text
stringlengths
3
16.2k
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAKAZI wa mtaa wa Mazembe viungani mwa mji wa Nakuru wamekiri kuhangaishwa na wezi ambao huwaibia na kuwasindikiza hadi nyumbani. Huwawekea ulinzi huo makusudi ili kuhakikisha kwamba wateja wao wanafika nyumbani salama salimini. Kwa kawaida, wahuni wamebuni mbinu mpya ya kutembea na mbwa wakubwa nyakati za usiku, ili kujiwekea ulinzi wa kibinafsi. Owen Shibala mwendeshaji bodaboda kati ya Nakuru mjini na Mazembe, anasema hajui walikotoa ujasiri walio nao kushika doria usiku utadhani ni polisi. Mazembe ni mojawapo ya mitaa ambayo hushuhudia visa vya kihalifu na utumiaji wa mihadarati mara kwa mara. “Ukikutana nao usiku ni lazima usalimishe kila kitu lau sivyo utaona cha mtema kuni. Watakucharaza viboko na kuiba kila kitu cha nguvu,”akasema. Hata hivyo, wanapoiba hujitwika jukuma la kuwasindikiza wakazi, wasije wakakutana na vibaka wengine barabarani. Aidha, wanalia sare za polisi jambo linalowafanya baadhi ya raia kuamini huenda wanashirikiana na maafisa wa polisi. Baadhi yao wanajifanya ni maafisa wa polisi ambao huwa wameshika doria, wakilenga kuhangaisha wapita njia wanaotoka kazini usiku. Agnes Wahome mfanyibiashara mtaani Rhonda anasema huwa wamejihami kwa visu, rungu na wako tayari kupigana. Kulingana na Bi Wahome, hii ni hali ya kawaida siku hizi katika mitaa ya Manyani, Bondeni na Freearea ambapo vijana wengi wamejiingiza kwenye uhalifu. Bi Wahome anasema wahalifu wengi wanajulikana, kwani ni vijana wadogo kutoka mitaa jirani ya Flamingo na Lakeview. Mkazi huyo angependa polisi kushika doria katika maeneo husika ili kuzuia kuzuka kwa magenge hatari yanayohangaisha wenyeji. Hili linajiri siku chache baada ya Taifa Leo Dijitali kufichua visa vya wizi ambapo baadhi ya wezi kutoka kwenye mtaa wa Gioto, Nakuru wamekuwa wakipika chakula katika kila nyumba wanamoingia kuiba. Mtaa wa Bondeni, Kaunti ya Nakuru ambapo wezi huwaibia wakazi na kuwasindikiza mpaka nyumbani. PICHA|RICHARD MAOSI
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MUNGUTI MASKWOTA wapatao 10,000 wamewasilisha upya kesi katika Mahakama ya Upeo wakiomba ibatilishe uamuzi kwamba wafukuzwe kutoka kwa shamba la ukubwa wa ekari 25,000 wanalong’ang’ania umiliki wake na familia ya mwanasiasa marehemu Mark Too. Maskwota hao wanaodai mababu zao ndio waliotimuliwa kutoka kwa shamba hilo enzi za ukoloni, wanasema walipewa shamba hilo rasmi na aliyekuwa Rais hayati Daniel arap Moi, kisha Kamishna wa Ardhi M Okundu akaratibisha uamuzi huo mwaka 2007. Katika ombi lililowasilishwa na wakili William Arusei chini ya sheria za dharura, kikundi cha maskwota hao–Sirikiwa Squatters Group–kimeomba mahakama ibatilishe uamuzi huo kwa vile ilitegemea ushahidi ambao haukuwa umewasilishwa katika kesi waliyoshtaki katika Mahakama ya kuamua kesi za mashamba (ELC), Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu. Pia wameeleza bayana Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaack Lenaola, na William Ouko walitegemea ushahidi wa Afisa wa Ugavi wa Mashamba R J Simiyu kutoa uamuzi wang’atuke shambani. Maskwota hao wamesema ushahidi wa Bw Simiyu uliowasilishwa mbele majaji hao saba kwa njia ya afidaviti ni mpya na kamwe “haukuwasilishwa mbele ya Jaji Antony Ombwayo aliposikiliza na kuamua kesi hiyo 2017.” Pia wanasema ushahidi huo haukuwasilishwa Mahakama ya Rufaa iliyosikiliza rufaa iliyowasilishwa na kampuni ya Fanikiwa, familia ya marehemu Mark Too, kampuni ya Lonrho Agribusiness (EA) Ltd, na Bw David K Korir. Hivyo basi, maskwota hao wanaeleza mahakama hii ya upeo kwamba ni kinyume cha sheria kutegemea ushahidi mpya kutoa uamuzi wa kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma. “Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu wa Desemba 15, 2023, hauna mashiko kisheria na kamwe hauna nguvu kisheria kuwatimua maskwota hawa kutoka kwa shamba lao,” asema Bw Arusei. Pia maskwota hawa wanadai kwamba badala ya Mahakama ya Juu kujadili masuala ya kikatiba jinsi ilivyo jukumu lake, majaji hao walianza kufafanua na kutafsiri ushahidi wa watu binafsi na kuelezea maana ya ‘skwota’. Mahakama hii imeombwa ikague upya uamuzi iliyotoa kwa vile ilidanganywa na walalamishi na pia kutendewa ujanja. Akinukuu maamuzi ya majaji wastahiki kama vile Lord Dening, Bw Arusei amesema, mahakama ikigundua ilipotoshwa au kudanganywa na upande mmoja, iko na mamlaka na uwezo wa kufutilia mbali uamuzi iliyotoa na kuandika mwingine. Maskwota hao wanaomba Mahakama ya Juu iwarudishe shambani kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Ombwayo na Mahakama ya Rufaa. Vile vile mahakama hiyo imekosolewa kwa kumshambulia hayati Moi katika uamuzi huo pasi kutoa agizo wasimamizi wa mali yake wafike mbele yao kutoa mwanga kuhusu suala la umiliki wa shamba hili lililorudishwa kwa serikali na kampuni iliyokuwa inakuza miti inayotumika katika viwanda vya ngozi. Naibu msajili wa Mahakama ya Juu Nelly Kariuki aliwaamuru maskwota hao wawakabidhi nakala za kesi hii yao mpya wahusika wote kabla ya Januari 31, 2024, kesi itakapotajwa tena kwa maagizo zaidi. Jaji aliyesikiliza kesi hii mpya hakuiratibisha kuwa ya dharura ila aliamuru pande zote ziwasilishe ushahidi katika muda wa siku 14 kuanzia Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti,  baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MUNGUTI WASHUKIWA watano wa wizi wa Sh94 milioni za Quickmart wamefikishwa katika mahakama ya Milimani mnamo Jumanne. Polisi wameomba kuwazuilia kwa siku 21 ili kukamilisha uchunguzi. Tunaandaa habari kamili…  You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA FARHIYA HUSSEIN BAADHI ya wakimbizi wanaoishi katika maeneo ya mijini nchini Kenya, wanatoa malalamishi kwamba vikwazo vikali vinavyowazuia kupata fursa za ajira, na hivyo kusababisha ugumu wa kukidhi mahitaji yao ya kila siku. Wanasema licha ya kukaa kwao kwa muda mrefu nchini, wanaendelea kukabiliana na maisha ya hatari. Wanakabiliana na vizuizi vingi ambavyo vinazuia uwezo wao wa kustawi na kujumuika kikamilifu katika jamii ya Kenya. Miaka 10 iliyopita Bw Razene Zarai alikimbilia nchini Kenya akiepuka mizozo ya kisiasa nchini mwake Eritrea. Katika miaka hiyo yote, Bw Zarai anasema hajawahi kukanyaga nje ya Kaunti ya Mombasa. “Si kwamba sitaki kusafiri, lakini ni kwa sababu ya vikwazo ambavyo mimi na familia yangu tunapaswa kupitia kwa hali yetu ya ukimbizi,” anaeleza Bw Zarai. Kwake, imekuwa vigumu kwa sababu wakati anasajiliwa rasmi kama mkimbizi nchini Kenya, hawezi kupata leseni ya udereva au kuendesha shughuli za benki. Bw Zarai anaishi nje ya kambi, kwa hivyo anaainishwa kama mkimbizi wa mjini. Yeye ni miongoni mwa wakimbizi 580,792 waliosajiliwa na wanaotafuta hifadhi wanaohifadhiwa nchini Kenya kufikia Februari 2023, kulingana na takwimu kutoka Idara ya Huduma kwa Wakimbizi. Ripoti hiyo inasema asilimia 12 ya watu wanatafuta hifadhi, huku asilimia 88 ya watu wakiwa wamesajiliwa rasmi kuwa wakimbizi. Asilimia 84 ya wakimbizi na wanaotafuta hifadhi wanaishi katika kambi, huku asilimia 16 iliyosalia wakiishi mijini. “Kitambulisho cha mkimbizi kinakusudiwa kusasishwa kila baada ya miaka mitano, lakini inaonekana hakina matumizi hata kidogo. Licha ya kuwa katika taifa kwa zaidi ya mwongo mmoja, hatuwezi kupata huduma zozote za serikali. Siwezi kufanya kazi au kushughulikia pesa,” Bw Zarai anadai. Kwao, ni hitaji la mara kwa mara la kuimaliza siku nzima nchini Kenya. Alipokuwa na umri wa miezi mitatu mwaka 1994, Bi Firdaus Ahmed alitoroka nchini Somalia. “Marafiki wangu wa utotoni na shuleni wameajiriwa. Kuwa katika hali hii ni kitu kibaya na ninahuzunika,” Bi Ahmed anasema. Wakimbizi hao walikuwa wakizungumza katika Hoteli ya Travelers Beach mjini Mombasa kama sehemu ya mazungumzo ya Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KNCHR) inayoleta pamoja wakimbizi, jumuiya zinazowahifadhi na mashiriki ya kijamii yasiyokuwa ya kiserikali. Kesi yao ni sawa na ile ya Eugene Lubangi, ambaye alitoroka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) mnamo 1999. Lubangi anasema alipata bahati na kuolewa na Mkenya, na kwa pamoja walibarikiwa kupata watoto. “Licha ya kuwa nchini Kenya kwa miaka zaidi ya 20 na kuongeza, ninapata taabu kuomba vibali vya kufanya kazi ikiwemo leseni ya udereva,” anasema Lubangi. Wakimbizi wa mijini wanataja maisha yao kuwa magumu zaidi kwani hali ngumu huwalazimisha kutafuta kazi kulisha familia zao. Lubangi anaongeza: “Si kama tunaishi kwenye kambi na kila kitu kimetolewa kwa ajili yetu, na nilipokimbia vurugu katika nchi yangu, Mombasa haikuwa chaguo langu la kwanza. Ingawa hivyo, nilijipata Mombasa na kutokana na vikwazo vya kutembea, sikuweza kuhamia sehemu nyingine yoyote tangu wakati huo. Sijawahi kuenda kwenye kambi na sifahamu sehemu yoyote nje ya Mombasa.” Miongoni mwa hao wakimbizi kuna maprofesa, madaktari, na wahandisi ambao sasa wanalazimika kukaa nyumbani kwa sababu hawawezi kufanya kazi au kuendesha biashara ya aina yoyote nchini Kenya. Walitaja suala jingine kubwa wanaloshughulikia kuwa ni kunyanyaswa na baadhi ya polisi. “Nilipokuja katika nchi hii (Kenya) kutoka katika nchi yangu ya asili Somalia, nilikuwa na umri wa miaka miwili. Sikujua kwa nini tunahama; kama ungeniuliza wakati huo, nisingekuwa na ujuzi au sababu za kuelezea. Nilifuata taratibu na kupata kitambulisho changu cha mkimbizi, lakini zaidi ya kukibeba, hakina thamani nyingine. Afisa wa sheria wa Muungano wa Wakimbizi usiokuwa wa kiserikali (RCK), ambao unatetea wakimbizi na jumuiya zinazowahifadhi, anahisi panahitajika pawepo na ushawishi mkubwa na elimu miongoni mwa maafisa tofauti wa serikali. Kulingana na kundi hilo, wakimbizi wanaoishi nchini Kenya bado wanabaguliwa na kwa muda mrefu, wamekuwa wakitafsiriwa vibaya kama wahamiaji haramu. “Hakuna anayechagua kuitoroka nchi yake na kutafuta hifadhi katika nchi nyingine. Watu hawa wanastahili kutendewa utu na heshima,” akasema afisa wa masuala ya kisheria wa RCK Bi Cindy Adundo. Takwimu za Idara ya Huduma za Wakimbizi zinaonyesha kuwa kufikia Februari 2023, wakimbizi na waomba hifadhi 289,701 walitoka nchini Somalia. Wengine ni wa kutoka Sudan Kusini (155,852), DRC (54,860), na Ethiopia (32,221). Nao wengine ni wa kutoka Burundi (26,667), Sudan (10,517), Uganda (3,835), Eritrea (2,682), Rwanda (2,482), na mataifa mengine kwa ujumla (1,085). You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MASHIRIKA MAHAKAMA moja ya kijeshi nchini Uganda imewapata wanajeshi wawili na hatia ya kuwa waoga, wakati wanajeshi wa taifa hilo waliposhambuliwa na wanamgambo wa Kiislamu nchini Somalia mnamo Mei. Mameja Zadock Abor na John Oluka walitoroka baada ya wanamgambo wa kundi la Al-Shabab kuanza mashambulizi dhidi yao katika eneo la Bulo Marer, kusini mwa jiji kuu la Somalia, Mogadishu. Karibu wanajeshi 50 wa Uganda waliuawa kwenye shambulio hilo. Wakati huo huo, Umoja wa Ulaya (EU) unataka uchunguzi mkali kuanzishwa kufuatia ripoti za mauaji ya karibu watu 100 nchini Burkina Faso mapema wiki iliyopita. “Karibu raia 100, wakiwemo watoto na wanawake, wanaaminika kuangamia katika mkasa huo wa kikatili,” akasema mkuu wa sera ya Kigeni katika muungano huo, Joseph Borrell, kwenye taarifa. Amerika pia imekashifu vikali shambulio hilo. Hadi sasa, haijabainika kuhusu watu waliohusika kwenye shambulio hilo lililofanyika Jumatatu wiki iliyopita katika kijiji cha Zaongo. Borrell aliurai utawala wa kijeshi nchini humo kutoa ufafanuzi kamili kuhusu kilichosababisha maafa hayo. Kufikia jana, utawala huo haukuwa umetoa taarifa yoyote. Burkina Faso imekuwa ikijaribu kukabiliana na wanamgambo wa Kiislamu, ambapo baadhi yao wamekuwa wakiingia katika taifa hilo kutoka Mali. Utawala huo umekuwa ukiwalazimisha raia kujiunga na vita dhidi ya makundi hayo ya wanamgambo, yanayodaiwa kudhibiti karibu nusu ya taifa hilo. Karibu robo ya shule zote nchini humo zimefungwa kutokana na wimbi la mashambulio hatari ambayo yamekuwa yakitekelezwa na makundi hayo. Mkazi mmoja aliwaambia wanahabari kwamba kijiji cha Zaongo kilikuwa miongoni mwa vijiji vichache vilivyokuwa vimebaki ambavyo havikuwa “vimeshambuliwa na magaidi”. “Ilidaiwa baadhi ya wanakijiji walikuwa wakishirikiana na wanamgambo,” akaeleza. Jeshi lilichukua uongozi nchini humo mwaka uliopita, ambapo liliapa kukabiliana na makundi hayo. Kinaya ni kwamba, mashambulio hayo yameongezeka, licha ya ahadi ya utawala huo kuyakomesha ukiwa enzini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MERCY KOSKEI KATIBU katika Wizara ya Afya Mary Muthoni amehimiza magavana kuajiri wahudumu zaidi wa afya zaidi ili kupunguza uhaba unaoshuhudiwa katika vituo vya afya nchini. Kulingana na Bi Muthoni, uchunguzi wa serikali ya kitaifa unaonyesha kuwa hospitali nyingi zina wafanyikazi wachache, licha ya kuwa ni jukumu ya kila serikali ya kaunti kuhakikisha kuwa vituo vyao vina wafanyikazi tosha. Chini ya Katiba ya sasa iliyopitishwa na kuidhinishwa 2010, Sekta ya Afya imegatuliwa magavana wakipaswa kuiwajibikia. Katibu Muthoni alisema kuwa kuajiri wafanyakazi wengi, kutasaidia kukidhi mahitaji ya idadi ya watu wanaotafuta huduma za afya. Alisema hayo mnamo Jumamosi, Novemba 11, 2023 baada ya kukutana na wanawake katika eneo la Nkoben, Kaunti Ndogo ya Narok Kusini, Kaunti ya Narok. “Tumezuru hospitali zote nchini na tumegundua kwamba kuna hitaji la wafanyikazi zaidi kwa sababu serikali za kaunti zina majukumu ya kuajiri madaktari na wauguzi ili wahudumie wananchi,” Bi Muthoni alisema. Hata hivyo, aliwaomba Wakenya kutembelea vituo vya afya mara kwa mara ili wapate uchunguzi na kukaguliwa ugonjwa hatari wa Saratani akisema hatua hiyo itasaidia madaktari kuugundua mapema kwa minajili ya matibabu. Akihutubia wanawake hao, alisema ni muhimu watu kushiriki hafla za uhamasishaji Kansa (Saratani) kwa sababu wataelewa umuhimu wa kaguzi za mara kwa mara. Katibu huyo alimpongeza Rais William Ruto kwa kutia saini miswada minne kuwa sheria ambayo itaboresha afya ya Wakenya. Pia alifichua kuwa serikali inapania kuendesha mchakato utakaochukua data ya wafanyikazi wa matibabu kote nchini, ili kuweza kubaini pengo lilipo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA WYCLIFFE NYABERI  WAZIRI wa Leba Florence Bore amewaomba Wakenya hasa wakazi wa Gusii kujiepusha na upanzi wa miti ya mikaratusi maarufu kama Eucalyptus. Bi Bore, Jumatatu asubuhi, Novemba 13, 2023 aliwaongoza wakazi wa Nyamira katika Sikukuu ya upanzi wa miti ya kitaifa. Akizungumza katika Shule ya Upili ya Manga Nyaisa, Waziri Bore aliwaomba wakazi wa Gusii kuiondoa miti hiyo kwenye chemchemi za maji kwani inafyonza maji kwa viwango vikubwa na kupelekea mito kukauka. “Tukome kupanda miti ya Eucalyptus na badala yake tupande spishi zingine na miti ya matunda. Tumetoka katika kipindi cha kiangazi na hatutaki kurejea huko na ndiposa serikali imetujukumisha kupanda miti kwa wingi kwani miti husaidia kuvuta mvua,” waziri Bore alisema. Upanzi wa miti yenye thamani kama vile matunda, unatajwa kama njia mojawapo kusaidia kuangazia uhaba wa chakula. Katika eneo zima la Gusii, upanzi wa mikaratusi umepewa kipaumbele na imepandwa kote katika sehemu oevu ili ikue kwa kasi. Wakazi waliigeukia ili iwe kitega uchumi kwao baada ya kilimo cha majanichai na kahawa kudorora. Katika hafla ya Jumatatu kupanda miti, Waziri Bore aliandamana na Gavana Amos Nyaribo, mbunge wa Kitutu Masaba Clive Gisairo, Mbunge Mwakilishi wa Kike Jerusha Momanyi miongoni mwa viongozi wengine kutoka jamii ya Abagusii. Gavana Nyaribo alidokeza kuwa kuanzia mwezi ujao, wataanzisha mchakato wa kuikata mikaratusi yote iliyopandwa karibu na vyanzo vya maji.       You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA SAMMY WAWERU RAIS William Ruto anatarajiwa Jumatatu, Novemba 13, 2023 kuongoza nchi katika upanzi wa miti. Hii ni baada ya Wizara ya Usalama wa Ndani na Mikakati ya Serikali kutenga leo, Jumatatu, kuwa siku maalum ya kitaifa kufanya upanzi wa miti ili kusaidia kukabiliana na athari hasi za mabadiliko ya tabianchi. Aidha, serikali ya Rais William Ruto imetuma mawaziri katika kaunti zote nchini kutekeleza oparesheni hiyo. Waziri wa Utalii, Dkt Alfred Mutua amekita kambi katika Kaunti ya Kitui kuongoza wakazi kupanda miche ya miti naye mwenzake wa Leba, Bi Florence Bore akiamba hema Nyamira. Dkt Ruto ataongoza shughuli hiyo ya kitaifa katika Kaunti ya Makueni. Mwaka uliopita, 2022, Rais Ruto alizindua kampeni ya upanzi wa miti bilioni 15 kufikia 2032. Hatua hiyo, kiongozi wa nchi anasema itasaidia kukabiliana na athari za tabianchi. Viongozi ulimwenguni wanaendeleza mjadala kuzima mabadiliko ya hali ya hewa, ambayo yameathiri ulimwengu kwa kiwango kikubwa. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA LABAAN SHABAAN MTAALAMU wa Teknolojia ya Fedha (Fintech) ambaye ni mwajiri nchini Kenya, Jason Marshall, amekashifu serikali kwa kutangaza Jumatatu, Novemba 13, 2023 kuwa Sikukuu. Serikali ilishangaza Wakenya kwa kutangaza kuwa leo, Jumatatu itakuwa Sikukuu kwa minajili ya upanzi wa miti nchini. “Siku hii, wananchi wote wanatarajiwa kupanda miti kuonyesha uzalendo kwa juhudi za kitaifa za kuokoa nchi dhidi ya athari mbaya ya mabadiliko ya tabianchi,” alitangaza Waziri wa Usalama wa Ndani, Prof Kithure Kindiki kupitia Gazeti Rasmi la Serikali Novemba 6, 2023. Tangazo hili lilimkera Bw Jason Marshall, ambaye ni mwajiri kutoka Amerika akishangaa ni kwa nini wafanyakazi wake washerehekee upandaji miti, badala ya kufanya kazi. “Kuna Sikukuu nyingi sana Kenya. Wafanyakazi wetu wa Kenya hawatakuwa kazini Jumatatu ili waadhimishe siku ya kupanda miti. Hii ni nini sasa?” Bw Marshall alisikitika katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa X (awali Twitter). Mwajiri huyu amelinganisha taifa la Kenya na America (US), akisema nchi yake ina Sikukuu chache. Kulingana na Bw Marshall, Kenya husherehekea Sikukuu ambazo hazina maana. “Kule Amerika, Sikukuu ni za serikali na wafanyakazi wa benki tu,” alisema. “Wanabenki na wafanyakazi wa serikali huwa na Sikukuu 11. Wafanyakazi wa sekta ya kibinafsi huwa na siku ya mapumziko 7 ama 8 Amerika,” aliongeza. Kulingana na bwanyenye Marshall, kampuni yake itagharamika kulipa wafanyakazi wake licha ya wao kuadhimisha Sikukuu ambayo anasema walipewa bure. Siku hii, serikali inalenga kupanda miche 100 milioni kote nchini. Wakenya wanaoshiriki upandaji miti wanatakiwa kupokea miche kutoka kwa afisi za chifu zilizo karibu nao bila malipo. Mwaka uliopita, 2022, Rais William Ruto alizindua kampeni ya upanzi wa miti bilioni 15 kufikia 2032. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA SPIKA wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula ameitaka serikali kuweka kikosi maalum cha maafisa wa usalama katika eneo la Baragoi kupambana na kero la wizi wa mifugo katika Kaunti ya Samburu. Alipendekeza kuundwa kwa kambi maalum ya kikosi cha usalama, chenye mafunzo maalum, kupambana na wahalifu hao ambao huua kabla ya kuiba mifugo. “Serikali imeimarisha juhudi za kupambana na wizi wa mifugo katika maeneo kadha ya Kaskazini mwa Bonde la Ufa kwa kubuni vituo maalum kwa maafisa wa usalama,” Bw Wetang’ula akaeleza. Spika alisema hayo alipowahutubia waumini katika Kanisa Katoliki la Maralal Jumapili, Novemba 12, 2023 ambapo aliongoza hafla ya kuchanga fedha za kufadhili ujenzi wa kituo cha afya katika kanisa hilo. Bw Wetang’ula alisema: “Wizi wa mifugo sio mila bali ni biashara ya wahalifu. Kwa hivyo, sharti utokomezwe kabisa.” Kwa hivyo, Spika Wetang’ula aliwataka viongozi na wakazi kushirikiana na serikali katika juhudi zake za kupambana na wahalifu eneo hilo. “Masuala ya usalama hayafai kuachiwa serikali pekee. Ninyi kama viongozi wa hapa na wananchi mna na wajibu wa kusaidia serikali kumaliza visa vya uhalifu kama wizi wa mifugo miongoni mwenu,” akashauri. Bw Wetang’ula alimpongeza Mbunge Mwakilishi wa Kike Kaunti ya Samburu Pauline Lenguris kwa kumwalika kuenda kusaidia kuchanga fedha za kukamilisha ujenzi wa kituo hicho cha afya. “Nilikubali mwaliko kwa sababu baada ya mradi huu kukamilishwa utapiga jeki juhudi za serikali kuhakikisha kuwa wananchi wetu wanapata huduma za afya, haswa maeneo ya mashambani,” akaongeza. “Ushirikiano huu ni mzuri. Na baada ya mradi huu kukamilika, serikali itaweka vifaa katika kituo hiki cha afya ili kihudumie jamii,” Bw Wetang’ula akasema. Aliongeza kuwa mradi huo unaendeleza ajenda ya serikali kutekeleza Mpango wa Afya kwa Wote (UHC). Kando na Bi Lenguris Spika Wetang’ula aliandamana na wabunge kadha wa eneo hilo na wengine kutoka maeneo  mengine. Wao ni pamoja na; Letipila Eli (Samburu Kaskazini), Joseph Makilap (Baringo Kaskazini), Victor Bwire (Taveta), Martin Wanyonyi (Webuye Mashariki) miongoni mwa wengine.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MHARIRI
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini.
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na BENSON MATHEKA
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na MASHIRIKA
LONDON, Uingereza
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya... Na ELIZABETH MERAB
WANASAYANSI wanachunguza kuhusu mchipuko wa virusi vipya vya corona aina ya Delta, katika nchi za Amerika, Uingereza,... Na MAUREEN ONGALA
MASAIBU ambayo wagonjwa wa Covid-19 hupitia katika kaunti za Pwani, yameanikwa wazi baada ya kifo cha afisa mkuu wa... SIAGO CECE na ANTHONY KITIMO
UFISADI miongoni mwa baadhi ya maafisa wa serikali katika mpaka wa Kenya na Tanzania, umezidi kuwaweka... Na WAANDISHI WETU
WINGU la maangamizi limetanda kote nchini huku aina mpya ya corona maarufu kama 'Delta' ikiua watu kwa... Na WINNIE ONYANDO
HUENDA visa vya wasafiri kulazimishwa kupima upya corona mpakani mwa Kenya na Tanzania vikakoma baada ya serikali hizo... NA WANGU KANURI
AGIZO la serikali la kudhibiti mkurupuko wa ugonjwa wa corona mwaka jana limewashurutisha Wakenya wengi kufanyia kazi... Na Titus Ominde
VIONGOZI wa kidini Kaskazini mwa Rift Valley (North Rift) wameshutumu wanasiasa kwa kupepeta usambazaji wa virusi vya... Na WANTO WARUI
Huku wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiripoti katika shule zao mpya za sekondari hii leo, kuna uwezekano wa maambukizi... Na CHARLES WASONGA
NAKUBALIANA na kauli ya maafisa wa afya katika kaunti ya Nairobi kwamba wanasiasa ndio wanachochea ongezeko la visa... Na SAMMY WAWERU
DICKSON Muceri amekuwa mkazi wa Nairobi kwa muda wa miaka kadhaa ila sasa kitovu hicho cha jiji kuu la nchi hakikaliki... Na MARY WANGARI
WANASAYANSI wamethibitisha kuwa kuchelewesha upokeaji dozi ya pili ya chanjo ya Covid-19 kwa kiasi cha miezi 10 baada ya... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na KINYUA BIN KINGORI
WAKATI huu viongozi wa kisiasa wameanza mapema kampeni zao kwa kuzuru maeneo mbalimbali nchini, ili kushawishi... Na WANDERI KAMAU
KULINGANA na Ripoti ya Jaji Mstaafu Akilano Akiwumi (1997) kuhusu chimbuko la ghasia za kikabila nchini, wanasiasa ndio... Na WANTO WARUI
KWA mara nyingine tena tuzo inayoenziwa sana kote ulimwenguni imerudi katika eneo letu la Afrika Mashariki mara hii... Na DOUGLAS MUTUA