text
stringlengths 3
16.2k
|
---|
T L |
Tags |
You can share this post! |
Previous article |
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya... |
Next article |
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika... |
T L |
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA RICHARD MAOSI WAKAZI wa mtaa wa Mazembe viungani mwa mji wa Nakuru wamekiri kuhangaishwa na wezi ambao huwaibia na kuwasindikiza hadi nyumbani. Huwawekea ulinzi huo makusudi ili kuhakikisha kwamba wateja wao wanafika nyumbani salama salimini. Kwa kawaida, wahuni wamebuni mbinu mpya ya kutembea na mbwa wakubwa nyakati za usiku, ili kujiwekea ulinzi wa kibinafsi. Owen Shibala mwendeshaji bodaboda kati ya Nakuru mjini na Mazembe, anasema hajui walikotoa ujasiri walio nao kushika doria usiku utadhani ni polisi. Mazembe ni mojawapo ya mitaa ambayo hushuhudia visa vya kihalifu na utumiaji wa mihadarati mara kwa mara. “Ukikutana nao usiku ni lazima usalimishe kila kitu lau sivyo utaona cha mtema kuni. Watakucharaza viboko na kuiba kila kitu cha nguvu,”akasema. Hata hivyo, wanapoiba hujitwika jukuma la kuwasindikiza wakazi, wasije wakakutana na vibaka wengine barabarani. Aidha, wanalia sare za polisi jambo linalowafanya baadhi ya raia kuamini huenda wanashirikiana na maafisa wa polisi. Baadhi yao wanajifanya ni maafisa wa polisi ambao huwa wameshika doria, wakilenga kuhangaisha wapita njia wanaotoka kazini usiku. Agnes Wahome mfanyibiashara mtaani Rhonda anasema huwa wamejihami kwa visu, rungu na wako tayari kupigana. Kulingana na Bi Wahome, hii ni hali ya kawaida siku hizi katika mitaa ya Manyani, Bondeni na Freearea ambapo vijana wengi wamejiingiza kwenye uhalifu. Bi Wahome anasema wahalifu wengi wanajulikana, kwani ni vijana wadogo kutoka mitaa jirani ya Flamingo na Lakeview. Mkazi huyo angependa polisi kushika doria katika maeneo husika ili kuzuia kuzuka kwa magenge hatari yanayohangaisha wenyeji. Hili linajiri siku chache baada ya Taifa Leo Dijitali kufichua visa vya wizi ambapo baadhi ya wezi kutoka kwenye mtaa wa Gioto, Nakuru wamekuwa wakipika chakula katika kila nyumba wanamoingia kuiba. Mtaa wa Bondeni, Kaunti ya Nakuru ambapo wezi huwaibia wakazi na kuwasindikiza mpaka nyumbani. PICHA|RICHARD MAOSI |
Tags |
You can share this post! |
Previous article |
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya... |
Next article |
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika... |
T L |
Tags |
You can share this post! |
Previous article |
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya... |
Next article |
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika... |
T L |
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA RICHARD MUNGUTI MASKWOTA wapatao 10,000 wamewasilisha upya kesi katika Mahakama ya Upeo wakiomba ibatilishe uamuzi kwamba wafukuzwe kutoka kwa shamba la ukubwa wa ekari 25,000 wanalong’ang’ania umiliki wake na familia ya mwanasiasa marehemu Mark Too. Maskwota hao wanaodai mababu zao ndio waliotimuliwa kutoka kwa shamba hilo enzi za ukoloni, wanasema walipewa shamba hilo rasmi na aliyekuwa Rais hayati Daniel arap Moi, kisha Kamishna wa Ardhi M Okundu akaratibisha uamuzi huo mwaka 2007. Katika ombi lililowasilishwa na wakili William Arusei chini ya sheria za dharura, kikundi cha maskwota hao–Sirikiwa Squatters Group–kimeomba mahakama ibatilishe uamuzi huo kwa vile ilitegemea ushahidi ambao haukuwa umewasilishwa katika kesi waliyoshtaki katika Mahakama ya kuamua kesi za mashamba (ELC), Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu. Pia wameeleza bayana Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaack Lenaola, na William Ouko walitegemea ushahidi wa Afisa wa Ugavi wa Mashamba R J Simiyu kutoa uamuzi wang’atuke shambani. Maskwota hao wamesema ushahidi wa Bw Simiyu uliowasilishwa mbele majaji hao saba kwa njia ya afidaviti ni mpya na kamwe “haukuwasilishwa mbele ya Jaji Antony Ombwayo aliposikiliza na kuamua kesi hiyo 2017.” Pia wanasema ushahidi huo haukuwasilishwa Mahakama ya Rufaa iliyosikiliza rufaa iliyowasilishwa na kampuni ya Fanikiwa, familia ya marehemu Mark Too, kampuni ya Lonrho Agribusiness (EA) Ltd, na Bw David K Korir. Hivyo basi, maskwota hao wanaeleza mahakama hii ya upeo kwamba ni kinyume cha sheria kutegemea ushahidi mpya kutoa uamuzi wa kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma. “Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu wa Desemba 15, 2023, hauna mashiko kisheria na kamwe hauna nguvu kisheria kuwatimua maskwota hawa kutoka kwa shamba lao,” asema Bw Arusei. Pia maskwota hawa wanadai kwamba badala ya Mahakama ya Juu kujadili masuala ya kikatiba jinsi ilivyo jukumu lake, majaji hao walianza kufafanua na kutafsiri ushahidi wa watu binafsi na kuelezea maana ya ‘skwota’. Mahakama hii imeombwa ikague upya uamuzi iliyotoa kwa vile ilidanganywa na walalamishi na pia kutendewa ujanja. Akinukuu maamuzi ya majaji wastahiki kama vile Lord Dening, Bw Arusei amesema, mahakama ikigundua ilipotoshwa au kudanganywa na upande mmoja, iko na mamlaka na uwezo wa kufutilia mbali uamuzi iliyotoa na kuandika mwingine. Maskwota hao wanaomba Mahakama ya Juu iwarudishe shambani kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Ombwayo na Mahakama ya Rufaa. Vile vile mahakama hiyo imekosolewa kwa kumshambulia hayati Moi katika uamuzi huo pasi kutoa agizo wasimamizi wa mali yake wafike mbele yao kutoa mwanga kuhusu suala la umiliki wa shamba hili lililorudishwa kwa serikali na kampuni iliyokuwa inakuza miti inayotumika katika viwanda vya ngozi. Naibu msajili wa Mahakama ya Juu Nelly Kariuki aliwaamuru maskwota hao wawakabidhi nakala za kesi hii yao mpya wahusika wote kabla ya Januari 31, 2024, kesi itakapotajwa tena kwa maagizo zaidi. Jaji aliyesikiliza kesi hii mpya hakuiratibisha kuwa ya dharura ila aliamuru pande zote ziwasilishe ushahidi katika muda wa siku 14 kuanzia Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti, baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na CHARLES WASONGA WAZIRI wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki amesitisha hatua ya wizara yake ya kupandisha ada zinazotozwa huduma mbalimbali zinatolewa na Idara ya Uhamiaji. Hii ni baada ya Profesa Kindiki kufutilia mbali notisi aliyochapisha kwenye gazeti rasmi la serikali kuongeza ada hizo ikiwemo ile ya kupata kitambulisho cha kitaifa na ile ya pasipoti. Kwa mfano kulingana na ilani hiyo, ada ya wanaotaka kupewa kitambulisho cha kitaifa, kwa mara ya kwanza ilipandishwa kutoka Sh100 hadi Sh1000, hatua ambayo ilipingwa vikali na Wakenya akiwemo kiongozi wa upinzani Raila Odinga. Lakini akibadilisha hatua hiyo waziri Kindiki mnamo Jumanne alisema hivi: “Notisi inatolewa kwa umma kwamba Notisi Kwenye Gazeti Rasmi la Serikali Nambari 15239 ya 2023, 15240 ya 2023, 15241 ya 2023 na 15242 ya 2023 katika toleo rasmi la CXXVNO Nambari 239 iliyotolewa Novemba 7, 2023, na kuchapishwa na Waziri wa Usalama kuhusiana na kuongeza kwa ada na matozo mbalimbali kwa huduma zinazotolewa na Idara ya Uhamiaji na Huduma za Rais imefutiliwa mbali kutoa nafasi kwa ushirikishwaji wa maoni ya umma kuhusu suala hilo.” Waziri huyo aliagiza Idara Uhamiaji kuendesha shughuli ya ukusanyaji maoni ya umma kuhusu suala hilo kufikia Desemba 10, 2023. “Na idara hiyo imeagizwa kukamilisha shughuli hiyo haraka iwezekanavyo,” Profesa Kindiki akaongeza. Waziri alisema mpango wa kubadilisha ada zinazotozwa huduma za Idara ya Uhamiaji unachochewa na haja ya kuifanya Kenya kujitegemea katika kufadhili Bajeti ya Kitaifa. “Hatua hii inaondoa nchi katika minyororo na mzigo wa madeni ambao umegeuka tishio kwa uhuru wetu na heshima kwa vizazi vijavyo,” Profesa Kindiki akaeleza. Kufikia sasa, watu wawili wamewasilisha kesi mahakamani kupinga kupandishwa kwa ada ya huduma za idara hiyo kama vile utoaji wa pasipoti miongoni mwa nyingine. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA SIAGO CECE WAZIRI wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen amesema mapaa yanayovujisha maji katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), ni matokeo ya kazi duni ya mkandarasi na wahandisi waliokuwa wakifanya ukarabati katika sehemu za Terminal 1C na 1E. Ameilaumu serikali iliyotangulia ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta akisema ‘ililala darasani’. Bw Murkomen alisema ukarabati uliofanywa baada ya sehemu ya JKIA kushika moto miaka michache iliyopita, ulikuwa duni na ulifanywa bila kukidhi viwango vinavyohitajika. Akizungumza Jumanne katika uwanja wa ndege wa Diani katika Kaunti ya Kwale alipokuwa akikagua upanuzi wa uwanja huo, Bw Murkomen alisema ukarabati huo utafanywa upya kukidhi viwango vinavyohitajika. “Tulipoingia ofisini, tuligundua kuwa miradi ya serikali iliyopita ilikuwa dhaifu. Ukarabati huo ulipofanywa kwenye Kituo cha 1C na E, ulikuwa wa haraka. Lakini tumezungumza na wakandarasi ili wafanye kazi upya,” Bw Murkomen alisema. Alisisitiza kwamba wahandisi na mkandarasi waliokuwa wakisimamia ukarabati huo watalazimika kuelezea kwa nini kulikuwa na kazi mbovu iliyosababisha maji ya mvua kuvuja mnamo Jumatatu. “Watalazimika kueleza kwa nini mvua kubwa inaponyesha lazima paa livujishe maji,” Bw Murkomen akasema. Hata hivyo alisema mapaa yanayovuja yamerekebishwa kwa muda ili kuzuia kuvuja zaidi katika msimu huu wa mvua. Waziri huyo alisema mkandarasi mpya atapewa kazi ili kujenga sehemu mpya ya uwanja wa ndege. Mkataba huo utakuwa wa kati ya mwekezaji wa kibinafsi na serikali na ambao utaanza Januari 2024. “Tayari tumeanza kujitayarisha na Rais William Ruto amesema inabidi tumalize kujenga uwanja mpya wa ndege ifikapo 2027,” Bw Murkomen akaahidi. Kuhusu usambazaji wa kawi katika Uwanja wa Ndege Bw Murkomen alisema kuwa serikali tayari imesuluhisha changamoto ya stima kupotea kwa kuweka jenereta lakini bado ukarabati haujamalizika kuhakikisha kuwa stima haipotei kwa zaidi ya sekunde 30. Alisema njia ya kupishana umeme kwa sasa inachukua dakika 20 lakini wanajitahidi kuhakikisha wanapunguza muda hadi sekunde 30. Mwango Capital ambao walichapisha video ikionyesha mapaa yakivujisha maji, walisema Jumanne wanashangaa namna serikali ya Kenya Kwanza imezembea kwa mwaka mzima tangu iingie madarakani mnamo Septemba 13, 2022. “Waziri wa Uchukuzi @kipmurkomen ametoa kauli yake baada ya kuona video ambayo tulirekodi na kuchapisha Jumatatu ikionyesha mapaa yakivujisha maji JKIA akiilaumu serikali iliyotangulia. Hata hivyo, hii serikali imekuwa uongozini kwa mwaka mmoja, na utepetevu umekuwepo kipindi hicho chote,” wakachapisha kwa mtandao wa X. Tazama video yenyewe hapa chini. Meanwhile JKIA is very ready for El Nino rains ? pic.twitter.com/nwXeqOLm8y — Mwango Capital (@MwangoCapital) November 13, 2023 You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA RICHARD MUNGUTI CHUO Kikuu cha Nairobi (UoN) kimepinga vikali kesi ambapo mwanakandarasi aliyepewa kazi ya kujenga mabweni katika Bewa la Kabete mwaka 1990 anataka alipwe Sh137 milioni kwa ujenzi wa mabweni uliosimama. Ujenzi wa mabweni hayo ulikwama Juni 1990 mashirika ya kigeni yalipofunga mikoba kuipa Kenya misaada. Mwanakandarasi huyo ameshtaki UoN akiomba alipwe kitita cha Sh137 milioni. Lakini UoN kupitia kwa wakili Patrick Lutta imemweleza Jaji Profesa Nixon Sifuna wa Mahakama Kuu ya Milimani jijini Nairobi kwamba kampuni ya NK Brothers Limited ililipwa na Serikali mnamo Machi 2, 2000, na “haistahili kulipwa hata senti moja.” “N K Brothers hawastahili kulipwa hata senti moja kwa vile walilipwa na Wizara ya Fedha yapata miaka 23 iliyopita,” akafichua msanifu majengo wa UoN Jerret Odwallo. Jaji huyo alielezwa kwamba NK Brothers walilipwa Sh27 milioni na endapo “malipo mengine yatatolewa basi huo utakuwa ni ufisadi.” Jaji Sifuna alielezwa Wizara ya Fedha iliandika barua ikisema “NK Brothers walipokea malipo na hawafai kudai malipo mengine.” Katika ushahidi uliowasilishwa na Bw Odwallo, Mahakama ilielezwa kuwa NK Brothers walilipwa kwa hundi nambari 001939 ya benki ya National Bank. Hundi hiyo ilikuwa ya Sh27,965,254.60. Malipo hayo yalifuatia muafaka uliotiwa saini kati ya NK Brothers na Serikali kwamba ipewe bima za biashara za thamani sawa na pesa ilizokuwa inakidai chuo hicho kikuu. NK Brothers walipewa bima hizo za biashara mnamo Oktoba 19, 1999. Kufuatia makubaliano hayo, mahakama ikaelezwa sasa haina deni inalodai UoN. Mahakama ilielezwa ujenzi wa mabweni hayo ulikwamishwa na mashirika ya kigeni kukoma kuifadhili serikali mwaka 1990 wakati wa utawala wa hayati Daniel Toroitich arap Moi. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA CHARLES WASONGA WAKENYA wanaotaka kupata kitambulisho kipya cha kitaifa sasa watahitajika kulipa Sh300 na wala si Sh1,000 jinsi ilivyotangazwa awali na serikali. Hii ni kulingana na mwongozo mpya wa ada zinazotozwa huduma za kimsingi na Idara ya Uhamiaji na Huduma za Raia ambao ulitolewa na Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki mnamo Jumanne jioni. Profesa Kindiki alitoa mwongozo huo baada ya kufutilia mbali notisi ya awali iliyoongeza ada ya kuchukua vitambulisho vya kitaifa kutoka Sh100 hadi Sh1,000, ili kutoa nafasi kwa ushirikishaji wa maoni kutoka kwa umma. Wakenya maskini hohehahe, wakiwemo mayatima na wale ambao wataonyesha kuwa hawawezi kulipa Sh300 kupata stakabadhi hizo, watalipiwa ada hizo na serikali. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA MASHIRIKA PALESTINA, GAZA SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA limeonya kwamba bohari yake ya mafuta imekauka na huenda likasimamisha shughuli zake ndani ya saa 48. Mkuu wa shirika hilo, Thomas White, aliandika kwenye mtandao wa kijamii ya X, “Operesheni zetu huko Gaza huenda zikasimama ndani ya kipindi hicho kwa kuwa hakuna mafuta Gaza.” White aliongezea kuwa UNRWA imekuwa ikitumia mafuta kutoka hifadhi yake lakini imeishiwa na bidhaa hiyo muhumu kwa kuwa hakuna mafuta yanayoingia Gaza tangu Oktoba 7 wakati Hamas waliposhambulia Israeli. Wizara ya Afya inayoendeshwa na Hamas pia ilisema mapema Jumatatu kwamba hospitali zote kaskazini mwa Gaza hazifanyi kazi tena kutokana na uhaba wa mafuta. Katika hatua nyingine, Rais wa Amerika, Joe Biden ametoa wito kwa Israeli kuilinda hospitali kubwa ya Al-Shifa katika Ukanda wa Gaza wakati shirika la afya ulimwenguni WHO likisema hospitali hiyo haitoi huduma tena. Wafanyakazi katika hospitali hiyo wamedai kuzingirwa, baada ya kituo hicho kushambuliwa mara kadhaa kwa mabomu na kuongeza kuwa Israeli inawapiga risasi watu wanaotoka nje ya jengo hilo. Hata hivyo, Israeli imekanusha madai hayo, ikisema Hamas inatumia mahandaki chini ya hospitali hiyo kushambuliwa wanajeshi wa Israeli, ingawa haijatoa ushahidi wowote kuhusu hilo. Wakati hayo yakiripotiwa, jeshi la ulinzi la Israeli, IDF, limesema kuwa linaendelea na msako mkali kwenye viunga vya kambi ya wakimbizi ya Al-Shati ndani ya Jiji la Gaza. IDF ilisema vikosi vyake vilikuwa “vinailenga miundombinu ya kigaidi iliyoko katika taasisi za serikali zikiwemo shule, vyuo vikuu, misikiti na makazi ya magaidi.” Aidha, taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa kupitia mtandao wa Telegram ilisema wanajeshi wake waliingia kwenye makazi ya mwanachama wa ngazi ya juu wa kundi la Islamic Jihad na kukuta “idadi kubwa ya silaha kwenye chumba cha watoto”. Islamic Jihad ni kundi dogo la wanamgambo linalofanya oparesheni zake ukanda wa Gaza na lenye mafungamano na Hamas. Kwa mujibu wa wizara ya Afya inayoongozwa na Hamas, zaidi ya Wapalestina 11,000 wameuawa tangu vita kuanza. Hapo jana, jamaa wa watu waliotekwa nyara na kundi la Hamas wakati wa mashambulio yake ya Oktoba 7 dhidi ya Israeli, walikusanyika mjini Jerusalem kuushinikiza Umoja wa Mataifa (UN) kuingilia kati suala hilo ili waliotekwa waachiliwe. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA BRIAN OCHARO MWANABIASHARA Anne Njeri Njoroge ambaye ametajwa katika sakata ya mafuta yenye thamani ya Sh1.7 bilioni, amejitokeza baada ya kudaiwa kupotea kwa siku nne. Akiandamana na mawakili wake Cliff Ombeta na David Chumo, mfanyabiashara huyo alionekana kuwa mnyonge alipoingia ndani ya mahakama ya Mombasa na kuketi. Baada ya kusubiri kwa takriban dakika 45, Bi Njeri na mawakili wake waliondoka mahakamani baada ya kugundua kuwa kesi yao haikuwa imewekwa kwenye orodha ya kesi ambazo zingeshughulikiwa. Katika mahojiano na Taifa Leo, Bi Njeri alielezea siku zake nne mikononi mwa watu wanne aliodai walikuwa polisi. Alieleza kuwa baada ya kuandikisha ripoti katika makao makuu ya upelelezi wa makosa ya jinai (DCI), aliombwa kuenda katika afisi nyingine ya pili kuandikisha ripoti nyingine. “Nilipofika katika afisi hiyo, nikagundua kuwa haikuwa afisi. Nilikutana na watu wawili walioniuliza iwapo nilikuwa nikitumia dawa zozote kwa ajili ya matibabu. Waliniomba iwapo ilikuwa hivyo nihakikishe nimezibeba,” akasema. Aliuliza jinsi gani afya yake ilivyohusiana na ripoti alizopaswa kuandikisha, ila akaambiwa walikuwa wakisafiri kuelekea sehemu ambayo hangeelezwa. Aliitishwa simu yake na kuambiwa aseme neno-siri la kuifungua. “Niliwauliza mbona walikuwa wananitenganisha na mawakili wangu ila wakajibu kuwa hilo halikuwahusu ndewe wala sikio,” akasema. Aliingizwa haraka kwenye gari lililokuwa likisubiri karibu, ila giza lilikuwa limeanza kuingia. Gari hilo liliendeshwa kuelekea upande wa Kiambu. “Kila mara nilikuwa ninawauliza walikokuwa wakinipeleka ila walinieleza nisiwe na wasiwasi kuwa kila kitu kilikuwa sawa. Niliwaomba wasiniue nikiwaeleza nilikuwa na familia iliyokuwa ikinitegemea. Niliwaeleza kuwa sikuwa nimeiba chochote kutoka kwa yeyote na nilikuwa nala kutokana na jasho langu,” akasema. Maafisa hao waliokuwa wamejifunika nyuso zao, walimwambia atulie kwani hakuna lolote ambalo lingemfanyikia. Baada ya muda, alisema gari hilo liliondoka kwenye barabara ya lami na kuingia kwenye barabara ya mchanga, safari hiyo ikichukua dakika kadhaa. Bi Njeri alieleza kuwa gari hilo lilisimama baada ya muda na maafisa hao wakamwamuru avue nguo zake na kujifunika usoni, la sivyo wamfunike wenyewe. Walishuka kutoka kwenye gari na wakamwelekeza kwenye nyumba. “Nilipoingia ndani kulikuwa na kigodoro ambacho niliambiwa nikalie. Waliniambia nizungumze ukweli kuhusu mafuta ya Sh17 bilioni,” akasema. ‘Maafisa’ hao kulingana na Bi Njeri, walimwonya asijaribu kuwadanganya kwani ikiwa angefanya hivyo angeuawa. “Walinieleza kuwa nisingewaona watoto wangu iwapo ningetoa taarifa za uongo. Nikawaeleza kuwa yale niliyokuwa nimeandika katika ripoti ya DCI yalikuwa ya kweli na kuwa ningekufa nayo,” akasema Bi Njeri. Kwa kushikilia msimamo wake, na kupitia mateso kwa siku nne ikiwemo kutokubaliwa kwenda kujisaidia, aliachiliwa na maafisa hao wakisema kuwa hakuwa na kosa lolote. “Asubuhi ya mwisho kabla ya kuachiliwa, walinijia na kuniambia niseme ukweli au niuawe. Niliona kifo kikija. Niliwaambia kuwa mafuta hayo ni yangu na niliyaagiza ili niyauze. Niliwaambia nilikuwa na stakabadhi zote kuyahusu. Wakaniambia ni sawa,” akasema. Bi Njeri alisema kuwa alitolewa huko na kuingizwa kwenye gari na kuachwa katika eneo la Embakasi. Mawakili wake walieleza kuwa mwanamke huyo alitishiwa maisha kuhusu mafuta hayo wakitaka aondoe kesi aliyokuwa amewasilisha katika mahakama kuu jijini Mombasa. Mawakili hao walieleza kuwa kesi hiyo haingeondolewa mahakamani. Alipoulizwa mbona hakujua alipoagiza mafuta hayo alijitetea akisema ilikuwa mara yake ya kwanza kuagiza mafuta. Bi Njeri alieleza kuwa hajaingia kwenye makubaliano yoyote na kampuni ya Galana Energies kuashiria kuwa mafuta hayo ni ya kampuni hiyo. Washtakiwa wote wamepewa siku nyingine ambayo wote watajitetea mbele ya mahakama. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA MWANDISHI WETU BEI ya mafuta ya petroli imesalia kuwa Sh217.36 kwa lita, baada ya Serikali kuwekea ruzuku ya Sh12.01 kwa lita, katika hali ambayo itawapa Wakenya nafasi ya kupumua kidogo. Kumekuwa na hofu kubwa kwamba mafuta yataongezeka katika kiwango ambacho hakijawahi kufikiriwa, haswa kufuatia mahojiano ya Waziri wa Kawi Davis Chirchir majuma mawili yaliyopita. Alipofika mbele ya Kamati ya Maridhiano ya Kitaifa kuzungumzia kuhusu suala la gharama ya maisha, Bw Chirchir alisema kuna uwezekano kwamba bei ya mafuta inaweza kukagonga Sh300 kutokana na athari za vita vinavyoendelea kati ya Israel na Hamas. Lakini kulingana na tangazo lililotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Kawi nchini EPRA Jumanne Novemba 14, 2023, serikali imesema imesawazisha bei kwa kutumia hazina ya mafuta ili kuzuia mafuta kupanda bei katika kipindi cha Novemba 14 hadi Disemba 14. Kulingana na taarifa hiyo, bei ya dizeli itashuka na kuuzwa Sh203.47 baada ya kuwekewa ruzuku ya Sh19.82, nayo mafutataa yatauzwa Sh203.06 baada ya kuwekewa ruzuku ya Sh3.64. Haya yanajiri saa chache tu baada ya baadhi ya viongozi wa serikali kuelezea hali ya mchecheto kuhusu tangazo la bei mpya, huku wakitaka mamlaka ya EPRA kuwa na saa maalum ya kutoa tangazo hilo ili kupunguza hali ya wasiwasi. Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Seneti Aaron Cheruiyot ni mmoja wa viongozi ambao wamekuwa na tumbojoto akisubiri bei mpya ya bidhaa za petroli. Mnamo Oktoba 14, 2023, mamlaka hii ilitangaza bei mpya saa saba usiku. Inaonekana EPRA itashurutishwa kutangaza bei hizi wakati ambao umebainishwa baada ya Bw Cheruiyot kudokeza uwezekano wa kubuni sheria bungeni. “Hatujawahi kungoja bei ya kila mwezi ya mafuta kutoka EPRA kama siku za hivi karibuni. Ili tuwe watulivu, huenda ikatubidi kubuni sheria ya saa mwafaka ya kutoa tangazo,” alisema Bw Cheruiyot kwenye mtandao wa kijamii wa X. “Tumeambiwa (bei ya petroli) itapanda hadi Sh300. Hatutarajii chochote chini ya hiyo,” Mkenya mmoja alisema kwenye mtandao wa X akirejelea hofu ya Waziri wa Kawi Davis Chirchir hivi maajuzi. “Wataongeza kwa Sh1, kisha wajisifu. Tena miezi mitatu ijayo wataongeza kwa Sh20,” alishuku mkenya mwengine mtandaoni. Mwezi mmoja uliopita, Wakenya wamekuwa wakinunua petroli, dizeli na mafuta taa kwa Sh217.36, Sh205.47 na 205.06 kwa kila lita mtawalia. Hizi ni bei za juu zaidi za bidhaa ya petroli katika historia ya Kenya na hali hii imewalemea wananchi wanaokabiliwa na hali ngumu ya maisha. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA RICHARD MUNGUTI MLALAMISHI mwingine amewasilisha kesi katika mahakama akiiomba kusitisha utekelezaji wa notisi ya gazeti la serikali iliyopandisha gharama za kutuma maombi ya pasipoti na huduma nyingine za serikali. Kupitia kwa wakili Danstan Omari, Mkenya Fredrick Bikeri anasema kuna haja ya kusitisha notisi zilizopandisha ada hizo kwa sababu zitawaongezea wananchi ugumu wa maisha na hata kuchangia wao kuendelea kuteseka. Bw Bikeri anasema kwamba hakuna sababu ya maana ya serikali kupandisha ada kwa huduma hizo, akiongeza kwamba hata umma haukuhusishwa kabla ya uamuzi huo kufikiwa. Jaji Lawrence Mugambi ameagiza kesi hiyo itajwe Novemba 29, 2023, wakati kesi kama hiyo, iliyowasilishwa na daktari wa upasuaji jijini Nakuru Magare Gikenyi itatajwa. Kupitia kwa notisi nambari 15239-15242 za gazeti la serikali mnamo Novemba 6, 2023, Waziri wa Usalama wa Ndani Profesa Kithure Kindiki aliagiza kuchapishwa kwa ada mpya za kupata stakabadhi hizo na huduma nyingine kutoka kwa serikali. Stakabadhi nyingine ambazo ada zake zimepandishwa ni cheti cha kuzaliwa, cheti cha kifo, cheti cha ndoa, na kibali cha kazi. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA RICHARD MUNGUTI MAHAKAMA ya Milimani imewaruhuru polisi kuwazuilia kwa siku 10 washukiwa watano wa wizi wa Sh94 milioni za dukakuu la Quickmart ambazo ziliibwa zikisafirishwa na kampuni ya huduma za ulinzi ya Wells Fargo. Ismael Patrick Gitonga, Michael Matolo Njeru, Samuel Onyango Haya, Martin Nderi Ng’ang’a, na James Mbatia Kariuki walipofikishwa mbele ya mahakama ya Milimani, Nairobi mnamo Jumanne, polisi wameomba siku 21. Wakili wa serikali Abel Omariba amemuambia Hakimu Mwandamizi Mkuu wa Milimani Bi Zainab Abdul kwamba polisi walihitaji siku 21 kukamilisha uchunguzi wao katika eneo pana kijiografia. Bw Omariba amesema polisi walifanikiwa tu kupata Sh9.1 milioni huku wakishuku kwamba Sh84.9 milioni zilizosalia, zilifichwa na washukiwa hao watano na wengine ambao bado wako mafichoni. “Ninaiomba hii mahakama iruhusu polisi kuwazuilia washukiwa hawa waliokamatwa Novemba 10, 2023, kwa siku 21 kukamilisha uchunguzi,” Bw Omariba akaiomba mahakama. Hata hivyo, mawakili wa washukiwa wamepinga wateja wao kuzuiliwa kwa siku 21, wakisema waliteswa. Mawakili hao wamesema Mbatia aliteswa na hawezi kutembea vizuri. Badala yake, waliomba Bi Abdul kuagiza washukiwa kuzuiliwa kwa siku saba. Akitoa uamuzi, hakimu aliweka zingatio kwa kiasi kikubwa cha pesa zilizopotea. “Washukiwa walikamatwa hivi majuzi na polisi wanahitaji muda kuchunguza kesi hiyo, ikitiliwa maanani kwamba zaidi ya Sh80 milioni hazijapatikana,” akasema Bi Abdul. Kesi itatajwa mnamo Novemba 27, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA PIUS MAUNDU SHUGHULI za usafiri na uchukuzi katika barabara kuu ya Mombasa-Nairobi zimeathirika katika eneo la Sultan Hamud, Kaunti ya Makueni mnamo Jumanne baada ya Mto Sultan kuvunja kingo zake na maji ya mafuriko kutapakaa barabarani. Hali hii imesababishwa na mvua kubwa iliyonyesha katika kaunti jirani ya Kajiado. Wenye magari na pikipiki wanaonekana wakiwa waangalifu zaidi barabarani kufuatia hali hiyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA MHARIRI |
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI |
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI |
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI |
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI |
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI |
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI |
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI |
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI |
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI |
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini. |
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI |
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI |
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na BENSON MATHEKA |
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU |
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA |
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA |
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA |
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU |
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA |
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO |
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI |
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA |
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON |
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA |
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na MASHIRIKA |
LONDON, Uingereza |
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya... Na ELIZABETH MERAB |
WANASAYANSI wanachunguza kuhusu mchipuko wa virusi vipya vya corona aina ya Delta, katika nchi za Amerika, Uingereza,... Na MAUREEN ONGALA |
MASAIBU ambayo wagonjwa wa Covid-19 hupitia katika kaunti za Pwani, yameanikwa wazi baada ya kifo cha afisa mkuu wa... SIAGO CECE na ANTHONY KITIMO |
UFISADI miongoni mwa baadhi ya maafisa wa serikali katika mpaka wa Kenya na Tanzania, umezidi kuwaweka... Na WAANDISHI WETU |
WINGU la maangamizi limetanda kote nchini huku aina mpya ya corona maarufu kama 'Delta' ikiua watu kwa... Na WINNIE ONYANDO |
HUENDA visa vya wasafiri kulazimishwa kupima upya corona mpakani mwa Kenya na Tanzania vikakoma baada ya serikali hizo... NA WANGU KANURI |
AGIZO la serikali la kudhibiti mkurupuko wa ugonjwa wa corona mwaka jana limewashurutisha Wakenya wengi kufanyia kazi... Na Titus Ominde |
VIONGOZI wa kidini Kaskazini mwa Rift Valley (North Rift) wameshutumu wanasiasa kwa kupepeta usambazaji wa virusi vya... Na WANTO WARUI |
Huku wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiripoti katika shule zao mpya za sekondari hii leo, kuna uwezekano wa maambukizi... Na CHARLES WASONGA |
NAKUBALIANA na kauli ya maafisa wa afya katika kaunti ya Nairobi kwamba wanasiasa ndio wanachochea ongezeko la visa... Na SAMMY WAWERU |
DICKSON Muceri amekuwa mkazi wa Nairobi kwa muda wa miaka kadhaa ila sasa kitovu hicho cha jiji kuu la nchi hakikaliki... Na MARY WANGARI |
WANASAYANSI wamethibitisha kuwa kuchelewesha upokeaji dozi ya pili ya chanjo ya Covid-19 kwa kiasi cha miezi 10 baada ya... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na KINYUA BIN KINGORI |
WAKATI huu viongozi wa kisiasa wameanza mapema kampeni zao kwa kuzuru maeneo mbalimbali nchini, ili kushawishi... Na WANDERI KAMAU |
KULINGANA na Ripoti ya Jaji Mstaafu Akilano Akiwumi (1997) kuhusu chimbuko la ghasia za kikabila nchini, wanasiasa ndio... Na WANTO WARUI |
KWA mara nyingine tena tuzo inayoenziwa sana kote ulimwenguni imerudi katika eneo letu la Afrika Mashariki mara hii... Na DOUGLAS MUTUA |
MWAFRIKA akiwajibishwa na Mzungu hupiga kamsa na kudai anaonewa, ati msingi wa maonevu ni ubaguzi wa rangi... Na WANDERI KAMAU |
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.