani, yameanikwa wazi baada ya kifo cha afisa mkuu wa... SIAGO CECE na ANTHONY KITIMO
UFISADI miongoni mwa baadhi ya maafisa wa serikali katika mpaka wa Kenya na Tanzania, umezidi kuwaweka... Na WAANDISHI WETU
WINGU la maangamizi limetanda kote nchini huku aina mpya ya corona maarufu kama 'Delta' ikiua watu kwa... Na WINNIE ONYANDO
HUENDA visa vya wasafiri kulazimishwa kupima upya corona mpakani mwa Kenya na Tanzania vikakoma baada ya serikali hizo... NA WANGU KANURI
AGIZO la serikali la kudhibiti mkurupuko wa ugonjwa wa corona mwaka jana limewashurutisha Wakenya wengi kufanyia kazi... Na Titus Ominde
VIONGOZI wa kidini Kaskazini mwa Rift Valley (North Rift) wameshutumu wanasiasa kwa kupepeta usambazaji wa virusi vya... Na WANTO WARUI
Huku wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiripoti katika shule zao mpya za sekondari hii leo, kuna uwezekano wa maambukizi... Na CHARLES WASONGA