text
stringlengths 3
16.2k
|
---|
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti, baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

KALUME KAZUNGU, JURGEN NAMBEKA NA CECE SIAGO SEHEMU mbalimbali katika ukanda wa Pwani zimeathiriwa na mvua ya El-Nino inayoendelea kushuhudiwa katika sehemu tofauti nchini. Katika kaunti ya Mombasa, maeneo ya Bamburi, Utange, Kiembeni wakazi walipatwa na taabu baada ya mafuriko kuwazuia hata kutoka nyumbani kwao. Maelfu ya wakazi walisambaza picha mitandaoni kuelezea gadhabu yao kuhusu mvua hiyo iliyoanika mfumo duni wa usambazaji majitaka Kaunti ya Mombasa. Katika eneo la Bangladesh, msichana wa Kidato cha nne aliaga dunia baada ya kukanyaga waya wa umeme uliokuwa majini. Kulingana na afisa wa elimu wa kaunti ndogo ya Jomvu Bi Maimuna Ahmed, mwendazake alikuwa amekamilisha mtihani wake wa mwisho wa sekondari(KCSE). Kwenye eneo la Majajani Kaunti ya Kilifi, mzee mmoja aliaga dunia baada ya kuporomokewa na nyumba. “Tulimwomba Bw Kenga Baya aende akalale kwa wajukuu pamoja na familia yake ila akakataa kuwa hawezi kulala kwa wajukuu zake. Jamaa zake walikubali wito ila yeye aliyebaki tuliamkia habari za kuwa nyumba ilikuwa imeporomoka,” akasema jamaa yake Bw Sammy Kashindo. Katika Kaunti ya Lamu, karibu wakazi 3,000 wa vijiji vya Pandanguo na Jima, tarafa ya Witu, walibaki katika hofu ya ukosefu wa chakula baada ya barabara yao ya pekee ya Pandanguo kuelekea Witu kukatika katika eneo la Ziwa la Kiboko. Hii ni baada ya mafuriko yaliyochangiwa na mvua kubwa, inayoendelea kunyesha eneo hilo kwa karibu juma zima sasa. Ikumbukwe kuwa barabara hiyo ndiyo kiunzi cha pekee kwa wakazi wa Pandanguo na Jima kufikia maduka na bidhaa yapatikanayo mji wa Witu. Akizungumza na Taifa Leo Dijitali kwa njia ya simu, Mzee wa Nyumba Kumi katika kijiji cha Pandanguo, Bw Ali Sharuti alisema familia nyingi zimekuwa zikitatizika kupata chakula, ikizingatiwa kuwa eneo la kipekee kujinunulia bidhaa ni mji Wa Witu. Bw Sharuti aliiomba serikali ya kaunti kushirikiana na ile ya kitaifa na mashirika, ikiwemo lile la Msalaba Mwekundu, kuwafikishia misaada ya chakula na vyandarua. “Barabara yetu imekatika kumaanisha hatuwezi kufikia maduka kujinunulia chakula. Tunaomba hata kama ni ndege kupitia ufadhili wa kaunti, serikali kuu na mashirika itufikishie vyakula vya msaada, vyandarua na dawa za maji. Tunahofia baa la njaa na mlipuko wa maradhi vijijini mwetu,” akasema Bw Sharuti. Kule Kwale, usafiri katika barabara kuu ya Likoni kuelekea Lungalunga ulikwama kwa siku ya pili huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha Kaunti ya Kwale na kusababisha mafuriko. Mabasi, matrela na mamia ya abiria walilazimika kukesha usiku karibu na Daraja la Ramisi baada ya mto huo kuvunja kingo zake na kufanya barabara kutopitika. Kulingana na Kamishna wa Kaunti ya Kwale, Michael Meru, mvua kubwa inayoendelea kunyesha kwa siku ya tatu sasa, imesababisha mito yote katika kaunti hiyo kufurika. Mito hiyo ni Ramisi, Mkurumudzi, Umbea, Mwena na Mbadi, huku akitoa onyo kwa wakazi wanaoishi sehemu za chini kuchukua tahadhari. Katika eneo la Kinango, abiria waliokuwa kwenye gari la kibinafsi walinusurika kifo wakati gari lao lilisombwa na mafuriko walipokuwa wakijaribu kuvuka daraja lililofurika la Mto Mbadi. Barabara ya Kinango kuelekea Kwale pia iliathirika magari yakikwama kwenye matope. Hali ilikuwa iyo hiyo katika Kaunti ya Tana River. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA WANDERI KAMAU RAIS George Weah wa Liberia amekubali kushindwa na mwaniaji urais wa Upinzani, Joseph Boakai, kwenye matokeo ya kura yaliyoendelea kutolewa Ijumaa jioni, Novemba 17, 2023 na tume ya uchaguzi nchini humo. Bw Weah, ambaye alikuwa ameliongoza taifa hilo tangu 2017, alishindwa na Boakai, aliyezoa asilimia 50.9 ya kura huku yeye akipata asilimia 49.1 ya matokeo ya kura yaliyokuwa yametolewa. Hiyo ilikuwa duru ya pili ya uchaguzi, baada ya mshindi wa moja kwa moja kukosa kupatikana kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 10, 2023. “Kulingana na matokeo ambayo yametangazwa, ijapokuwa si yote….Yanaonyesha kuwa Boakai anaongoza kwa kiwango ambacho hatuwezi kumfikia,” akasema Bw Weah kwenye hotuba aliyotoa kupitia kituo rasmi cha redio cha serikali. “Chama cha Congress for Democratic Change (CDC) kimepoteza uchaguzi huo, lakini Liberia imeibuka mshindi. Huu ni wakati wa kuonyesha shukrani hata ikiwa tumeshindwa. Ni wakati wa kuweka mbele maslahi ya kitaifa kuliko ya mtu binafsi,” akasema Rais huyo anayeondoka. Ushindi wa Bw Boakai unaonekana kuwa kisasi cha kisiasa dhidi ya Weah, kwani alimshinda kwenye duru ya pili ya uchaguzi wa urais iliyofanyika 2017. Kulingana na matokeo hayo, Boakai alikuwa akiongoza kwa zaidi ya kura 28, 000. Amerika ni miongoni mwa mataifa ambayo tayari yametuma ujumbe wa pongezi wa Boakai. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA CECIL ODONGO UMOJA wa Afrika (AU) umesema uvumbuzi wa kiteknolojia ndiyo nguzo kuu ambayo inastahili kukumbatiwa na vijana kusuluhisha matatizo mengi yanayozonga Bara la Afrika. Mkurugenzi wa Masuala ya Wanawake, Jinsia na Vijana kwenye AU Prudence Ngwenya Ijumaa, Novemba 17, 2023 alisema vijana sasa wanastahili kukumbatia matumizi ya teknolojia ili kusuluhisha matatizo yanayowakabili. Ni kupitia njia hiyo Afrika itastawi kiuchumi na kupiga hatua kimaendeleo. “Mambo sasa yanabadilika kila kukicha na ni uvumbuzi wa kiteknolojia utasaidia kusuluhisha matatizo ibuka. Huu ndio mwelekeo ambao unastahili kukumbatiwa na vijana,” akaongeza Bi Ngwenya. Afisa huyo wa AU alikuwa akizungumza jana kwenye Hoteli ya Boma alipofungua Kongamano la siku tatu la YMCA ambalo lilishirikisha mataifa 24 ya Afrika. “Tunaendeleza miradi mbalimbali ili vijana wawe mabalozi bora. Pia tunaendesha mafunzo ya kiufundi ili kupata njia bora ya kuwasaidia vijana wanaopitia changamoto mbalimbali,” akasema Bw Musima. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA STEVE OTIENO POLISI wa cheo cha Inspekta amegeuzwa mahabusu katika kituo cha polisi cha Ruiru, Kiambu, baada ya kukamatwa akijaribu kuibia mteja kwenye duka la M-pesa akitumia bastola. Nahason Ekidor alikamatwa na walinzi wa benki ya Equity mjini Ruiru, alipokuwa akitoroka umati wa watu waliojawa na hasira. Kwenye tukio hilo la Jumamosi asubuhi, mwanaume aliyetambuliwa kama Peter Kimani ambaye pia anamiliki duka la M-pesa, alikuwa ameenda kuweka Sh200,000 kwa duka la M-pesa linalohudumiwa na Bi Mary Anne Njoki. Ripoti za polisi zinasema punde tu Bw Kimani alipofika kwenye duka la M-pesa, mwanaume aliyekuwa na bastola aliingia humo na kumwamuru ampe pesa alizokuwa akiweka. Bw Kimani aliambia Taifa Leo kwamba alikuwa tayari amempokeza Bi Njoki pesa hizo. Kwa kuwa alikuwa karibu na mlango wa duka hilo, alitoka nje mbio na kuanza kupiga mayowe. Naye Bi Njoki alipiga nduru kutaka usaidizi zaidi, kwa kuwa alikuwa amechwa ndani ya duka lake pamoja na mwanaume huyo mwenye silaha. Umati uliitikia wito wa kelele na kuanza kufika sukani hapo. Alipogundua kuwa hakuwa na uwezo wa kukabiliana na umati uliokuwa unazidi kuongezeka, mwanaume huyo alifyatua risasi hewani na kuamua kutorokea usalama wake kwenye benki ya Equity. Hapo, walinzi kwenye benki walimkamata na kumpokonya bastola hiyo. Koplo Thomas Mungai aliiwasilisha bastola hiyo kwa Kamanda wa DCI katika kituo cha polisi cha Ruiru. Polisi waliokuwa karibu na eneo la tukio walimchukua Bw Ekidor na kumfungia seli, huku umati ukomba nafasi umfunze adabu. Uchunguzi wa awali ulithibitisha kuwa Ekidor ni afisa wa polisi wa kitengo cha Recce cha Ruiru. Kitengo hicho kuwa na maafisa wa polisi wanaohusika na usalama wa watu mashuhuri, hasa Rais na naibu wake. Bastola yake aina ya glock ambayo kawaida hubeba risasi 15, ilikuwa na risasi 14. Polisi pia walifanikiwa kupata Sh54,100, huku wakiendeleza uchunguzi wa kisa hicho. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

Na KEVIN MUTAI MADIWANI wa Kaunti ya Meru wamekerwa na pendekeza la gavana wa kaunti hiyo Kawira Mwangaza kwamba serikali hiyo ivunjwe na viongozi wote kutafuta viti upya kupitia kwa kura. Sehemu ya madiwani 59 wanaopinga uongozi wa gavana huyo wanasema kuwa watashughulikia ombi la watu 22 wanaotaka serikali ya kaunti hiyo ivunjwe. Madiwani hao wanataka kuwasilisha hoja ya kuwatimua afisini mawaziri kadha wa Gavana Mwangaza ili kulemaza serikali yake. Madiwani hao wako Mombasa kwa warsha ya mafunzo na kujadili masuala kadha yanayowahusu yakiwemo majaribio mawili ya kumng’oa mamlakani gavana wao. Majaribio ya Taifa Leo ya kupata kauli kutoka kwa madiwani hao yalifeli. Ni diwani wa wadi ya Abogeta Magharibi Dennis Kiogora alizungumzia suala hilo kwa njia ya simu. Bw Kiogora akasema: “Raia wako na haki ya kuwasilisha maombi yoyote katika bunge lolote, liwe la kaunti au bunge la kitaifa. Na hauwezi kuwazuia kufanya hivyo, hivyo maombi hayo yakifika mbele yetu tutayashughulikia.” Upande wa wengi katika bunge la Kaunti ya Meru umetaja hatua ya Bi Mwangaza kushinikiza kuvunjwa kwa serikali hiyo kama ambayo ni ngumu kutekelezwa kwani utaratibu wake ni mrefu. Madiwani wa mrengo huo wanasema mchakato huo unaweza kudumu kwa miezi mingi mno kutokana na hatua za kisheria na hali kwamba uteuzi wa makamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) haujafanywa. Mnamo Alhamisi Gavana Mwangaza alisema amepokea mapendekezo kutoka kwa mashirika mbalimbali yanayotaka kuanzisha zoezi la ukusanyaji wa sahihi za kufanikisha kuvunjwa kwa serikali ya Kaunti ya Meru. “Ikiwa masuala yanayoibua kutoelewana kati ya viongozi hayatatatuliwa, nitaunga mkono pendekezo la kuvunjwa kwa serikali hii,” Gavana Mwangaza akasema kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio kinachopeperusha matangazo kwa lugha ya Kimeru. Kipengele cha 192 cha Katiba kinatoa utaratibu kuhusu njia za kusimamisha kwa muda serikali ya kaunti nchini Kenya. Aidha, kinasema kuwa Rais anaweza kusimamisha kwa muda serikali ya kaunti kwa sababu mbili; mzozo wa ndani ambao unahujumu utendakazi wake, kulipuka kwa vita au hali nyingi maalum. Kulingana na kipengele hicho, sharti sahihi zikusanywe kutoka kwa angalau asilimia 10 ya wapiga kura waliosajiliwa katika kaunti husika. Sahihi hizo sharti zithibitishwe na IEBC. Baada ya hapo, tume hiyo itawasilisha pendekezo hilo kwa Rais ambaye atabuni tume huru ya uchunguzi kuchunguza madai ya kutaka serikali ya kaunti ivunjwe. Ikiwa Rais ataridhika kuwa sababu zilizowasilishwa za kutaka kaunti ivunjwe zina mashiko, atawasilisha ripoti katika Seneti ili ijadiliwe na kupitishwa. “Utaratibu huo unaweza kuchukua muda wa zaidi ya miezi 18 hivi. Huu ni muda mrefu zaidi na ambao utachosha hata wakazi wa Meru,” akasema Bw Kiogora. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

Na CHARLES WASONGA KIONGOZI wa wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wah amepuuzilia mbali madai ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwamba mkataba kati ya Kenya, Saudi Arabia na Umoja wa Milki ya Kiarabu (UAE) kuhusu uuzaji mafuta kwa Kenya ulisheheni ufisadi. Kwenye taarifa aliyotoa sasa chache baada ya Bw Odinga kutoa madai hayo Novemba 16, 2023, mbunge huyo wa Kikuyu alisema hayana msingi wowote “ni propanda na uvumi wa kisiasa usio na msingi wowote.” “Ni wazi kuwa kile alichodai ni ufichuzi ni propaganda zake za kawaida zisizo na chembe yoyote ya ukweli,” Bw Ichung’wa akasema kwenye taarifa kwa vyombo vya habari. “Wizara ya Kawi na Mafuta ilitia saini mkataba na kampuni za serikali za Mashariki ya Kati (Saudi Arabia na UAE). Ikiwa hiyo sio mkataba kati ya serikali na serikali basi sijui Odinga anataka kuelezwa vipi,” akauliza. Bw Ichung’wah pia amepuuzilia mbali madai ya Bw Odinga kuwa kampuni za Gulf Energy, Galana Oil Kenya Ltd na Oryx Energy Kenya Ltd ni maajenti wa serikali ya Kenya. “Kampuni hizi zilizoleta mafuta nchini zilikodishwa na kampuni za Aramco na ADNOC za Saudi Arabia na UAE, mtawalia. Sio haja ya Kenya kujua zile kampuni za humu nchini ambazo kampuni hizo mbili zilitumia kufikisha mafuta yao nchini,” akaeleza. Awali, Bw Odinga alidai kuwa kampuni hizo zilikuwa na uhusiano wa karibu na maafisa wakuu katika serikali na kwamba ziliuzia Kenya mafuta kwa bei ya juu ili kufaidi watu hao. Bw Odinga alisema mkataba huo pia ulikuwa na njama ya kuzikinga kampuni hizo zisilipe ushuru wa asilimia 30 kwa bidhaa hizo. “Huo mkataba ulijaa ufisadi. Ulikuwa ni njama ya kuzuia kampuni hizo kulipa ushuru. Na mzigo wa ushuru huo usiolipwa unapitishwa kwa Wakenya wanaponunua mafuta kwa bei ya juu kupita kiasi,” kiongozi huyo wa Azimio akawaambia wanahabari jijini Nairobi. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

Na BENSON MATHEKA KIONGOZI wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga, sasa anataka mkataba wa ununuzi wa mafuta baina ya serikali ya Kenya na mataifa mawili ya Kiarabu ufutwe na waliohusika kuchunguzwa na kufutwa kazi serikalini. Bw Odinga anasema mpango huo uliotangazwa na Rais William Ruto Aprili mwaka huu ni kashfa kubwa ambayo imechangia gharama ya juu ya maisha nchini. Mnamo Aprili mwaka huu, Rais William Ruto alitangaza kuwa, serikali yake ilitia saini Mkataba wa Makubaliano kati ya Serikali ya Kenya na Saudi Arabia na Milki ya Kiarabu kuuzia Kenya mafuta kwa bei nafuu. Ruto aliambia taifa kuwa, baadhi ya maafisa katika utawala wake walifanikiwa kuweka pamoja mpango ambao ungepunguza gharama ya mafuta nchini. “Leo, tunaweza kununua mafuta kwa shilingi za Kenya, jambo ambalo watu wengi hawakuwahi kufikiria kuwa lingewezekana. Kwa kweli, katika muda wa mwezi mmoja ujao au zaidi, utaona kiwango cha ubadilishaji kikishuka kwa njia ya ajabu sana. Kwa makadirio yangu, katika miezi michache ijayo, kiwango cha ubadilishaji kitakuwa chini ya Sh120, hata kinaweza kuwa Ksh115,” rais alisema kuhusu mpango huo. Lakini Raila anasema Kenya haikutia saini mkataba wowote na Saudi Arabia au UAE bali na kampuni za serikali za mafuta za petroli katika Mashariki ya Kati. “Wizara ya Nishati na Petroli ilitia saini mkataba na kampuni za petroli zinazomilikiwa na serikali katika Mashariki ya Kati. Kwa nini Ruto alichagua kutambulisha mpango huo kama wa serikali kwa serikali? Hii ni ishara ya kwanza ya ufisadi katika mpango huu,” kiongozi huyo wa ODM alisema. Bw Odinga alisema kubatiza mpango huo kuwa wa serikali kwa serikali kulikusudiwa kukinga kampuni tatu za Kenya kutokana na kulipa asilimia 30 ya ushuru wa kampuni. Kulingana na Raila, mkataba huo haujashughulikia matatizo yoyote ambayo Ruto alisema yangeshughulikia. “Gharama ya mafuta ilipanda hata zaidi baada ya mpango huo. Kwa nini hali imekuwa mbaya zaidi tangu mpango huo utangazwe? Mpango huo ulikuwa ulaghai ambao sasa tunataka ufichuzi na uwajibikaji kamili. Ni kashfa kubwa,” alidai. Raila aliitaka serikali kufutilia mbali kandarasi hiyo mara moja na kurejelea Mfumo wa Zabuni ya wazi ambao anasema ulihakikisha upatikanaji wa bidhaa za petroli kwa ushindani. Pia anataka Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi kuchunguza “kwa nini tuliingia katika mpango huu na nani ananufaika nao.” Zaidi ya hayo, Raila anaomba shirika la kupambana na ufisadi kuhakikisha waliohusika wanalipa hasara waliyoingiza nchi na kufutwa kaziKiongozi huyo wa chama cha ODM alishangaa kwa nini gharama ya mafuta haijashuka tangu mkataba huo utiwe saini na kwa nini thamani ya shilingi ya Kenya imeendelea kudidimia dhidi ya dola. “Ni wazi mpango huo haujashughulikia matatizo yoyote ambayo Ruto alisema ingeshughulikia. Ruto alipoanzisha mpango huu, kiwango cha ubadilishaji cha dola ya Amerika hadi shilingi ya Kenya kilikuwa Sh132. Leo, miezi sita baadaye, ni Ksh159 kwa dola. Gharama ya mafuta ilipanda sana baada ya mpango huo,” alisema. “Tunamtaka Ruto kuchapisha mkataba huu. Hakuna anayejua jinsi Gulf Energy, Galana Oil Kenya Ltd na Oryx Energies Kenya Limited zilivyoteuliwa kushughulikia usambazaji wa humu nchini,” akasema. Ili kupunguza gharama za juu za mafuta, alidai serikali lazima irejeshe ushuru wa ziada wa thamani hadi asilimia 8 kutoka asilimia 16 iliyoanzishwa na Sheria ya Fedha ya 2023. “Serikali lazima itangaze hadharani kile inadai ni mkataba kati ya Kenya na Saudi Arabia na Milki ya Kiarabu na Wizara ya Nishati na Petroli lazima iweke hadharani makubaliano ambayo ilitia saini na kampuni za mafuta,” alisema Waziri Mkuu huyo wa zamani. Pia, anataka Wizara ya Nishati na Petroli kutangaza hadharani Mkataba wa Ununuzi iliyotia saini na kampuni za mafuta na EACC na Idara ya Upelelezi wa Jinai kuchunguza muundo wa bei wa kampuni hizo tatu za mafuta. “Lazima Mamlaka ya Ushuru ya Kenya ijitokeze wazi na kueleza ni kwa nini zinawezeshwa kukwepa mabilioni ya ushuru huku Wakenya wa kawaida wakinyanyaswa kwa ushuru,” alisema. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA FRIDAH OKACHI KIONGOZI wa Chama cha Narc Kenya Martha Karua ametishia kurejesha Wakenya barabarani iwapo serikali haitasikiza matakwa ya Azimio kuhusu gharama ya maisha. Bi Karua alisema muafaka wa mazungumzo yaliyofanyika Bomas huenda usipatikane, iwapo serikali itashikilia msimamo kuwa gharama ya maisha si suala la dharura. Akizungumza Alhamisi, Novemba 16, 2023 katika makao makuu ya chama cha Narc Kenya jijini Nairobi, Bi Karua alisema gharama ya maisha iko juu, lakini serikali badala yake inaendeleza mipango iliyo na kashfa za ufisadi. Alidai Rais William Ruto amekuwa akiwateua wale wanaokabiliwa na mashataka ya ufisadi na kuamrisha Afisi ya Mkurungezi wa Mashataka kuondoa kesi hizo. “Jambo la kwanza serikali imepuuza Katiba na sheria za Kenya. Hali hii imezidi. Watumishi wa umma wanaokabiliwa na uhalifu, kesi zao zinaondolewa na kupewa kazi katika afisi za umma,” alisema Bi Karua. Alilaumu Kiongozi wa Mashtaka kuhujumu kesi za ufisadi na kukosa kutoa ushahidi wowote dhidi ya maafisa wakuu wanaokabiliwa na uhalifu. “Tunakumbuka vizuri kesi ya mabwawa ya Kimwarer na Arror. Walitoa hati ya kukamwatwa aliyekuwa Waziri wa Kilimo Peter Munya kukosa kwenda kutoa ushahidi, ilhai upande wa mashtaka haukuwa umemfahamisha. Bw Munya alijipeleka mahakamani na kusema yupo tayari kutoa ushahidi na kiongozi wa mashtaka alisema hana maswali ya kumuuliza. Kesi nyingi zinahujumiwa na wanaowekwa huru ni wanatoka jamii ya Rais,” aliendelea. Alikashifu vitisho vinavyotolewa na Rais William Ruto kuwa ‘Mambo ni Matatu’ akisema ni tishio la kuuawa kwa raia kwa njia isiyoeleweka. “Hili ni tishio la kuua kutoka kwa Bw Ruto. Jambo la pili ni kuondoa kesi mahakamani. Shinikizo ya aina hii haikubaliki,” alisema Bi Karua. Vile vile, alimtetea mfanyabiashara Ann Njeri, kwenye sakata ya kutoweka kwa mafuta ya Sh17 bilioni, akisema kutekwa nyara ilikuwa njama ya serikali kuingilia ushahidi. “Mfanyabiashara huyu hajulikani. Sijui mafuta hayo ni ya nani. Serikali haitaki tujue ni nani anamiliki?” alisema. Alidai kuwepo ubaguzi katika ufadhili wa elimu na kutaka elimu ya shule za msingi na sekondari ifadhiliwe vilivyo. Alisema ni kwa njia hiyo ambapo viwango vya elimu nchini vitarejeshwa mahali pake kama awali, ili kuepuka wanafunzi kusalia nyumbani. “Suala la unga ni muhimu lakini pia elimu hapa nchini inadunishwa. Tunataka kuona ufadhili wa wanafunzi wa vyuo vikuu kupitia mikopo kwa wanafunzi. Wanafunzi wote wapokee mkopo huo na si kubagua jinisi serikali ya Kenya kwanza inataka kuazisha, tunakataa kubaguliwa kwa kila njia,” alisema Bi Karua. |
Tags |
You can share this post! |
Previous article |
Serikali yatangaza kusimamisha kazi maafisa wakuu sita wa... |
Next article |
Haiya, sikujua binti yangu ni tajiri hivi, asema mamake... |
T L |
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

Na FATUMA BARIKI Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei ametangaza kwamba maafisa sita wakuu wa mashirika ya kiserikali, mhasibu na maafisa 67 wa polisi wamesimamishwa kazi kutokana na tuhuma za ufisadi. Kulingana na taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed, Mkuu huyo wa Utumishi wa Umma ameeleza kwamba wamepokea mapendekezo kutoka kwa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, EACC. Afisa Mkuu Mtendaji wa shirika la Tanathi Fredrick Mwamati ni wa kwanza kupendekezwa asimamishwe kazi, kulingana na ombi lililotumwa kwa Waziri wa Maji na Unyunyuziaji Zachariah Njeru. Bw Mwamati ambaye ni mhandisi anashukiwa kuhusika na utoaji zabuni kwa njia ya kifisadi kwenye mradi wa usambazaji maji wa eneo la kibiashara la Leather Industrial Park. Wa pili ambaye Waziri wa Leba Florence Bore anashauriwa kumsimamisha kazi ni Stephen Ogenga, ambaye ni mkuu wa Idara ya Mafunzo ya Kitaifa ya Kiviwanda (NITA) kwa tuhuma za ufisadi katika ununuzi na utoaji zabuni. Vile vile, Stanvas Ong’alo ambaye ni kaimu mkurugenzi mkuu wa Makavazi ya Kitaifa amesimamishwa kazi kwa tuhuma za wizi wa Sh490 milioni. Naye Bw Benjamin Kai Chilumo wa Huduma Centre ambaye yuko chini ya Waziri wa Utumishi wa Umma Moses Kuria, ameambiwa aache kazi mara moja kutokana na madai ya kuhusika katika wizi wa pesa alipokuwa anahudumu kama Afisa Mkuu wa Fedha katika Kaunti ya Kilifi. Mwingine aliyesimamishwa kazi ni Afisa Mkuu wa Bomas Of Kenya, Peter Gitaa Koria, ambaye anatuhumiwa kushiriki ununuzi visivyo kwenye shirika lake hilo ambalo limo chini ya Waziri Aisha Jumwa. Vilevile, Anthony Wamukota ambaye ni Meneja Msimamizi wa kitengo cha Ubunifu na Ujenzi katika KETRACO amesimamishwa kazi kutokana na ubadhirifu wa mali ya umma katika ujenzi wa Kituo cha kuzalisha nguvu za umeme cha 400KV Loiyangalani. Esther Wanjiru Chege ambaye ni mhasibu wa shirika la KeRRA pia amesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuwa na utajiri usioelezeka. Aidha, Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome ametakiwa kuachilia maafisa 67 ambao wamehusishwa na ufisadi. EACC inasema kwamba kuendelea kuwepo kwa maafisa hao kazini kutahujumu uchunguzi na mashtaka yanayowakabili. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

Na CHARLES WASONGA KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini, Kenya Power sasa inashirikiana na maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) katika mpango wake wa kuzima uharibifu na wizi wa mitambo yake kuzuia visa vya kupotea kwa kawi hiyo. Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Joseph Siror amesema kuwa DCI imewatuma maafisa wake 42 kushirikiana na maafisa wa kampuni hiyo kuzima wizi wa nyaya za stima, uharifu wa transfoma na kuwafurusha watu waliojenga vibanda sehemu za kupitishiwa nyaya za stima. “Katika mwaka wa kifedha uliopita, kampuni hiyo iliandikisha ongezeko la visa vya uharibifu wa transfoma kwa kima cha asilimia 46 ambapo jumla ya transfoma 242 ziliharibiwa ikilinganishwa na 165 iliyoharibiwa mwaka uliotangulia. Visa kama hivi pamoja na wizi wa nyaya ndivyo huchangia stima kupotea na kuathiri wateja wetu,” Bw Siror akasema kwenye taarifa Alhamisi, Novemba 16, 2023. “Hii ndio maana kampuni hii sasa inashirikiana na asasi mbalimbali, ikiwemo DCI kupambana na maovu haya. Tunaamini ushirikiano huu na DCI utaimarisha uwezo wetu wa kuzima wizi wa mitambo yetu na maovu mengine kwa kukumbatia mfumo wa kijasusi,” Bw Siror akaongeza. Alieleza kando na visa hivyo kuchangia Kenya Power kupata hasara, uharibifu wa transfoma na wizi wa stima unaweka hatarini maisha ya wananchi. “Vile vile, maovu haya yanaathiri pakubwa ukuaji wa kiuchumi kwa sababu kawi ni hitaji kubwa katika ufanikishaji wa shughuli za uzalishaji wa bidhaa,” Bw Siror akasema. Kulingana na afisa huyo, tangu Julai mwaka jana, jumla ya watu 1, 026 wamekamatwa sehemu mbalimbali nchini kwa kuhusika katika uvurugaji wa mtandao wa usambazaji umeme. Watu 472 miongoni mwao walikuwa ni washukiwa wa uharibifu wa transfoma na mitambo mingine ya Kenya Power. Bw Siror aliongeza kuwa watu 320 wamekamatwa kwa tuhuma za wizi wa stima huku 33 walikitiwa mbaroni kwa kujenga vibanda katika maeneo yaliyotengewa kupitishiwa nyaya za stima. Jumamosi wiki jana, stima zilipotea sehemu nyingi nchini, tukio ambalo Kenya Power ilisema lilichangiwa na hitilafu katika kituo chake cha Olkaria. Kilikuwa ni kisa cha tano cha stima kupotea kote nchini ndani ya miaka mitatu. Mnamo Agosti 20, mwaka huu stima zilipotea kote nchini kwa zaidi ya saa 20, hali iliyochangia wateja kupata hasara kubwa. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

Na CHARLES WASONGA BUNGE la Kitaifa limeidhinisha mpango wa serikali wa kutuma maafisa 1,000 wa polisi kulinda usalama nchini Haiti. Katika kura waliopiga Alhamisi asubuhi, wabunge walipitisha ripoti ya kamati ya pamoja ya Bunge hilo na Seneti iliyopendekeza kuwa bunge likubali ombi hilo la serikali. Wabunge wametoa idhini hiyo licha ya kesi iliyowasilishwa mahakamani na kiongozi wa chama cha Thirdway Alliance Ekuru Aukot kupinga kupelekwa kwa maafisa hao Haiti. Kesi hiyo haijaamuliwa. “Baada ya kamati husika za usalama kukagua wajibu wa serikali kwa Umoja wa Mataifa, sheria zilizoko, mawasilisho katika vikao vya kukusanya maoni kutoka kwa umma na wadau, inapendekeza kuwa bunge liidhinishe ombi la kuwatuma maafisa wa polisi Haiti kulingana na hitaji la Katiba,” kamati hiyo ya pamoja ikasema. Kamati hiyo iliongozwa kwa pamoja na mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Kitaifa kuhusu Usalama Gabriel Tongoyo na mwenyekiti wa Kamati ya Usalama katika Seneti William Cheptumo. Polisi hao 1,000 wanatarajiwa kuongoza kikosi cha walinda usalama kutoka mataifa mbalimbali (MSS) watakaotumwa Haiti kusaidiana na maafisa wa nchi hiyo kupambana na magenge ya wahalifu waliosambaratisha usalama nchini humo. Ripoti hiyo pia itawasilishwa katika Seneti juma lijalo ambako inatarajiwa kupitishwa, kwa misingi kuwa maseneta wa Kenya Kwanza ni wengi. Mwezi jana, baraza la mawaziri liliidhinisha mpango wa Kenya kutuma polisi wake nchini Haiti, siku chache baada Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) kutoa kibali. Wiki jana, Waziri wa Usalama Kithure Kindiki alisema kuwa serikali ya Kenya itatumia Sh19 bilioni kugharamia mpango wa kuwatuma polisi wake Haiti hapo mwakani. Hata hivyo, alieleza kuwa Umoja wa Mataifa utairejeshea Kenya pesa hizo baada “ya kuidhinisha bajeti ya mpango wa kulinda usalama Haiti.” You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA MHARIRI |
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI |
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI |
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI |
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI |
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI |
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI |
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI |
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI |
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI |
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini. |
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI |
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI |
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na BENSON MATHEKA |
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU |
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA |
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA |
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA |
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU |
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA |
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO |
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI |
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA |
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON |
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA |
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na MASHIRIKA |
LONDON, Uingereza |
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya... Na ELIZABETH MERAB |
WANASAYANSI wanachunguza kuhusu mchipuko wa virusi vipya vya corona aina ya Delta, katika nchi za Amerika, Uingereza,... Na MAUREEN ONGALA |
MASAIBU ambayo wagonjwa wa Covid-19 hupitia katika kaunti za Pwani, yameanikwa wazi baada ya kifo cha afisa mkuu wa... SIAGO CECE na ANTHONY KITIMO |
UFISADI miongoni mwa baadhi ya maafisa wa serikali katika mpaka wa Kenya na Tanzania, umezidi kuwaweka... Na WAANDISHI WETU |
WINGU la maangamizi limetanda kote nchini huku aina mpya ya corona maarufu kama 'Delta' ikiua watu kwa... Na WINNIE ONYANDO |
HUENDA visa vya wasafiri kulazimishwa kupima upya corona mpakani mwa Kenya na Tanzania vikakoma baada ya serikali hizo... NA WANGU KANURI |
AGIZO la serikali la kudhibiti mkurupuko wa ugonjwa wa corona mwaka jana limewashurutisha Wakenya wengi kufanyia kazi... Na Titus Ominde |
VIONGOZI wa kidini Kaskazini mwa Rift Valley (North Rift) wameshutumu wanasiasa kwa kupepeta usambazaji wa virusi vya... Na WANTO WARUI |
Huku wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiripoti katika shule zao mpya za sekondari hii leo, kuna uwezekano wa maambukizi... Na CHARLES WASONGA |
NAKUBALIANA na kauli ya maafisa wa afya katika kaunti ya Nairobi kwamba wanasiasa ndio wanachochea ongezeko la visa... Na SAMMY WAWERU |
DICKSON Muceri amekuwa mkazi wa Nairobi kwa muda wa miaka kadhaa ila sasa kitovu hicho cha jiji kuu la nchi hakikaliki... Na MARY WANGARI |
WANASAYANSI wamethibitisha kuwa kuchelewesha upokeaji dozi ya pili ya chanjo ya Covid-19 kwa kiasi cha miezi 10 baada ya... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na KINYUA BIN KINGORI |
WAKATI huu viongozi wa kisiasa wameanza mapema kampeni zao kwa kuzuru maeneo mbalimbali nchini, ili kushawishi... Na WANDERI KAMAU |
KULINGANA na Ripoti ya Jaji Mstaafu Akilano Akiwumi (1997) kuhusu chimbuko la ghasia za kikabila nchini, wanasiasa ndio... Na WANTO WARUI |
KWA mara nyingine tena tuzo inayoenziwa sana kote ulimwenguni imerudi katika eneo letu la Afrika Mashariki mara hii... Na DOUGLAS MUTUA |
MWAFRIKA akiwajibishwa na Mzungu hupiga kamsa na kudai anaonewa, ati msingi wa maonevu ni ubaguzi wa rangi... Na WANDERI KAMAU |
MOJA ya changamoto kuu zinazokikumba kizazi cha sasa nchini ni ukosefu wa ufahamu wa lugha zao asili. |
Ingawa lugha... Na KINYUA BIN KINGORI |
JUHUDI za kuhakikisha taifa limefanikiwa kupiga vita ufisadi lazima ziendeshwe kuambatana na Katiba, bila njama... Na WANDERI KAMAU |
UFICHUZI wa sakata ambapo watu maarufu duniani wamekuwa wakificha mabilioni ya fedha katika akaunti za siri ng’ambo... Na FAUSTINE NGILA |
NINA imani kuwa iwapo kufikia sasa hujawahi kuelewa teknolojia ya blokcheni, leo utaelewa kwa kuwa jana uliathirika... Na CHARLES WASONGA |
NI jambo la kusikitisha kuwa ni wakati kama huu ambapo uchaguzi mkuu unakaribia ndipo wanasiasa wametambua umuhimu wa... Na MARY WANGARI |
IDADI ya watu wanaoandaa hafla za uchangishaji pesa za kugharamia matibabu imeongezeka pakubwa katika siku za hivi... Na CECIL ODONGO |
CHAMA cha Kanu bado kina safari ndefu kurejelea umaarufu wake wa enzi za utawala wa chama kimoja na miaka ya 90 hata... Na CHARLES WASONGA |
Subsets and Splits
No saved queries yet
Save your SQL queries to embed, download, and access them later. Queries will appear here once saved.