text
stringlengths
3
16.2k
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MUNGUTI MASKWOTA wapatao 10,000 wamewasilisha upya kesi katika Mahakama ya Upeo wakiomba ibatilishe uamuzi kwamba wafukuzwe kutoka kwa shamba la ukubwa wa ekari 25,000 wanalong’ang’ania umiliki wake na familia ya mwanasiasa marehemu Mark Too. Maskwota hao wanaodai mababu zao ndio waliotimuliwa kutoka kwa shamba hilo enzi za ukoloni, wanasema walipewa shamba hilo rasmi na aliyekuwa Rais hayati Daniel arap Moi, kisha Kamishna wa Ardhi M Okundu akaratibisha uamuzi huo mwaka 2007. Katika ombi lililowasilishwa na wakili William Arusei chini ya sheria za dharura, kikundi cha maskwota hao–Sirikiwa Squatters Group–kimeomba mahakama ibatilishe uamuzi huo kwa vile ilitegemea ushahidi ambao haukuwa umewasilishwa katika kesi waliyoshtaki katika Mahakama ya kuamua kesi za mashamba (ELC), Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu. Pia wameeleza bayana Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaack Lenaola, na William Ouko walitegemea ushahidi wa Afisa wa Ugavi wa Mashamba R J Simiyu kutoa uamuzi wang’atuke shambani. Maskwota hao wamesema ushahidi wa Bw Simiyu uliowasilishwa mbele majaji hao saba kwa njia ya afidaviti ni mpya na kamwe “haukuwasilishwa mbele ya Jaji Antony Ombwayo aliposikiliza na kuamua kesi hiyo 2017.” Pia wanasema ushahidi huo haukuwasilishwa Mahakama ya Rufaa iliyosikiliza rufaa iliyowasilishwa na kampuni ya Fanikiwa, familia ya marehemu Mark Too, kampuni ya Lonrho Agribusiness (EA) Ltd, na Bw David K Korir. Hivyo basi, maskwota hao wanaeleza mahakama hii ya upeo kwamba ni kinyume cha sheria kutegemea ushahidi mpya kutoa uamuzi wa kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma. “Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu wa Desemba 15, 2023, hauna mashiko kisheria na kamwe hauna nguvu kisheria kuwatimua maskwota hawa kutoka kwa shamba lao,” asema Bw Arusei. Pia maskwota hawa wanadai kwamba badala ya Mahakama ya Juu kujadili masuala ya kikatiba jinsi ilivyo jukumu lake, majaji hao walianza kufafanua na kutafsiri ushahidi wa watu binafsi na kuelezea maana ya ‘skwota’. Mahakama hii imeombwa ikague upya uamuzi iliyotoa kwa vile ilidanganywa na walalamishi na pia kutendewa ujanja. Akinukuu maamuzi ya majaji wastahiki kama vile Lord Dening, Bw Arusei amesema, mahakama ikigundua ilipotoshwa au kudanganywa na upande mmoja, iko na mamlaka na uwezo wa kufutilia mbali uamuzi iliyotoa na kuandika mwingine. Maskwota hao wanaomba Mahakama ya Juu iwarudishe shambani kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Ombwayo na Mahakama ya Rufaa. Vile vile mahakama hiyo imekosolewa kwa kumshambulia hayati Moi katika uamuzi huo pasi kutoa agizo wasimamizi wa mali yake wafike mbele yao kutoa mwanga kuhusu suala la umiliki wa shamba hili lililorudishwa kwa serikali na kampuni iliyokuwa inakuza miti inayotumika katika viwanda vya ngozi. Naibu msajili wa Mahakama ya Juu Nelly Kariuki aliwaamuru maskwota hao wawakabidhi nakala za kesi hii yao mpya wahusika wote kabla ya Januari 31, 2024, kesi itakapotajwa tena kwa maagizo zaidi. Jaji aliyesikiliza kesi hii mpya hakuiratibisha kuwa ya dharura ila aliamuru pande zote ziwasilishe ushahidi katika muda wa siku 14 kuanzia Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti,  baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

Na WINNIE ATIENO SERIKALI ya kaunti ya Mombasa ikiongozwa na waziri wa uchukuzi Bw Dan Manyala, imeeleza kuwa shughuli za kuopoa miili ya watu watatu waliosombwa na maji wakiendelea shughuli ya kusafisha mfumo wa maji taka katika mzunguko wa Makupa bado unaendelea. “Vibarua hao watatu walikuwa wakiondoa uchafu kwenye mabomba ya kupitisha maji taka ila kuna maji yaliyokuja ghafla kwa sababu ya mvua nyingi zinazoshuhudiwa,” akasema Bw Manyala. Licha ya hayo, Bw Manyala alieleza kuwa miili hiyo ingetolewa kabla ya siku kukamilika. “Ni shughuli hatari, na hatutaki kuhatarisha maisha ya watu wengine kwa kuwatuma kule chini ambako hakuna hewa ya kutosha. Maji pia yanatokea pande zote,”akasema bw Manyala. Bw Salim Mwanyiro mwenye umri wa miaka 34, alinusurika kifo baada ya mjomba wake na wafanyakazi wenzake wawili kuaga dunia kazini. Wenzake hao, walizama wakati ambapo walikuwa wakizibua mfumo wa kupitisha maji taka katika mzunguko wa Makupa katika Kaunti ya Mombasa, Ijumaa jioni. “Niliponea kifo, na sasa nimejawa na hofu,” akasema huku akilia. Yeye ni miongoni mwa watu saba, ambao walizama katika eneo hilo, ila aliokolewa akiwa hai. “Nafanya kazi hii kwa kuwa ndicho kitega uchumi changu. Jumatano tuliingia humo ndani tukafanya kazi na tukatoka tukiwa hai. Leo tuliingia tukakwama, ila wanne wakaokolewa,”akaongezea. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA WINNIE ONYANDO BARAZA la Mitihani nchini (KNEC) Jumamosi Novemba 25, 2023 lilikiri kulikuwa na dosari katika matokeo ya mtihani wa mwisho wa Darasa la Nane (KCPE) uliotangazwa Alhamisi na Waziri wa Elimu Eekiel Mochogu. Hii ni baada ya walimu na wazazi kutoka shule mbalimbali kuonyesha kutoridhishwa kwao na matokeo hayo. Afisa Mkuu Mtendaji wa baraza hilo, David Njengere katika barua alisema kwamba baraza hilo limepokea malalamishi kadhaa kutoka kwa wazazi, walimu na watahiniwa kuhusu matokeo hayo. “Tumepokea malalamishi kuhusiana na matokeo hayo. Hata hivyo, tumeshughulikia malalamishi 133,” akasema Dkt Njengere. Kando na hayo, Dkt Njengere alisema kwamba watahiniwa wote watembele shule zao ili kupata nakala ya matokeo ya mtihani na kuwasilisha malalamishi yao ndani ya siku 30. Haya yanajiri siku moja tu baada ya wazazi Kuanti ya Meru kuandamana kupinga jinsi mtihani huo ulivyosahihishwa kwa haraka. Wazazi hao walidai kuwa hatua ya KNEC kuharakisha usahihishaji wa mtihani huo huenda ulichangia dosari nyingi. Kando na hayo, kuna baadhi ya watahiniwa ambao walipata alama ya Lugha ya Ishara ilhali hawakufanya somo hilo. Kadhalika, kuna shule ya msingi ambayo kila mtahiniwa alipata alama 75 katika somo la Sayansi. Naye mtahiniwa Samuel Smith aliyepata alama ya 378 alisema kwamba hakutarajia kupata chini ya 400. “Mwanangu alipata 378 ila kuna somo moja hakufanya na akawekewa alama ya 68. Kiingereza alipata A (78), KSL B (68), Hisabati A (82), Sayansi B (72), na SSR A (78) jumla ya 378,” akasema Arbigail Timinah, mamake mwathiriwa. “Mwanangu hakufanya Lugha ya Ishara (KSL) ila akapewa alama ya 68.” Haya yote yalizua masuala kuhusu jinsi mtihani huo ulivyosahihishwa. KNEC, hata hivyo, lilisema kuwa itashughulikia suala hilo na kuchukua hatua mwafaka ili kuhakikisha kuwa makosa hayo yameshughulikiwa ipasavyo. Zaidi ya wanafunzi milioni 1.4 walifanya mitihani huo ulioanza Novemba 30. Hata hivyo, zaidi ya wanafunzi 9,000 hawakufanya mtihani huo kutokana na changamoto mbalimbali. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MASHIRIKA GAZA, Palestine KUNDI la Hamas limeachilia mateka 24 waliokuwa wamezuiliwa Gaza kwa juma kadhaa na wafungwa 29 wa Kipalestina wakiachiliwa kutoka jela kwa awamu ya kwanza ya mabadilishano chini ya mpango wa kusitisha mapigano kwa siku nne. Qatar ambayo ilikuwa mpatanishaji wa mpango wa kusitisha vita, ilisema tayari familia 13 za Israeli zimeachiliwa na Hamas na zimefarijika kurudi kwao. Kundi hilo lililojumuisha watoto, wanawake na wanamme, walirejea nchini Israeli baada ya Shirika la msalaba kuwasaidia kuwatoa Gaza na kuwapeleka Misri. Raia kumi wa Thailand na Mfilipino mmoja pia wameachilia, katika mkataba tofauti na ule uliopatanishwa na Qatar. Mkataba huo ulikuwa na makubaliano ya jumla ya mateka Israeli 50 na wafungwa 150 wa Kipalestina ambao wanakusudiwa kuachiliwa kwa siku nne zijazo wakati wa kusitisha mapigano kwa muda. Watu wa familia hizo 13 walipelekwa katika hospitali ya Misri ili kupata huduma za matibabu kabla ya kurudishwa Israeli. Waisraeli hao, walikuwa watoto wanne wenye umri wa miaka 2, 4, 6 na tisa pamoja na bibi wa miaka 85. Waziri Mkuu wa Israeli Benjamini Netanyahu alisema wameweza kurejesha kundi la kwanza la wale waliokuwa wametekwa nyara. “Nasisitiza kwenu, familia na raia wa Israeli tumejitolea kuwarudisha wote walitekwa nyara,” alisema Bw Netanyahu. Miongo mwa walioachiliwa ni mke wa Yoni Asher Doron Katz Asher 34 na wanawe wawili. Bw Asher aliambia BBC aliazimia kuangana na familia yake tena iliyokuwa imetekwa. Aliongezea hatasherekea hadi wale wote waliotekwa nyara wamerejea nchini Israeli. “Familia zilizotekwa si mabango, ni watu halisi. Familia za waliotekwa ni familia yangu mpya. Nitahakikisha nimefanya chochote kile kuhakikisha wamerejea nyumbani,” alisema Bw Asher. Pia, familia za raia wa Thailand na Filipino wanayonafuu baada ya Hama kuwaachilia. Kittiya Thuengsaeng aliambia maafisa wa Thai kuwa mpenzi wake wa miaka 3 aliaga kwenye mapigano hayo ila maafisa hao wakatangaza maajina ya waliouliwa na jina la mpenziwe halikuwepo. Siku tano alipokea taarifa yupo miongoni mwa wale waliokuwa wametekwa nyara. Wafungwa 39 wakipalestina waliachiliwa baada ya kutumika kwenye mabadilishano kwenye mkataba uliokuwa umewekwa. Watuhumiwa hao, walishtakiwa na makosa mbalimbali kama vile kurusha mawe na kujaribu kuua. Wengine wakihukumiwa kwa uhalifu baadhi yao wakisubiri kesi za kusikillzwa. Wafungwa hao walichanguliwa kutoka kwenye orodha ya wanawake na watoto 300 waliokuwa wamekamatwa na Israeli. Robo ya orodha hiyo wengi wamehukumiwa na kuzuiliwa rumande huku wakisubiri kesi zao kusikilizwa. Asilimia 40 ikiwa ni wavulana matinées chini ya miaka 18. Hamas waliwateka watu zaidi ya 200 wakati wa kuvuka mpaka wa Kusini Israeli Oktoba 7 na kuwaua watu 1200. Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema idadi ya wapalestina waliotiwa baroni bila kufunguliwa mashtaka katika jela za Israeli imeongezeka tangu shambulizi hilo. Takribani malori 60 ya misaada imefika Gaza na manne nchini Israeli ikiwa na mafuta lita 130,000 baada ya mapigano hayo kusitoshwa.
Tags
You can share this post!
Previous article
Baba wa watoto 16 Mandera ashangaza wengi kwa kujizolea...
Next article
KNEC yakiri kulikuwa na dosari katika matokeo ya KCPE

Na RICHARD MUNGUTI MAAFISA wawili wa polisi waliopatikana na hatia ya kupokea hongo ya Sh200,000 na kuvuruga utendakazi wa maafisa wa tume ya kupambana na ufisadi (EACC) katika kituo cha polisi cha Kabete kaunti ya Nairobi, wamehukumiwa kifungo. Polisi hao walikuwa wamemzuilia Bi Gong Huan, mke wa muwekezaji Pan Xido Yan, katika kituo hicho cha polisi cha Kabete, wakilenga kumfungulia mashtaka ya kuishi nchini kinyume cha sheria za uhamiaji. Hakimu mkuu mahakama ya kesi za ufisadi Milimani Bw Thomas Nzioki, alisema Gong alizuiliwa katika kituo cha polisi cha Kabete kinyume cha sheria, bila rekodi rasmi kunakiliwa kuonyesha alikuwa amewekwa korokoroni kama mahabusu. “Hii mahakama imegadhabishwa na tabia hii ya Polisi kuwazuilia washukiwa bila kuweka rekodi zozote. Hivi ndivyo watu wametoweka na hatimaye kupatikana wameuawa na miili yao kutupwa. Miili ya mahabusu hawa hutupwa misituni au mitoni kama ile miili ilipatikana Mto Yala Kaunti ya Siaya. Polisi hukiuka sheria za kuwazuilia watu bila rekodi zozote kuwekwa,”alisema Bw Nzioki. Alisema sheria zinazodhibiti idara ya polisi ndizo amri ambazo maafisa wa polisi wanapasa kufuata. Baada ya kusema hayo, Bw Nzioki alifikia uamuzi kwamba ushahidi uliowasilishwa umethibitisha Koplo Julius Onyango Oguma na Konstebo Charles Macharia Wanjiru wako na hatia. Bw Nzioki alimpata na hatia Koplo Oguma ya kuuma mlungula wa Sh200,000 kutoka kwa Bw Pan Xido Yan aliyekuwa amemwitisha kitita cha Sh1,000,000 asimshtaki mkewe Gong Huan kwa makosa ya kuishi nchini Kenya bila stakabadhi rasmi kutoka kwa idara ya uhamiaji. “Wewe Koplo Oguma ulijitangaza mwenyewe kuwa sheria na kufanya vile ilikupendeza kuzuilia mshukiwa na kumweka chini ya uangalizi wa makachero bila kuandikisha katika daftari ya mahabusu Gong Huan yuko rumande katika kituo cha Polisi cha Kabete,” alisema Bw Nzioki. Mbali na Koplo Oguma pia Bw Nzioki alimpata na hatia Konstebo Charles Macharia Wanjiru ya kuvuruga maafisa wa EACC waliokuwa wamefika kituo cha Kabete kumkamata (Oguma). Konstebo Wanjiru alitoa bastola na kufyatua risasi hewani. “Milio ya mitutu ya bunduki ilisikika katika eneo la egesho la Kituo cha Polisi cha Kabete. Hii mahakama ilielezwa na mashahidi,” Bw Nzioki alisema. Mahakama ilisema wakati wa kizaazaa hicho Koplo Oguma alitoroka na hongo na kuificha lakini akatiwa nguvuni. Miongoni mwa Sh200,000 alizopokea kama hongo Sh100,000 zilikuwa zimetiwa alama na EACC. Pesa hizo zilitambuliwa kortini na pia sauti ya Koplo Oguma ilikuwa imenaswa na maafisa wa EACC. Huku akiwasukuma gereza, Bw Nzioki, pia aliwaachilia huru maafisa wengine wawili wa polisi  Samuel Yunah Kukhuvillo na Joseph Kigara Gatheca. Hakimu alisema hakukuwa na ushahidi kwamba walikuwa katika kituo cha polisi cha Kabete uhalifu huo ulipotendeka. Polisi hao waliondoka kizimbani lakini Gatheca alidondokwa na machozi kwa muda mrefu. Koplo Oguma na Konstebo Wanjiru watarudishwa kortini Novemba 29,2023 adhabu kutolewa na wakili wao Njenga Kiarie kutoa malilio. Koplo Oguma na Wanjiru walishtakiwa kutekeleza uhalifu huo mnamo Novemba 28, 2018 katika kituo cha polisi cha Kabete Nairobi. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA SHABAN MAKOKHA Mfuasi sugu wa Kinara wa Azimio Raila Odinga, Nuru Okanga aliyefanya mtihani wa Darasa la Nane mwaka huu, bado hajapokea matokeo yake kufikia Ijumaa Novemba 24, 2023. Bw Okanga aliye na umri wa miaka 32 ni miongoni mwa watahiniwa 1.4 milioni ambao walikalia mtihani huo mwezi jana kama mtaniniwa wa kujitegemea. KCPE ya mwaka huu ilifanywa na idadi kubwa ya watahiniwa baada ya serikali kukubalia wanafunzi ambao hawakuwa wamesajiliwa kukalia mtihani huo ambao ni wa mwisho kufuatia kufungwa kwa mtaala wa 8-4-4. Okanga alikalia mtihani huo katika Shule ya Msingi ya Mumias, Kaunti ya Kakamega akisema dhamira yake ilikuwa kujipatia cheti cha shule ya msingi ambacho kitamsaidia kuwania kiti cha udiwani cha Kholera, Matungu ufikapo mwaka wa 2027. Kwenye mahojiano, alikuwa amesema alitaka kuenda kusoma shule ya upili na baadaye kujiunga na chuo kikuu akiwa na maono ya kuwa rais wa Kenya katika miaka zijazo. “Sitakomea hapa (KCPE). Ninataka kuendelea hadi shule ya upili na kisha niingie chuo kikuu kwa sababu humu Kenya, ili mwaniaji agombee urais lazima awe na shahada. Hapa ndipo ninapolenga hata kama umri utakuwa umesonga mpaka nikagonga miaka 70. Lazima zitagombea urais,” alisema. Alisema mgombeaji wa Roots Party, George Wajackoyah alikuwa amemuajiria mwalimu jijini Nairobi, ambaye alimfunza na kumuandaa kwa mtihani huo wa kitaifa. Lakini mwanasiasa huyo anayejulikana kwa kumtetea Bw Odinga na chama cha ODM sasa analalamikia kucheleweshwa kwa matokeo yake, huku akitaka Baraza la Mitihani, Knec, kujitokeza na kumwelezea kwa nini hajapokea matokeo yake kufikia sasa. Alisema aliwekeza juhudi zake na hata akakosa usingizi alipokuwa anasomea mtihani na kwamba kuchelewa huku kunamtesa kisaikolojia. “Ninataka kujua kwa nini matokeo yangu hayaji wakati wenzagu tuliofanya nao mtihani washapokea yao. Kwani tatizo ni nini? Knec inafaa kuachilia alama zangu mara moja kwa sababu nilifanya mtihani. Nina mipango mingi ya kujiendeleza kimasomo na kucheleweshwa huku kunanitia wasiwasi,” akasema. Alisema alitarajia kupata angalau alama 250 kati ya 500 kumwezesha kujiunga na shule ya sekondari katika ari yake ya kutafuta uongozi baadaye. Asubuhi ya Novemba 24, Okanga alikuwa bado hajapokea matokeo. SMS iliyo na nambari ya usajili ya Okanga (Index Number) na neno KCPE iliyotumwa kwa nambari 40054 ilionyesha kwamba matokeo hayo hayapatikani. “Mteja mpendwa, ni ama hakuna matokeo yanayohusu nambari ya usajili 37961701022, au huenda pia haijulikani. Tafadhali thibitisha nambari ya usajili. KNEC Helpline 08000724900,” ilisema arafa. Mnamo Alhamisi, mitandaoni kulizagaa matokeo feki yaliyokuwa yanaonyesha Okanga amepata alama za juu, 401 kwenye mtihani wake. Hata baadhi ya viongozi wa Azimio walijitokeza kumpongeza kwa kupita KCPE huku Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino akimpa ufadhili wa masomo yake ya sekondari na zaidi. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA TITUS OMINDE WATAHINIWA bora wa KCPE kutoka Uasin Gishu wamepongeza mradi wa Magazeti Masomoni wa Nation Media Group Newspapers in Education (NiE) kwa kuchangia kufaulu kwao katika KCPE mwaka huu. Katika shule ya Eldoret Archivers Academy, watahiniwa na mkurugenzi wa shule Willy Mbote walihusisha matokeo yao bora haswa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza kutokana na mazoezi hayo kupitia karatasi za mfano wa KCPE zilizochapishwa na NMG kupitia Taifa Leo na Daily Nation. “Kufaulu kwetu kama shule kumeimarishwa sana na matumizi ya mara kwa mara ya magazeti ya NMG hasa ukurasa wa Elimu Msingi, karatasi za mitihani, miongoni mwa machapisho mengine yanayohusu elimu,” alisema Bw Mbote. Maoni sawa na hayo yalitolewa na Juliet Chepchirchir aliyepata alama 413 shuleni humo. “Ninamshukuru Mungu kwa shule yetu kwa kutuandikisha katika NIE tumekuwa tukitumia Nation Newspapers kwa manufaa tuliyopata kutokana na magazeti yaliyochangia kufaulu kwetu.” Juliet anataka kujiunga na Shule ya Upili ya Wasichana ya Kipsigis na katika siku zijazo angependa kuwa mhasibu. Katika Chuo cha Greenvale huko Eldoret, mwanafunzi bora aliyepata alama 420 anataka kuwa mwanahabari kutokana na ushawishi wa magazeti ya Nation Media Group. Christine Ayako aliyepata alama 420 alisema alichochewa na magazeti aliyosoma ambayo yalimsaidia kufaulu katika lugha na ndio maana ananuia kujiunga na shule ya upili ya Moi Girls mjini Eldoret na kisha baadaye kusomea uandishi wa habari katika Chuo Kikuu ili kuwa sauti kwa wasio na sauti katika jamii. “Nilifaulu kwa sababu ya ushawishi wa waandishi wa habari, hasa magazeti na namshukuru Mungu kwa kila jambo. Ningependa kuwa mwandishi wa habari siku zijazo ili niwasemee wasio na sauti katika jamii,” alisema Christine. Katika shule ya Hill mjini Eldoret ambayo ilikuwa miongoni mwa shule bora za umma, mwalimu mkuu shule hiyo Osborn Ngaira alisema shule yake imepata matokeo bora mwaka huu ikilinganishwa na miaka mingine. Zaidi ya watahiniwa 20 kutoka Shule ya Hill walipata zaidi ya alama 400. Bw Ngaira alisema mradi wa NiE umekuwa kiungo kikubwa cha masomo shuleni humo na ufanisi huo bila shaka ulichangiwa na mradi huo. Sherehe kama hiyo ilifanyika katika Shule ya Little Lambs ambapo zaidi ya watahiniwa 60 walipata zaidi ya alama 400. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

Na SHABAN MAKOKHA Jacinta Khasungu aliweka eneo la Magharibi kwenye ramani ya kitaifa  baada ya kuibuka kuwa wasichana bora  kote nchini katika mitihani ya darasa la nane (KCPE) ambao matokeo yake yalitangazwa na Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu jana. Bi Khasungu wa shule ya msingi ya wasichana ya St Anne’s Mumias, kaunti ya Kakamega, alipata alama 427 kati ya 500 na kuibuka msichana bora zaidi nchini  katika mtihani huo ulioashiria  mwisho wa mtaala wa 8-4-4. Bensel Okwemba wa Shule ya St Joseph,Kakamega alijiunga na wanafunzi wengine waliofanya vizuri akiwa na alama 423 akifuatiwa kwa karibu na Clifford Alusiola wa Fesbeth Academy aliyepata alama 420. Ingawa Khasungu aliibuka msichana bora, alama alizopata ni chini ya matarajio aliyokuwa nayo. “Sishangai nimepata alama 427. Lakini hizo sio nilizotarajia. Nilitarajia kupata 430 na zaidi, lakini ninaridhika na kile ambacho Mungu amenipa kwa sababu nimeibuka kuwa msichana bora zaidi nchini Kenya,” alisema msichana huyo mwenye umri wa miaka 14. Binti  huyo ambaye ni mzaliwa wa pili, anahusisha matokeo bora na kusikiliza ushauri kutoka kwa walimu na wazazi huku akimtanguliza Mungu katika shughuli zake. Nia yake ni kujiunga na shule ya Upili ya Kenya High ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa Mhandisi wa Matibabu. Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya St Anne’s Sister Cyrila Sanya alisema darasa la nane la 2023 lilionyesha ishara zote za kufanya vizuri katika mitihani yao ya kitaifa. “Msichana aliyeibuka bora alikuwa  ameongoza katika darasa lake kutoka madarasa ya chini. Tulitarajia mema kutoka kwake na Mungu amejibu maombi yetu. Nafasi aliyoshika si kwa makosa, alistahili,” alisema Sister Sanya. Shule hiyo ilikuwa na watahiniwa 289 wa mitihani ya KCPE na matokeo ya mwaka huu yalikuwa bora kuliko ya mwaka jana ambapo mtahiniwa bora alipata alama 422. Mjomba wa Khasung, Mathews Mwanza alimsifu msichana huyo akisema amekuwa fahari kwa familia.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

Na BENSON MATHEKA Kaunti sita zilikuwa na watahiniwa wa umri wa miaka 18 na zaidi katika mtihani wa KCPE wa mwaka huu. Akitangaza matokeo ya mwaka huu ya mtihani huo, Waziri wa Elimu, Ezekiel Machogu alitaja kaunti hizo kama Garissa ambayo asilimia 25.86 ya waliofanya mtihani huo walikuwa watu wazima, Turkana (asilimia 24.5), Kwale (asilimia 16.09), Kilifi (asilimia 15.66) na Mandera ( asilimia 33.90). Wakati huo huo, kaunti tano za Baringo, Wajir, Bomet, Kericho na Pokot Magharibi zilikuwa na idadi kubwa ya watahiniwa katika KCPE waliokuwa na umri wa chini ya miaka 12. Bw Machogu alisema kwamba, idadi kubwa ya watahiniwa katika KCPE ya mwaka huu walikuwa na umri wa kati ya miaka 13 na 15 wakiwa ni 1,023,859.( asilimia 72.31) ya watahiniwa wote. Alisema kwamba, ingawa KCPE ilisaidia kuafikia usawa wa jinsia katika elimu, ni kaunti ya Isiolo pekee iliyoongoza kwa kuwa na watahiniwa wengi wasichana kuliko wavulana. Kaunti kumi za Mandera, Garissa, Turkana, Wajir, Machakos, Nyamira, Samburu Baringo, Nandi na Makueni zilikuwa na pengo kubwa kati ya wavulana na wasichana waliofanya KCPE mwaka huu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA SAMMY WAWERU MICHAEL Warutere, ndiye mtahiniwa bora zaidi nchini katika Mtihani wa Kitaifa Darasa la Nane (KCPE) 2023. Kijana Waturere alizoa alama 428, kutoka jumla ya 500 zinazowezekana na anasema akihitimu Kidato cha Nne, angependa kuwa mhandisi (Software Engineer). Mtahiniwa huyo amekuwa mwanafunzi wa Riara Springs Academy, mojawapo ya Shule za Kibinafsi katika Kaunti ya Nairobi. Akihojiwa na vyombo vya habari Alhamisi, Novemba 23, 2023 saa chache baada ya Waziri wa Elimu, Ezekiel Machogu kutoa rasmi matokeo, Warutere alisema hakutarajia kukwangura alama hizo – 428. Akielezea kufurahishwa kwake na matokeo yake, alisema alikuwa anatarajia kupata alama 410. “Nina furaha sana…Sikuwa nikitarajia kupata alama zilizotangazwa, mtahiniwa bora zaidi nchini. Aidha, nilitarajia kuzoa alama 410. Ninashukuru Mungu, wazazi wangu na walimu kwa kazi nzuri waliyonifanyia,” mvulana Warutere akasema akizungumza shuleni Riara Springs Academy. Alikuwa ameandamana na babake, walimu, wazazi wengine na wanafunzi wenza, mazingira ya shule hiyo yakisheheni shangwe, vifijo na nderemo. Kulingana na babake, alipigiwa simu na walimu wa Riara Springs Academy akaarifiwa kuwa mwanawe ndiye kidedea nchini. Huku Somo la Hisabati, Kiingereza, Kiswahili na Jiografia/Dini, akizoa alama A kila moja, mtahiniwa huyo alisema Sayansi pekee ndiyo ilimkalia ngumu. “Si mimi pekee, hata watahiniwa wengine walilalamikia ugumu wa Somo la Sayansi,” Warutere akaambia wanahabari. Alidokeza kwamba ndoto yake ni kuwa mhandisi. Watahiniwa 8, 525 walizoa alama 400 hadi 500. Idadi ya waliopata alama 300 – 399, ni 352, 782 na 200 hadi 299 wakiwa watahiniwa 658, 278. Hali kadhalika, waliozoa alama 100 hadi 199 wameandikishwa kuwa 383, 025, huku 0 – 99 wakiwa 2, 060. Jumla ya watahiniwa 1, 406, 559 walifanya KCPE 2023, wa kiume wakiwa 721, 544 na kike 685, 017. Katika zoezi hilo ambalo limekunja jamvi mfumo wa 8-4-4 na kukaribisha mfumo mpya wa CBC, kulikuwa na vituo jumla 28, 533 vya kuandika mtihani. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA SAMMY WAWERU MTAHINIWA bora zaidi katika mtihani wa Kitaifa Darasa la Nane (KCPE) 2023 amezoa alama 428, kwa jumla ya 500 zinazowezekana. Alama ya 2023, ni punguo la alama 3 ikilinganishwa na mwaka uliopita, 2022, ambapo mtahiniwa bora alipata alama 231. Akitoa matokeo rasmi ya KCPE 2023 katika makao makuu ya mitihani nchini, Mitihani House, Jijini Nairobi, Waziri wa Elimu, Ezekiel Machogu alisema watahiniwa 8, 525 walizoa alama kati ya 400 hadi 500. “Mtahiniwa bora zaidi KCPE 2023, alizoa alama 428 kwa jumla ya 500 zinazowezekana,” akasema. Idadi ya waliopata alama 300 – 399, ni 352, 782 na 200 hadi 299 wakiwa watahiniwa 658, 278. Hali kadhalika, waliozoa alama 100 hadi 199 wameandikishwa kuwa 383, 025, huku 0 – 99 wakiwa 2, 060. Jumla ya watahiniwa 1, 406, 559 walifanya KCPE 2023, wa kiume wakiwa 721, 544 na kike 685, 017. Katika zoezi hilo ambalo limekunja jamvi mfumo wa 8-4-4, kulikuwa na vituo jumla 28, 533 vya kuandika mtihani. Waziri Machogu alisema serikali ya William Ruto imeweka mikakati maalum kuhakikisha kila mtahiniwa anajiunga na kidato cha kwanza 2024. “Usajili wa wanafunzi watakaojiunga na shule za upili 2024, utakuwa asilimia 100 kwa 100,” Bw Machogu akahakikishia taifa. Ni visa viwili pekee vya udanganyifu kwenye mtihani vilivyoandikishwa katika KCPE 2023, Bw Machogu akisema mtahiniwa mmoja alipatikana akiwa na karatasi feki na mwingine simu wakati wa mtihani. Wakati huohuo, Waziri wa Elimu alitangaza kwamba shughuli ya kuteua watahiniwa kujiunga na kidato cha kwanza itaanza mnamo Jumanne, Novemba 28, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA SAMMY WAWERU HALI ya taharuki imekumba watahiniwa wa Mtihani wa Kitaifa Darasa la Nane (KCPE) 2023, walimu na wazazi kufuatia kukawia kwa matokeo kwa njia ya kieletroniki. Baada ya Waziri wa Elimu kutoa rasmi matokeo hayo, Alhamisi, Novemba 23, 2023 katika makao makuu ya mitihani, Mitihani House, Jijini Nairobi, ili kuyapokea upesi watahiniwa wametakiwa kutuma ujumbe mfupi wa nambari zao za kuandika mtihani (INDEXNUMBER) kwa nmabari 40054. Ujumbe huo aidha unatumwa kwa simu ya mkono. Nambari hizo, hata hivyo, zinakawisha matokeo walimu, wanafunzi na wazazi wakihimiza serikali kuangazia tatizo hilo. Saa moja baada ya matokeo hayo kutangazwa rasmi, hakukuwa na mtahiniwa kote nchini aliyekuwa amejua alama alizopata. “Mteja mpendwa, matokeo ya KCPE 2023 hayapo kwa sasa. Tafadhali jaribu tena baadaye. Nambari ya usaidizi ya KNEC ni 08007224900,” ilisema sehemu ya ujumbe kwenye simu ya mzazi mmoja Mombasa aliyetuma ujumbe akitafuta matokeo. Mtahiniwa bora zaidi amezoa alama 428, kwa jumla ya 500 zinazowezekana. Jumla ya watahiniwa 1, 406, 559 walifanya KCPE 2023, wa kiume wakiwa 721, 544 na kike 685, 017. Hadi wakati wa kuchapisha taarifa hii, hitilafu hiyo ya kimitambo haikuwa imetatuliwa. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA FATUMA BARIKI Wazazi, wanafunzi na wadau katika mtihani wa KCPE walikabiliana na hali ya sintofahamu Alhamisi Novemba 23,2023 huku waking’ang’ana kutuma jumbe za simu kwa ajili ya kupokea matokeo yao. Wizara ya Elimu ilikuwa imetangaza kwamba kwa kutuma nambari ya usajili (index number) kwa nambari ya simu 40054, mhusika angeweza kupokea matokeo yake. Lakini zaidi ya dakika 30 baada ya kuhakikishiwa kwamba matokeo yameachiliwa, bado waliotuma jumbe walikuwa wanakosa kupata matokeo. “Mteja mpendwa, matokeo ya KCPE 2023 hayapo kwa sasa. Tafadhali jaribu tena baadaye. Nambari ya usaidizi ya KNEC ni 08007224900,” ilisema sehemu ya ujumbe kwenye simu ya mzazi mmoja Mombasa aliyetuma ujumbe akitafuta matokeo. Ni hali iliyojirudia sehemu tofauti tofauti huku mchecheto ukiendelea kugubika wanafunzi na wazazi waliokamia kujua walichopata kwenye mtihani huo. Duru ziliambia Taifa Leo kwamba maafisa wa kitengo cha utaalamu wa mitambo wa Baraza la Mitihani walikuwa wanang’ang’ana kushughulikia tatizo hilo, lakini kufikia wakati wa kuchapisha taarifa hii hali haikuwa imekuwa shwari. Awali, Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu alikuwa ametangaza rasmi kutolewa kwa matokeo hayo huku akisema kwamba mwanafunzi bora zaidi katika KCPE 2023 amepata alama 428, hii ikiwa ni kushuka, kwa sababu 2022, mwanafunzi bora alipata alama 431. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MHARIRI
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini.
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na BENSON MATHEKA
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na MASHIRIKA
LONDON, Uingereza
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya... Na ELIZABETH MERAB
WANASAYANSI wanachunguza kuhusu mchipuko wa virusi vipya vya corona aina ya Delta, katika nchi za Amerika, Uingereza,... Na MAUREEN ONGALA
MASAIBU ambayo wagonjwa wa Covid-19 hupitia katika kaunti za Pwani, yameanikwa wazi baada ya kifo cha afisa mkuu wa... SIAGO CECE na ANTHONY KITIMO
UFISADI miongoni mwa baadhi ya maafisa wa serikali katika mpaka wa Kenya na Tanzania, umezidi kuwaweka... Na WAANDISHI WETU
WINGU la maangamizi limetanda kote nchini huku aina mpya ya corona maarufu kama 'Delta' ikiua watu kwa... Na WINNIE ONYANDO
HUENDA visa vya wasafiri kulazimishwa kupima upya corona mpakani mwa Kenya na Tanzania vikakoma baada ya serikali hizo... NA WANGU KANURI
AGIZO la serikali la kudhibiti mkurupuko wa ugonjwa wa corona mwaka jana limewashurutisha Wakenya wengi kufanyia kazi... Na Titus Ominde
VIONGOZI wa kidini Kaskazini mwa Rift Valley (North Rift) wameshutumu wanasiasa kwa kupepeta usambazaji wa virusi vya... Na WANTO WARUI
Huku wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiripoti katika shule zao mpya za sekondari hii leo, kuna uwezekano wa maambukizi... Na CHARLES WASONGA
NAKUBALIANA na kauli ya maafisa wa afya katika kaunti ya Nairobi kwamba wanasiasa ndio wanachochea ongezeko la visa... Na SAMMY WAWERU
DICKSON Muceri amekuwa mkazi wa Nairobi kwa muda wa miaka kadhaa ila sasa kitovu hicho cha jiji kuu la nchi hakikaliki... Na MARY WANGARI
WANASAYANSI wamethibitisha kuwa kuchelewesha upokeaji dozi ya pili ya chanjo ya Covid-19 kwa kiasi cha miezi 10 baada ya... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na KINYUA BIN KINGORI
WAKATI huu viongozi wa kisiasa wameanza mapema kampeni zao kwa kuzuru maeneo mbalimbali nchini, ili kushawishi... Na WANDERI KAMAU
KULINGANA na Ripoti ya Jaji Mstaafu Akilano Akiwumi (1997) kuhusu chimbuko la ghasia za kikabila nchini, wanasiasa ndio... Na WANTO WARUI