text
stringlengths
3
16.2k
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAKAZI wa mtaa wa Mazembe viungani mwa mji wa Nakuru wamekiri kuhangaishwa na wezi ambao huwaibia na kuwasindikiza hadi nyumbani. Huwawekea ulinzi huo makusudi ili kuhakikisha kwamba wateja wao wanafika nyumbani salama salimini. Kwa kawaida, wahuni wamebuni mbinu mpya ya kutembea na mbwa wakubwa nyakati za usiku, ili kujiwekea ulinzi wa kibinafsi. Owen Shibala mwendeshaji bodaboda kati ya Nakuru mjini na Mazembe, anasema hajui walikotoa ujasiri walio nao kushika doria usiku utadhani ni polisi. Mazembe ni mojawapo ya mitaa ambayo hushuhudia visa vya kihalifu na utumiaji wa mihadarati mara kwa mara. “Ukikutana nao usiku ni lazima usalimishe kila kitu lau sivyo utaona cha mtema kuni. Watakucharaza viboko na kuiba kila kitu cha nguvu,”akasema. Hata hivyo, wanapoiba hujitwika jukuma la kuwasindikiza wakazi, wasije wakakutana na vibaka wengine barabarani. Aidha, wanalia sare za polisi jambo linalowafanya baadhi ya raia kuamini huenda wanashirikiana na maafisa wa polisi. Baadhi yao wanajifanya ni maafisa wa polisi ambao huwa wameshika doria, wakilenga kuhangaisha wapita njia wanaotoka kazini usiku. Agnes Wahome mfanyibiashara mtaani Rhonda anasema huwa wamejihami kwa visu, rungu na wako tayari kupigana. Kulingana na Bi Wahome, hii ni hali ya kawaida siku hizi katika mitaa ya Manyani, Bondeni na Freearea ambapo vijana wengi wamejiingiza kwenye uhalifu. Bi Wahome anasema wahalifu wengi wanajulikana, kwani ni vijana wadogo kutoka mitaa jirani ya Flamingo na Lakeview. Mkazi huyo angependa polisi kushika doria katika maeneo husika ili kuzuia kuzuka kwa magenge hatari yanayohangaisha wenyeji. Hili linajiri siku chache baada ya Taifa Leo Dijitali kufichua visa vya wizi ambapo baadhi ya wezi kutoka kwenye mtaa wa Gioto, Nakuru wamekuwa wakipika chakula katika kila nyumba wanamoingia kuiba. Mtaa wa Bondeni, Kaunti ya Nakuru ambapo wezi huwaibia wakazi na kuwasindikiza mpaka nyumbani. PICHA|RICHARD MAOSI
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MUNGUTI MASKWOTA wapatao 10,000 wamewasilisha upya kesi katika Mahakama ya Upeo wakiomba ibatilishe uamuzi kwamba wafukuzwe kutoka kwa shamba la ukubwa wa ekari 25,000 wanalong’ang’ania umiliki wake na familia ya mwanasiasa marehemu Mark Too. Maskwota hao wanaodai mababu zao ndio waliotimuliwa kutoka kwa shamba hilo enzi za ukoloni, wanasema walipewa shamba hilo rasmi na aliyekuwa Rais hayati Daniel arap Moi, kisha Kamishna wa Ardhi M Okundu akaratibisha uamuzi huo mwaka 2007. Katika ombi lililowasilishwa na wakili William Arusei chini ya sheria za dharura, kikundi cha maskwota hao–Sirikiwa Squatters Group–kimeomba mahakama ibatilishe uamuzi huo kwa vile ilitegemea ushahidi ambao haukuwa umewasilishwa katika kesi waliyoshtaki katika Mahakama ya kuamua kesi za mashamba (ELC), Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu. Pia wameeleza bayana Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaack Lenaola, na William Ouko walitegemea ushahidi wa Afisa wa Ugavi wa Mashamba R J Simiyu kutoa uamuzi wang’atuke shambani. Maskwota hao wamesema ushahidi wa Bw Simiyu uliowasilishwa mbele majaji hao saba kwa njia ya afidaviti ni mpya na kamwe “haukuwasilishwa mbele ya Jaji Antony Ombwayo aliposikiliza na kuamua kesi hiyo 2017.” Pia wanasema ushahidi huo haukuwasilishwa Mahakama ya Rufaa iliyosikiliza rufaa iliyowasilishwa na kampuni ya Fanikiwa, familia ya marehemu Mark Too, kampuni ya Lonrho Agribusiness (EA) Ltd, na Bw David K Korir. Hivyo basi, maskwota hao wanaeleza mahakama hii ya upeo kwamba ni kinyume cha sheria kutegemea ushahidi mpya kutoa uamuzi wa kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma. “Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu wa Desemba 15, 2023, hauna mashiko kisheria na kamwe hauna nguvu kisheria kuwatimua maskwota hawa kutoka kwa shamba lao,” asema Bw Arusei. Pia maskwota hawa wanadai kwamba badala ya Mahakama ya Juu kujadili masuala ya kikatiba jinsi ilivyo jukumu lake, majaji hao walianza kufafanua na kutafsiri ushahidi wa watu binafsi na kuelezea maana ya ‘skwota’. Mahakama hii imeombwa ikague upya uamuzi iliyotoa kwa vile ilidanganywa na walalamishi na pia kutendewa ujanja. Akinukuu maamuzi ya majaji wastahiki kama vile Lord Dening, Bw Arusei amesema, mahakama ikigundua ilipotoshwa au kudanganywa na upande mmoja, iko na mamlaka na uwezo wa kufutilia mbali uamuzi iliyotoa na kuandika mwingine. Maskwota hao wanaomba Mahakama ya Juu iwarudishe shambani kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Ombwayo na Mahakama ya Rufaa. Vile vile mahakama hiyo imekosolewa kwa kumshambulia hayati Moi katika uamuzi huo pasi kutoa agizo wasimamizi wa mali yake wafike mbele yao kutoa mwanga kuhusu suala la umiliki wa shamba hili lililorudishwa kwa serikali na kampuni iliyokuwa inakuza miti inayotumika katika viwanda vya ngozi. Naibu msajili wa Mahakama ya Juu Nelly Kariuki aliwaamuru maskwota hao wawakabidhi nakala za kesi hii yao mpya wahusika wote kabla ya Januari 31, 2024, kesi itakapotajwa tena kwa maagizo zaidi. Jaji aliyesikiliza kesi hii mpya hakuiratibisha kuwa ya dharura ila aliamuru pande zote ziwasilishe ushahidi katika muda wa siku 14 kuanzia Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti,  baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA FRIDAH OKACHI Kiongozi wa Chama cha Narc Kenya Martha Karua amefanya mkutano na wanachama wake ambapo ametumia fursa hiyo kushambulia utawala wa Rais William Ruto. Bi Karua ameshtumu serikali ya Ruto kwa kile alichosema ni kukosa kuchukulia hatua wale wanaoiba mali ya umma. “Wengi wa wanaoachiliwa katika kesi za ufisadi wanatoka jamii ya Rais Ruto,” akasema Bi Karua. Bi Karua vile vile amelaani Serikali kuhusu elimu hapa nchini, akisema kuwa shule za msingi na upili zinatoa elimu duni ilhali serikali inalimbikizia Wakenya mzingo wa kulipa karo. Kuhusu suala la Ann Njeri, mfanyabiashara kwenye sakata ya kutoweka kwa mafuta ya Sh17 bilioni, Bi Karua anasema kutekwa nyara kwa mfanyabiashara huyo kulikuwa njama ya Serikali kuingilia ushahidi. Kiongozi huyo ametishia kurai wafuasi wa Upinzani kurudi kwenye maandamano iwapo serikali haitapunguza gharama ya maisha. Chama hicho kimesema Bi Karua atasimama katika kinyanganyiro cha Urais mwaka 2027. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MUNGUTI MZEE wa umri wa miaka 70 ameshtakiwa kwa kukataa kuchukua kitambulisho cha kitaifa na wizi wa Sh362,000. Stanley Nguriathi Muchina alishtakiwa mbele ya hakimu mwandamizi katika mahakama ya Milimani Gilbert Shikwe kwa “kukataa kuchukua kitambulisho ilhali amepitisha umri wa miaka 18.” Alishtakiwa kwamba mnamo Agosti 14, 2023, katika kijiji cha Kinoo, Kaunti ya Kiambu alipatikana na polisi akiwa hana kitambulisho ilhali alikuwa amehitimu umri wa kuchukua kitambulisho. “Ulipatikana na polisi ukiwa huna kitambulisho ilhali wewe umehitimu umri wa kujiandikisha na kuchukua kitambulisho,” mshtakiwa alifahamishwa na Bw Shikwe. Mshtakiwa alikana shtaka hilo sawia na shtaka la pilli kwamba aliiba Sh362,463.99 Mahakama ilifahamishwa na kiongozi wa mashtaka Judy Koech kwamba pesa hizo zilikuwa mali ya kampuni ya East Coast Horizon Limited. Shtaka lilisema mshtakiwa aliiba pesa mnamo Agosti 26, 2023, katika afisi za shirika la Postal Corporation katika jengo la General Post Office (GPO). Jengo hilo la GPO liko kwenye barabara ya Koinange, Nairobi. Bw Muchina alikanusha mashtaka dhidi yake na kuomba aachiliwe kwa dhamana akisema “ni mtumishi wa umma aliyestaafu.” “Naomba hii mahakama iniachilie kwa dhamana isiyo ya kiwango cha juu. Mimi ni Mzee niliyestaafu kutoka utumishi wa umma na sina mapato hata!” Bw Muchina alimsihi hakimu. Bi Koech hakupinga ombi hilo la dhamana ila aliomba korti izingatie pesa hizo ziliibwa kutoka GPO. Akitoa uamuzi, hakimu alimwamuru mshtakiwa awasilishe dhamana ya Sh400,000 na mdhamini mmoja wa kiasi sawa na hicho. Pia hakimu alimweleza mshtakiwa anaweza kulipa dhamana ya badala ya Sh200,000 pesa taslimu akishindwa kupata dhamana ya Sh400,000. Kesi hiyo iliorodheshwa kutajwa Novemba 27, 2023, kutengewa siku ya kusikilizwa. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MERCY KOSKEI NI miaka miwili sasa tangu Bw Abraham Mogaka Mogere alipotoweka kwa njia tatanishi baada ya kutoka nyumbani kwao katika eneo la 58, Kaunti ya Nakuru. Kulingana na ndugu yake Felix Ogero, Bw Mogaka Mogere alitoweka Desemba 13, 2021, baada ya kueleza familia yake alikuwa na shughuli mjini Nakuru (sasa jijini Nakuru). Mwanafunzi huyo wa mwaka wa nne katika Chuo Kikuu cha Egerton hakurejea nyumbani jioni hiyo. Isitoshe, hakuweza kupatikana kwa simu, hali na matukio yalioacha familia yake na hofu na maswali mengi. Muda huu wote tangu kutoweka kwake, familia yake inaendelea kumtafuta kila mahali kwa matumaini ya kumpata ili aungane tena nao. Mara nyingi juhudi zao zimekuwa zikiambulia patupu. Bw Ogero alieleza Taifa Leo kuwa walizungumza na nduguye mara ya mwisho Desemba 11, 2021, saa nane mchana alipokuwa akiuliza alikoweka funguo za nyumba. Alisema kuwa walipozungumza, kakake alikuwa na furaha kwani alikuwa anapanga kukutana na mchumba wake. “Kipindi hicho nilikuwa jijini Mombasa alipopotea. Tulizungumza mara ya mwisho na kuniuliza nitarudi Nakuru lini kwani tulikuwa tunapanga mikakati ya kutembelea wazazi katika Kaunti ya Kisii kwa sherehe za Krismasi,” alisema. Hata hivyo, baada ya siku mbili Bw Ogero alitamatisha shughuli za biashara Mombasa na  kurejea nyumbani. Alipokea taarifa ya kusikitisha kwamba Bw Mogere alikuwa ametoweka nyumbani. “Imekuwa safari ngumu kwa familia ya kumtafuta kaka yangu. Inasikitisha kuwa wakati mwingi huwa namuwaza. Kupotea kwake kunafanya naumwa sana haswa wakati wa hafla za kifamilia kwa sababu kila mtu huuliza aliko, marafiki wake pia humuulizia. Unabaki tu na maswali ikiwa yuko sawa… ikiwa yuko hai bado,” alisema. Bw Ogero alisema kuwa wametembelea hospitali na hifadhi ya maiti ya Nakuru Level 5, makafani ya Nakuru City na gereza la Nakuru GK ila hawajafanikiwa kumpata au mwili wake. “Tumekuwa tukitembelea vyumba vya kuhifadhia maiti popote wanapotangaza kuwa wana miili ya watu wasiojulikana lakini hatujawahi kumpata. Tumefika kwa Mto Yala hasa wanapopata miili majini lakini juhudi zetu hazijazaa matunda yoyote,” alisimulia. Kwa sasa familia hiyo ina matumaini kuwa maafisa wa usalama watawasaidia kumtafuta na pengine kumrejesha nyumbani. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

Na WINNIE ATIENO WAZIRI wa Uchukuzi, Bw Kipchumba Murkomen ametaja sakata ya mafuta ya thamani Sh17 bilioni ambayo Bi Anne Njeri Njoroge anadai umiliki wake kuwa hekaya za abunuwasi. Bw Murkomen alisema hakuna agizo la mahakama ambalo linazuia bandari ya Mombasa kupakua mafuta hayo ya dizeli. Akihojiwa na kituo kimoja cha redio Mombasa, waziri huyo alisema mafuta hayo yalipakuliwa kitambo sana na kuyasafirisha nchi nyingine ambayo hakutaja. “Tunajua yule mama amerudi mahakamani kujaribu kupigania mafuta akidai ni yake. Hata kama hujaenda shule kusomea uwakili kuna mambo mengi unajionea kwa macho. Hata tabia ya mtu vile anajibeba inaelezea mengi,” alisema Bw Murkomen. Alisema ni maajabu kuwa Bi Njeri anamiliki mafuta hayo au hata kuingia katika makubaliano na serikali kuagiza mafuta hayo. “Mtu binafsi hawezi kuandikisha mkataba na serikali nyingine na isijulikane. Harakati kama hiyo huwa wazi. Hii ilikuwa biashara ya mkataba wa makubaliano kati ya serikali moja na nyingine,” alifafanua waziri huyo. Bw Murkomen alisema bandari ya Mombasa ilipakua mafuta hayo na kusafirisha nchi zengine ambayo ilikuwa inatakiwa. “Wakati mama huyu anajitokeza akisema mafuta ni yake, tunajiuliza mafuta gani tena? Sababu mwenye stakabadhi alikuja nazo na mwenye aliletewa mzigo na meli alikuja na wale ambao walikuwa wanayasafirisha hadi nchi nyingine walikuja na tukapakua mzigo,” alisema. Hata hivyo, alisema shehena ambayo ilikuwa ibakie nchini ilisalia. Bi Njeri, alijitokeza mahakamani akisema shehena hiyo ambayo tayari ilipakuliwa na serikali ni yake. Hata hivyo, huenda mfanyabiashara huyo anapiga vita asivyoweza baada ya serikali kusema kuwa ilishapakua mzigo huo, ikaukabidhi kwa mwagizaji bidhaa ambaye naye aliisafirisha hadi nchi nyingine. “Pengine kuna meli nyingine yenye shehena yake iliyopotea baharini. Hilo hatuwezi kupinga. Lakini kwa ile shehena iliyopakuliwa katika bandari ya Mombsa, tulishapakua mzigo sababu stakabadhi zote tulizoonyeshwa zilikuwa halali,” aliongeza. Alisisitiza kuwa meli hiyo haikuagizwa na mtu mmoja sababu maafikiano yalikuwa kati ya serikali moja na nyingine. Bi Njeri alijitokeza Jumanne baada ya kudaiwa kutekwa nyara kwa siku nne akiandamana na mawakili wake Cliff Ombeta na David Chumo, na kuelezea masaibu aliyoyapata mikononi mwa watu wanne aliodai walikuwa polisi. “Niliwaambia kuwa mafuta hayo ni yangu na niliyaagiza ili niyauze. Niliwaambia nilikuwa na stakabadhi zote kuyahusu. Wakaniambia ni sawa,” alisema. Bi Njeri anahoji kuwa alitolewa huko alikotekwa na kuingizwa katika gari na kuachwa katika eneo la Embakasi, Nairobi. Mawakili wake walileza kuwa mwanamake huyo alitishiwa maisha kuhusu mafuta hayo wakitaka aondoe kesi aliyokuwa amewasilisha katika mahakama kuu jijini Mombasa. Mawakili hao walieleza kuwa kesi hiyo haingeondolewa mahakamani. Bi Njeri alieleza kuwa hajaingia kwenye makubaliano yoyote na kampuni ya Galana Energies, ya kusema kuwa mafuta ni ya kampuni hiyo.Washtakiwa wote wamepewa siku nyingine ambayo wote watajitetea mbele ya mahakama. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MUNGUTI IDARA ya urekebishaji tabia imeomba Mahakama ya Milimani, Nairobi ipewe siku saba kuandaa ripoti ya mhasiriwa aliyelaghaiwa Sh700,000 na mganga kutoka nchini Chad miaka mitano iliyopita. Abdoulaye Tamba Kouro aliyeachiliwa huru katika shtaka la kumlaghai Seneta wa Tana River Danson Muungatana Dola za Marekani ($) 1,000,000 (Sh76 milioni) atarudishwa kortini Novemba 22, 2023, kuhukumiwa. Kufuatia ombi hilo la afisa wa urekebishaji tabia (afisa wa probesheni) hakimu mkazi mahakama ya Milimani Bw Ben Mark Ekhubi aliamuru uamuzi katika kesi inayomkabili Kouro uahirishwe hadi Novemba 22, 2023. Bw Ekhubi alisema afisa huyo wa probesheni anahitaji muda zaidi kukamilisha kuandaa ripoti hiyo. “Sijafanikiwa kumhoji mlalamishi Bw Makau Muteke aliyelaghaiwa Sh700,000 na Kouro mnamo Machi 9, 2017, katika eneo la Sandalwood mtaani Westlands, Nairobi. Naomba nipewe siku saba kuikamilisha ripoti hii,” afisa wa urekebishaji tabia alimweleza Bw Ekhubi. Bw Ekhubi alimpata na hatia Kouro ya kumlaghai Bw Muteke Dola za Marekani $6,796 (Sh700,000) akidai ataziwekeza katika biashara kupata faida. Hakimu pia alimpata Kouro na hatia ya kuwa na pesa bandia sawa na Sh960,120,000 mnamo Oktoba 1, 2018. Miongoni mwa pesa bandia alizopatikana nazo Kouro ni Dola za Marekani 54,000 (sawa na Sh8,218,800) na Euro 19,000 (sawa na Sh3,139,626) katika sarafu mbalimbali. Kouro aliachiliwa huru katika shtaka la kumlaghai Seneta wa Tana River Danson Muungatana Dola za Marekani ($)1,000,000 (Sh76 milioni) akidai ataziwekeza katika biashara ya mafuta kati ya Aprili 20, 2011, na Aprili 29, 2013. Wakili Stanley Kang’ahi anayemtetea Kouro hakupinga ombi hilo la afisa wa urekebishaji tabia aruhusiwe kuandaa ripoti ya mhasiriwa aliyelaghaiwa Sh700,000. Mbali na Bw Muteke, pia afisa huyo wa idara ya urekebishaji tabia atamhoji Kouro kufahamu maisha yake na kazi anazofanya akiwa nchini Kenya kabla ya adhabu kutolewa. Akimshauri afisa huyo wa urekebishaji tabia aharakishe ripoti hiyo, Bw Ekhubi alisema “ripoti hiyo inasubiriwa kwa hamu na ghamu na wahusika wengine.” Mganga huyo sasa amesukumwa gereza la Industrial Area baada ya kujitetea katika shtaka la kumlaghai Bw Muteke $6796 (Sh700,000) alizodai ataziwekeza katika biashara ya mafuta mnamo Machi 9, 2017. Kouro aliyeponyoka kutumbukizwa jela miaka mingi kwa kumtapeli Bw Mungatana Sh76 milioni anazuiliwa katika Gereza la Viwandani baada ya. Akimwachilia Kouro katika shtaka la kumfilisi Bw Mungatana Sh76 milioni, Bw Ekhubi alisema upande wa mashtaka ulishindwa kuwasilisha ushahidi wa moja kwa moja kumhusisha mganga huyo na ulaghai huo. “Upande wa mashtaka haukuwasilisha ushahidi kuthibitisha jinsi Bw Mungatana alivyomkabidhi Kouro mamilioni hayo ya pesa,” Bw Ekhubi alisema akitoa uamuzi ikiwa raia huyo kutoka Afrika Magharibi alikuwa na kesi ya kujibu. “Muungatana alishindwa kuwasilisha ushahidi kuthibitisha alimpa Kouro mamilioni hayo ya pesa. Lilikuwa ni neno la Mungatana dhidi ya neno la Kouro,” Bw Ekhubi alisema katika uamuzi wake. Hakimu alisema upande wa mashtaka kuwasilisha ushahidi wa moja kwa moja ulilemaza shtaka hilo na kwamba “hana budi ila kulizamisha.” You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA BAADHI ya maseneta wamependekeza kuwa Spika wa Seneti, Amason Kingi afike mbele ya mojawapo ya Kamati za Bunge hilo kufafanua kuhusu sakata ya wizi wa Sh51 milioni katika Kaunti ya Kilifi katika mwaka wa kifedha wa 2015-2026. Bw Kingi alikuwa gavana wa kaunti hiyo kwa miaka 10 kati ya 2013 na 2022. Jana Jumanne, baadhi ya wanachama wa Kamati ya Seneti kuhusu Uhasibu wa Pesa za Umma (CPAC) walisema maelezo ya Bw Kingi na maafisa waliohudumu katika serikali yake yatasaidia pakubwa katika kutanzuliwa kwa kitendawili kuhusu sakata hiyo. Hii ni baada ya Gavana wa Kilifi, Gideon Munga’ro, kuwashangaza wanachama wa kamati hiyo alipodai kuwa pesa hizo (Sh51 milioni) ziliibiwa usiku mmojawapo katika mwaka huo wa kifedha. “Ndiyo, naiambia kamati hii kwamba pesa hizo ziliibiwa usiku na watu ambao walikuwa na nambari za siri za maafisa wa serikali ya kaunti. Pesa hizo zilipitishwa kutoka kwa akaunti ya kaunti hadi kwa akaunti ya wamiliki wa kampuni ambazo hazikupewa kandarasi yoyote na kaunti,” akaiambia kamati hiyo ya CPAC inayoongozwa na Seneta wa Homa Bay, Moses Kajwang’. Bw Mung’aro alikuwa amefika mbele ya kamati hiyo katika jumba la KICC, Nairobi, kujibu maswali yaliyoibuliwa na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kuhusu matumizi ya fedha za umma katika Kaunti ya Kilifi katika mwaka wa kifedha wa 2020/2021. Suala kuhusu sakata hiyo liliibuliwa kwenye ripoti hiyo ya Bi Nancy Gathungu ilhali lilitokea katika mwaka wa kifedha wa 2015/2016 kwa sababu halikuwa limetatuliwa. Hii ni kutokana na uchunguzi wa muda mrefu ulioendeshwa na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC). Jumanne, wanachama wa CPAC walisisitiza kuwa sharti mkuu wa zamani wa kaunti hiyo, na maafisa husika, wafike mbele yake kutoa mwanga kuhusu sakata hiyo. “Sharti gavana wa zamani wa Kilifi aagizwe kufika mbele ya kamati hii kwa sababu imebainika kuwa alikuwa akisimamia kundi la wahalifu. Na afike mbele yetu akiandama na maafisa wa idara ya fedha katika serikali yake wakati huo,” akasema Seneta wa Busia, Okiya Omtata. Seneta wa Nandi, Samson Cherargei, aliunga mkono pendekezo hilo akisema washukiwa wote wa wizi huo sharti walazimishwe kurejesha pesa hizo ili zitumiwe kuwafaidi wakazi wa Kilifi. “Kwa kuwa Sh51 milioni ziliibiwa mnamo 2015, sharti gavana afike mbele ya kamati hii kujibu maswali kuhusu wizi wa pesa hizi. Ingawa yeye ni spika wetu, Katiba inaipa kamati hii mamlaka ya kuita mtu yeyote kutoa ushahidi utakaoisaidia katika utekelezaji wa majukumu yake,” akaeleza. Kauli hiyo pia iliungwa mkono na maseneta Richard Onyonka (Kisii) na Fatuma Dullo (Isiolo). Hata hivyo, Bw Kajwang’ hakufichua ni lini Bw Kingi atafika mbele ya kamati hiyo. Aidha, maseneta Omtata na Dullo waliilaumu EACC kwa kile walichodai ni kuchelewesha uchunguzi kuhusu sakata hiyo. Hata hivyo, maafisa wa tume hiyo waliowakilisha Bi Gathungu katika kamati hiyo walisema kuwa kufikia sasa EACC imefaulu kukomboa Sh9 milioni pekee kati ya Sh51 milioni zilizoporwa. Lakini mnamo Julai 2021 Bw Kingi alijiondolea lawama na kusema kuwa serikali yake ndio ilichukua hatua ya kwanza kuwasilisha kesi mahakama na ikapewa kibali cha kukomboa fedha hizo kutoka kwa washukiwa. Aliambia kamati hiyo ya CPAC wakati huo ikiongozwa na seneta wa Migori Ochilo Ayacko (sasa gavana), kwamba EACC ndio ilihujumu juhudi hizo. “Tuliwasilisha kesi kortini na tukafaulu kupewa uamuzi. Lakini kabla ya sisi kupewa kibali cha kukomboa fedha hizo, EACC ilipinga uamuzi huo ikisema kuwa hatukuwa na mamlaka ya kisheria kukomboa fedha zilizoibiwa,” akasema. Bw Mung’aro jana Jumanne aliwaambia wanachama wa CPAC kwamba serikali yake sasa imeziba mianya yote ya ufisadi huku akitoa hakikisho kuwa sakata aina hiyo haitatokea tena chini ya utawala wake. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA WYCLIFFE NYABERI POLISI mjini Kisii wamemkamata mwanamume anayedaiwa kumuua mke wa kaka yake mkubwa pamoja na wanawe wawili kufuatia ugomvi uliozuka baina ya ndugu hao. Inadaiwa Alex Migosi,27, aliamua kulipiza kisasi cha malumbano yao kwa kumuua kikatili shemeji yake pamoja na wanawe wawili, mmoja wa kiume na mwingine wa kike kwa kuwakatakata kwa upanga. Watoto hao walikuwa wa umri wa miaka mitatu na minne. Tukio hilo la kustaajabisha lilifanyika Jumanne katika kata ndogo ya Mesaria, wadi ya Kegogi, eneobunge la Kitutu Chache Kaskazini. Kulingana na kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Marani Benjollife Munuve, mshukiwa amekuwa akizozana na nduguye kwa miaka mingi. “Alipojisalimisha, alitueleza kuwa hiyo ndiyo njia ya pekee aliyoitaka kufuatia ugomvi na nduguye,” Bw Munuve ameambia wanahabari afisini mwake. Habari ambazo zimetufikia kwa sasa ni kuwa wanakijiji wenye ghadhabu wanaiteketeza nyumba ya mshukiwa huyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MAUREEN ONGALA NI afueni kwa maelfu ya wavuvi katika Kaunti ya Kilifi baada ya serikali ya kitaifa kuanza kuwapa mafunzo ambayo wakifuzu wanatunukiwa vyeti vya kuwawezesha kufanya kazi yao rasmi bila vikwazo. Mafunzo hayo yanaendeshwa na Mamlaka ya Masuala ya Baharini (KMA) na wavuvi kutoka kaunti zote sita za Pwani watanufaika. Mbali na Kilifi pia kuna Mombasa, Kwale, Tana River, Taita-Taveta, na Lamu. Kwa miaka mingi, wavuvi hao wamejipata pabaya, wakishikwa wakati wa opereshini zinazofanyika baharani na vitengo mbalimbali kuimarisha usalama. Wakishakamatwa huwa wanashtakiwa kwa kufanya kazi bila vibali. Hali hiyo imekuwa ikichangia pakubwa wavuvi hao kufanya kazi kwa kujifichaficha ili kupata riziki kukimu mahitaji ya familia zao. Mara nyingi wamekuwa wakienda baharini usiku kuhepa kunaswa na pia kuficha maboti yao katika ufuo wa bahari. Kuwa huru kwa wavuvi hao kulitegemea na kukamilishwa kwa operesheni na vitengo hivyo vya usalama. Kuna wakati ambapo wavuvi walikita kambi majini kwa takriban wiki mbili na kipindi hicho chote, baadhi ya wavuvi waligeuka kuwa ombaomba kwa viongozi Pwani. Mwenyekiti wa Muungano wa Manahodha wa Maboti Kilifi Bw Issa Shallo alisema wiki jana kuwa umaskini mkubwa unaowakumba wavuvi katika kaunti hiyo ulichangia pakubwa kwa wao kutokuwa na uwezo wa kulipia maelfu ya pesa kupata mafunzo hayo. “Wavuvi walikuwa hawana uwezo wa kujilipia kupata mafunzo kwa sababu ili kupata cheti hicho kila mmoja alihitaji Sh120,000,” akasema Bw Shallo. Bw Shallo alisema kuwa wakazi wa Kilifi waliwakilisha matakwa yao kwa Rais William Ruto alipokuwa Naibu Rais, katika kampeni zake za kuwa rais katika uchaguzi mkuu wa 2022 na akawaahidi kuwa angepunguza kiwango hicho hadi Sh40,000. Dkt Ruto pia aliahidi ya kuwa wabunge wangefadhili wavuvi hao kupitia kitita cha hazina ya ustawi wa maeneo bunge (NG-CDF) ila haikuwezekana kufuatia kesi iliyowasilishwa kortini kupinga hazina hiyo. “Kesi hiyo ilituvunja mioyo na vijana wengi walikosa matumaini lakini Rais Ruto alitujali na kutenga Sh250 milioni ili vijana wapate mafunzo,” akasema. Kulingana na Bw Shallo, imekuwa tabia tokea enzi ya akina babu kuwa manahodha hawana vibali vya kufanya kazi licha ya kuwa na ujuzi. “Katika hali hii, serikali haiwezi kukutambua kwamba wewe ni nahodha kwa sababu huna kibali,” akasema. Bw Shallo alieleza kuwa licha ya Halmashauri ya Bandari Nchini (KPA) kuendeleza zoezi na kuwapa vibali baada ya mafunzo, ni idadi ndogo sana iliweza kugharimia. Alisema kuwa takribani wavuvi 10 pekee katika Kaunti ya Kilifi ndio walikuwa na vibali hivyo. Kaunti ya Kilifi ina vitengo 17 vya Usimamizi wa Fuo za Bahari (BMU) kutokea Mtwapa hadi Ngomeni katika eneobunge la Magarini na zaidi ya wavuvi 6,000. Alieleza kuwa vibali hivyo vya wavuvi ni vya kiwango cha chini lakini ambavyo vitawawezesha kuwa katika bahari nchini tu. Alisema kuna vingine ambavyo huwapa uwezo wa kuzunguka Afrika Mashariki na hata zaidi ya hapo kimataifa. “Wavuvi wetu walikuwa wanahangaika sana na mapato yao yalikuwa ya chini lakini sasa ni afueni kwani watakuwa huru,” akasema. Bw Chivatsi Ngala ambaye anasema kufikia sasa amefanya kazi ya uvuvi kwa takriban miaka 15 anafichua imekuwa ni safari yenye changamoto tele kwa kukosa vibali. “Tulikuwa tunafanya kazi kiharamu lakini kwa sasa tunashukuru serikali kwa kutupa mafunzo,” akasema Bw Ngala. Alieleza kuwa hali hiyo ilichangia umaskini miongoni mwao. Mara kwa mara waliomba serikali ya kitaifa na ya kaunti kutenga kitita maalum cha pesa kuwasaidia wakati wa misako na upepo mkali wa kusi ambapo hawawezi kuenda baharini. Kapteni Peter Munga kutoka KMA alisema kuwa zoezi hilo la kuwapa mafunzo wavuvi na vijana litachukuwa mwezi mmoja. Tayari limeanza katika kaunti za Kilifi na Mombasa na linatarajiwa kuanza rasmi katika kaunti ya Kwale kisha Taita-Taveta, Lamu, na Tana River. Alisema mafunzo hayo yanaendeshwa kwa ushikiriano wa Kenya Coast Guard na serikali ya kaunti ya Kilifi. “Hawa ni watu ambao wana uzoefu wa kuendesha maboti lakini hawana vibali na tumepewa amri na Rais Ruto tuwape mafunzo, tuwatahini na kuhakikisha wanapata vyeti,” akasema. Mbali na kufanya majaribio baharini, watapitia mafunzo wakiwa darasani. Kapteni Munga alisema wanalenga kuwafunza wavuvi na vijana 500 katika kila mojawapo ya kaunti hizo lakini idadi hiyo itaongezeka kwani hawatafungia mtu yeyote nje. Alitoa wito kwa watu wote wenye uwezo wa kuendesha maboti na hawana vyeti kujitokeza kwa wingi. Bw Munga alisema kuwa mbali na ukosefu wa pesa, wavuvi wengi hawana muda wa kuenda kwa mafunzo kwa sababu za kikazi. Kwa kawaida mafunzo hayo huchukua wiki mbili. Mafunzo hayo yanajumuisha usalama wa wavuvi baharini ikiwemo mawasiliano wakati wa dharura. “Idadi kubwa ya mikasa inayotokea baharini ni kwa sababu ya kubeba mizigo au shehena kiwango cha juu, kutokuwa na vifaa vya usalama na mawasiliano duni,” akaeleza. Kwa upande wake Afisa wa Operesheni na Masuala ya Leba katika KMA Bw Ali Mohamed Mubarak, alisema kuwa eneo la Pwani lina mabaharia wengi ambao wana vyeti walivyopewa na KPA kabla ya kubuniwa kwa KMA. “KMA ilibuniwa na sheria zilibadilika na tutazingatia wale wenye vyeti vya kitambo kwa kuwapa mafunzo na kuwabadishia vyeti,” akasema Bw Mubarak. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA COLLINS OMULO NJAMA ya eneo la Mlima Kenya kutaka chama cha United Democratic Alliance (UDA) kuwa na naibu kiongozi mmoja na eneo hilo kumezea mate wadhifa wa katibu mkuu imezua dhoruba ndani ya chama tawala. Vita vipya vya ubabe wa kisiasa sasa vinatishia uchaguzi wa mashinani wa chama hicho kinachoongozwa na Rais William Ruto unaopangwa mwezi ujao, huku kukiwa na mvutano mkali wa kikanda. Wabunge wa Magharibi wanashinikiza kupanuliwa kwa muundo wa chama kiwe na naibu viongozi wawili huku Kiranja wa Wengi katika Seneti Boni Khalwale akipendekezwa kuwa mmoja wao. Hata hivyo, wenzao wa Mlima Kenya wamepinga mpangilio huo na sasa wanataka kugombania wadhifa wa katibu mkuu, ambao kwa sasa unashikiliwa na aliyekuwa Seneta wa Kakamega Cleophas Malala anayetoka Magharibi huku Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro akipendekezwa. Wabunge wengi wa Mlima Kenya sasa wanadai mpango wa kuwa na zaidi ya naibu mmoja wa kiongozi wa chama ni sehemu ya mpango mpana wa kisiasa unaolenga kupunguza ushawishi wa Naibu Rais Rigathi Gachagua katika siasa za urithi kwenye uchaguzi wa 2032. Haya yanajiri baada ya Bw Khalwale kuanzisha dhoruba katika chama tawala kwa kumuonya Bw Gachagua ajiandae kuona eneo la Magharibi likitawala Ikulu, muhula wa Rais Ruto utakapokamilika 2032 endapo atachaguliwa tena. Seneta huyo wa Kakamega alionya kuwa, hakuna mtu katika ngazi ya kitaifa na kaunti atakayetumia watu wa Magharibi ya Kenya kabla na katika uchaguzi wa 2032. “Naibu Rais anapaswa kunisikiliza na apende asipende, 2032 ni wakati wa urais wa Waluhya,” akasema Dkt Khalwale. Huku kukiwa na hali ya wasiwasi katika nchi nzima chini ya mwezi mmoja kabla ya uchaguzi wa chama, Dkt Khalwale alimshutumu Bw Gachagua kwa kuwapandikiza viongozi aliowataja kuwa ‘wavulana wadogo’ katika maeneo tofauti huku akijinadi kumrithi Rais Ruto. “Huko Mombasa, amepanda Omar Hassan, Magharibi, ana Malala na kuna wengine kadhaa katika maeneo mengine kuwazima wanasiasa wakuu katika maeneo ili wazee wasivuruge azima yake ya urais. Lakini narudia kusema apende asipende, 2032 ni wakati wa urais wa Waluhya,” alisema. Jumapili, viongozi wa Mlima Kenya walisema hawataruhusu muundo wa chama ambao utakuwa na zaidi ya naibu mmoja wa kiongozi wa chama. Gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga alisema nafasi hiyo inafaa kutengewa Bw Gachagua huku akitaka nafasi ya katibu mkuu ipewe kiongozi kutoka eneo hilo. “Lazima kuwe na kiongozi wa chama na naibu kiongozi wa chama. Wengine wanaweza kuwa chochote wanachotaka kuwa na tunadai hivyo kama wanachama wa UDA,” akasema Bw Kahiga. Wadhifa huo kwa sasa unashikiliwa na Bw Gachagua, hata hivyo, kuna ripoti chama hicho kinanuia kuanzisha nafasi nyingine ya naibu kiongozi kuhakikisha usawa wa kieneo. “Tuna kiongozi mmoja wa chama na ni muhimu pia tuwe na naibu kiongozi mmoja wa chama,” alisema Seneta wa Nyeri Wahome Wamatinga. Alisema katiba ya chama hairuhusu manaibu wawili wa chama kwa kuwa hii itasababisha kuundwa kwa vituo vingi vya mamlaka ambavyo vitasababisha migogoro ya kisiasa. Seneta wa Kirinyaga James Murango alisema hakuna haja ya kupanua muundo wa chama ili kuwa na viongozi zaidi wa kanda wakati UDA tayari ina mwonekano wa kitaifa. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MHARIRI
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini.
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na BENSON MATHEKA
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na MASHIRIKA
LONDON, Uingereza
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya... Na ELIZABETH MERAB
WANASAYANSI wanachunguza kuhusu mchipuko wa virusi vipya vya corona aina ya Delta, katika nchi za Amerika, Uingereza,... Na MAUREEN ONGALA
MASAIBU ambayo wagonjwa wa Covid-19 hupitia katika kaunti za Pwani, yameanikwa wazi baada ya kifo cha afisa mkuu wa... SIAGO CECE na ANTHONY KITIMO
UFISADI miongoni mwa baadhi ya maafisa wa serikali katika mpaka wa Kenya na Tanzania, umezidi kuwaweka... Na WAANDISHI WETU
WINGU la maangamizi limetanda kote nchini huku aina mpya ya corona maarufu kama 'Delta' ikiua watu kwa... Na WINNIE ONYANDO
HUENDA visa vya wasafiri kulazimishwa kupima upya corona mpakani mwa Kenya na Tanzania vikakoma baada ya serikali hizo... NA WANGU KANURI
AGIZO la serikali la kudhibiti mkurupuko wa ugonjwa wa corona mwaka jana limewashurutisha Wakenya wengi kufanyia kazi... Na Titus Ominde
VIONGOZI wa kidini Kaskazini mwa Rift Valley (North Rift) wameshutumu wanasiasa kwa kupepeta usambazaji wa virusi vya... Na WANTO WARUI
Huku wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiripoti katika shule zao mpya za sekondari hii leo, kuna uwezekano wa maambukizi... Na CHARLES WASONGA
NAKUBALIANA na kauli ya maafisa wa afya katika kaunti ya Nairobi kwamba wanasiasa ndio wanachochea ongezeko la visa... Na SAMMY WAWERU
DICKSON Muceri amekuwa mkazi wa Nairobi kwa muda wa miaka kadhaa ila sasa kitovu hicho cha jiji kuu la nchi hakikaliki... Na MARY WANGARI
WANASAYANSI wamethibitisha kuwa kuchelewesha upokeaji dozi ya pili ya chanjo ya Covid-19 kwa kiasi cha miezi 10 baada ya... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na KINYUA BIN KINGORI
WAKATI huu viongozi wa kisiasa wameanza mapema kampeni zao kwa kuzuru maeneo mbalimbali nchini, ili kushawishi... Na WANDERI KAMAU
KULINGANA na Ripoti ya Jaji Mstaafu Akilano Akiwumi (1997) kuhusu chimbuko la ghasia za kikabila nchini, wanasiasa ndio... Na WANTO WARUI
KWA mara nyingine tena tuzo inayoenziwa sana kote ulimwenguni imerudi katika eneo letu la Afrika Mashariki mara hii... Na DOUGLAS MUTUA
MWAFRIKA akiwajibishwa na Mzungu hupiga kamsa na kudai anaonewa, ati msingi wa maonevu ni ubaguzi wa rangi... Na WANDERI KAMAU
MOJA ya changamoto kuu zinazokikumba kizazi cha sasa nchini ni ukosefu wa ufahamu wa lugha zao asili.
Ingawa lugha... Na KINYUA BIN KINGORI
JUHUDI za kuhakikisha taifa limefanikiwa kupiga vita ufisadi lazima ziendeshwe kuambatana na Katiba, bila njama... Na WANDERI KAMAU
UFICHUZI wa sakata ambapo watu maarufu duniani wamekuwa wakificha mabilioni ya fedha katika akaunti za siri ng’ambo... Na FAUSTINE NGILA
NINA imani kuwa iwapo kufikia sasa hujawahi kuelewa teknolojia ya blokcheni, leo utaelewa kwa kuwa jana uliathirika... Na CHARLES WASONGA