text
stringlengths
3
16.2k
NA RICHARD MAOSI WAKAZI wa mtaa wa Mazembe viungani mwa mji wa Nakuru wamekiri kuhangaishwa na wezi ambao huwaibia na kuwasindikiza hadi nyumbani. Huwawekea ulinzi huo makusudi ili kuhakikisha kwamba wateja wao wanafika nyumbani salama salimini. Kwa kawaida, wahuni wamebuni mbinu mpya ya kutembea na mbwa wakubwa nyakati za usiku, ili kujiwekea ulinzi wa kibinafsi. Owen Shibala mwendeshaji bodaboda kati ya Nakuru mjini na Mazembe, anasema hajui walikotoa ujasiri walio nao kushika doria usiku utadhani ni polisi. Mazembe ni mojawapo ya mitaa ambayo hushuhudia visa vya kihalifu na utumiaji wa mihadarati mara kwa mara. “Ukikutana nao usiku ni lazima usalimishe kila kitu lau sivyo utaona cha mtema kuni. Watakucharaza viboko na kuiba kila kitu cha nguvu,”akasema. Hata hivyo, wanapoiba hujitwika jukuma la kuwasindikiza wakazi, wasije wakakutana na vibaka wengine barabarani. Aidha, wanalia sare za polisi jambo linalowafanya baadhi ya raia kuamini huenda wanashirikiana na maafisa wa polisi. Baadhi yao wanajifanya ni maafisa wa polisi ambao huwa wameshika doria, wakilenga kuhangaisha wapita njia wanaotoka kazini usiku. Agnes Wahome mfanyibiashara mtaani Rhonda anasema huwa wamejihami kwa visu, rungu na wako tayari kupigana. Kulingana na Bi Wahome, hii ni hali ya kawaida siku hizi katika mitaa ya Manyani, Bondeni na Freearea ambapo vijana wengi wamejiingiza kwenye uhalifu. Bi Wahome anasema wahalifu wengi wanajulikana, kwani ni vijana wadogo kutoka mitaa jirani ya Flamingo na Lakeview. Mkazi huyo angependa polisi kushika doria katika maeneo husika ili kuzuia kuzuka kwa magenge hatari yanayohangaisha wenyeji. Hili linajiri siku chache baada ya Taifa Leo Dijitali kufichua visa vya wizi ambapo baadhi ya wezi kutoka kwenye mtaa wa Gioto, Nakuru wamekuwa wakipika chakula katika kila nyumba wanamoingia kuiba. Mtaa wa Bondeni, Kaunti ya Nakuru ambapo wezi huwaibia wakazi na kuwasindikiza mpaka nyumbani. PICHA|RICHARD MAOSI
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L

You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MUNGUTI MASKWOTA wapatao 10,000 wamewasilisha upya kesi katika Mahakama ya Upeo wakiomba ibatilishe uamuzi kwamba wafukuzwe kutoka kwa shamba la ukubwa wa ekari 25,000 wanalong’ang’ania umiliki wake na familia ya mwanasiasa marehemu Mark Too. Maskwota hao wanaodai mababu zao ndio waliotimuliwa kutoka kwa shamba hilo enzi za ukoloni, wanasema walipewa shamba hilo rasmi na aliyekuwa Rais hayati Daniel arap Moi, kisha Kamishna wa Ardhi M Okundu akaratibisha uamuzi huo mwaka 2007. Katika ombi lililowasilishwa na wakili William Arusei chini ya sheria za dharura, kikundi cha maskwota hao–Sirikiwa Squatters Group–kimeomba mahakama ibatilishe uamuzi huo kwa vile ilitegemea ushahidi ambao haukuwa umewasilishwa katika kesi waliyoshtaki katika Mahakama ya kuamua kesi za mashamba (ELC), Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu. Pia wameeleza bayana Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaack Lenaola, na William Ouko walitegemea ushahidi wa Afisa wa Ugavi wa Mashamba R J Simiyu kutoa uamuzi wang’atuke shambani. Maskwota hao wamesema ushahidi wa Bw Simiyu uliowasilishwa mbele majaji hao saba kwa njia ya afidaviti ni mpya na kamwe “haukuwasilishwa mbele ya Jaji Antony Ombwayo aliposikiliza na kuamua kesi hiyo 2017.” Pia wanasema ushahidi huo haukuwasilishwa Mahakama ya Rufaa iliyosikiliza rufaa iliyowasilishwa na kampuni ya Fanikiwa, familia ya marehemu Mark Too, kampuni ya Lonrho Agribusiness (EA) Ltd, na Bw David K Korir. Hivyo basi, maskwota hao wanaeleza mahakama hii ya upeo kwamba ni kinyume cha sheria kutegemea ushahidi mpya kutoa uamuzi wa kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma. “Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu wa Desemba 15, 2023, hauna mashiko kisheria na kamwe hauna nguvu kisheria kuwatimua maskwota hawa kutoka kwa shamba lao,” asema Bw Arusei. Pia maskwota hawa wanadai kwamba badala ya Mahakama ya Juu kujadili masuala ya kikatiba jinsi ilivyo jukumu lake, majaji hao walianza kufafanua na kutafsiri ushahidi wa watu binafsi na kuelezea maana ya ‘skwota’. Mahakama hii imeombwa ikague upya uamuzi iliyotoa kwa vile ilidanganywa na walalamishi na pia kutendewa ujanja. Akinukuu maamuzi ya majaji wastahiki kama vile Lord Dening, Bw Arusei amesema, mahakama ikigundua ilipotoshwa au kudanganywa na upande mmoja, iko na mamlaka na uwezo wa kufutilia mbali uamuzi iliyotoa na kuandika mwingine. Maskwota hao wanaomba Mahakama ya Juu iwarudishe shambani kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Ombwayo na Mahakama ya Rufaa. Vile vile mahakama hiyo imekosolewa kwa kumshambulia hayati Moi katika uamuzi huo pasi kutoa agizo wasimamizi wa mali yake wafike mbele yao kutoa mwanga kuhusu suala la umiliki wa shamba hili lililorudishwa kwa serikali na kampuni iliyokuwa inakuza miti inayotumika katika viwanda vya ngozi. Naibu msajili wa Mahakama ya Juu Nelly Kariuki aliwaamuru maskwota hao wawakabidhi nakala za kesi hii yao mpya wahusika wote kabla ya Januari 31, 2024, kesi itakapotajwa tena kwa maagizo zaidi. Jaji aliyesikiliza kesi hii mpya hakuiratibisha kuwa ya dharura ila aliamuru pande zote ziwasilishe ushahidi katika muda wa siku 14 kuanzia Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti,  baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

FATUMA BARIKI na MARY WANGARI Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu anatarajiwa kutangaza rasmi matokeo ya KCPE kesho Novemba 23, 2023 katika mchakato ambao utakamilisha zoezi hilo lililoanza mwezi jana. Duru zimeambia Taifa Leo kwamba Waziri Machogu atatoa tangazo hilo saa mbili asubuhi katika Jumba la Mitihani, Nairobi, muda mfupi baada ya kukabidhi ripoti ya mtihani huo kwa Rais kama ilivyo tamaduni. Mtihani wa KCPE wa mwaka huu ni wa mwisho chini ya mfumo wa elimu wa 8-4-4 baada ya serikali kuanzisha mtaala wa Umilisi na Utendaji (CBC) ambao umeingia Sekondari Msingi na ambao wanafunzi watakuwa wakifanyiwa tathmini ya Umilisi na Utendaji (CBA).
Wakenya zaidi ya 24 milioni waliofanya mitihani ya KCPE wana kumbukumbu mseto kuhusu mfumo wa elimu wa 8-4-4. Kwa takriban miongo minne, mtihani wa KCPE umekuwa kama suala la kufa kupona kwa wazazi, walimu, wanafunzi na wadau wengine wa elimu na hali itakuwa hiyo hiyo matokeo yatakapotangazwa mwaka huu. Mitihani ya KCPE ilikuwa kigezo kilichotumiwa kuteua wanafunzi waliojiunga na shule za upili ushindani ukiwa kati ya kitaifa na zile za mkoa. Idadi ya masomo yaliyotahiniwa katika KCPE vilevile imezidi kubadilika kadri miaka inavyosonga kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara kwenye mtaala wa elimu nchini. Baadhi ya masomo kama vile Sayansikimu, Kilimo, Muziki na Sanaa yalifutiliwa mbali. Katika juhudi za kuwaandaa watahiniwa kwa KCPE, kulizuka mitindo isiyofaa kama vile masomo ya ziada almaarufu kama tusheni. Vipindi vya masomo haya ya ziada vingefanyika alfajiri kabla ya kuanza kwa ratiba rasmi ya masomo, nyakati za jioni baada ya vipindi vya masomo mchana kutwa, wikendi na hata nyakati za likizo wanafunzi wanapostahili kupumzika kutokana na kazi za shuleni. Mwisho wa KCPE unatazamiwa kubadilisha mtindo wa shule nchini ikiwemo uorodheshaji wa “wanafunzi bora” na “siri za ufanisi” kwenye runinga za kitaifa. Idadi ya watahiniwa wa KCPE mwaka huu iliongezeka kwa 170,982, ikilinganishwa na watahiniwa 1, 244,333 waliofanya mtihani huo mnamo 2022, kwa mujibu wa Ripoti iliyowasilishwa Bungeni kuhusu Maandalizi ya Mitihani na Masuala mengineyo katika Elimu ya Msingi. Endelea kutegea humu kwa habari na matukio kuhusu mwanafunzi bora, shule bora pamoja na mengine mengi yatakayoibuka kutokana na zoezi hili. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MASHIRIKA PRETORIA, AFRIKA KUSINI WABUNGE nchini Afrika Kusini walipiga kura siku ya Jumanne kuunga mkono kufungwa kwa ubalozi wa Israel jijini Pretoria. Aidha, walifanya hivyo kushinikiza kusimamishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia hadi makubaliano ya kusitisha mapigano yatakapokubaliwa katika vita vyake na kundi la Kiislamu la Palestina, Hamas, eneo la Gaza. Azimio hilo kwa kiasi kikubwa litakuwa alama iliyowekwa kwani itakuwa juu ya serikali ya Rais Cyril Ramaphosa iwapo itatekeleza; msemaji wa ofisi ya rais alisema Ramaphosa “anakumbuka na kuthamini” mwongozo wa bunge kuhusu uhusiano wa kidiplomasia wa Afrika Kusini na Israel, hasa kuhusu hadhi ya ubalozi. “Rais na Baraza la Mawaziri wanahusika katika suala hilo, ambalo linabaki kuwa jukumu la afisa mkuu mtendaji wa kitaifa,”Vincent Magwenya alisema. Ramaphosa na maafisa wakuu wa wizara ya mambo ya nje wamekuwa wakikosoa vikali uongozi wa Israel wakati wa kampeni yake mbaya ya kijeshi dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza wenye wakazi wengi, wakiitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kuwachunguza kwa uhalifu wa kivita unaoweza kutokea. Hata hivyo, Ubalozi wa Israel haukujibu chochote kuhusiana na tukio hilo. Fauka ya hayo, manmo Jumatatu wiki hii, Balozi wa Israel jijini Pretoria aliitwa tena Tel Aviv kwa mashauriano kabla ya upigaji kura, ambao siku ya Jumanne ulipitishwa kwa sauti ya juu huku matokeo yakiwa kura 248 dhidi ya kura 91. Zaidi ya hayo, azimio hilo la bunge lililetwa na chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF) wiki iliyopita wakati chama tawala cha African National Congress kilipoahidi kuunga mkono kile ambacho kimekuwa msimamo mkuu wa kidiplomasia kwa Afrika Kusini tangu Nelson Mandela awe rais wa kwanza kuwahi kuchaguliwa kidemokrasia katika nchi hiyo mnamo 1994. Kiranja wa Wengi wa ANC, Pemmy Majodina, alirekebisha hoja ya mwisho ya rasimu ya azimio la EFF la kutaka ubalozi huo kufungwa na kusimamishwa kazi kwa njia ya kidiplomasia, na kujumuisha maneno haya: “… Mazungumzo yanayoratibiwa na Umoja wa Mataifa ambayo matokeo yake lazima yawe amani ya haki, endelevu na ya kudumu.” Vilevile, EFF ilipendekeza hoja hiyo siku ya Alhamisi kwa mshikamano na watu wa Palestina kuhusu mashambulizi ya Israel kwa mabomu na uvamizi wa Gaza inayotawaliwa na Hamas, iliyochochewa na uvamizi mbaya wa wanamgambo wa Hamas ndani ya Israel mnamo Oktoba 7. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA JURGEN NAMBEKA NAIBU wa Rais, Rigathi Gachagua, ameitaka Idara ya Uchunguzi wa Jinai (DCI) kuwapa nafasi wataalamu mbalimbali kujiunga nayo, ili kusaidia katika uchunguzi wa makosa na visa mbalimbali vya uhalifu. Akizungumza jijini Mombasa wakati wa ufunguzi wa Kongamanao la Wahasibu (ICPAK), Bw Gachagua alieleza kuwa maafisa kadhaa husishia kufanya makosa katika uchunguzi kwa sababu ya kutoelewa ipasavyo masuala fulani. “DCI inafaa ikubali wataalamu wawe katika vikosi vyao. Baadhi ya maafisa hawa wanaochunguza makosa yanayohusu fedha hawaelewi lolote. Sasa ikiwa anapaswa kuandika ripoti katika masuala ambayo yeye mwenyewe haelewi, itawezekanaje?” akauliza Bw Gachagua. Kulingana naye, alikuwa ametatizwa sana na maafisa wa upelelezi ambao hawakuwa wakielewa masuala ya fedha, akaunti yake ilipofungwa mwaka 2020. Bw Gachagua anasema wapelelezi hao hawakuelewa jinsi Sh200 milioni zilikuwa zikitumika kuzaa faida kwa kuhamishwahamishwa kutoka kwa akaunti hiyo hadi nyingine kwa ajili ya shughuli za kibiashara. “Maafisa walitumwa kuchunguza maisha yangu. Nilikuwa nimeweka pesa zangu katika akaunti moja ya kibiashara kwa miaka minane. Faida ya riba nayoipata naihamisha kwenda kwenye akaunti nyingine, inapata faida nairejesha. Aliyekuwa akinichunguza kwa kutoelewa alisema ninapata Sh800 milioni kila mwaka. Hili halingefanyika kama kungekuwa na mhasibu katika kikosi,” akasema Naibu wa Rais. Aliwashauri wahasibu kutuma maombi ya kuwa maafisa makadeti kusaidia vikosi vya ulinzi kufanya uchunguzi wa makosa ya kifedha.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

WINNIE ATIENO NA JURGEN NAMBEKA BARAZA la magavana (CoG) limevunja kimya chake kuhusu mvutano ambao umekuwa ukishuhudiwa baina ya gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir na Naibu wa Rais Rigathi Gachagua kuhusiana na kutolewa kwa fedha za kukabiliana na mvua za El-Nino. Katika barua iliyotazamwa na Taifa Leo Dijitali baraza hilo kupitia kwa mwenyekiti wake, Bi Anne Waiguru, lilikanusha madai ya kupokea fedha za kukabiliana na mvua hizo. “Hadi tarehe ya leo (Jumatano, Novemba 22, 2023, tungependa kueleza kuwa serikali za kaunti hazijapokea fedha zozote kutoka kwa hazina ya kitaifa zilizotengwa kushughulikia mvua nyingi inayoshuhudiwa katika sehemu mbalimbali humu nchini,” ikasema sehemu ya barua hiyo. Baraza hilo lilieleza kuwa serikali za kaunti zilikuwa zikisubiri mgao wa hadi Sh62.58 bilioni ambao hupeanwa kwa kila kaunti kila mwezi. Baraza hilo lilikashifu semi zinazotolewa kuashiria kuwa serikali za kaunti zilikuwa zimepewa mgao kukabiliana na El Nino, na athari zake. “Tunataka kueleza kuwa semi hizo zinakiuka umoja na ushirikiano wa serikali za kaunti na ya kitaifa kama ilivyo kwenye Kipengee cha Sita sehemu ya Pili ya Katiba,” ikasema barua hiyo. Haya yanajiri magavana wa upinzani wakipinga semi za Naibu wa Rais Rigathi Gachagua, kwamba wamepokea fedha za kukabiliana na athari za mafuriko. Wakiongozwa na Bw Abdulswamad Nassir (Mombasa) na mwenzake James Orengo (Siaya), magavana hao wamemtaja Bw Gachagua kuwa mwongo. “Ukweli ni kwamba, serikali kuu mpaka wa leo hawajatoa hata senti moja kwa serikali za kaunti zote nchini. Hata kule kwake Nyeri, hawajatoa hata ndururu. Hata kule Siaya tumekabiliwa na mafuriko, watu wamehama na wahanga wana matatizo ya makazi na chakula,” alisema Bw Orengo. Gavana Orengo na Bw Nassir waliitaka serikali kuu kueleza bayana fedha zilizotengwa kukabiliana na El Nino zilikopelekwa. Alisema serikali ya Kenya Kwanza ni ya unafiki na imekumbwa na shutma za ufisadi. “Naibu wa Rais ni muongo, kila anachoongea ni uongo mtupu. Ahadi anazotoa hatimizi. Watu waache utapeli,” aliongeza Bw Orengo. Aliwasihi wakazi wa Mombasa kusimama kidete na ODM ili chama hicho cha upinzani kiendelee kupata uungwaji mkono mkubwa. Naye Bw Nassir alisema ataendelea kuwa mwanachama wa ODM akisisitiza kuwa kinara wa upinzani Bw Raila Odinga amemlea kisiasa. Alimtaka Bw Gachagua kuwa mkweli. “Waswahili wanamsemo, ‘Ukweli hauna haja ya nguzo ya kusimama. Hakuna hata ndururu imefika Mombasa’,” alisema Bw Orengo. Naibu wa Rais akihutubu eneo la Karen, Jijini Nairobi, alieleza kuwa magavana hawapaswi kusubiri fedha zozote kutoka kwa serikali kuu. “Nimesikia magavana wakisema hawajapokea fedha za El Nino, hakuna fedha kama hizo zinazokuja. Tunawataka watumie fedha za dharura au wabadilishe mkondo wa fedha zingine,” akasema Bw Gachagua. Gavana Nassir alisema serikali za kaunti zimekuwa zikishirikiana na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kusaidia wahanga wa El Nino. “Mimi hata naomba Mungu tupewe hizo fedha. Usidanganye watu wakati wanapitia dhiki, usidhulumu watu,” alisema Bw Nassir.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA WINNIE ATIENO MAFURIKO yaliyoshuhudiwa Mombasa yamegeuzwa kuwa uwanja wa kisiasa baada ya Mbunge wa Nyali Bw Mohammed Ali, na Naibu Rais Rigathi Gachagua kumkashifu Gavana Abdulswamad Nassir kwa ‘kutosaidia’ waathiriwa wa janga la mafuriko. Mombasa na Tana River ni mojawapo ya kaunti zilizoathirika pakubwa kutokana na mafuriko ambayo yaliacha zaidi ya wakazi 3, 000 bila makao. Msaada wa vyakula kutoka serikali kuu unakabidhiwa na kusambazwa na Mbunge wa Nyali badala ya Gavana. Bw Gachagua ambaye alikuwa ametoka kuhudhuria mkutano wa wahasibu alisimama eneo la Kisauni akiandamana na Bw Ali wakamshtumu Bw Nassir kwa kutosaidia wahanga wa janga la mafuriko. Bw Ali alimtaka Bw Nassir kuweka maslahi ya wakazi wa Mombasa mbele na kutumia fedha za kaunti kusaidia wakazi walioachwa bila makao baada ya majumba yao kusombwa au kuzingirwa na maji. “Naibu wa Rais nashukuru ujio wako, nilikuambia Mombasa inazama, kina mama na watoto hawana chakula nyumba zimechukuliwa na maji mufike haraka mutusaidie. Tunashukuru ulitupatia chakula ambacho tulisambaza kwa wakazi wa Nyali na Kisauni,” alisema Bw Ali. Naibu wa Rais alisema mvua inayoendelea ya El-Nino imeathiri pakubwa nusu ya taifa hili. Hata hivyo, alisema serikali kuu inaweka juhudi kukabiliana na athari hasa kuokoa maisha. “Tunaweka kila juhudi tukishirikiana na kaunti na wawekezaji wengine ili watu wetu wasiumie au kuteseka. Hata hivyo, tunasaka suluhu la kudumu,” alisema Bw Gachagua katika eneo la Barawa, wilayani Kisauni ambapo alikutana na familia zilizoathirika na mafuriko. Alizitaka serikali za kaunti kuweka juhudi za kukabiliana na athari za mafuriko. “Serikali za kaunti zifanye bidii na mikakati ambayo itaokoa maisha na kuepuka maafa, sababu mvua itaendelea hadi mapema mwaka ujao,” alionya Bw Gachagua ambaye alikuwa ameandamana na Waziri Penina Malonza (Maeneo Kavu), Wabunge, Kuria Kimani (Molo), Feisal Bader (Msambweni MP), Stanley Muthama (Lamu Magharibi), Paul Biego (Chesumei), na seneta wa Lamu Bw Joseph Kamau. Bw Ali alimtaka Gavana Nassir atoe fedha za kusaidia wahanga wa mafuriko. “Toa pesa Gavana, wacha kuziweka mfukoni na watu wanakufa huku nje,” alisema Bw Ali. Bw Ali ambaye ndiye mbunge pekee aliyechaguliwa kupitia chama cha UDA Mombasa, aliwahakikishia wakazi kuwa atawasaidia kukabiliana na athari za mafuriko. Mwanasiasa huyo alisema atazuru wilaya zote, ikiwemo Jomvu, Likoni, Changamwe na Mvita kupeleka chakula cha msaada. Mnamo Jumapili, Bw Ali alisema amepokea chakula cha msaada kutoka kwa serikali kuu kusaidia wahanga wa mafuriko. Alisema serikali ilisambaza chakula hicho baada ya kutoa ombi hilo. Bw Ali alisaidiwa na Mawaziri Penina Malonza (Maeneo Kavu) na mwenzake Bw Salim Mvurya (Uchumi Samawati) kusambaza chakula kwa wakazi. Alisema ataendelea kusaidia waathiriwa wote katika kaunti ya Mombasa na Pwani kwa jumla. Hata hivyo, Gavana Nassir alisema Naibu wa Rais anamlenga kisiasa. “Hatujapewa fedha zozote na serikali kuu za El Nino. Ninaomba wanahabari wawasiliane na Hazina ya Kitaifa ya Fedha na Msimamizi wa Bajeti Kuu kutathmini ukweli,” alisema Bw Nassir. Alisema fedha za mwisho kaunti yake ilipokea ilikuwa Sh600 milioni mwezi wa Oktoba 2023. Gavana huyo alisema Bw Gachagua amekuwa akimshtumu kisiasa kutokana na msimamo wake kuhusu kupinga hatua ya serikali ya kutaka kubinafsisha bandari ya Mombasa.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MERCY SIMIYU CHAMA cha Wiper kimetishia kushinikiza wananchi kurejea barabarani, iwapo Mazungumzo ya Maridhiano yanayoendelea hayatazingatia umuhimu wa kupunguza gharama ya maisha. Katibu mkuu wa chama hicho, Bi Aisa Abdallah alisema viongozi wa Wiper wako tayari kurejelea maandamano, na kusisitiza kwamba Wakenya wanakabiliwa na changamoto ya maisha magumu. “Endapo gharama ya maisha haitawekwa kwenye meza ya mazungumzo na kutafutiwa suluhu, basi mazungumzo haya yatagonga mwamba. Jambo muhimu linalotushughulisha ni hali ngumu ya uchumi. Gharama ya maisha imechangia mahangaiko miongoni mwa Wakenya, hasa wazazi,” akasema. Bw Kalonzo Musyoka ndiye kiongozi wa Wiper, na mmoja wa wanaoongoza mazungumzo ya maridhiano. Akihutubu Jumanne, Novemba 21, 2023 katika makao makuu ya chama hicho jijini Nairobi, mbunge huyo wa zamani Lamu, alisema chama cha Wiper kinajiandaa kwa njia nyingi za kukataa gharama ya sasa ya maisha, ikiwemo maandamano na kushinikiza kura ya kutokuwa na imani na uongozi wa Kenya Kwanza. “Hali hii mbaya iliyopo hatuwezi kuendelea nayo kwa miaka minne ijayo. Kwa hivyo, kwa njia yoyote iwezekanayo, hata kama ni kupitia maandamano, tutaifuata kuhakikisha hali hii inarekebishwa. “Katiba yetu inawapa nguvu wananchi kushiriki katika hatua kama hizi, na ni wazi kwamba hatuwezi kuvumilia mateso haya kwa miaka minne. Wakati wa kuleta mabadiliko ni sasa. Tumevumilia vya kutosha,” akasema. Kauli yake mbele ya kinara wake Kalonzo Musyoka ambaye ni mmoja wa wenyekiti wa mazungumzo ya Bomas, inajiri siku chache baada ya kinara wa Narc Kenya, Bi Martha Karua kutoa vitisho kama hivyo. Bi Karua wiki jana alikariri kuwa iwapo mazungumzo hayo hayatafanikiwa kutatua shida ya gharama ya maisha, watatekeleza haki za kisiasa na kibinadamu kulingana na Katiba kwa kufanya maandamano yatakayoshinikiza gharama ya maisha kupungua. “Hata kama tutasafirishwa mbinguni kupitia vifo wakati wa maandamano, sisi kama Narc Kenya tunasema iwapo mazungumzo hayo yatakosa kumalizika inavyofaa, hatutasahau haki zetu. “Tutarudi kufanya maandamano iwapo yatastahili.Tunasema hakuna kutishwa na tunaita Wakenya kujiunga nasi na kushikana mikono,” alisema Bi Karua. Vyama hivyo viwili vimekumbatia msimamo tofauti na wa kinara wa Azimio la Umoja, Bw Raila Odinga, anayeamini kwamba muda wa kurejea barabarani kwa maandano haujawadia. Jumanne, Bi Abdallah alisisitiza kwamba Kenya Kwanza imeshindwa kuonyesha uongozi bora, hivyo basi, chama cha Wiper kinaunga mkono pendekezo la kinara wake kupeperusha bendera ya urais ifikapo 2027. Wanasiasa wa Wiper wanaamini kwamba Bw Musyoka ana tajriba na ni mtu mwenye huruma, atakayewapunguzia Wakenya masaibu wanayopitia chini ya utawala wa Kenya Kwanza. “Sisi kama Wiper, hatutabembelezana tena. Punda amechoka. Ni lazima tuchukue msimamo kuhusu suala hili. Wakenya wanatamani sana uongozi mpya, wanatamani kuona uongozi sawa na wa (marehemu Mwai Kibaki), ambao haupatikani kwingine isipokuwa kwa mheshimiwa Kalonzo,” akasema Bi Abdallah. Alidai kuwa nchi inakumbwa na janga lisiloweza kutatuliwa isipokuwa kupitia Bw Musyoka, anayeamini kuwa anaweza kurejesha hali ya kawaida. Wakati huo huo, chama cha Wiper kiliwakaribisha viongozi waliohama vyama vyao.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA JUSTUS OCHIENG TUME ya Maadili na Kupamabana na Ufisadi nchini (EACC) imerejelea ubadhirifu wa fedha za umma kama aina ya ufisadi ulioenea zaidi katika Kaunti zote nchini. Tume hiyo ilisema kwamba imepokea takriban madai 1,337 ya ufisadi yanayogusa serikali za kaunti katika miaka miwili iliyopita. EACC pia ilifichua kuwa kati ya ripoti 1,337 ilizopokea kati ya 2021 na 2023, 843 zilikuwa ndani ya mamlaka hiyo na inachunguzwa, huku zilizosalia zikitolewa kama ushauri, ambazo zilirejelea taasisi zingine za Serikali lakini hakuna hatua iliyochukuliwa. Kamishna wa EACC, Dkt Cecilia Mutuku, alisema kuwa ufujaji wa pesa za umma ndio aina ya ufisadi iliyoenea zaidi katika Kaunti, ilhali wizi wa zabuni, ufisadi miongoni mwa wafanyikazi na makosa ya kanuni za adhabu ndio aina ya ufisadi ambayo haijakithiri. Dkt Mutuku alikuwa akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo kwa Kamati za Kuzuia Ufisadi (CPC) za kaunti za Elgeyo Marakwet, Bungoma na Kakamega mjini Kisumu Jumanne Novemba 21, 2023. Magavana Kenneth Lusaka (Bungoma), Fernandez Barasa (Kakamega), Profesa Anyang’ Nyong’o (Kisumu) na Wesley Rotich (Elgeyo Marakwet) ni miongoni mwa magavana waliohudhuria hafla hiyo. Muhtasari wa ripoti kuhusu ufisadi iliyogusa vitengo vilivyogatuliwa katika miaka miwili iliyopita unaonyesha kuwa angalau 303 zilitokana na ubadhirifu na ufujaji wa fedha za umma, 113 ulitokana na ukiukwaji wa maadili huku 97 ulitokana na ukiukaji wa sheria za ununuzi. Dkt Mutuku alidokeza kuwa mali ya thamani ya Sh23. 74 bilioni ilikuwa imerejeshwa na tume hiyo katika miaka mitano iliyopita, huku EACC ikisaka kutwaa mali iliyopatikana kwa ufisadi ya takriban Sh40.78 bilioni katika mahakama mbalimbali kote nchini. “Katika miaka mitano iliyopita, tume hiyo pia iliepusha hasara ya takriban Sh36.5 bilioni kupitia uchunguzi wa kina na kuvuruga mitandao ya ufisadi, alisema Dkt Mutuku. Pia alibainisha kuwa katika miaka mitano iliyopita, EACC iliidhinisha maombi ya maafisa 1,342 wa Umma kuendesha akaunti za benki nje ya Kenya na kufanya uhakiki wa kufaa kwa watahiniwa 48,383 kwa uteuzi wa umma.
Tags
You can share this post!
Previous article
Aliniweka mimba akahepa na nikalea mtoto peke yangu, sasa...
Next article
Utaoshwa! Hisia mseto, wasiwasi kufuatia kuzinduliwa kwa...

NA MANASE OTSIALO Naibu Mwalimu Mkuu ameuawa baada ya kukatwa kichwani na mbawa za helikopta. Kisa hicho cha Novemba 21, 2023 asubuhi kilifanyika eneo la Masalani, katika kaunti ndogo ya Ijara, Kaunti ya Garissa. Akithibitisha kisa hicho, Kamishna wa Kaunti ya Garissa Solomon Chesut alisema bado haijabainika kuhusu kilichomfanya mwendazake akaribie helikopta hiyo iliyokuwa inajiandaa kupaa. “Kumekuwa na kisa ambapo mwalimu alifariki papo hapo baada ya kukatwa na mbawa za helikopta. Tumeanzisha uchunguzi kubaini alichokuwa akifanya karibu na helikopta,” akasema Bw Chesut. Mkuu huyo wa kiusalama Garissa alitaja tukio hilo kuwa la kusikitisha. “Marehemu aamekuwa akifungua makasha ya mtihani katika afisi ya DCC,” akasema. Walioshuhudia wanasema walimu huyo alikimbilia kuabiri ndege hiyo kwa kuwa alikuwa anahusika katika usambazaji wa mitihani katika shule mbali mbali katika kaunti ndogo ya Ijara. Sehemu nyingi za Garissa zimekuwa zikifurahia huduma za helikopta katika usambazaji wa mitihani baada ya barabara kukosa kupitika kutokana na mafuriko ya mvua ya El Nino. Helikopta mbili ambazo zinahudumu Garissa pia hutumika katika kaunti jirani ya Tana River. Kaunti tatu za Kaskazini Mashariki zina helikopta mbili kila moja zinazotumika katika usambazaji wa mtihani wa KCSE unaoendelea. Wajir imebakia na helikopta moja baada ya nyingine kuanguka Jumatatu Novemba 20, asubuhi ilipokuwa inaondoka uwanja wa ndege wa Wajir. Soma kisa hicho hapa: https://taifaleo.nation.co.ke/habari/habari-za-kitaifa/ndege-mbili-za-helikopta-zahusika-katika-ajali-tofauti-wajir Takriban watu watatu akiwemo rubani na mwanasiasa wa eneo hilo walijeruhiwa katika mkasa huo na kukimbizwa hospitalini. Helikopta nyingine ya jeshi ilianguka vile vile katika eneo la Buna, Wajir Kaskazini hiyo hiyo Jumatatu ilipokuwa inasambaza msaada kwa wahanga wa mafuriko. Katika taarifa, Jeshi lilisema kwamba wote waliokuwemo kwenye ndege hiyo waliponyoka bila majeraha na kwamba uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha ajali hiyo huku wakazi wakisema wanashuku ilikuwa imebeba mizigo kupita kiasi.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MHARIRI
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini.
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na BENSON MATHEKA
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON