text
stringlengths
3
16.2k
UFICHUZI wa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko kwamba mtu aliingia kwenye seli anamozuiliwa katika kituo cha... Na BENSON MATHEKA
Aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Bw Mike Sonko anajuta kwa vitendo alivyofanya akiwa mamlakani; akiepuka kuadhibiwa kwa... Na RICHARD MUNGUTI
KAMA kuna wakati wenye changamoto tele kwa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko ni sasa.
Maji yalizidi unga hata... Na RICHARD MUNGUTI
MASAIBU ya aliyekuwa gavana wa Nairobi, Bw Mike Sonko, yaliongezeka Jumatano ilipofichuka kuwa serikali inapanga... Na RICHARD MUNGUTI
ALIYEKUWA Gavana wa Nairobi, Mike Sonko aliangua kilio kortini Jumatano wakati wa kusikizwa kwa kesi ya ufisadi wa... Na CHARLES WASONGA
WANASIASA na watu ambao majina yao yatawekwa katika orodha ya aibu ya Tume ya Uwiano na Utangamano ya Kitaifa (NCIC)... BENSON MATHEKA na SIMON CIURI
Masaibu ya aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Mike Sonko yaliendelea kuongezeka jana alipozuiliwa rumande baada... Na RICHARD MUNGUTI
MASAIBU ya aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko Mbuvi Gidion Kioko yameongezeka baada ya  kusukumwa ndani hadi... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA SAMMY WAWERU MSANII tajika wa nyimbo Mugithi, Samuel Muchoki maarufu kama Samidoh huenda ametengana na mpenzi wake mwanasiasa Karen Nyamu. Hii ni kutokana na video iliyochipuka ambayo anaskika akisema “nilikuwa kwenye ndoa ya mitara, sasa niko singo”. Samidoh amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Seneta Maalum Karen Nyamu, na wamejaaliwa kupata watoto wawili. Msanii huyo wa nyimbo za Agikuyu, alifichua kuachana na Karen kupitia video ya mbashara ya Tiktok (live) ambapo alikuwa akijibu maswali ya mashabiki wake. Wakati wa mafichuzi hayo, alionekana kuwa kwenye eneo la burudani alikoandamana na msichana ambaye hakuweka wazi endapo ndiye mchumba wake mpya. “Ati hongera kwa kuwa na mpenzi mpya…” Samidoh akasoma mojawapo ya jumbe zilizotumwa na mashabiki wake. Alijibu, “Si wewe pekee ulishushwa madaraka kutoka kiwango cha hadhi hadi dereva wangu…Nilikuwa kwenye ndoa ya mitara ila sasa niko singo”. Mfuasi huyo aliendelea kumdadisi, akitaka kujua iwapo Samidoh anafahamu kuhusu ukurasa wa kimitandao unaohusishwa na mchumba wake – Karen Nyamu Fun Page. Kwa ucheshi, mwimbaji huyo wa kibao tajika cha Kairetu Gakwa (Binti yangu) na Ndiri Mutwe Mwega (Sina kichwa kizuri) alisema kwa sasa anajishughulisha na biashara. “Kwa sasa, ninajishughulisha na masuala biashara. Ikiwa si mradi au biashara, ishi na mama yako,” alielezea. Shabiki wake alimkejeli akitaka kujua aliko nina yake, isijulikane ikiwa alimaanisha mama yake mzazi au mpenzi wake. “Ameoleka na kwa sasa anafurahia fungate (honeymoon),” Samidoh alidokeza. Kidosho aliyeandamana naye alitambua shabiki huyo kama Shabaan, akisema kwamba yeye ni mchochezi. “Wee acha hiyo, unajua Shabaan wewe ni mchochezi sana… (Yuko hapa (akimaanisha Karen Nyamu),” mwanadada huyo alisema. Naye Samidoh aliendelea, “Tunataka Karen, naona hivo ndivo mchango safuni unasema…Naona, lakini sasa yuko online kweli?” Kipusa aliyeandamana naye, alijibu, “Yuko online, mjaribu”. Aidha, shabiki wa Samidoh alitaka Karen Nyamu ajumuishwe kwenye mazungumzo hayo ya mbashara Tiktok. Kilichoshangaza zaidi na kuashiria utengano wa Samidoh na Karen, ni kudai kwamba alimbloki mtandaoni na angeweza kushiriki endapo atamuondoa alikomuweka. “Yuko kwenye orodha ya kublokiwa, sasa hiyo ndio shida. Labda nisitishe mazungumzo haya ya moja kwa moja ili nimuondoa aweze kujumuika nasi,” Samidoh alifafanua. Mahusiano kati ya Samidoh na Karen, ndiyo yalichangia kuachana na mkewe, Edday Nderitu ambaye alihamia Amerika Mei 2023. Edday alikuwa ameonya msanii huyo mapema 2023, akisisitiza kwamba hakuwa tayari kuwa kwenye ndoa ya mitara. Samidoh na Edday wana watoto watatu pamoja. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MAOSI WAKAZI wa mtaa wa Mazembe viungani mwa mji wa Nakuru wamekiri kuhangaishwa na wezi ambao huwaibia na kuwasindikiza hadi nyumbani. Huwawekea ulinzi huo makusudi ili kuhakikisha kwamba wateja wao wanafika nyumbani salama salimini. Kwa kawaida, wahuni wamebuni mbinu mpya ya kutembea na mbwa wakubwa nyakati za usiku, ili kujiwekea ulinzi wa kibinafsi. Owen Shibala mwendeshaji bodaboda kati ya Nakuru mjini na Mazembe, anasema hajui walikotoa ujasiri walio nao kushika doria usiku utadhani ni polisi. Mazembe ni mojawapo ya mitaa ambayo hushuhudia visa vya kihalifu na utumiaji wa mihadarati mara kwa mara. “Ukikutana nao usiku ni lazima usalimishe kila kitu lau sivyo utaona cha mtema kuni. Watakucharaza viboko na kuiba kila kitu cha nguvu,”akasema. Hata hivyo, wanapoiba hujitwika jukuma la kuwasindikiza wakazi, wasije wakakutana na vibaka wengine barabarani. Aidha, wanalia sare za polisi jambo linalowafanya baadhi ya raia kuamini huenda wanashirikiana na maafisa wa polisi. Baadhi yao wanajifanya ni maafisa wa polisi ambao huwa wameshika doria, wakilenga kuhangaisha wapita njia wanaotoka kazini usiku. Agnes Wahome mfanyibiashara mtaani Rhonda anasema huwa wamejihami kwa visu, rungu na wako tayari kupigana. Kulingana na Bi Wahome, hii ni hali ya kawaida siku hizi katika mitaa ya Manyani, Bondeni na Freearea ambapo vijana wengi wamejiingiza kwenye uhalifu. Bi Wahome anasema wahalifu wengi wanajulikana, kwani ni vijana wadogo kutoka mitaa jirani ya Flamingo na Lakeview. Mkazi huyo angependa polisi kushika doria katika maeneo husika ili kuzuia kuzuka kwa magenge hatari yanayohangaisha wenyeji. Hili linajiri siku chache baada ya Taifa Leo Dijitali kufichua visa vya wizi ambapo baadhi ya wezi kutoka kwenye mtaa wa Gioto, Nakuru wamekuwa wakipika chakula katika kila nyumba wanamoingia kuiba. Mtaa wa Bondeni, Kaunti ya Nakuru ambapo wezi huwaibia wakazi na kuwasindikiza mpaka nyumbani. PICHA|RICHARD MAOSI
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L

You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MUNGUTI MASKWOTA wapatao 10,000 wamewasilisha upya kesi katika Mahakama ya Upeo wakiomba ibatilishe uamuzi kwamba wafukuzwe kutoka kwa shamba la ukubwa wa ekari 25,000 wanalong’ang’ania umiliki wake na familia ya mwanasiasa marehemu Mark Too. Maskwota hao wanaodai mababu zao ndio waliotimuliwa kutoka kwa shamba hilo enzi za ukoloni, wanasema walipewa shamba hilo rasmi na aliyekuwa Rais hayati Daniel arap Moi, kisha Kamishna wa Ardhi M Okundu akaratibisha uamuzi huo mwaka 2007. Katika ombi lililowasilishwa na wakili William Arusei chini ya sheria za dharura, kikundi cha maskwota hao–Sirikiwa Squatters Group–kimeomba mahakama ibatilishe uamuzi huo kwa vile ilitegemea ushahidi ambao haukuwa umewasilishwa katika kesi waliyoshtaki katika Mahakama ya kuamua kesi za mashamba (ELC), Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu. Pia wameeleza bayana Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaack Lenaola, na William Ouko walitegemea ushahidi wa Afisa wa Ugavi wa Mashamba R J Simiyu kutoa uamuzi wang’atuke shambani. Maskwota hao wamesema ushahidi wa Bw Simiyu uliowasilishwa mbele majaji hao saba kwa njia ya afidaviti ni mpya na kamwe “haukuwasilishwa mbele ya Jaji Antony Ombwayo aliposikiliza na kuamua kesi hiyo 2017.” Pia wanasema ushahidi huo haukuwasilishwa Mahakama ya Rufaa iliyosikiliza rufaa iliyowasilishwa na kampuni ya Fanikiwa, familia ya marehemu Mark Too, kampuni ya Lonrho Agribusiness (EA) Ltd, na Bw David K Korir. Hivyo basi, maskwota hao wanaeleza mahakama hii ya upeo kwamba ni kinyume cha sheria kutegemea ushahidi mpya kutoa uamuzi wa kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma. “Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu wa Desemba 15, 2023, hauna mashiko kisheria na kamwe hauna nguvu kisheria kuwatimua maskwota hawa kutoka kwa shamba lao,” asema Bw Arusei. Pia maskwota hawa wanadai kwamba badala ya Mahakama ya Juu kujadili masuala ya kikatiba jinsi ilivyo jukumu lake, majaji hao walianza kufafanua na kutafsiri ushahidi wa watu binafsi na kuelezea maana ya ‘skwota’. Mahakama hii imeombwa ikague upya uamuzi iliyotoa kwa vile ilidanganywa na walalamishi na pia kutendewa ujanja. Akinukuu maamuzi ya majaji wastahiki kama vile Lord Dening, Bw Arusei amesema, mahakama ikigundua ilipotoshwa au kudanganywa na upande mmoja, iko na mamlaka na uwezo wa kufutilia mbali uamuzi iliyotoa na kuandika mwingine. Maskwota hao wanaomba Mahakama ya Juu iwarudishe shambani kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Ombwayo na Mahakama ya Rufaa. Vile vile mahakama hiyo imekosolewa kwa kumshambulia hayati Moi katika uamuzi huo pasi kutoa agizo wasimamizi wa mali yake wafike mbele yao kutoa mwanga kuhusu suala la umiliki wa shamba hili lililorudishwa kwa serikali na kampuni iliyokuwa inakuza miti inayotumika katika viwanda vya ngozi. Naibu msajili wa Mahakama ya Juu Nelly Kariuki aliwaamuru maskwota hao wawakabidhi nakala za kesi hii yao mpya wahusika wote kabla ya Januari 31, 2024, kesi itakapotajwa tena kwa maagizo zaidi. Jaji aliyesikiliza kesi hii mpya hakuiratibisha kuwa ya dharura ila aliamuru pande zote ziwasilishe ushahidi katika muda wa siku 14 kuanzia Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti,  baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA JOSEPH NDUNDA MZEE wa miaka 50 aliyemuoa msichana wa miaka 16 anakabiliwa na mashtaka ya unajisi kinyume na kifungu cha 8 (1) (4) cha Sheria. Caleb Oguma alishtakiwa kwa kumnajisi mtoto huyo tarehe tofauti kati ya Agosti 1 na Desemba 2, 2023 katika eneo la Darfur huko Kariobangi, Nairobi alikokuwa akiishi naye. Anakabiliwa na shtaka lingine la kumnajisi msichana huyo kinyume na kifungu cha 11 (1) cha SOA ambapo anadaiwa kumshika mtoto huyo sehemu zake za siri kwa makusudi na isivyo halali katika kipindi hicho. Mshukiwa huyo anayetoka Kaunti ya Migori alikutana na mtoto huyo na kumshawishi aandamane naye Nairobi baada ya kuahidi kuwa atampeleka kufanya kozi ya kushona nguo. Alikuwa mwanafunzi wa Kidato cha Tatu. Aliandamana naye hadi Nairobi baada ya kukubali ombi lake la kumsajili kwa kozi hiyo. Hata hivyo, alipofika Nairobi, alimpeleka kwa mkewe na wakaendelea kuishi pamoja hadi afisa wa Nyumba Kumi alipogundua kuwa Oguma alikuwa ameoa msichana huyo. Hata hivyo, Oguma alikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkuu Irene Gichobi wa Mahakama ya Makadara. Mshukiwa huyo aliachiliwa kwa dhamana ya Sh200, 000 akisubiri kufikishwa mahakamani. Kesi hiyo itatajwa Januari 10, 2024. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA TITUS OMINDE Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu amepuuzilia mbali madai ya kasoro katika usahihishaji wa mtihani wa KCPE mwaka huu huku akipongeza maafisa wake kwa kutenda kazi njema. Akizungumza katika taasisi ya mafunzo anuai ya Eldoret National Polytechnic wakati wa hafla ya kufuzu ya 18, Bw Machogu alisifu jinsi mtihani ulivyosahihishwa, akisisitiza kwamba waliosahihisha walifanya kazi nzuri. Bw Machogu alidai kuwa hitilafu chache zilizoshuhudiwa wakati wa uwekaji alama zilitokana na changamoto za kiufundi ambazo ni za kawaida. “Usahihishaji wa KCPE uliomalizika hivi punde ulikuwa mzuri, nina maafisa waliohitimu ambao walifanya kazi nzuri wakati wa uwekaji alama, na changamoto chache ambazo zilishuhudiwa zilitokana na hitilafu za kiufundi ambazo zitatatuliwa hivi karibuni,” alisema Bw Machogu. Kulingana na Bw Machogu, madai ya kusahihishwa vibaya kwa mtihani huo hayana msingi ambapo alisema maafisa wa KNEC na wataalamu kutoka wizara ya elimu iko tayari kudhihirisha kamati ya bunge kuhusu elimu jinsi zoezi hilo lilivyofanywa kwa njia bora. Bw Machogu aliwapongeza maafisa waliohusika katika kusahihisha mtihani huo kuanzia mwanzo hadi mwisho. Waziri huyo alisisitiza kuwa shughuli nzima ya kutia alama ilikuwa kamilifu licha ya malalamiko kutoka kwa watahiniwa na wazazi kutoka maeneo tofauti nchini. Alisema kuwa matokeo ya mitihani yaliyoonyeshwa katika tovuti ya KNEC yalikuwa bora na changamoto ziliibuka kutokana na uwasilishaji. “Tulipotoa mtihani, kila kitu kilikuwa sawa na Wakuu wa Shule mbalimbali wanaweza kuthibitisha kwamba matokeo katika tovuti ya KNEC kwa shule yalikuwa kamili, katika uwasilishaji kulikuwa na hitilafu za kiufundi,” alisema Bw Machogu. Aliondoa hofu yoyote kabla ya matokeo ya KCSE akisema kuwa kila kitu kiko sawa na hakuna haja ya kuwa na wasiwasi. Akijibu hoja za Mbunge wa Kesses Julius Rutto aliyesema kuwa matukio yalifuata baada ya kutangazwa kwa mtihani huo wa KCPE 2023 yanatia doa uadilifu wa KNEC . “Matokeo ya hivi majuzi ya KCPE ambapo wanafunzi wengi hawakuridhishwa na jinsi mtihani ulivyosahihishwa yanaweka uadilifu wa baraza la mitihani hatarini na lazima wizara ijieleze waziwazi kuhusu suala hilo tunapotarajia matokeo ya KCSE kufikia mwisho wa mwezi huu,” akasema Bw Rutto. [email protected]   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA BRIAN OCHARO RIPOTI ya matibabu imefichua jinsi uchunguzi wa waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono katika vituo vya matibabu unavyoweza kutumiwa vibaya kwa faida za kibinafsi. Uchunguzi wa tatu uliofanyiwa msichana wa miaka tisa ambaye alidaiwa kunajisiwa sasa unafafanua kuwa mtoto huyo hajanajisiwa. Hii inapingana na ripoti ya awali ambayo ilikuwa imetoa matokeo chanya ya unajisi. Uchunguzi huo wa tatu wa matibabu ulifanywa na madaktari wanne. “Mtoto huyo yuko sawa. Hakuna michubuko wala makovu yaliyoonekana,” ripoti hiyo iliyotiwa saini na madaktari watatu na muuguzi anayesimamia Kituo cha waathiriwa wa Unyanyasaji wa Kijinsia katika hospitali kuu ya eneo la Pwani (CGTRH), ambapo uchunguzi huo ulifanyika ilisema. Uchunguzi huo wa tatu ulifanyika mbele ya watu 10, ikiwa ni pamoja na madaktari watu, muuguzi mmoja, afisa wa watoto, na mama wa mtoto huyo. Ripoti hii inakinzana na ripoti ya awali kutoka kituo hicho kimoja iliyothibitisha kuwa msichana huyo alinajisiwa. Ripoti hiyo ambao sasa imewasilishwa kortini, iliamriwa na Mahakama Kuu mjini Mombasa kutokana na ripoti zinazokinzana za uchunguzi wa awali. Mahakama Kuu ilipokea taarifa za fomu mbili zinazokinzana za Huduma ya Baada ya Ubakaji (PRC), moja ikionyesha kuwa mtoto huyo alinajisiwa huku ingine ikitoa matokeo tofauti ilisababisha wasiwasi kuwa taratibu za matibabu zilikuwa zikichezewa ili kufikia matokeo mahususi. Jaji wa Mahakama Kuu ya Mombasa Olga Sewe alitoa agizo kwa mtoto huyo kufanyiwa uchuguzi wa matibabu kwa mara ya tatu ili kubaini ukweli, baada ya ripoti mbili zinazokinzana kutolewa kutokana na uchunguzi huo wa kimatibabu. Uchunguzi huo wa tatu ambao kwa sasa umeondoa shauku juu ya madai ya unajisi wa mtoto huyo uliamriwa kufanywa na daktari wa uzazi na mshauri wa magonjwa ya wanawake katika CGTRH, mbele ya matabibu wawili ambao walitayarisha ripoti zinazokinzana, pamoja na wazazi au walezi wa mtoto huyo. Kesi hiyo ilifika Mahakama Kuu baada ya shirika la kutetea haki za binadamu Commission for Human Rights and Justice (CHRJ) kuomba kufutwa kwa fomu mbili za awali za PRC zenye matokeo yanayokinzana, zikitaja nia mbaya kwa mmoja wa wahusika waliokuwa wakishinikiza madai ya unajisi wa mtoto huyo. Mkurugenzi mtendaji wa CHRJ Julius Ogogoh alimweleza Jaji Sewe kwamba mojawapo ya ripoti hizo inaonekana kubadilishwa kwa nia mbaya, hivyo basi mahakama ilihitaji kuwa wazi kuhusu hali ya mtoto huyo. Baba mzazi wa mtoto huyo aliaga dunia kabla ya kuzaliwa kwake. Baadaye, mamake aliingia katika uhusiano wa kimapenzi na mwanamume mwingine, ambaye sasa ni baba wa kambo wa mtoto huyo. Mtoto huyo alipelekwa hospitali kuchunguzwa baada ya kudaiwa kuwa alionekana kuwa alinajisiwa. Mtoto huyo alipelekwa hadi CGTRH kwa uchunguzi, na fomu ya PRC ilionyesha kuwa alinajisiwa. Stakabadhi za mahakama zinaonyesha kuwa mtoto huyo alipekwa katika Hospitali ya Pandya kwa uchunguzi ambapo daktari alithibitisha kuwa mtoto huyo hajanyanyaswa kingono. Baadaye, mtoto huyo alirejeshwa katika hospitali ya CGTRH kwa uchunguzi zaidi ampapo fomu ya PRC ilijazwa na kuonyesha kuwa mtoto huyo hajanajisiwa. Karatasi za mahakama zinaonyesha kwamba kuna mzozo kati ya mama ya mtoto huyo na familia ya baba mzazi kuhusu malezi yake. Mahakama itatoa mwelekeo kuhusu kesi hiyo Desemba 13. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA WINNIE ONYANDO WANAOTUMIA mtandao wa kijamii wa TikTok kwa minajili ya kuendeleza biashara sasa wataweza kujichumia hela kupitia maudhui yao. Hii ni kulinagna na Mkurugenzi wa Idara ya Sera ya Umma serikalini TikTok Barani Afrika, Fortune Mgwili-Sibanda. Akizungumza jijini Nairobi, mkurugenzi huyo alisema jukwaa hilo linalenga kuanzisha mfumo ambapo watumiaji wataweza kupata hela au zawadi mbalimbali kupitia maudhui yao. “Tumezindua mifumo mbalimbali ambapo mtumiaji anaweza kujichumia hela. Kwa mfano, Tiktok series inawaruhusu watumiaji kudai malipo kutoka kwa wafuasi au watu wanaotazama maudhui yao,” akasema Sibanda. Hata hivyo, alisema mifumo kama hiyo haijashika kasi nchini Kenya na hata mataifa mengine Afrika. Hatua hiyo itawezekana tu kupitia mfumo kama vile live gift na TikTok series. Kwa mfano, unapojirekodi ukipika, basi wafuasi wako wanaweza kukutumia zawadi mbalimbali na baadaye unaweza kubadilisha kuwa fedha. Haya yanajiri miezi michache tu baada ya Rais William Ruto kuzungumza na Afisa Mkuu Mtendaji wa TikTok, Shou Zi Chew kuhusiana na masuala ya kudhibiti maudhui yanayopeperushwa kwenye mtandao huo wa kijamii. Kumekuwa na mazungumzo yanayoendelea nchini kuhusu ikiwa mtandao huo upigwe marufuku au la. Baadhi ya watu wanalalama kuwa mitandao ya kijamii inatumiwa na waliopotoka na ambao huweka video za ngono na wengine kujirekodi wakiwa uchi. Agosti 15, 2023, Afisa Mkuu Mtendaji wa shirika la kutoa ushauri la Bridget Connect Consultancy, Bob Ndolo katika ombi lake kwa Bunge la Kitaifa, aliwataka wabunge kupiga marufuku utumiaji wa TikTok nchini, akisema mtandao huo unachangia kuenea kwa maudhui ya ngono. Ombi hilo litazingatiwa na kamati ambayo itatoa uamuzi wake baada ya siku 60 (tangu lilipowasilishwa bungeni). Hata hivyo, mjadala mkali ulishuhudiwa, baadhi ya wabunge wakisema mtandao huo unatumiwa kama chanzo cha mapato kwa watu wengi, wakiwemo vijana.     You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MWANGI MUIRURI  MWANAMUME Mkenya ameshtakiwa nchini Amerika kwa makosa ya kujaribu kupanga njama kuua mwanamke wa familia yao. Bw Leonald Thuo Mwithaga, mwenye umri wa miaka 52 ameshtakiwa kwamba alijaribu kufadhili njama hiyo nchini Amerika. Stakabadhi ambazo zimewasilishwa mahakamani ambapo ameachiliwa kwa bodi ya Dola 5 milioni za Amerika (Sh766.5 milioni) zinadai kwamba alijaribu kumshawishi dereva wa teksi kumsaidia kupata muuaji wa kutekeleza mauti hayo. Bw Mwithaga alishtakiwa rasmi Desemba 5, 2023 baada ya kukamatwa Desemba 4, 2023. Dereva wa teksi ndiye alifika katika kituo cha polisi na kuripoti kwamba Bw Mwithaga alikuwa amejaribu kumsajili katika njama hiyo ya mauaji. “Bw Mwithaga ambaye alikuwa akifanya kazi nchini humo kama meneja wa benki alikuwa amepanga mauaji hayo yatekelezwe kati ya Januari 28, 2024 na Februari 3, 2024 kwa kuwa angekuwa amesafiri hadi nchini Kenya basi kumwondolea hatari ya kuwa mshukiwa,” taarifa ya mashtaka inasema. Baada ya kuacha kazi Juni 2023, alipania kurudi nchini Kenya Desemba 7, 2023. Bw Mwithaga anasemwa kwamba alikuwa katika maandalizi ya kutekeleza mauaji hayo na ambapo kati ya Septemba 9 na Desemba 1, 2023 alikuwa akizidisha njama hiyo kupitia kusaka muuaji wa kulipwa. Tarehe ambazo zimetiliwa mkazo katika mashtaka hayo ni Oktoba 26, 2023 ambapo Bw Mwithaga anadaiwa kutumia maneno kwamba “nataka muuaji ambaye anaweza kuweka huyo mwanamke chini”. Novemba 3, 2023 anadaiwa kwamba alisema “natamani sana mtu wa kugonga mwanamke huyu na ammalize”. Nayo Desemba 1, 2023 Mwithaga anadaiwa kwamba alitaka mwanamke huyo “adungwe na sumu ambayo itamsababishia maradhi makuu sawa na Kansa”. Baada ya dereva huyo wa teksi kupiga ripoti kuhusu njama ya Bw Mwithaga, stakabadhi za mashtaka zinaeleza, mpelelezi wa polisi alijitokeza akijitambulisha kama muuaji ambaye angempeleka mlengwa kwa hepi na amuwekee sumu kwa mapochopocho ya sherehe. Ni baada ya Bw Mwithaga kujadiliana na afisa huyo kuhusu njama hiyo ya mauaji bila kujua alikuwa akijiingiza kikangaoni ambapo alitiwa mbaroni na akashtakiwa kwa madai ya ujambazi wa kupanga mauaji na pia kutishia maisha ya shahidi. Kwa sasa, Bw Mwithiga ameamrishwa kurejesha kwa serikali ya Amerika na bunduki zote alizokuwa amesajiliwa kumiliki, huku akionywa kubakia umbali wa futi 2, 500 kutoka kwa shahidi wote katika mashtaka hayo yanayomkabili. Aidha, pasipoti yake imetwaliwa na hawezi akatoka Mji wa Connecticut na kwa wakati wote atakuwa chini ya ujasusi wa kiteknolojia kwa masaa 24 hadi kesi yake iamuliwe. Atarejea kortini mnamo Januari 26, 2024.   [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MARY WANGARI KUNDI la wabunge kutoka Kisii limemtetea vikali Mdhibiti wa Bajeti Margaret Nyakang’o, likidai kuwepo maafisa nje na ndani ya serikali wenye nia ya kuhujumu utawala wa Rais William Ruto na Naibu Rais Rigathi Gachagua. Wakiongozwa na Kiranja Mkuu katika Bunge la Kitaifa, Silvanus Osoro, waundasheria hao wametaja hatua ya kumkamata hadharani Bi Nyakang’o kama njama za kisiasa wakiapa kumtetea kisheria. Waundasheria hao wamedai wahusika, wanaojumuisha maafisa wa serikali iliyopita waliosalia mamlakani, wamekuwa wakitumia nyakati ambapo Rais Ruto amesafiri nje ya nchi na Naibu wake ameshughulishwa na masuala ya El Nino, kuwalenga maafisa wakuu wa umma kwa nia ya kusawiri vibaya utawala wa UDA. “Tumegundua katika siku za hivi karibuni kama miezi sita iliyopita na baada ya kufuatilia kwa makini tukio hili kwamba kuna makundi ndani na nje ya serikali wanaotumika kula njama za kuhujumu nia njema ya Rais na Naibu Rais ya kusawazisha wanajamii kwenye ajira katika asasi za umma,” alisema Bw Osoro. Mbunge huyo wa Mugirango Kusini alisema kuwa Kiongozi wa Taifa na Naibu wake hawana habari kabisa kuhusiana na masaibu yaliyomkumba Mdhibiti wa Bajeti kwa kuwa “Rais alikuwa amesafiri naye Naibu Rais alikuwa anashughulikia El Nino ambayo tunavyojua imesababisha majanga.” “Leo Rais atawasili na sisi kama viongozi tutamwona kwa sababu tunajua hajui, tulipata habari pia naibu rais hajui, EACC pia hawajui.” Mbunge huyo alirejelea kisa cha hivi majuzi ambapo Mkurugenzi wa Ukumbi wa Kitaifa wa Bomas, Peter Gitaa ikiwemo maafisa wengine 11 walisimamishwa kazi kufuatia mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC). Walikashifu namna ambavyo EACC ilimkamata Bi Nyakango alipokuwa katika ziara ya kikazi Mombasa wakisema ni kinyume na msimamo wa serikali ya Kenya Kwanza kuhusu kulinda hadhi ya maafisa wa umma. “Ziara hiyo ililipiwa na walipa ushuru, mbona hawangesubiri hadi arejee Nairobi au wamchukue nyumbani kwake, aina hii ya kufedhehesha sio tulichoahidi watu wetu, nadhani hata si jambo ambalo Rais na Naibu Rais wanataka. Haya ni mambo tuliyopinga tulipokuwa tukifanya kampeni kama muungano wa Kenya Kwanza. Tulisema hakutakuwa tena na kuandamwa kisiasa, watu hasa maafisa wakuu wa umma hawataaibishwa hivyo,” alisema. “Haingekuwa vigumu kumwagiza Bi Nyakango kujiwasilisha kwa EACC au popote pale kwa sababu ni mtumishi wa umma na kisha kumfikisha kortini. Lakini mnasubiri, mnamkamata kama mwizi, mtu ambaye amehudumia taifa hili, hatuwezi kukaa kimya. Tulimpiga msasa alipoteuliwa na akaidhinishwa kuhudumu katika wadhifa wake, kwa nini masuala hayo hayakujitokeza wakati huo?” Waundasheria hao sasa wameapa kusimama imara na Bi Nyakango wakiwalaumu baadhi ya watu wenye dhana kwamba baadhi ya wanajamii hawafai kushikilia nyadhifa muhimu serikalini.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA SHIRIKA la Kukadiria Ubora wa Bidhaa Nchini (Kebs) limefafanua mafuta ya kupikia yaliyoingizwa nchini na Shirika la Kitaifa la Biashara (KNTC) ni salama kwa matumizi ya binadamu. Kupitia taarifa Jumatano, Desemba 6, 2023 Kebs ilisema kuwa mafuta hayo ya maji maji (salad) yaliyonunuliwa kutoka ng’ambo, yamefanyiwa ukaguzi hitajika na kubainika kuafiki viwango hitajika. Hata hivyo, shirika hilo lilisema kuwa sampuli za mafuta hayo zilizochunguzwa hazikutimiza viwango hitajika vya madini ya Vitamin A. “Kutokana na vipimo vilivyofanyika mafuta hayo yalifikia mahitaji yote ya kiafya na kiusalama yanayotumika nchini. Hata hivyo, sampuli zilizochunguzwa hazikuwa na viwango vinavyokubalika nchini vya Vitamin A. Hii sio kigezo cha kiafya na kiusalama na KEBS imewasilisha matokeo hayo kwa KNTC,” Kebs ikaeleza katika taarifa hiyo iliyotumwa kwa vyombo vya habari. Taarifa hiyo kutoka Kebs inajiri kufuatia ripoti zilizotolewa hivi majuzi kwamba baadhi ya mitungi ya mafuta hayo ya kupikia yaliyochunguzwa hayakuwa salama kwa matumizi ya binadamu. Mafuta hayo yalikuwa yameagizwa kutoka ng’ambo mapema mwaka huu kama sehemu ya mkakati wa serikali kupunguza gharama ya maisha. “Tunataka kuwahakikishia wananchi kwamba Kebs imejitolea kuhakikisha ubora za bidhaa zinazotengenezwa nchini na zile zinazoagizwa kutoka nje,” Kebs ikaeleza. Wiki hii, maafisa wa KNTC walihojiwa na maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) kutokana na tuhuma kwamba sheria haikufuatwa wakati wa utoaji wa zabuni ya uagizaji wa mafuta hayo ya kupikia ya thamani ya Sh9 bilioni. 00 You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA WINNIE ATIENO NAIBU Rais Rigathi Gachagua ameendelea kusuta magavana kutokana na janga la mafuriko nchini, akisema kazi yao kubwa ni kufanya vikao na wanahabari kwa nia ya kulalamika. Bw Gachagua alisema magavana wamekuwa wakishinda kwenye vyombo vya habari kueleza masuala ya mafuriko badala ya kwenda sehemu zilizoathirika kusaidia wahanga. Akizungumza Tana River, Bw Gachagua alisema ni sharti magavana waende mashinani ambapo Wakenya wameathirika na mafuriko badala ya kufanya vikao vya kulalamika tu. Naibu Rais alisema ameshuhudia madhara ya mafuriko hasa katika Kaunti za Garissa, Tana River na Mombasa hapo awali akieleza kuwa Rais William Ruto ameahidi kuwa hakuna Mkenya ambaye atakufa njaa kwa sababu ya mafuriko. Alimpongeza Gavana wa Tana River, Dadho Godhana, kwa juhudi zake za kusaidia wakazi waliaothiriwa na mafuriko. “Ndiyo maana tunataka tushikane kati ya Serikali Kuu na ile ya kaunti tusaidie waathiriwa. Tumefurahi kumpata Gavana papa hapa mashinani mahala wananchi wako. Wenzako wengine wameshinda kwenye vyombo vya habari wakipiga kelele. Hakuna lolote ambalo linaweza kutatuliwa kwenye vyombo vya habari,” alisema Bw Gachagua. Hii ni baada ya Baraza la Magavana kufanya kikao na wanahabari wiki mbili zilizopita na kumshtumu Bw Gachagua kwa ‘kuhadaa’ Wakenya kuwa kaunti zimetumiwa fedha za kusaidia waathiriwa wa mafuriko. “Shida za mafuriko ziko mashinani mahali wananchi wako, nendeni huko mjue shida iko wapi. Mahali dawa au chakula inatakikana unasaidia. Tusaidianeni katika hili janga la mafuriko,” alisema Bw Gachagua. Alisema Serikali Kuu imejizatiti kutoa ndege, magari ya jeshi na helikopta kusaidia wahanga wa mafuriko. Alisisitiza kuwa serikali pia imesambaza dawa za matibabu, neti za mbu na vyakula ambavyo vinakusudiwa kusaidia waathiriwa. “Tunahakikishia wananchi kuwa tunaelewa changamoto mnazopitia na si mwaka huu tu, hata miaka iliyopita kutokana na mafuriko ambayo yamekuwa yakiwahangaisha kila mwaka,” alisema Bw Gachagua. Alimsihi Gavana Godhana kujiunga na chama tawala cha Kenya Kwanza ili anufaike zaidi na matunda ya serikali. Kwa upande wake Gavana Godhana alisema kaunti yake imeathirika pakubwa kwa sababu Tana River iko sehemu ya chini. “Kuna mito mingine midogo 10 ambayo imefurika kutokana na mvua na kumwaga maji yote katika Mto Tana. Asilimia 70 ya kaunti hii imeathiriwa na mafuriko na hiyo ni idadi ya takriban watu 200, 000 ambao hawawezi kupata huduma muhimu,” alisema Bw Godhana. Gavana huyo alisema ametumia raslimali zote za kaunti kusaidia wahanga wa janga la mafuriko baada ya nyumba zao kufurika na mali kusombwa na mafuriko. “Tumekata miradi yote ili kuleta pesa kusaidia watu lakini mambo bado ni magumu zaidi,” alisema Bw Godhana. Haya yanajiri huku Mwakilishi wa wadi eneo la Garsen Kusini Bw Sammy Dumbe akiomba msaada akisema vijiji vya Wema, Hewani, Kulesa, Vumbwe, Lazima, Mwangaza, Peponi na Mikameni ambayo vina idadi ya zaidi ya watu 20, 000 vinahitaji chakula, matibabu ya afya na maji ya kunywa.     You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA KUKAMATWA na kushtakiwa kwa Msimamizi wa Bajeti (CoB) kwa kosa analodaiwa kutenda 2016, sasa kumechukua mkondo wa kikabila. Hii ni baada ya wanasiasa kutoka jamii ya Abagusii, wakiongozwa na Seneta wa Nyamira kudai ni njama ya serikali ya kudhulumu watu kutoka jamii hiyo “bila sababu maalum”. Dkt Nyakang’o ni mzawa wa eneobunge la Mugirango Magharibi, Kaunti ya Nyamira. “Tunachukulia kitendo hiki kama kuteswa kwa jamii ya Omogusii na utawala wa Rais William Ruto. Na sisi kama viongozi kutoka jamii hii hatutavumilia kudhulumiwa kwa mmoja wa wataalamu wetu kama Dkt Nyakang’o kwa kufanyakazi kazi yake kwa uadilifu na kisheria,” Bw Omogeni akasema. Bw Omogeni alikuwa ameandamana na wenzake; Richard Onyonka (Seneta wa Kisii), Jerusa Momanyi (Mbunge Mwakilishi wa Nyamira), Gloria Orwoba (Seneta Maalum), Stephen Mogaka (Mbunge wa Mugirango Magharibi) na Antony Kibagendi (Kitutu Chache Kusini), Jumanne, Desemba 5, 2023 katika kikao na wanahabari Jijini Nairobi. Bw Mogaka alisema Dkt Nyakang’o anaandamwa kwa kufichua sakata za ufisadi na ubadhirifu wa pesa katika serikali ya kitaifa. “Tunajua kwamba serikali hii ya Kenya Kwanza inakerwa na ripoti za kila mara ambazo Dkt Nyakang’o hutoa zikianika uozo wa ufisadi ndani ya serikali. Kwa mfano, majuzi afisa huyu alifika mbele ya Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (NADCO) na kuelezea jinsi pesa zinazotengewa mgao wa bajeti ya kulipa mishahara ya maafisa katika asasi mbalimbali huwa ni zaidi ya maradufu ya kiwango ambacho maafisa hao hupokea kila mwaka, kulingana na mwongozo wa tume ya kukadiria mishahara (SRC),” akasema. Viongozi hao walidai kushtakiwa kwa Dkt Nyakang’o ni sehemu ya njama ya serikali kumvua wadhifa wake na kuteua mtu ambaye atafumbia macho “maovu kama ufisadi na ubadhirifu wa pesa za umma.” Afisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma (ODPP) ilipendekeza kukamatwa kwa Dkt Nyakang’o baada ya uchunguzi wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kubaini kuwa alimlaghai Bi Claudia Mueni Sh29 milioni. EACC inasema afisa huyo alilipwa pesa hizo kwa kudai kuendesha chama cha akiba na mikopo (Sacco) kisheria, ilhali hakuwa amepata leseni ya kuendesha biashara hiyo.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MHARIRI
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini.
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na BENSON MATHEKA
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na MASHIRIKA
LONDON, Uingereza
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya... Na ELIZABETH MERAB