text
stringlengths
3
16.2k
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti,  baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MAOSI. WAKULIMA wadogo vijijini wameanza kukumbatia mfumo wa kufuga nyuki ili kukabiliana na wezi ambao wamekuwa wakivamia mashamba na kuiba mazao nyakati za usiku. Wahalifu wanatajwa kulenga kuvuna ndizi, mahindi, viazi vitamu, miwa, parachichi, maharagwe na mihogo, hivyo basi kuwasababishia hasara wakulima, wengi wao wakikosa mazao ya kupeleka sokoni. Taifa Leo Dijitali ilizuru eneo la Gwa Kungu, Kaunti ya Laikipia katika barabara ya Nyahururu-Nyeri, ambapo tulibaini wakulima wamegeukia kilimo cha ufugaji nyuki, baada ya kuchoka kuibiwa matunda. Hali ni kama hiyo katika eneo la Ikonge, Busiango, Ekerenyo na Kebirigo Kaunti ya Nyamira. Mwalimu Edwin Nyariki kutoka Kebirigo aliambia Taifa Leo Dijitali kuwa changamoto inayokumba wakulima wengi hapa ni wizi wa mazao yakiwa shambani. Anasema wakulima ambao wamekuwa wakipata masaibu ni wenye mashamba yaliyo mbali na makazi yao. Anasema ufugaji nyuki, umeonekana kuzaa matunda kwa sababu wezi wanapotambua kuwa mkulima amefuga nyuki, huwa wanaogopa kukaribia mashamba yao. Isitoshe, baadhi yao huwa wanapata taabu sana kwa sababu hawajui ilikowekwa mizinga ya nyuki. Kulingana na Nyariki, kumeshuhudiwa idadi ndogo sana ya wizi katika mashamba ambayo wakulima wameamua kuwekeza kwenye miradi ya kufuga nyuki. Alifichulia Taifa Leo Dijitali kwamba siku za hivi karibuni, wakulima wengi wameingilia ufugaji nyuki ili kuwasaidia kulinda mashamba yao hasa nyakati za usiku, wanapokuwa wamelala. Kwa Kawaida, mwalimu Nyariki anasema nyuki huwa hawapendi kusumbuliwa ndiposa akaamua kuwafuga kwa sababu mbali na kumtunuku asali hutumika kama walinzi usiku. Aidha, Mwalimu Nyariki anasema ni lazima polisi waweke mikakati kusaidia wakulima kulinda mazao yao, akipendekeza wahusika wa wizi wachukuliwe hatua kali kisheria. Kwa upande mwingine, Faith Kemunto muuzaji wa ndizi na miwa katika kituo cha kibiashara cha Ikonge anasema wezi huchunguza mashamba ya wakulima nyakati za mchana kabla ya kutekeleza wizi usiku. Jumatano wiki iliyopita (Novemba 22, 2023), anadokeza kwamba wezi walivamia shamba lake na kuvuna sehemu kubwa ya miwa katika shamba lake. “Ingawa tumekuwa tukiripoti visa hivi kwenye vituo vya polisi, hawajakuwa wakichukua hatua yoyote huku wazee wa nyumba kumi na machifu wakionekana kulemewa,” akasema. Kemunto anasema alikasirika sana, ikizingatiwa kuwa alikuwa anategemea miwa hiyo kulipia watoto wake karo ya mwaka ujao, 2024. Anasema visa kama hivi vilianza kuripotiwa mwishoni mwa 2022, baada ya shughuli za kampeni za uchaguzi kukamilika.       You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MAOSI RAIS William Ruto amesema serikali itaanza kutafuta mikopo kutoka kwa akaunti za Wakenya. Wale ambao wamewekwa kwenye mpango wa kukopesha serikali ni mama mboga, mtu wa bodaboda na Mkenya yeyote yule mwenye kipato. Dkt Ruto alitoa matamshi hayo mnamo Jumapili, Novemba 26, 2023, hilo likionekana kama mojawapo ya hatua kustawisha uchumi wa taifa bila kutegemea mikopo kutoka mataifa ya nje. Kulingana na Rais, hivi sasa Kenya inategemea mikopo kutoka nje kwa sababu wakopeshaji wetu walitutangulia kwa kuweka akiba. “Badala ya kusaka hela kutoka kwa wale ambao walijiwekea akiba mapema, tunataka kuweka akiba yetu ili tujitegee,”akasema kiongozi wa nchi. Alisema Kenya inastahili kujifunza kutoka kwa nchi zilizoendelea, akisisitiza kwamba zimekuwa zikikopa pesa kutoka kwa wananchi wake. Awali, Rais Ruto aliungama kuwa serikali ilikuwa ikilemewa na mzigo mzito wa madeni na kwamba haikuwa na akiba ya kutosha kujitosheleza, ndiposa bado taifa linategemea mikopo. Akizungumza katika kanisa la Faith Evangelical Ministry, Karen Nairobi, Rais alisema miaka 10 hadi 15 ijayo, Kenya haitakuwa ikitegemea mikopo kutoka mataifa ya ng’ambo. Julai 2023, Naibu Rais Rigathi Gachagua alihimiza Wakenya wajifunze namna ya kuweka akiba ili nchi isitegemee mikopo kutoka ughaibuni.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA SAMMY WAWERU SERIKALI za Ugatuzi ni kati ya asasi zinazotarajiwa kuvuna pakubwa kupitia Ripoti ya Kamati ya Mazungumzo (NADCO), iliyotolewa Jumamosi, Novemba 25, 2023. Ripoti hiyo ya pamoja, iliyowasilishwa na wenyevikiti, Kimani Ichungwah (Kenya Kwanza) na Kalonzo Musyoka (Azimio la Umoja), miongoni mwa wanachama wengine, kamati hiyo inapendekeza mgao wa serikali ya kitaifa kwa kwa kaunti usipungue asilimia 20. Kwa sasa, serikali kuu huzipa serikali za ugatuzi asilimia 15 ya mapato yake. “NADCO inapendekeza Bunge lifanye marekebisho ya Katiba ili kuwezesha usawa wa ugavi wa raslimali, Serikali za Kaunti ziwe zinapokea asilimia isiyopungua 20 kwa mapato yote yanayouksanywa na Serikali ya Kitaifa, kutoka kiwango cha sasa cha asilimia 15,” inasema Ripoti ya Kamati hiyo. NADCO ilibuniwa kufuatia kupanda kwa joto la kisiasa nchini kati ya mrengo wa upinzani (Azimio) na serikali ya Kenya Kwanza), ili kupatanisha pande zote mbili. Kati ya Machi na Julai 2023, taifa lilishuhudia maandamano yaliyosababisha maafa ya watu, uharibifu wa mali na biashara. Ripoti ya NADCO pia inapendekeza kudumishwa kwa Fedha zinazotengewa Kuboresha Maeneobunge (NG-CDF), mgao wa National Government Affirmative Action Fund (NGAAF), na ule unaotengewa maseneta. Madiwani (MCAs), pia, huenda wakavuna kutokana na mapendekezo ya ripoti hiyo, NADCO ikitaka wadi kutengewa fedha zitakazokabidhiwa wabunge wawakilishi wa wadi kufanya maendeleo. Wakenya wakitarajia kuwa Ripoti ya Kamati hiyo ingewaletea afueni kupunguza gharama ya juu ya maisha, Kenya Kwanza na Azimio hawakukubaliana kuhusu kushushwa kwa ushuru (VAT) unaotozwa mafuta ya petroli kutoka asilimia 16 hadi 8, na kuondolewa kwa ada ya asilimia 3 inatozwa mwajiri na mfanyakazi kwa minajili ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu. Badala yake, masuala hayo yaliachiwa Rais William Ruto (Kenya Kwanza) na kinara wa Azimio, Bw Raila Odinga kutoa maamuzi. Aidha, wawili hao walitumiwa ripoti hiyo kwa njia ya kielektroniki. Bunge la Kitaifa, baadaye litakabidhiwa ripoti hiyo kuijadili, aidha, kuipitisha au kuiangusha.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA KALUME KAZUNGU MIKAHAWA na hoteli zaidi ya 20 zimefungwa huku wachuuzi wa vyakula vya barabarani wakifurushwa vichochoroni katika harakati za serikali ya Kaunti ya Lamu kudhibiti mlipuko wa maradhi ya Kipindupindu unaoshuhudiwa eneo hilo kwa sasa. Karibu watu 16 tayari wamefikishwa hospitalini, ambapo 9 wamelazwa na wengine wakitibiwa na kwenda nyumbani kufuatia maradhi hayo ambayo dalili yake ni kuharisha na kutapika. Katika mahojiano na Taifa Leo Dijitali Ijumaa, Novemba 24, 2023 Waziri wa Afya, Kaunti ya Lamu, Dkt Mbarak Bahjaj alisema miongoni mwa mikakati iliyochukuliwa kudhibiti maambukizi zaidi ni kunyunyizia dawa aina ya klorini visima karibu 200 hasa kwenye mitaa ya Lamu iliyoathiriwa na maradhi hayo. Dkt Bahjaj aliwasihi wananchi kudumisha usafi, ikiwemo ule wa vyoo na kunywa maji safi na yaliyotibiwa. Alisema mfuatilio na uorodheshaji wa visa zaidi vya maambukizi ya Kipindupindu kote Lamu inaendelea huku kituo maalumu cha karantini kuweka na kuwatibu wagonjwa wa Kipindupindu kikitengwa katika hospitali kuu ya rufaa ya King Fahd kisiwani Lamu. “Ni kweli tuna mkurupuko wa Kipindupindu Lamu, japo hatujaandikisha maafa yoyote. Watu 9 wamelazwa hospitalini, wengine 5 wakitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani. Hali inaendelea kudhibitiwa,” akasema Dkt Bahjaj.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA HATIMAYE Kamati ya Kitaifa kuhusu Mazungumzo (NADCO) imetoa ripoti yake ya mwisho lakini imefeli kukubaliana kuhusu suala nyeti la kupunguzwa kwa gharama ya maisha. Kwenye taarifa baada ya kutoa ripoti hiyo Jumamosi usiku, Novemba 25, 2023 Jijini Nairobi, wenyeviti wenza Kimani Ichung’wah na Kalonzo Musyoka walisema hawakukubaliana kuhusu pendekezo la kuondolewa kwa ushuru wa nyumba na kupunguzwa kwa VAT kwa mafuta kutoka asilimia 16 hadi asilimia 8. “Masuala haya ambayo yako kwenye Sheria ya Fedha ya 2023 sasa yamewasilishwa kwa vinara wetu Rais William Ruto (Kenya Kwanza) na Raila Odinga (Azimio) ili watoe mwelekeo kuyahusu,” wakasema. Aidha, Kamati hiyo imependekeza kuwa Wizara ya Kawi na Mamlaka ya Kusimamia Sekta ya Kawi na Mafuta (EPRA) kwa ushirikiano na Wizara ya Fedha zipunguze ada za utunzaji wa barabara na kuzuia kushushwa kwa ubora wa mafuta (anti adulteration levy) kwa kima cha Sh5 na Sh3, mtawalia. Wakati huu wenye magari hulipa Sh18 kwa lita kama ada ya kutunza barabara na kiasi sawa na hicho kama ada ya kuzuia mwenendo wa wafanyabiashara walaghai kuchanganya mafuta taa kwa petroli au dizeli. Aidha, kamati hiyo imekubaliana na pendekezo la Rais Ruto kwamba matawi yote matatu ya serikali yapunguze bajeti za usafiri kwa maafisa wao kwa kima cha asilimia 50. “Aidha, Tume ya Mishahara (SRC) ipunguze kiwango cha marupurupu yanayolipwa maafisa wanaosafiri kwa kima cha asimilia 30,” Mbw Ichung’wah na Musyoka wanaeleza. NADCO imekubaliana kwamba muda wa kushughulikiwa kwa kesi ya kupinga uchaguzi wa urais uongezwe kutoka siku 14 hadi siku 21. Kamati hiyo pia imekubaliana kuhusu pendekezo la kubuniwa kwa Afisi ya Kiongozi Rasmi wa Upinzani. “Wadhifa huo utamwendea mgombea urais atakayeibuka wa pili katika uchaguzi wa urais,” Ichung’wah na Musyoka wanasema. Aidha, ripoti hiyo imekubaliana kuhusu pendekezo la kubuniwa kwa wadhifa wa Waziri Mkuu. “Mshikilizi wa cheo hicho atapendekezwa, na baada ya kuidhinishwa na Bunge la Kitaifa, atateuliwa rasmi na Rais,” wenyekiti hao wanaeleza. NADCO pia imependekeza kuwa uanachama wa jopo la uteuzi wa  mwenyekiti na makamishna wapya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) upanuliwe kutoka watu saba hadi tisa. Hata hivyo, kamati hiyo haijatoa maelezo zaidi kuhusu suala hilo. Mbw Ichung’wah na Musyoka pia wanasema kuwa kamati hiyo imependekeza kuwa na hazina ya ustawi wa maeneo bunge (NG-CDF), hazina ya usawazishaji (NGAF) na ile ya kufadhili mpango wa kufuatilia utendakazi wa serikali za kaunti (SOF) ziwekwe kwenye Katiba. Nakala za ripoti hiyo zimewasilishwa kieletroniki kwa Rais Ruto na Bw Odinga. Baadaye itawasilishwa katika Bunge la Kitaifa na Seneti ili ijadiliwe na kupitishwa au ikataliwe.
Tags
You can share this post!
Previous article
EL-NINO: Serikali yaahidi bei ya umeme itapungua hivi...
Next article
Athari za El Nino: Mkurupuko wa Kipindupindu Lamu...
T L
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA WYCLIFFE NYABERI Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula amezitaka serikali za kaunti kutumia rasilimali wanazopewa na serikali ya kitaifa vyema. Bw Wetang’ula amesema utekelezaji wa Katiba ya Kenya ya 2010, ulianzisha mfumo wa ugatuzi wa serikali na kwa hivyo rasilimali zozote zinazoelekezwa kwa kaunti zinafaa kutumiwa kuboresha ustawi wa raia na jamii kwa ujumla. Akiwahutubia waumini katika Kanisa Katoliki la Nyabururu Kaunti ya Kisii mnamo Jumamosi, Novemba 25, 2023, Bw Wetang’ula alikiri hali ngumu ya kiuchumi na dhiki ya kisiasa ambayo Kenya ilikuwa ikipitia lakini alieleza matumaini yake kwamba Wakenya wataibuka washindi. “Sisi matatizo yetu tunayajua na sisi ndio wa kuyatatua, asitoke mtu wa nje aseme anatusaidia. Ndiyo maana uliona bungeni tulikubali kuundwa kwa Kamati ya Kitaifa ya Maridhiano (NADCO). Muda wao umekwisha. Ripoti watakayotoa itakuja Bungeni na itajadiliwa humo,” Bw Wetang’ula alisema. Aliwataka viongozi wote waliochaguliwa kushirikiana na kuepuka maneno matupu. “Kila kiongozi anafaa kuchangia maendeleo ya taifa letu. Tuepuke siasa za migawanyiko. Viongozi wanapopigana, wanaoteseka zaidi ni raia wa kawaida,” Spika Wetang’ula alisema. Hii ni mara ya pili kwa Bw Wetang’ula kuzuru eneo la Kisii katika muda wa mwezi mmoja. Katika ziara zake zote, aliwaomba watu wa Kisii kusalia na umoja na kuunga mkono utawala wa Kenya Kwanza. Aliwasifu watu kutoka jamii ya Gusii kwa uthabiti wao ulioonyeshwa kwa bidii na kujitolea. Alisema hilo lilijiri tangu alipofanya kazi Kisii kama Hakimu mapema miaka ya 90 kabla ya kujiingiza katika siasa. Katika ziara yake ya Jumamosi, ya kupamba nusu-Jubilii ya makasisi watatu wa Dayosisi ya Kisii, Bw Wetang’ula aliandamana na Seneta Richard Onyonka, Wabunge Silvanus Osoro (Mugirango Kusini), Daniel Manduku (Nyaribari Masaba), Charles Onchoke (Bonchari), Innocent Obiri (Bobasi), Japheth Nyakundi (Kitutu Chache Kaskazini) na Mwakilishi wa Wanawake Dorice Aburi. Idadi kubwa ya Madiwani pia waliandamana na Spika. Seneta Onyonka aliendeleza ukosoaji wake kwa Gavana Simba Arati kwa jinsi alivyokuwa akiendesha kaunti. Alidai kuwa tangu gavana achukue wadhifa huo, amekataa kabisa kuwasikiliza viongozi wengine waliochaguliwa. Dkt Manduku na Bi Aburi walisema gavana Arati alikuwa amekataa waziwazi kuwalipa wanakandarasi pesa kwa kazi waliyofanya. Bw Arati mara kadhaa amebainisha kuwa bili nyingi ambazo wanakandarasi walikuwa wakidai si za kweli. Chama cha wakandarasi hata hivyo kimesema kuwa kazi yao ilikuwa ya kweli na wanapaswa kulipwa stahiki zao. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MHARIRI
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini.
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na BENSON MATHEKA
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na MASHIRIKA
LONDON, Uingereza
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya... Na ELIZABETH MERAB
WANASAYANSI wanachunguza kuhusu mchipuko wa virusi vipya vya corona aina ya Delta, katika nchi za Amerika, Uingereza,... Na MAUREEN ONGALA
MASAIBU ambayo wagonjwa wa Covid-19 hupitia katika kaunti za Pwani, yameanikwa wazi baada ya kifo cha afisa mkuu wa... SIAGO CECE na ANTHONY KITIMO
UFISADI miongoni mwa baadhi ya maafisa wa serikali katika mpaka wa Kenya na Tanzania, umezidi kuwaweka... Na WAANDISHI WETU
WINGU la maangamizi limetanda kote nchini huku aina mpya ya corona maarufu kama 'Delta' ikiua watu kwa... Na WINNIE ONYANDO
HUENDA visa vya wasafiri kulazimishwa kupima upya corona mpakani mwa Kenya na Tanzania vikakoma baada ya serikali hizo... NA WANGU KANURI
AGIZO la serikali la kudhibiti mkurupuko wa ugonjwa wa corona mwaka jana limewashurutisha Wakenya wengi kufanyia kazi... Na Titus Ominde
VIONGOZI wa kidini Kaskazini mwa Rift Valley (North Rift) wameshutumu wanasiasa kwa kupepeta usambazaji wa virusi vya... Na WANTO WARUI
Huku wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiripoti katika shule zao mpya za sekondari hii leo, kuna uwezekano wa maambukizi... Na CHARLES WASONGA
NAKUBALIANA na kauli ya maafisa wa afya katika kaunti ya Nairobi kwamba wanasiasa ndio wanachochea ongezeko la visa... Na SAMMY WAWERU
DICKSON Muceri amekuwa mkazi wa Nairobi kwa muda wa miaka kadhaa ila sasa kitovu hicho cha jiji kuu la nchi hakikaliki... Na MARY WANGARI
WANASAYANSI wamethibitisha kuwa kuchelewesha upokeaji dozi ya pili ya chanjo ya Covid-19 kwa kiasi cha miezi 10 baada ya... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na KINYUA BIN KINGORI
WAKATI huu viongozi wa kisiasa wameanza mapema kampeni zao kwa kuzuru maeneo mbalimbali nchini, ili kushawishi... Na WANDERI KAMAU
KULINGANA na Ripoti ya Jaji Mstaafu Akilano Akiwumi (1997) kuhusu chimbuko la ghasia za kikabila nchini, wanasiasa ndio... Na WANTO WARUI
KWA mara nyingine tena tuzo inayoenziwa sana kote ulimwenguni imerudi katika eneo letu la Afrika Mashariki mara hii... Na DOUGLAS MUTUA
MWAFRIKA akiwajibishwa na Mzungu hupiga kamsa na kudai anaonewa, ati msingi wa maonevu ni ubaguzi wa rangi... Na WANDERI KAMAU
MOJA ya changamoto kuu zinazokikumba kizazi cha sasa nchini ni ukosefu wa ufahamu wa lugha zao asili.
Ingawa lugha... Na KINYUA BIN KINGORI
JUHUDI za kuhakikisha taifa limefanikiwa kupiga vita ufisadi lazima ziendeshwe kuambatana na Katiba, bila njama... Na WANDERI KAMAU
UFICHUZI wa sakata ambapo watu maarufu duniani wamekuwa wakificha mabilioni ya fedha katika akaunti za siri ng’ambo... Na FAUSTINE NGILA
NINA imani kuwa iwapo kufikia sasa hujawahi kuelewa teknolojia ya blokcheni, leo utaelewa kwa kuwa jana uliathirika... Na CHARLES WASONGA
NI jambo la kusikitisha kuwa ni wakati kama huu ambapo uchaguzi mkuu unakaribia ndipo wanasiasa wametambua umuhimu wa... Na MARY WANGARI
IDADI ya watu wanaoandaa hafla za uchangishaji pesa za kugharamia matibabu imeongezeka pakubwa katika siku za hivi... Na CECIL ODONGO
CHAMA cha Kanu bado kina safari ndefu kurejelea umaarufu wake wa enzi za utawala wa chama kimoja na miaka ya 90 hata... Na CHARLES WASONGA
UTEUZI wa waliokuwa maafisa wanne wa ngazi za juu katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kushikilia nyadhifa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Naomi Wamboi, 21, ndiye anatupambia yeye ni mwanamitindo aliyewahi kushinda tuzo za Miss Nakuru. Akipata muda anapenda kusafiri na... Winnie Miriam Nechesa 21, ni mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu Cha Maasai Mara kaunti ya Narok.Anapenda kuchora, na kujumuika na... Lilian Njeri mwenye umri wa miaka 21 ndiye anatupambia jarida letu leo.Yeye ni mwanamitindo na mkaazi wa Narok.Uraibu wake ni kusafiri na... Mary Njeri mwenye umri wa miaka 21 ni mkaazi wa mtaa wa Langalanga kaunti ya Nakuru.Yeye ni mwanafasheni wa mapambo na vipodozi.Uraibu wake... Marylene Watiri mwenye umri wa miaka 22 ni mtaalam wa Beauty Therapy jijini Nairobi, aidha yeye ni mwanamitindo na mlimbwende.Uraibu wake... Zaweria Njoki mwenye umri wa miaka 21 ni Video Vixen kutoka kaunti ya Nakuru.Uraibu wake ni kuandika makala ya kitaaluma na kujumuika na...
Malkia wetu leo ni  Babra Ingasiani mwenye umri wa miaka 21, yeye ni mzaliwa wa kaunti ya Kakamega.Uraibu wake ni kusakata densi ya... Pauline Kimani mwenye umri wa miaka 23 ndiye anatupambia jarida letu leo.Yeye ni mkaazi wa eneo la Lanet na mfanyikazi mjini Nakuru.Uraibu...
Sayfer Godez ni mkaazi wa Nakuru .Anapenda kushiriki kwenye majukwaa ya mapambo na urembo.Uraibu wake ni kusafiri na kujumuika na... Sylvia Wangeci 23 ni mzaliwa wa Molo, na mwanafunzi katika Chuo Kikuu Cha MKU tawi la Nakuru.Uraibu wake ni kusafiri na... Mical Abulatsia Imbukwa, 28, ni mwanahabari katika shirika moja jijini Nairobi. Uraibu wake ni kutazama filamu za Afro sinema na kujumuika... Faith Karungari mwenye umri wa miaka 22 ni mwanafasheni na mwanamitindo maarufu kutoka Nakuru.Uraibu wake ni kuogelea na kusikiliza muziki... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na RICHARD MUNGUTI
MAHAKAMA ya Juu jana ilianza kusikiza rufaa ya mpango wa kubadilisha katiba (BBI) huku Mwanasheria Mkuu Bw Paul... Na BENSON MATHEKA
RAIS Uhuru Kenyatta jana Jumapili alisema kuwa ndoto yake ya kubadilisha katiba ya Kenya iliyopitishwa 2010 kupitia... Na CHARLES WASONGA
KWA mara nyingine Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza kuwa mageuzi ya katiba yaliyopendekezwa katika Mswada wa Mpango wa... Na JOSEPH WANGUI
Mwanasheria Mkuu, Paul Kihara Kariuki hatimaye amewasilisha rasmi rufaa katika Mahakama ya Juu kupinga uamuzi wa... Na Gitonga Marete
KIONGOZI wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi amesisitiza kuwa Bunge linapaswa kurejelea Mpango... Na Leonard Onyango
NAIBU wa Rais William Ruto amewataka wabunge kujadili masuala nyeti yanayoathiri Wakenya badala ya kujaribu kufufua... Na CHARLES WASONGA
JUHUDI za wabunge wanaoegemea mrengo wa Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga kutumia bunge kupitisha... Na WALTER MENYA
JUHUDI za kuokoa mchakato wa marekebisho ya katiba kupitia mpango wa maridhiano (BBI) zimefikishwa rasmi katika Mahakama... Na FRANCIS MUREITHI
KUSAMBARATIKA kwa Mpango wa Kubadilisha Katiba (BBI) kumefifisha pakubwa ushawishi wa kisiasa wa mwenyekiti wa Kanu,... Na WANDERI KAMAU
KUHARAMISHWA kwa Mpango wa Kubadilisha Katiba (BBI) na Mahakama ya Rufaa kunatarajiwa kutoa mwelekeo mpya kwa siasa za... Na WANDERI KAMAU