text
stringlengths
3
16.2k
KUNDI jipya la mawakili sita waliokuwa wanamwakilisha aliyekuwa gavana wa Nairobi Bw Mike Sonko Jumanne walijiondoa... Na RICHARD MUNGUTI
RIPOTI ya daktari wa tiba za akili imesema Alhamisi kuwa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko anaugua maradhi ya... Na RICHARD MUNGUTI
MAHAKAMA ilielezwa jana kuwa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko angali amelazwa katika Nairobi Hospital... Na RICHARD MUNGUTI
UFICHUZI wa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko kwamba mtu aliingia kwenye seli anamozuiliwa katika kituo cha... Na BENSON MATHEKA
Aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Bw Mike Sonko anajuta kwa vitendo alivyofanya akiwa mamlakani; akiepuka kuadhibiwa kwa... Na RICHARD MUNGUTI
KAMA kuna wakati wenye changamoto tele kwa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko ni sasa.
Maji yalizidi unga hata... Na RICHARD MUNGUTI
MASAIBU ya aliyekuwa gavana wa Nairobi, Bw Mike Sonko, yaliongezeka Jumatano ilipofichuka kuwa serikali inapanga... Na RICHARD MUNGUTI
ALIYEKUWA Gavana wa Nairobi, Mike Sonko aliangua kilio kortini Jumatano wakati wa kusikizwa kwa kesi ya ufisadi wa... Na CHARLES WASONGA
WANASIASA na watu ambao majina yao yatawekwa katika orodha ya aibu ya Tume ya Uwiano na Utangamano ya Kitaifa (NCIC)... BENSON MATHEKA na SIMON CIURI
Masaibu ya aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Mike Sonko yaliendelea kuongezeka jana alipozuiliwa rumande baada... Na RICHARD MUNGUTI
MASAIBU ya aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko Mbuvi Gidion Kioko yameongezeka baada ya  kusukumwa ndani hadi... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA SAMMY WAWERU MSANII tajika wa nyimbo Mugithi, Samuel Muchoki maarufu kama Samidoh huenda ametengana na mpenzi wake mwanasiasa Karen Nyamu. Hii ni kutokana na video iliyochipuka ambayo anaskika akisema “nilikuwa kwenye ndoa ya mitara, sasa niko singo”. Samidoh amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Seneta Maalum Karen Nyamu, na wamejaaliwa kupata watoto wawili. Msanii huyo wa nyimbo za Agikuyu, alifichua kuachana na Karen kupitia video ya mbashara ya Tiktok (live) ambapo alikuwa akijibu maswali ya mashabiki wake. Wakati wa mafichuzi hayo, alionekana kuwa kwenye eneo la burudani alikoandamana na msichana ambaye hakuweka wazi endapo ndiye mchumba wake mpya. “Ati hongera kwa kuwa na mpenzi mpya…” Samidoh akasoma mojawapo ya jumbe zilizotumwa na mashabiki wake. Alijibu, “Si wewe pekee ulishushwa madaraka kutoka kiwango cha hadhi hadi dereva wangu…Nilikuwa kwenye ndoa ya mitara ila sasa niko singo”. Mfuasi huyo aliendelea kumdadisi, akitaka kujua iwapo Samidoh anafahamu kuhusu ukurasa wa kimitandao unaohusishwa na mchumba wake – Karen Nyamu Fun Page. Kwa ucheshi, mwimbaji huyo wa kibao tajika cha Kairetu Gakwa (Binti yangu) na Ndiri Mutwe Mwega (Sina kichwa kizuri) alisema kwa sasa anajishughulisha na biashara. “Kwa sasa, ninajishughulisha na masuala biashara. Ikiwa si mradi au biashara, ishi na mama yako,” alielezea. Shabiki wake alimkejeli akitaka kujua aliko nina yake, isijulikane ikiwa alimaanisha mama yake mzazi au mpenzi wake. “Ameoleka na kwa sasa anafurahia fungate (honeymoon),” Samidoh alidokeza. Kidosho aliyeandamana naye alitambua shabiki huyo kama Shabaan, akisema kwamba yeye ni mchochezi. “Wee acha hiyo, unajua Shabaan wewe ni mchochezi sana… (Yuko hapa (akimaanisha Karen Nyamu),” mwanadada huyo alisema. Naye Samidoh aliendelea, “Tunataka Karen, naona hivo ndivo mchango safuni unasema…Naona, lakini sasa yuko online kweli?” Kipusa aliyeandamana naye, alijibu, “Yuko online, mjaribu”. Aidha, shabiki wa Samidoh alitaka Karen Nyamu ajumuishwe kwenye mazungumzo hayo ya mbashara Tiktok. Kilichoshangaza zaidi na kuashiria utengano wa Samidoh na Karen, ni kudai kwamba alimbloki mtandaoni na angeweza kushiriki endapo atamuondoa alikomuweka. “Yuko kwenye orodha ya kublokiwa, sasa hiyo ndio shida. Labda nisitishe mazungumzo haya ya moja kwa moja ili nimuondoa aweze kujumuika nasi,” Samidoh alifafanua. Mahusiano kati ya Samidoh na Karen, ndiyo yalichangia kuachana na mkewe, Edday Nderitu ambaye alihamia Amerika Mei 2023. Edday alikuwa ameonya msanii huyo mapema 2023, akisisitiza kwamba hakuwa tayari kuwa kwenye ndoa ya mitara. Samidoh na Edday wana watoto watatu pamoja. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MAOSI WAKAZI wa mtaa wa Mazembe viungani mwa mji wa Nakuru wamekiri kuhangaishwa na wezi ambao huwaibia na kuwasindikiza hadi nyumbani. Huwawekea ulinzi huo makusudi ili kuhakikisha kwamba wateja wao wanafika nyumbani salama salimini. Kwa kawaida, wahuni wamebuni mbinu mpya ya kutembea na mbwa wakubwa nyakati za usiku, ili kujiwekea ulinzi wa kibinafsi. Owen Shibala mwendeshaji bodaboda kati ya Nakuru mjini na Mazembe, anasema hajui walikotoa ujasiri walio nao kushika doria usiku utadhani ni polisi. Mazembe ni mojawapo ya mitaa ambayo hushuhudia visa vya kihalifu na utumiaji wa mihadarati mara kwa mara. “Ukikutana nao usiku ni lazima usalimishe kila kitu lau sivyo utaona cha mtema kuni. Watakucharaza viboko na kuiba kila kitu cha nguvu,”akasema. Hata hivyo, wanapoiba hujitwika jukuma la kuwasindikiza wakazi, wasije wakakutana na vibaka wengine barabarani. Aidha, wanalia sare za polisi jambo linalowafanya baadhi ya raia kuamini huenda wanashirikiana na maafisa wa polisi. Baadhi yao wanajifanya ni maafisa wa polisi ambao huwa wameshika doria, wakilenga kuhangaisha wapita njia wanaotoka kazini usiku. Agnes Wahome mfanyibiashara mtaani Rhonda anasema huwa wamejihami kwa visu, rungu na wako tayari kupigana. Kulingana na Bi Wahome, hii ni hali ya kawaida siku hizi katika mitaa ya Manyani, Bondeni na Freearea ambapo vijana wengi wamejiingiza kwenye uhalifu. Bi Wahome anasema wahalifu wengi wanajulikana, kwani ni vijana wadogo kutoka mitaa jirani ya Flamingo na Lakeview. Mkazi huyo angependa polisi kushika doria katika maeneo husika ili kuzuia kuzuka kwa magenge hatari yanayohangaisha wenyeji. Hili linajiri siku chache baada ya Taifa Leo Dijitali kufichua visa vya wizi ambapo baadhi ya wezi kutoka kwenye mtaa wa Gioto, Nakuru wamekuwa wakipika chakula katika kila nyumba wanamoingia kuiba. Mtaa wa Bondeni, Kaunti ya Nakuru ambapo wezi huwaibia wakazi na kuwasindikiza mpaka nyumbani. PICHA|RICHARD MAOSI
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L

You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MUNGUTI MASKWOTA wapatao 10,000 wamewasilisha upya kesi katika Mahakama ya Upeo wakiomba ibatilishe uamuzi kwamba wafukuzwe kutoka kwa shamba la ukubwa wa ekari 25,000 wanalong’ang’ania umiliki wake na familia ya mwanasiasa marehemu Mark Too. Maskwota hao wanaodai mababu zao ndio waliotimuliwa kutoka kwa shamba hilo enzi za ukoloni, wanasema walipewa shamba hilo rasmi na aliyekuwa Rais hayati Daniel arap Moi, kisha Kamishna wa Ardhi M Okundu akaratibisha uamuzi huo mwaka 2007. Katika ombi lililowasilishwa na wakili William Arusei chini ya sheria za dharura, kikundi cha maskwota hao–Sirikiwa Squatters Group–kimeomba mahakama ibatilishe uamuzi huo kwa vile ilitegemea ushahidi ambao haukuwa umewasilishwa katika kesi waliyoshtaki katika Mahakama ya kuamua kesi za mashamba (ELC), Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu. Pia wameeleza bayana Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaack Lenaola, na William Ouko walitegemea ushahidi wa Afisa wa Ugavi wa Mashamba R J Simiyu kutoa uamuzi wang’atuke shambani. Maskwota hao wamesema ushahidi wa Bw Simiyu uliowasilishwa mbele majaji hao saba kwa njia ya afidaviti ni mpya na kamwe “haukuwasilishwa mbele ya Jaji Antony Ombwayo aliposikiliza na kuamua kesi hiyo 2017.” Pia wanasema ushahidi huo haukuwasilishwa Mahakama ya Rufaa iliyosikiliza rufaa iliyowasilishwa na kampuni ya Fanikiwa, familia ya marehemu Mark Too, kampuni ya Lonrho Agribusiness (EA) Ltd, na Bw David K Korir. Hivyo basi, maskwota hao wanaeleza mahakama hii ya upeo kwamba ni kinyume cha sheria kutegemea ushahidi mpya kutoa uamuzi wa kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma. “Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu wa Desemba 15, 2023, hauna mashiko kisheria na kamwe hauna nguvu kisheria kuwatimua maskwota hawa kutoka kwa shamba lao,” asema Bw Arusei. Pia maskwota hawa wanadai kwamba badala ya Mahakama ya Juu kujadili masuala ya kikatiba jinsi ilivyo jukumu lake, majaji hao walianza kufafanua na kutafsiri ushahidi wa watu binafsi na kuelezea maana ya ‘skwota’. Mahakama hii imeombwa ikague upya uamuzi iliyotoa kwa vile ilidanganywa na walalamishi na pia kutendewa ujanja. Akinukuu maamuzi ya majaji wastahiki kama vile Lord Dening, Bw Arusei amesema, mahakama ikigundua ilipotoshwa au kudanganywa na upande mmoja, iko na mamlaka na uwezo wa kufutilia mbali uamuzi iliyotoa na kuandika mwingine. Maskwota hao wanaomba Mahakama ya Juu iwarudishe shambani kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Ombwayo na Mahakama ya Rufaa. Vile vile mahakama hiyo imekosolewa kwa kumshambulia hayati Moi katika uamuzi huo pasi kutoa agizo wasimamizi wa mali yake wafike mbele yao kutoa mwanga kuhusu suala la umiliki wa shamba hili lililorudishwa kwa serikali na kampuni iliyokuwa inakuza miti inayotumika katika viwanda vya ngozi. Naibu msajili wa Mahakama ya Juu Nelly Kariuki aliwaamuru maskwota hao wawakabidhi nakala za kesi hii yao mpya wahusika wote kabla ya Januari 31, 2024, kesi itakapotajwa tena kwa maagizo zaidi. Jaji aliyesikiliza kesi hii mpya hakuiratibisha kuwa ya dharura ila aliamuru pande zote ziwasilishe ushahidi katika muda wa siku 14 kuanzia Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti,  baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA STANLEY NGOTHO WAHUDUMU wa bodaboda katika Kaunti ya Kajiado wamelalamikia ongezeko la visa vya wizi wa pikipiki zao ambapo watu 10 wameuawa na waendeshaji 50 kujeruhiwa, huku pikipiki 600 zikiibwa ndani ya mwaka mmoja uliopita. Kulingana na Muungano wa Wahudumu wa Boda Boda Nchini (BAK), tawi la Kaunti ya Kajiado, sekta hiyo imetekwa na magenge ya wahalifu wanaoua, kujeruhi na kuiba pikipiki hizo za uchukuzi. Data za boda boda zilizoibwa zinaonyesha kuwa 84 zimeibwa kutoka Loitoktok, Kajiado Mjini (109), Ong’ata Rongai (110), Ngong (101) na Kitengela (140). Kwa jumla, pikipiki 544 zimeripotiwa kuibwa ndani ya muda wa mwaka mmoja. Thamani ya vyombo hivyo vya uchukuzi ni Sh152, 320, 000 ikizingatiwa kuwa boda boda moja inagharimu Sh280, 000, kwa wastani. Mwenyekiti wa BAK, Kaunti ya Kajiado Alex Gitari aliambia Taifa Leo Dijitali kuwa pikipiki zilizoibwa hupelekwa katika eneo la makazi duni ya Lokolo nchini Tanzania baada ya kupitishwa katika vituo haramu vya mpakani. Pikipiki zingine pia hupelekwa katika vitongoji duni vya Kiamaiko na Mukuru Kwa Njenga, Jijini Nairobi. “Katika vitongoji hivi pikipiki hizo za wizi hubomolewa na vipuri kuuzwa,” akasema. “Aidha, pikipiki zingine zinazoibwa katika maeneo ya Loitoktok na Namanga, hupelekwa katika mitaa ya mabanda nchini Tanzania. Tunajaribu mara kadha kufuata pikipiki hizo lakini tumekumbana na upinzani mkali kutoka kwa wanachama wa genge linalohusika na wizi huo,” akasema Gitari. Inasemekana kuwa genge hilo la wezi hulenga pikipiki mpya zilizonunuliwa kwa njia ya mkopo. Lina majasusi katika kila mji ambao hujifanya waendeshaji boda boda au makanika. Huwa wanatekeleza wizi huo nyakati za usiku. “Baada ya pikipiki huibwa kutoka miji mbalimbali, mitambo ya kuzifuatilia huvurugwa baada ya kufikishwa katika vituo hivyo viwili vya jijini Nairobi. Mitaa hiyo ya mabanda haifikiki. Tumejaribu kufika huko lakini huwa tunazuiwa na wanachama wa magenge hayo,” akaeleza Bw Gitari akiwasuta polisi wa Nairobi kwa kushirikiana na wezi hao. Bw Justus Onjoke, 29, alivamiwa wiki jana na majambazi wenye silaha katika kona ya kuingia Mombasa Road majira ya usiku. Aliamriwa asalimishe pikipiki yake ili kuokoa maisha yake na akasalimu amri.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA AFISA Mkuu mtendaji wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) atasimamia chaguzi ndogo za maeneobunge na wadi ikiwa mswada uliodhaminiwa na Mbunge wa Mandera Kaskazini, Abdullahi Bashir utapitishwa kuwa sheria. Mbunge huyo Jumatano, Desemba 6, 2023 ametoa vidokezo kuhusu mswada huo ambao anasema unalenga kusuluhisha dosari iliyoko katika Sheria ya IEBC ya 2012. Kulingana na sheria hii inayotumika sasa, ni mwenyekiti wa tume hiyo, akisaidiwa na angalau makamishna wawili, walio na mamlaka ya kuendesha chaguzi ndogo za maeneo hayo wakilishi baada ya nafasi hizo kusalia wazi. “Dhima ya mswada wangu ni kumpa afisa mwenye cheo cha juu zaidi katika IEBC mamlaka ya mwenyekiti kiasi kwamba anaweza kuteua afisa wa kusimamia chaguzi ndogo endapo itatokea kwamba makamishna hawapo,” Bw Bashir akasema wakati wa kikao cha Bunge la Kitaifa cha alasiri. Alisema mswada wake unalenga kuifanyia mageuzi sehemu ya 18 ya Sheria ya IEBC ya 2012 inayosema kuwa ni mwenyekiti wa tume hiyo pekee aliye na mamlaka ya kuteua afisa wa kusimamia uchaguzi mdogo katika eneo lolote wakilishi. “Ingawa Katiba inasema kuwa kila Mkenya ana haki kupata uwakilisha bunge au eneo lolote wakilishi hadi kufikia sasa wakazi wa maeneobunge ya Banisa na Magarini hawana mwakilishi katika bunge hili. Zaidi ya wadi 20 ziko wazi baada ya madiwani kufariki au mahakama kubatilisha ushindi wao katika uchaguzi mkuu wa 2022. Hii sio haki na dosari hii inapaswa kurekebishwa licha ya kwamba IEBC haina makamishna wakati huu,” Bw Bashir akasema. Kiti cha ubunge cha Banisa kilisalia wazi baada ya kifo cha mbunge Hassan Maalin Hassan mnamo Machi 29, 2023. Kiongozi huyo alikata roho akitibiwa katiika hospitali ya Mater, Nairobi baada ya kugongwa na mwendeshaji bodaboda akivuka barabara kuelekea katika msikiti mtaani South B, Nairobi. Nacho kiti cha ubunge cha Magarini, kilibaki wazi baada ya mahakama kuu kubatilisha ushindi wa Harrison Garama Kombe katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022. Mahakama Kuu ya Malindi ilibatilisha ushindi wake Mei 26, 2023 baada kugundua dosari katika uhesabu wa kura.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA BRIAN OCHARO MANUSURA wa mauaji ya halaiki ya Shakahola wamepata pigo baada ya mahakama kuzuia Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu (KNCHR) kushiriki katika kesi hiyo. Katika kesi hiyo, serikali imeeleza kuwa walionusurika sasa watachukuliwa kama watuhumiwa na kufunguliwa mashtaka — mara tu uchunguzi kuhusu mfungo mbaya, uliopelekea mamia ya wafuasi wa kanisa la Good News Internal la Paul Mackenzie kuaga dunia, utakapokamilika. Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Shanzu Joe Omido aliamua kwamba ombi la KNCHR kukubaliwa kushiriki kesi hiyo kama mhusika halikuwa na msingi. “Nina hakika maombi ya sasa hayafai. Tume haijaeleza namna au aina ya hasara itakayopata iwapo mahakama haitaruhusu maombi yake kushiriki katika kesi hii,” alisema Hakimu Omido. Tume ilihoji kuwa ombi lake lilinuia kuhakikisha kwamba mara tu itakapojiunga katika kesi hiyo kama mhusika, ushahidi wote unaokusanywa wakati wa upelelezi unawasilishwa mahakamani na kwamba ikiwa ushahidi hautakubaliwa basi hautafanikiwa. Lakini korti ilisema uwasilishaji huo hauwezi kudumu kwani kesi dhidi ya watu hao bado haijaanza, na kwamba korti haitarajii kupokea ushahidi wowote kutoka kwa wahusika katika kesi hiyo. KNCHR pia ilihoji kuwa kuendelea kuzuiliwa kwa manusura hao bila kufunguliwa mashtaka rasmi, pamoja na ombi la serikali la kuwaweka kizuizini kwa siku 180 zaidi, ni kinyume cha katiba. Aidha, Tume ilisema serikali imekuwa na ulegevu katika suala hili na hivyo inataka kushiriki kesi ili kutoa msaada wa kisheria kuhakikisha haki inatendeka haraka. “Tume imekuwa sehemu ya mkasa wa Shakahola katika viwango tofauti ikiwemo kufuatilia ufukuaji, uchunguzi wa maiti na kushiriki kesi mahakamani. Kwa hivyo hatuwezi kupuuzwa,” KNCHR ilisema kupitia wakili Annemarie Okutoyi. Bi Okutoyi alihoji kwamba Tume inapaswa kuruhusiwa kushiriki kesi baada ya kushiriki katika michakato mbalimbali kuhusiana na mauaji hayo ya kutatanisha. Hata Hivyo, upande wa mashtaka ulipinga Tume hiyo kushiriki kesi hiyo ukidai KNCHR haikuwasilisha hoja za kisheria kujumuishwa. Kupitia kwa kiongozi wa mashtaka Victor Juma, serikali ilisema Tume haijaeleza athari ambazo zingetokea iwapo itanyimwa fursa ya kushiriki. Mkurugenzi Msaidizi wa Mashtaka ya Umma, Jami Yamina, aliteta kuingizwa kwa KNCHR katika kesi hiyo akisema tayari serikali inashugulikia kesi hiyo kisheria. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

Na WINNIE ATIENO Mbunge wa Likoni Bi Mishi Mboko ameishutumu serikali kuu akidai inasambaza chakula cha msaada kwa waathiriwa wa mafuriko huko Mombasa kiubaguzi. Hii ni baada ya serikali kuu kuendelea kusambaza chakula cha msaada kupitia Mbunge wa Nyali Bw Mohammed Ali badala ya Gavana wa Mombasa Bw Abdulswamad Nassir. Bw Ali ambaye ndio mbunge aliyechagulia kupitia chama tawala cha UDA, amekuwa akisambaza chakula mitaani Mombasa hasa mitaa ambayo wakazi waliathirika na mafuriko. Hata hivyo, Bi Mboko alisema ni wajibu wa serikali kuu kusambaza chakula hicho kwa kushirikiana na Gavana Nassir ambaye ndiye mwakilishi wa wakazi wa Mombasa katika serikali kuu. Bi Mboko alisema serikali kuu ilisambaza chakula cha msaada kwa waathiriwa wa janga la mafuriko kupitia mbunge. “Sisi kama viongozi tumeona suala hili limechukuliwa kisiasa. Sababu kama desturi, serikali kuu zilizopita imekuwa ikigawa chakula cha msaada wakati wa majanga kama haya kupitia kwa kamishna wa kaunti, manaibu wao na machifu lakini safari hii tulishangaa,” alisema Bi Mboko. Badala yake, Bi Mboko alisema chakula hicho kinafanyiwa siasa. “Si sawa kufanyia chakula siasa. Kiongozi wa kisiasa hafai kutumia chakula hicho kisiasa na hata kubagua wengine. Isitoshe watu wengi walikosa hicho chakula, na hakukuwa na mpangilio kisawasawa,” aliongeza mwandani huyo wa Bw Nassir. Alisema watu ambao wamekuwa wakisambaza chakula hicho cha msaada wamekuwa wakimponda Bw Nassir. Bw Ali amekuwa akisambaza chakula cha msaada mitaa kadha wa kadha. Alisema alimwambia Rais William Ruto asaidie waathiriwa wa janga la mafuriko na akakabidhiwa vyakula vya msaada azunguke Mombasa akiisambaza. “Kuna dhambi nikileta chakula? Nimeleta chakula hasa kwa wale ambao wamesahaulika. Lakini ninataka kumwambia Gavana wa Mombasa, awache kwenda mahotelini kula kaimati, aje asaidie watu,” alisema Bw Ali siku tano zilizopita pale Makande. Vile vile alishtumu wakazi kwa kujenga kwenye maeneo ya ziwa na kuathiri maisha yao wakati wa mafuriko. Hata hivyo alisema serikali ya kaunti ilijizatiti na kuwahamisha sehemu zengine. “Sehemu nyingi Kisauni kuna mafuriko ni kule kulikuwa na ziwa, lakini watu wakaenda kujenga. Lakini tumewasaidia na chakula, dawa, neti za mbu. Wale ambao nyumba zimeanguka tunashirikiana na Gavana kuwasaida kununua mabati,” alisema Bi Mboko. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

Na CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Azimio la Umoja-One Kenya Raila Odinga ameikashifu serikali kufuatia kukamatwa na kushtakiwa kwa Msimamizi wa Bajeti (CoB) Margaret Nyakang’o kwa tuhuma za ulaghai. Kwenye taarifa Jumanne Desemba 5, 2023, Bw Odinga amedai kuwa masaibu ya Dkt Nyakang’o yamechochewa na kujitolea kwake kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu na kitaalum na kufichua ufisadi serikalini. “Sawa na Wakenya wengine, kukamatwa kwa msimamizi wa bajeti sio jambo la kushangaza kwa sababu dalili zake zilionekana. Hii ni kutokana na kujitolea kwake kufanya kazi kwa uadilifu katika utawala uliojaa wafisadi na wahalifu wa aina mbalimbali,” akasema. “Tulijua wanapanga kumwelekea makosa yasiyo na msingi wowote ili wamwondoe afisini ili kutoa nafasi kwa mtu ambaye atafumbia macho uporaji unaondelea serikalini wakati huu,” Bw Odinga akaongeza. Kiongozi huyo wa Azimio alisema kama chama watasimama na Dkt Nyakang’o na kumpa usaidizi wowote wanaoweza kwa ajili ya kupiga jeki vita dhidi ya ufisadi nchini. Msimamizi huyo wa bajeti alikamatwa mjini Mombasa Jumanne asubuhi na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumlaghai Bi Claudia Mueni Sh29 milioni mnamo 2016. Aidha, alikabiliwa na mashtaka ya kuendesha shirika la akiba na mikopo (Sacco) bila leseni na kughushi stakabadhi. Alikana makosa hayo na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh2 milioni au Sh500, 000 pesa taslimu. Kesi hiyo itatajwa Desemba 13, 2023.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MASHIRIKA KAMPALA, UGANDA AMERIKA ilidokeza Jumatatu kuwa itafutilia mbali viza za maafisa wa Uganda ambao walihusika na sheria tata dhidi ya mashoga. Waziri wa Mambo ya Nje, Antony Blinken, alisema kuwa Amerika itawazuia maafisa wa sasa au wa zamani, na familia zao kuzuru nchi yao ikiwa watapatikana kuhusika na sheria tata dhidi ya mashoga. “Makundi hayo yanajumuisha, lakini sio tu, wanaharakati wa mazingira, watetezi wa haki za binadamu, waandishi wa habari, watu wa LGBTQI+ na waandamanaji wa mashirika ya kiraia,” Blinken alisema katika taarifa. “Kwa mara nyingine tena ninaihimiza sana serikali ya Uganda kufanya juhudi za pamoja za kutetea demokrasia na kuheshimu na kulinda haki za binadamu ili tuweze kudumisha ushirikiano wa miongo kadhaa kati ya nchi zetu ambao umewanufaisha Wamarekani na Waganda pia,” alisema. Rais wa Amerika, Joe Biden, Umoja wa Ulaya na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, wamekuwa wakiikosoa vikali Uganda kufuatia sheria kali dhidi ya ushoga. Hata hivyo, Rais Yoweri Museveni, ameapa kupinga shinikizo la kimataifa kuhusu sheria hiyo, ambayo inaungwa mkono na nchi nyingi. Mnamo Mei, Amerika ilifutilia mbali viza ya spika wa bunge la kitaifa wa Uganda Anita Among baada ya kupitisha sheria za kutotambua mashoga na wasagaji nchini humo. Kulingana Asuman Basalirwa, aliyewasilisha mswada huo, ujumbe huo wa kufutilia mbali viza ya spika huyo, ulithibitishwa kupitia barua pepe. Akinukuu ujumbe huo baada Rais Museveni, kupuuzilia mbali shinikizo kutoka kwa mataifa ya magharibi na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu kutaka kuunga mkono mswada kupinga ushoga kuwa sheria. “Taifa la Amerika limetupilia mbali viza ya spika wa Uganda. Kwa sasa Anita Among hana viza ya Anerika,” alisema huku akionyesha nakala ya barua pepe hiyo kwa wanahabari. Kulingana na sheria hiyo, wale wanaoshiriki ushoga wanakabiliwa na adhabu kali ambayo inaweza kujumuisha kifungo cha maisha.Mnamo Mei 29, 2023 Among alitangaza kuwa bunge litasimama kidete kukuza maadili ya watu wa Uganda. Kwa upande mwingine, Benki ya Dunia mnamo Agosti, ilitangaza kuwa ingesitisha mikopo mipya kwa Uganda kufuatia hatua yake ya kuharamisha mapenzi ya jinsia moja. Benki hiyo ilisema sheria hiyo inayoharamisha LGBTQ inakwenda kinyume na misingi na maadili yake ambayo hayabagui yeyote kwa misingi ya jinsia au rangi yake katika azma yake ya kukabiliana na umasikini duniani. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA ANTHONY KITIMO Msimamizi wa Bajeti Margaret Nyakang’o na watu wengine 10 wanatazamiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kuhusiana na kesi iliyofunguliwa kuhusiana nao mnamo 2016. Washukiwa hao 11 wanatarajiwa kushtakiwa kwa makosa mbali mbali, likiwemo lile la kupanga kulaghai mahakama ya Mombasa. Aidha, watashtakiwa pia kwa kuendesha shirika la akiba na mikopo (Sacco) bila leseni, na kuwasilisha stakabadhi ghushi. Mashtaka hayo yameidhinishwa na afisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma, ODPP, kwenye barua iliyotumwa kwa Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi (DCI) Novemba 30. Kulingana na stakabadhi ambazo Taifa Leo imeziona, Naibu DPP Jacinta Nyamosi anasema kundi hilo la watu 11 lina kesi ya kujibu. “Tumepokea barua yako yenye usajili DCI/SEC/LCA/4/4/16/Vol. VII/24 ya Oktoba 31, 2023 inayowasilisha tena upelelezi kuhusu jambo hili na inahitaji mwelekeo,” Bi Nyamosi anasema. Akaongeza: “Tunatambua kwamba faili hiyo iliwasilishwa kwa mara ya kwanza Julai 6, 2022 na baada ya kuikagua, ilipatikana ina sehemu ambazo zilihitaji kushughulikiwa…” Wengine ambao wanatarajiwa kufunguliwa mashtaka ni Jackson Ngure Wanjau, Susan Kendi, James Makena Wanyagi, John Muchira Kithaka, Jane Karuu Ndanyi na Muthoni Elphas, Joan Chumo, Mercy Ndura Mukosa, Gregory Mwangangi Mailu na Michael Kipkurui. “Faili imeletwa tena kwa ODPP na baada ya upekuzi na ushahidi mpya, tumeona kwamba washukiwa wanastahili kufunguliwa mashtaka ya pamoja,” akasema Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA MWENYEKITI  wa Kamati ya Bunge kuhusu Usalama Gabriel Tongoyo ameshikilia kuwa kamati hiyo itaendelea kuchunguza chanzo cha utovu wa usalama Kaskazini mwa Kenya licha ya vitisho anavyopokea kutoka kwa baadhi ya “wadhamini” wa visa hivyo. Akiongea wakati kamati yake ilikutana na wabunge kutoka kaunti za Samburu na Turkana Bw Tongoyo alifichua kuwa amekuwa akipokea simu zenye jumbe za kumtishia maisha kutoka kwa watu fulani wakimwonya dhidi ya kuendeleza uchunguzi kuhusu visa vya ujangili na wizi wa mifugo katika eneo la North Rift. “Sikutaka kufichua hili wakati huu, lakini ninataka kuwaambia kuwa nimekuwa nikipokea vitisho vya kifo kutoka kwa watu wanaonipigia simu wakinionya kuhusu uchunguzi unaoendelea kuhusu kiini cha utovu wa usalama haswa wizi wa mifugo kaskazini mwa Kenya,” Mbunge huyo wa Narok Magharibi akasema wakati wa kikao na wabunge hao katika majengo ya Bunge jijinu Nairobi mnamo Ijumaa. Wabunge waliofika mbele ya kamati hiyo ni; Naisula Lesuuda (Samburu Magharibi, John Ariko (Turkana Kusini), Protus Akuja (Loima), Paul Nabuin (Turkana Kaskazini) na Joseph Namuar (Turkana ya Kati). Bw Tongoyo, hata hivyo aliwahakikishia wabunge hao kuwa hatagutushwa na vitisho hivyo na kuapa kwamba kamati yake itaendelea na uchunguzi kuhusu visa hivyo. “Kufikia sasa tumeendesha uchunguzi wetu katika kaunti za Samburu na Turkana na sasa tutaendelea katika kaunti ya Pokot Magharibi. Lengo letu ni kubaini chanzo cha visa hivyo, kisha kuandaa ripoti itakayowasilishwa kwa serikali kwa utekelezaji,” akaeleza. Wakati wa kikao hicho, wabunge wa kaunti ya Turkana waliitaka serikali kuwapeleka wanajeshi wa KDF katika maeneo ya mpaka wa Kenya na Uganda ili kupambana na visa vya uhalifu. Hata hivyo, Bi Lesuuda alielezea Kamati hiyo jinsi ambavyo majangili na wezi wa mifugo huhangaisha wakazi wa Samburu Magharibi licha ya kuwepo kwa kambi ya KDF katika eneo hilo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA WINNIE ATIENO NAIBU Rais Rigathi Gachagua ameendelea kusuta magavana kutokana na janga la mafuriko nchini akisema kazi yao kubwa ni kufanya vikao na wanahabari kwa nia ya kulalamika. Bw Gachagua alisema magavana wamekuwa wakishinda kwenye vyombo vya habari kueleza masuala ya mafuriko badala ya kwenda sehemu zilizoathirika kusaidia wahanga. Akiongea huko Tana River, Bw Gachagua alisema ni sharti magavana waende mashinani ambapo Wakenya wameathirika na mafuriko badala ya kufanya vikao vya kulalamika tu. Naibu Rais alisema ameshuhudia madhara ya mafuriko hasa katika kaunti za Garissa, Tana River na Mombasa hapo awali akieleza kuwa Rais William Ruto ameahidi kuwa hakuna Mkenya ambaye atakufa njaa kwa sababu ya mafuriko. Alimpongeza Gavana wa Tana River, Dadho Godhana, kwa juhudi zake za kusaidia wakazi waliaothiriwa na mafuriko. “Ndiyo maana tunataka tushikane kati ya Serikali Kuu na ile ya kaunti tusaidie waathiriwa. Tumefurahi kumpata Gavana papa hapa mashinani mahala wananchi wako. Wenzako wengine wameshinda kwenye vyombo vya habari wakipiga kelele. Hakuna lolote ambalo linaweza kutatuliwa kwenye vyombo vya habari,” akasema Bw Gachagua. Hii ni baada ya Baraza la Magavana kufanya kikao na wanahabari wiki mbili zilizopita na kumshtumu Bw Gachagua kwa ‘kuhadaa’ Wakenya kuwa kaunti zimetumiwa fedha za kusaidia waathiriwa wa mafuriko. “Shida za mafuriko ziko mashinani mahali wananchi wako, nendeni huko mjue shida iko wapi. Mahali dawa au chakula inatakikana unasaidia. Tusaidianeni katika hili janga la mafuriko,” alisema Bw Gachagua. Alisema Serikali Kuu imejizatiti kutoa ndege, magari ya jeshi na helikopta kusaidia wahanga wa mafuriko. Alisisitiza kuwa serikali pia imesambaza dawa za matibabu, neti za mbu na vyakula ambavyo vinakusudiwa kusaidia waathiriwa. “Tunahakikishia wananchi kuwa tunaelewa changamoto mnazopitia na si mwaka huu tu, hata miaka iliyopita kutokana na mafuriko ambayo yamekuwa yakiwahangaisha kila mwaka,” alisema Bw Gachagua. Alimsihi Gavana Godhana kujiunga na chama tawala cha Kenya Kwanza ili anufaike zaidi na matunda ya serikali. Gavana Godhana alisema kaunti yake imeathirika pakubwa kwa sababu Tana River iko katika nyanda za chini. “Kuna mito mingine midogo 10 ambayo imefurika kutokana na mvua na kumwaga maji yote katika Mto Tana. Asilimia 70 ya kaunti hii imeathiriwa na mafuriko na hiyo ni idadi ya takriban watu 200,000 ambao hawawezi kupata huduma muhimu,” alisema Bw Godhana. Gavana huyo alisema ametumia raslimali zote za kaunti kusaidia wahanga wa janga la mafuriko baada ya nyumba zao kufurika na mali kusombwa na mafuriko. “Tumekata miradi yote ili kuleta pesa kusaidia watu lakini mambo bado ni magumu zaidi,” alisema Bw Godhana. Haya yanajiri huku Mwakilishi wa wadi wa eneo la Garsen Kusini Bw Sammy Dumbe kuomba msaada akisema vijiji vya Wema, Hewani, Kulesa, Vumbwe, Lazima, Mwangaza, Peponi na Mikameni ambavyo vina idadi ya zaidi ya watu 20,000 huku wakihitaji chakula, matibabu na maji ya kunywa. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA KALUME KAZUNGU VIJANA na wanawake wa vijiji vya mpakani mwa Kenya na Somalia wamepokezwa na kuhitimu ujuzi wa taaluma mbalimbali zitakazowasaidia kujinasua kutoka kwa itikadi kali na umaskini. Hafla ya kuwasherehekea vijana na akina mama hao zaidi ya 30 iliandaliwa katika kijiji cha Kiunga kilichoko Lamu Mashariki. Kupitia Shirika la Uhifadhi wa Mazingira na Biashara (NRTT), vijana na akina mama hao walipokezwa mafunzo na kisha  kufuzu na hata kukabidhiwa vyeti. Miongoni mwa ujuzi waliofuzu nao ni ufundi wa kukatabati mashine, pikipiki, mashua na maboti. Pia walifuzu ujuzi wa kushona na ulimbwende wa mavazi. Mradi wa NRTT uliofadhili mafunzo hayo unatambuliwa kwa jina Ujuzi Manyattani. Mwenyekiti wa NRTT Bw Kevit Desai alisema furaha yake ni kuona vijana na akina mama wengi zaidi wamepokezwa ujuzi ili kuwawezesha kupata ajira au kujiajiri na kujiendeleza kimaisha. Bw Desai alisema mradi huo Wa ufadhili wa akina mama na vijana unatekelezwa kwenye kaunti nane za hapa nchini. Mbali na Lamu, kaunti nyingine ni Marsabit, Samburu, Isiolo, Laikipia, Baringo, Pokot Magharibi na Garissa. Kulingana na Bw Desai, mradi huo wa Ujuzi Manyattani ulizinduliwa rasmi 2019 na kufikia sasa karibu vijana na wanawake 1,000 wamenufaika na mpango huo kote nchini. “Leo tuko hapa Kiunga kushuhudia kufuzu kwa vijana na wanawake kwenye taaluma mbalimbali walizopokezwa kupitia mpango wa Ujuzi Manyattani. Twashukuru kwamba kupitia mpango huu,vijana na akina mama wamepokezwa ujuzi wa taaluma tofauti tofauti ambazo tayari zimewawezesha kupata ajira ilhali wengine wakijiajiri. Tutaendelea na mpango huu ili kuinua maisha ya wakazi wa Lamu na kaunti nyingine za Kenya zinazonufaika na mradi huu,” akasema Bw Desai Bi Tima Mohamed ambaye ni mmoja wa waliofuzu alishukuru wafadhili wa mradi huo kwa kuwapokeza ujuzi. Bi Mohamed alisema ni kupitia mafunzo hayo ambapo wanawake, hasa wale wa asili ya Waswahili Wabajuni wamezingatia kufanya kazi zikiwemo zile ambazo awali zilinasibishwa kuwa za wanaume, hivyo kujipatia mtaji na kujitegemea. “Wanawake hapa tulitegemea sana waume wetu kwa mahitaji. Tangu tulipopokezwa mafunzo na NRTT, wengi wetu tumejiajiri, hivyo kujitegemea kwa mambo mengi ya kifamilia,” akasema Bi Mohamed. Kauli yake iliungwa mkono na kiongozi wa vijana eneo la Kiunga Bw Mohamed Shali aliyesema mafunzo na ujuzi waliopata vijana umewawezesha kutia bidii maishani na kujiendeleza. “Badala ya vijana kujiingiza kwenye itikadi Kali, ugaidi na matumizi ya dawa za kulevya, wengi wetu tulipopokezwa na kuhitimu ujuzi mbalimbali kwa sasa tumejukumika katika ajira nakadhalika. Hakuna nafasi ya kudanganywa kutumia dawa za kulevya au kuingia katika itikadi kali na ugaidi wakati kazi zikitungoja,” akasema Bw Shali. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MWANGI MUIRURI BARAZA Kuu la Usalama nchini (NSC) ambalo mwenyekiti wake ni Rais William Ruto limetoa orodha ya aina 30 za uhalifu ambao raia ni sharti wawe chonjo kuepuka msimu huu wa Krismasi na kuelekea sherehe za Mwaka Mpya. Maafisa kutoka vitengo vya ujasusi, jeshi, polisi, maafisa wa utawala katika maeneo mbalimbali na wanachama wa kamati zote za usalama mashinani wameagizwa kuwa makini na kuunda mikakati ya kukabiliana na aina yoyote ya uhalifu na ujambazi huo. Katika nyaraka rasmi kwa Wizara ya Ulinzi na Wizara ya Usalama wa Ndani ambazo zinatarajiwa kutoa sera za mwelekeo kwa vyombo vya kudumisha usalama mashinani, Rais Ruto amesema kwamba anatarajia taifa libakie tulivu na thabiti ili kutoa fursa kwa ustawi wa nchi. “Ni matumaini yangu kwamba juhudi ambazo tumekuwa tuykiweka katika kupambana na aina zote za ujambazi zitaendelea kuzidishwa na kudumishwa ili hata msimu huu wenye changamoto nyingi za kiusalama utuache tukiwa na uthabiti,” akasema Rais Ruto kwa wosia huo wake. Ya kwanza kwenye orodha ya changamoto hizo za kiusalama zinazotarajiwa katika msimu huu wa kuelekea sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya ni ugaidi ambao unakisiwa huenda ukumbe maeneo kadha ya nchi sanasana maeneo ya Pwani, Kaskazini Mashariki na Nairobi. Pia kuna wizi wa kujihami ambao unatarajiwa kunoga katika mitaa mbalimbali ya hapa nchini, kaunti zote zikiorodheshwa kama walengwa. Tatu kwenye orodha hiyo ni wizi wa mifugo ambao huathiri maeneo ya Rift Valley lakini hali kwa sasa ikiripotiwa katika maeneo mengi ya Mlima Kenya pia. Nne kuna utekaji nyara na kisha kudai malipo ambao huandamana pia na wizi wa magari, ambapo kaunti zote zimeonywa ziwe tayari. Tano kuna ukatili dhidi ya vijana wa kiume wanaotahiriwa msimu huu pia. Kuna malalamiko kwamba wahuni majirani hutesa vijana baada ya kupashwa tohara. Unyama wa sita ni upashaji wa tohara kwa wasichana na ambao unakisiwa kuchukua mkondo mpya ambapo wazazi wengine wanawapeleka wasichana wao kutekelezewa unyama huo katikahospitali za umma na zile za kibinafsi. Uavyaji mimba pia umeorodheshwa kama changamoto ya msimu wa Krismasi huku uhalifu wa nane ukiwa ni ndoa za mapema hasa kwa wasichana ambao wamemaliza masomo yao ya Darasa la Nane na wengine wa Kidato cha Nne. Ya tisa kuna ajira ya watoto ambayo pia imeorodheshwa kama mojawa ya ukiukaji wa haki za kimsingi na pia kuathitri usalama wa kitaifa. Kwenye listi hiyo pia kuna magari mabovu barabarani na spidi ya juu huku madereva na makondakta wakisaka kubeba abiria wengi kupita kiasi ili wavune kupitia nauli hivyo basi kuzua ajali kiholela. Sasa uhalifu mwingine kutoka nambari 11 hadi 30 tunauweka kwa jedwali hapa chini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MHARIRI
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini.
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na BENSON MATHEKA
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI