text
stringlengths
3
16.2k
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAKAZI wa mtaa wa Mazembe viungani mwa mji wa Nakuru wamekiri kuhangaishwa na wezi ambao huwaibia na kuwasindikiza hadi nyumbani. Huwawekea ulinzi huo makusudi ili kuhakikisha kwamba wateja wao wanafika nyumbani salama salimini. Kwa kawaida, wahuni wamebuni mbinu mpya ya kutembea na mbwa wakubwa nyakati za usiku, ili kujiwekea ulinzi wa kibinafsi. Owen Shibala mwendeshaji bodaboda kati ya Nakuru mjini na Mazembe, anasema hajui walikotoa ujasiri walio nao kushika doria usiku utadhani ni polisi. Mazembe ni mojawapo ya mitaa ambayo hushuhudia visa vya kihalifu na utumiaji wa mihadarati mara kwa mara. “Ukikutana nao usiku ni lazima usalimishe kila kitu lau sivyo utaona cha mtema kuni. Watakucharaza viboko na kuiba kila kitu cha nguvu,”akasema. Hata hivyo, wanapoiba hujitwika jukuma la kuwasindikiza wakazi, wasije wakakutana na vibaka wengine barabarani. Aidha, wanalia sare za polisi jambo linalowafanya baadhi ya raia kuamini huenda wanashirikiana na maafisa wa polisi. Baadhi yao wanajifanya ni maafisa wa polisi ambao huwa wameshika doria, wakilenga kuhangaisha wapita njia wanaotoka kazini usiku. Agnes Wahome mfanyibiashara mtaani Rhonda anasema huwa wamejihami kwa visu, rungu na wako tayari kupigana. Kulingana na Bi Wahome, hii ni hali ya kawaida siku hizi katika mitaa ya Manyani, Bondeni na Freearea ambapo vijana wengi wamejiingiza kwenye uhalifu. Bi Wahome anasema wahalifu wengi wanajulikana, kwani ni vijana wadogo kutoka mitaa jirani ya Flamingo na Lakeview. Mkazi huyo angependa polisi kushika doria katika maeneo husika ili kuzuia kuzuka kwa magenge hatari yanayohangaisha wenyeji. Hili linajiri siku chache baada ya Taifa Leo Dijitali kufichua visa vya wizi ambapo baadhi ya wezi kutoka kwenye mtaa wa Gioto, Nakuru wamekuwa wakipika chakula katika kila nyumba wanamoingia kuiba. Mtaa wa Bondeni, Kaunti ya Nakuru ambapo wezi huwaibia wakazi na kuwasindikiza mpaka nyumbani. PICHA|RICHARD MAOSI
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MUNGUTI MASKWOTA wapatao 10,000 wamewasilisha upya kesi katika Mahakama ya Upeo wakiomba ibatilishe uamuzi kwamba wafukuzwe kutoka kwa shamba la ukubwa wa ekari 25,000 wanalong’ang’ania umiliki wake na familia ya mwanasiasa marehemu Mark Too. Maskwota hao wanaodai mababu zao ndio waliotimuliwa kutoka kwa shamba hilo enzi za ukoloni, wanasema walipewa shamba hilo rasmi na aliyekuwa Rais hayati Daniel arap Moi, kisha Kamishna wa Ardhi M Okundu akaratibisha uamuzi huo mwaka 2007. Katika ombi lililowasilishwa na wakili William Arusei chini ya sheria za dharura, kikundi cha maskwota hao–Sirikiwa Squatters Group–kimeomba mahakama ibatilishe uamuzi huo kwa vile ilitegemea ushahidi ambao haukuwa umewasilishwa katika kesi waliyoshtaki katika Mahakama ya kuamua kesi za mashamba (ELC), Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu. Pia wameeleza bayana Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaack Lenaola, na William Ouko walitegemea ushahidi wa Afisa wa Ugavi wa Mashamba R J Simiyu kutoa uamuzi wang’atuke shambani. Maskwota hao wamesema ushahidi wa Bw Simiyu uliowasilishwa mbele majaji hao saba kwa njia ya afidaviti ni mpya na kamwe “haukuwasilishwa mbele ya Jaji Antony Ombwayo aliposikiliza na kuamua kesi hiyo 2017.” Pia wanasema ushahidi huo haukuwasilishwa Mahakama ya Rufaa iliyosikiliza rufaa iliyowasilishwa na kampuni ya Fanikiwa, familia ya marehemu Mark Too, kampuni ya Lonrho Agribusiness (EA) Ltd, na Bw David K Korir. Hivyo basi, maskwota hao wanaeleza mahakama hii ya upeo kwamba ni kinyume cha sheria kutegemea ushahidi mpya kutoa uamuzi wa kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma. “Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu wa Desemba 15, 2023, hauna mashiko kisheria na kamwe hauna nguvu kisheria kuwatimua maskwota hawa kutoka kwa shamba lao,” asema Bw Arusei. Pia maskwota hawa wanadai kwamba badala ya Mahakama ya Juu kujadili masuala ya kikatiba jinsi ilivyo jukumu lake, majaji hao walianza kufafanua na kutafsiri ushahidi wa watu binafsi na kuelezea maana ya ‘skwota’. Mahakama hii imeombwa ikague upya uamuzi iliyotoa kwa vile ilidanganywa na walalamishi na pia kutendewa ujanja. Akinukuu maamuzi ya majaji wastahiki kama vile Lord Dening, Bw Arusei amesema, mahakama ikigundua ilipotoshwa au kudanganywa na upande mmoja, iko na mamlaka na uwezo wa kufutilia mbali uamuzi iliyotoa na kuandika mwingine. Maskwota hao wanaomba Mahakama ya Juu iwarudishe shambani kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Ombwayo na Mahakama ya Rufaa. Vile vile mahakama hiyo imekosolewa kwa kumshambulia hayati Moi katika uamuzi huo pasi kutoa agizo wasimamizi wa mali yake wafike mbele yao kutoa mwanga kuhusu suala la umiliki wa shamba hili lililorudishwa kwa serikali na kampuni iliyokuwa inakuza miti inayotumika katika viwanda vya ngozi. Naibu msajili wa Mahakama ya Juu Nelly Kariuki aliwaamuru maskwota hao wawakabidhi nakala za kesi hii yao mpya wahusika wote kabla ya Januari 31, 2024, kesi itakapotajwa tena kwa maagizo zaidi. Jaji aliyesikiliza kesi hii mpya hakuiratibisha kuwa ya dharura ila aliamuru pande zote ziwasilishe ushahidi katika muda wa siku 14 kuanzia Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti,  baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA KASSIM ADINASI KIONGOZI wa Wachache katika Bunge la Kitaifa, Bw Opiyo Wandayi amedai ubora wa matokeo ya Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE) utakuwa wa kutiliwa shaka sawa na KCPE ya mwaka huu, 2023. Bw Wandayi Jumamosi, Desemba 9, 2023 aliwasuta Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu na mwenzake wa ICT Eliud Owalo kwa kufeli kupambana na magenge ya wahalifu waliovuruga matokeo ya KCPE. “Ninahofia kuwa matokeo ya KCSE pia yatavurugwa sawa na yale ya KCPE. Machogu na maafisa wake walikosa kujibu maswali mengi na hii inaharibu elimu nchini,” mbunge huyo wa Ugunja akaeleza. “Tunafahamu kwamba wizara za ICT na Elimu zinaendeshwa na watu ambao maadili yao ni ya kutiliwa shaka. Bw Machogu na Owalo hawana mamlaka yoyote kwani wizara zao zinaendeshwa na watu wengine,” Bw Wandayi akaongeza, bila kutoa ushahidi wowote. Mbunge huyo wa upinzani alisema hayo kwenye kikao na wanahabari nyumbani kwake katika kijiji cha Madeya, eneobunge. Lakini Waziri Owalo alikataa kushiriki mjadala huo kuhusu matokeo ya mitihani ya kitaifa ambayo yamevutia hisia kutoka kwa wadau mbalimbali. “Siwezi kuzungumzia madai hayo wakati huu,” akasema. Bw Wandayi alisema majibu ambayo Waziri Machofu alitoa kwa Kamati ya Bunge kuhusu Elimu kuhusiana na dosari zilizoibuka kwenye matokeo ya KCPE hayakuridhisha. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA KEVIN MUTAI HUENDA shughuli za usafiri na uchukuzi katika Kaunti ya Lamu zikatatizika baada ya mafuriko yanayoshuhudiwa kuchangia uhaba wa mafuta. Boti ambayo ndiyo mojawapo ya njia kuu za usafiri, imetatizika kutokana na mvua ya El Nino inayoendelea. Hali hiyo imechangiwa na maji ya mafuriko ambayo yameharibu sehemu mbili za barabara kutoka Mokowe kuelekea Minjila, ikiathiri uchukuzi ndani na nje ya kaunti ya Lamu. Mto Tana kuvunja kingo zake, kumewalazimisha wakazi kutegemea maboti kusafiri kutoka sehemu zilizoathirika huku ikiwagharimu angalau Sh500. Hali hiyo imezidi kuwa mbaya zaidi, shirika la Msalaba Mwekundu, likieleza kuwa kambi nne za kuwasitiri waliopoteza makazi yao zilikuwa zimefurika na kusababisha watu kuhama. Afisa wa walinzi wa fukwe na uokoaji Bi Susan Mtakai, anaeleza wasiwasi wa akina mama kujifungua kabla ya muda na ukosefu wa huduma za ujawazito ni suala kuu. “Tunawaokoa watu ila akina mama na watoto ndio wameathirika sana. Tumekuwa na visa vya akina mama kujifungua katika maeneo yaliyofurika na ni jambo la kutia wasiwasi. Tunaomba msaada kutoka kwa wasamaria wema,” akasema Bi Mtakai. Haya yanajiri, mshirikishi wa ukanda wa Pwani Bi Rhoda Onyancha akihoji kuwa serikali ilikuwa ikiwahamisha watu kutoka eneo hilo kwa ushirikiano na maafisa wa ulinzi na kaunti ya Lamu. “Serikali imekuwa ikisambaza chakula na bidhaa nyingine muhimu kwa kutumia ndege. Vijiji vya Ozi na Kipini vimezingirwa na maji na haviwezi kufikiwa kwa njia ya barabara au kwa boti,” akasema Bi Onyancha. Kulingana naye, “Viwango vya mafuta vimeenda chini katika kaunti ya Lamu na tunawazia kutumia meli za kijeshi, kusafirisha bidhaa adimu hadi kule ila tunatathmini hali.” Kulingana na mshirikishi wa shirika la Msalaba Mwekundu ukanda wa Pwani, Bw Hassan Musa, watu 2,119 wameathirika kaunti ya Lamu, 500 kati yao wakipoteza makazi yao. “Tumejenga kambi za kuwahifadhi na kuwapa chakula na bidhaa nyinginezo kama vile blanketi na neti za kuzuia mbu. Tumegundua kuna watoto wengi na akina mama wanaonyonyesha ambao wamekwama na wanahitaji msaada,” akasema Bw Musa. Familia zilizoathirika zimeitaka serikali kuingilia kati na kuwasaidia kuhamia sehemu salama na kujenga makazi ya muda. Aidha, ripoti zimeeleza kuwa wanaougua magonjwa mbalimbali hawawezi kufikia hospitali za daraja ya tano, na kulazimika kupata matibabu kwa hospitali zilizopo Lamu. “Kuna wale ambao hawawezi kumudu gharama ya kusafiri kwa ndege kupata matibabu zaidi. Serikali itabidi iangalie hali hiyo na kuwasaidia wagonjwa wanaohitaji huduma za rufaa,” akasema Bw Musa. Huduma za uchukuzi wa umma nazo zimekuwa kizungumkuti, kusafiri ikigharimu zaidi ya Sh 2, 000 ikilinganishwa na Sh1, 500 ya kawaida. Katika kaunti jirani ya Tana River, kambi 88 zimejengwa ili kuwashughulikia watu 11,167 ambao wamepoteza makazi yao kwa mafuriko hayo. Kufikia sasa, shughuli za kuokoa walio katika vijiji vilivyozingirwa na maji zinaendelea.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA LAWRENCE ONGARO MAHAFALI wapatao 5, 700 wa chuo Kikuu cha Mount Kenya waliofuzu mwaka huu, 2023 wamehimizwa kutilia maanani ujuzi waliopokea ili kujiajiri badala ya kutegemea nafasi finyu za kazi za serikali ambazo hazipatikani. Naibu Chansela Prof Deogratius Jaganyi, alisema licha ya masomo, wamepata ujuzi wa kuwa viongozi na kuonesha talanta zao katika uimbaji na masuala ya kitamaduni. “Nyinyi kwa wakati huu mumeanza safari ya kupambana na hali ya ulimwengu na hivyo hakuna sababu ya kulalamika,” aliwashauri mahafali hao. Hafla hiyo ya Ijumaa, Desemba 8, 2023 ilikuwa makala ya 24 kwa mahafali kufuzu katika chuo hicho. Kauli mbiu ya hafla hiyo ilikuwa “The Role of higher Education in Driving small scale Industry for socio- Economic Equity through Linkage”. Jaganyi alisema chuo hicho kimeweza kuwapa nafasi wanafunzi wanaosoma  masuala ya kiafya, kusafiri nchi za nje kama vile Uhispanoa, Ufaransa, na Italia ili kujionea mageni. Alisema cha muhimu zaidi wakati huu ni chuo hicho kuangazia masuala ya utafiti na ubunifu, kwa sababu yanaambatana na jinsi mambo yanavyobadilika maishani. Mgeni wa heshima katika hafla hiyo alikuwa Katibu wa masuala ya viwanda, biashara na uwekezaji, Dkt Juma Mukhwana aliyesifia sekta ya biashara katika kubuni kiwango kikubwa chaajira nchini. Aidha, sekta ya biashara ndogo ndogo na zile za kadri (MSMEs), inakadiriwa kuajiri watu wapatao 14.1 milioni ambao wanawakilisha asilimia 93. Alisema serikali itaendelea kuwapa motisha vijana ili waendelee kujihusisha na biashara ndogo ndogo kwa minajili ya manufaa yao kimaisha. Wakati wa hafla hiyo wanafunzi kutoka nchi 40 walijumuika na wa hapa nchini kufuzu kupokea shahada mbalimbali za kozi. Pro-Chansela wa Mount Kenya, Dkt Vincent Gaitho, alisema chuo hicho kinawapa wanfunzi wake ujuzi wa kujitegemea kupitia taaluma zinazohamasisha ubunifu. “Iwapo umepata maarifa masomoni, jukumu lako sasa ni kuanza kazi mradi tu upate fedha za kujikwamua,” alishauri Dkt Gaitho. Alisema tayari Mount Kenya imezindua mfumo wa masomo ya mbali kwa njia ya kielektroniki, ndio Open Distance Eletronic Learning (ODEL) ili wanafunzi wenye kiu cha masomo wapate fursa kusoma.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA COLLINS OMULO SHINIKIZO za kuwataka maspika wa Bunge la Kitaifa na mabunge ya Kaunti kuwa wamefuzu kwa shahada ya digrii zimeshika kasi, huku waundasheria wakijadili mswada uliowasilishwa kwa Seneti. Mlalamishi, Simon Lenguiya, amehoji kuwa hali ya kukosa maarifa ya kielimu na kitaaluma yanayohitajika ili mtu ateuliwe kama spika wa asasi tatu za uundaji sheria, ina athari ya moja kwa moja kwa ajenda ya sheria. Amelisihi Bunge kurekebisha sheria ili zijumuishe masharti ya kuwa na shahada ya digrii ili mtu achaguliwe kama Spika wa bunge la kaunti, Seneti au Bunge la Kitaifa. Kamati ya Seneti kuhusu Haki na Sheria sasa imeunga mkono mapendekezo hayo ya kuitisha shahada. Katika ripoti iliyowasilishwa Seneti, Kamati hiyo inayoongozwa na Seneta wa Bomet, Bw Hillary Sigei, ilipendekeza sheria hizo zirekebishwe ili kuwashurutisha maspika kuwa na digrii. Endapo mabunge yote yatakubaliana na kamati, wanaoshikilia nyadhifa hizo, watashurutishwa kuwa na digrii. Kamati hiyo imependekeza kuwa Bunge lirekebishe Kifungu 106 (1) (a) cha Katiba kuhusu spika na manaibu wa spika ili kutenganisha masharti yanayohitajika ili mtu ateuliwe kama Spika wa Bunge na yanayohitajika kwa wabunge. Kulingana na Katiba, matakwa yanayohitajika ili mtu achaguliwe kama Spika wa Bunge lolote lile, yanaambatana na masharti ambayo ni sharti yatimizwe ili mtu achaguliwe kama Mbunge. Sheria inasema: “Kutakuwa na Spika kwa kila Bunge, atakayechaguliwa na Bunge hilo kuambatana na Kanuni za Bunge kutoka miongoni mwa watu waliofuzu kuchaguliwa kama wabunge lakini wasio wabunge.” Kuhusiana na Manaibu wa maspika, sheria inasema kuwa mgombea kutoka kila Bunge atachaguliwa na Bunge husika kuambatana na kanuni, kutoka miongoni mwa wanachama wa Bunge hilo. Hata hivyo, sheria imekimya kuhusu suala la kufuzu kielimu au kitaaluma. Isitoshe, Kamati inataka Bunge kurekebisha Kipengee 21(1) cha Sheria ya Uchaguzi (Nambari. 24 ya 2011), ili kutenganisha matakwa yanayohitajika ili mtu awe Spika wa Bunge la Kaunti na yanayohitajika kwa madiwani. Sheria inasema: “Spika wa Bunge la Kaunti atachaguliwa na kila bunge la kaunti kuambatana na Kanuni za Bunge la Kaunti kutoka miongoni mwa watu waliofuzu kuchaguliwa kama madiwani lakini si madiwani.” Ili kusuluhisha udhaifu huo kwenye sheria, ripoti hiyo imeirai Bunge kuunda sheria kuhusu masharti yanayohitajika ili mtu awe Spika wa bunge la kaunti, Seneti au Bunge la Kitaifa. Kwa sasa, Katiba na Sheria kuhusu uchaguzi haisemi chochote kuhusu masharti ya kielimu yanayohitajika kwa anayeshikilia afisi ya spika wa Bunge la Kaunti, Seneti au Bunge la Kitaifa. “Wadhifa wa Spika wa Bunge la Kaunti, Seneti au Bunge la Kitaifa ni wajibu muhimu katika mfumo wa kidemokrasia ya nchi ambao ni sharti uzingatiwe kwa makini unavyotekelezwa, ikiwemo masharti yanayohitajika ili mtu afuzu kutwikwa wadhifa huo,” ilisema ripoti.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA FARHIYA HUSSEIN UCHUNGUZI wa Idara ya Upelelezi (DCI) umebaini kuwa baadhi ya magari ya kifahari yanatumika kusafirisha dawa za kulevya. Katika tukio la hivi punde gari aina ya Toyota Harrier, lilinaswa wakati wa oparesheni ya kusaka dawa za kulevya mnamo Jumatano, ambapo watu wawili walinaswa wakiwa na kilo 477 za bangi, yenye thamani ya takriban Sh14 milioni, kwenye barabara kuu ya Mombasa-Malindi. Wawili hao, Mabw George Nitti, 37 na Raphael Mbithi, 37, walikamatwa katika eneo la Swallows, Kilifi Kusini kufuatia oparesheni iliyotekelezwa na maafisa wa polisi wanaohudumu chini ya DCI. Oparesheni hiyo ilisababisha kutwaliwa kwa gari aina ya Toyota Harrier, lililosajiliwa nambari KDK 020B, lililokuwa likitumika kusafirisha dawa hizo haramu. Kulingana na ripoti ya polisi iliyowasilishwa katika Kituo cha Polisi cha Ndonya, eneobunge la Kilifi Kusini, dereva aligoma kusimamisha, na kuwalazimu maafisa kufyatua risasi kwenye tairi la kulia. Dawa zilizonaswa na ambazo zilichunguzwa na mwanakemia wa serikali Mombasa, zilifikia kilo 477 zikikisiwa kuwa na thamani Sh14 milioni. Hii sio mara ya kwanza kwa magari ya kifahari kuonekana yakitumika kusafirisha dawa za kulevya. Septemba 4, 2023, oparesheni nyingine ya DCI ilinasa gari jeusi aina ya Prado TX lililokuwa likitumiwa kusafirisha dawa za kulevya. Katika tukio hilo, kilo 316 za bangi zilizokadiriwa kuwa na thamani ya Sh9 milioni, zilipatikana baada ya gari hilo kupata ajali na kutua kwenye mtaro. Wakati wa uchunguzi, wapelelezi walipata nambari nyingi za usajili, zinazofanana na zile zinazoonekana kwenye magari ya umma, jambo ambalo lilizua shaka zaidi. Huku barabara kuu ya Mombasa-Malindi ikionekana kuwa sugu katika usafirishaji wa dawa hizo haramu, mamlaka imeweka wazi msimamo wao kuhusu vita dhidi ya utumizi wa dawa za kulevya katika eneo la Pwani na nchini kwa jumla. Mwaka jana, 2022, Rais William Ruto, alitangaza vita dhidi ya walanguzi wa dawa za kulevya na wauzaji mihadarati, akihakikishia umma kwamba utawala wake utakabiliana na tatizo la dawa za kulevya katika eneo la Pwani. Aliwaonya wafanyabiashara wa dawa za kulevya kuondoka nchini Kenya kabla ya sheria kuwafikia. “Nimetoa agizo kwamba wote wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya waondoke humu nchini. Wanafaa kwenda kutafuta mahali pengine pa kufanya hivyo,” Rais Ruto alionya. Rais pia alitoa wito wa kufungwa kwa mianya na njia zote zinazoshukiwa kutumiwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

Na CECIL ODONGO   KIONGOZI wa upinzani Raila Odinga ameonya kuwa Kenya inaelekea pabaya na hana haina mengi ya kusherehekea tangu ijinyakulie uhuru mnamo 1963. Bw Odinga alisema ni masikitiko kwamba baada ya  miaka 60 tangu nchi ijinyakulie uhuru, bado Kenya haijafanikiwa kupambana na umaskini, ujinga na magonjwa. Masuala hayo matatu ndiyo yalikuwa malengo makuu ya Kenya kutokomeza ilipojinyakulia uhuru. Bw Odinga pia alishutumu serikali ya Rais William Ruto kutokana na kile alichosema ni kuanzisha sera hasi ambayo imewafanya Wakenya walimbikizwe mzigo mkubwa wa ushuru na kupandisha deni la taifa. Kwa mujibu wa Bw Odinga, Wakenya wamepitia uchungu wa mkoloni, udikteta wa chama kimoja na kuporomoka kwa uchumi wa miaka ya 80 na 90. Rais William Ruto anatarajiwa kuongoza maadhimisho ya miaka 60 tangu Kenya ijiondoe kwenye utawala dhalimu wa Uingereza,  mnamo Jumanne Desemba 12, 2023. “Katika vipindi hivi, Wakenya wamepitia mengi. Familia zimesambaratishwa kupitia dhuluma na watu kuzuiliwa. Mahangaiko yamekuwa mengi ila Wakenya hawakukata tamaa,” akasema Bw Odinga. Waziri huyo mkuu wa zamani ambaye amekuwa kwenye siasa za upinzani kwa miaka mingi aliwataka waendelee kusimama kidete na kupinga udikteta. “Maadhimisho haya ya miaka 60 ni wakati mzuri wa kutafakari mahali ambapo tumetoka na pia tunakoelekea. Nchi hii itakuwa wapi tukiadhimisha miaka 120 ya uhuru mnamo 2083? Haya ni kati ya masuala ambayo tunastahili kufikiria,” akasema Bw Odinga. Alikuwa akizungumza katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki Afrika Mashariki ambapo alizungumzia demokrasia na safari ya Kenya tangu ijinyakulie uhuru. Aliandamana na mbunge wa Westlands Tim Wanyonyi, Naibu Kiranja wa Wachache Mark Mwenje, Mbunge Mteule Irene Mayaka  na aliyekuwa Kiongozi wa Mungiki Maina Njenga pamoja na mbunge wa zamani wa Narok Kaskazini Moitalel Ole Kenta. Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa ODM, Kenya inaweza kuinuka tena iwapo wananchi watamakinikia ndoto za wale waliopigania uhuru wa nchi. “Tutakuwa na nchi ambayo viongozi watakuwa wakiwekeza nguvu zao katika kufadhili elimu na kujenga shule, kupambana na ufisadi, kubuni nafasi za ajira  na kwa ujumla kuwapunguzia Wakenya mzigo mzito wa kutimiza masuala ya kimsingi,” akasema. Ingawa hivyo, alikiri kuwa Wakenya wamekosa imani na kila tawala baada ya uhuru na kwa sasa wamelimbikiziwa mzigo zaidi wa ushuru, ufisadi na uongozi usiojali maslahi yao. Aliwataka wanasiasa chipukizi wasimame imara na kukataa udikteta pamoja na kusema hadharani iwapo taifa linaelekea pabaya. Pia Bw Odingaa alishutumu serikali ya Kenya Kwanza akisema imejikita katika ukabila na unaendeleza ufisadi  huku wananchi wakiumia kutokana na gharama ya juu ya maisha. “Leo watu wetu wanaendea kazi nje ya nchi kama Israeli na Saudi Arabia na Rais wetu anasema kuwa anasaka wakazi wa Wakenya nje ya nchi badala ya kubuni nafasi hizo hapa nchini,” You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MASHIRIKA KAMPALA, UGANDA MWANASIASA wa Uganda Robert Kyagulanyi almaarufu Bobi Wine, amekosolewa vikali kwa kudai kwamba Rais Museveni alipitisha sheria tata kuhusu ushoga ili kumlenga yeye. Mwanasiasa huyo akiwa Uingereza, alisema wabunge wa chama chake cha National Unity Platform (NUP) ambao waliunga mkono sheria hiyo, ‘wanashirikiana na Jenerali Museveni’. “Nataka kusema kwamba sheria hii, Jenerali Museveni hakuileta kwa maslahi ya watu wa Uganda. Lakini ililetwa kulenga Upinzani, ikiwa ni pamoja na mimi. Hii ni kwa sababu anataka kutumia sheria hiyo kukandamiza mtu yeyote ambaye anaonekana kuwa rafiki kwa jamii hiyo (mashoga),” Bobi Wine alisema katika mahojiano. Alijibu hayo baada ya kuulizwa kwa nini chama chake kilipiga kura kuunga mkono mswada wa kuharamisha ushoga Uganda.“Hakika! Katika chama changu nina wabunge wanaofanya kazi na Jenerali Museveni”. Hata hivyo, Bobi Wine hakutoa ushahidi wowote kuthibitisha madai yake na hakutaja hata mmoja wa wabunge hao. Bobi Wine alitoa maoni hayo kwa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) mnamo Novemba 29 wakati wa ziara yake ya kwanza London, miaka kumi baada ya serikali ya Uingereza kumzuia kwa maoni yake kuhusu ushoga. Jijini Kampala, Chama cha Upinzani cha JEEMA kinachoongozwa na Asuman Basalirwa na ndicho kilichofadhili sheria ya kupinga ushoga, kilimkashifu Bobi Wine kwa matamshi hayo. “Unafahamu sheria ya kupinga ushoga ililetwa na Asuman Basalirwa, kiongozi wa JEEMA na iliendana na kile tunachokiamini kama JEEMA. Sheria hii iliungwa mkono kwa kiasi kikubwa na Bunge zima, (ikiwa ni pamoja na)wabunge wa NUP ambao walihatarisha maisha yao ili kulinda maadili yetu ya kitamaduni na kidini,” Katibu Mkuu wa JEEMA Mohamed Kateregga alibainisha katika barua iliyoelekezwa kwa Bobi Wine.
Tags
You can share this post!
Previous article
MAWAIDHA YA KIISLAMU: Maadili yako wapi, tunafunza nini...
Next article
Wasiwasi waibuka Embu watu 15 wakijitoa uhai ndani ya miezi...

Na DAVID MWERE WAKENYA ambao ni wafanyabiashara au wamejiajiri sasa wamefikiwa baada ya mswada kuwasilishwa katika Bunge la Kitaifa ili nao pia walipe ada ya nyumba za gharama nafuu. Wafanyakazi ambao wana ajira rasmi ndio wamekuwa wakikatwa ada hiyo tangu iasisiwe na utawala wa Rais William Ruto. Mswada wa Nyumba 2023 umewasilishwa bungeni baada ya Mahakama Kuu kusema kwamba ule uliokuwa ukitekelezwa, ulikuwa kinyume cha sheria na haukuwa ukizingatia msingi wa haki. Ada hiyo ilianza kutekelezwa baada ya Sheria ya Fedha kukumbatiwa huku wafanyakazi ambao wana ajira wakiwajibikia makato yake kila mwezi. Mswada wa sasa ambao unadhaminiwa na Kiongozi wa Wengi Kimani Ichung’wah pia unalenga kuoana na uamuzi wa Mahakama ya Juu ambao uliharamisha ada ya nyumba. Aidha mswada huo unapendekeza kubuniwa kwa Hazina ya Nyumba za Gharama nafuu ambapo ada za kila mwezi zitakuwa zikielekezwa na kusimamiwa na bodi maalum. “Ada ya nyumba itakuwa asilimia 1.5 ya mshahara wa mtu ambaye ameajiriwa au mapato ambayo mtu amepokea,” ikasema mswada huo ambao ulisomwa kwa mara ya kwanza bungeni. Rais William Ruto analenga kujenga nyumba 200,000 za bei nafuu kila mwaka na ameahidi kuwa shughuli hiyo itakuwa ikibuni kati ya nafasi za ajira 600,000 na milioni moja kila mwaka. Katika bajeti ya mwaka huu, Bunge iliamrisha Sh73 bilioni zielekezwe kwenye mradi huo ambao unalenga kuhakikisha Wakenya wote wana makao yanayostahiki na wanamiliki nyumba zao. Kwa kulenga mapato ya wale ambao hawana ajira rasmi au si watumishi umma, serikali inalenga kuwiana na uamuzi wa Mahakama Kuu ambao ulisema kuwa ilikuwa ubaguzi kuwataka walioajiriwa pekee wachangie ada ya nyumba. Wale ambao wamejiajiri au wana njia zao za kupata mapato watahitajika kulipa pesa zao kufikia tarahe tisa ya kila mwezi. Mahakama pia ilisema mswada wa awali kabla uwe sheria haukuwa unazingatia katiba kutokana na umma kukosa kushirikishwa wakati wa utoaji maoni. Mswada ambao upo bungeni kwa sasa kupitia mchakato unaohitajika kisheria utashirikisha Wakenya kualikwa watoe maoni yao. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

STEVE OTIENO NA CHARLES WASONGA MAKALA ya tano ya Kongamano la Kuzuzuana Mawazo la KUSI Ideas Festival limeanza huku viongozi wa Afrika wakitakiwa kuwa wabunifu, wenye bidii na kujitolea kusukuma ajenda ya maendeleo ya bara hili kufikia 2063. Mkutano huo unaendelea jijini Gaborone nchini Bostwana na umewaleta pamoja wajumbe kutoka nchi kadha za Afrika, wakiwemo marais, wakuu wa sekta mbalimbali, watungaji sera, wajasiriamali, wadau katika majukwaa ya kidijitali na wanafunzi katika vyuo vya elimu ya juu. Wajumbe wanaohudhuria kongamano hilo kimtandao na kibinafsi wanatarajiwa kuibua mawazo yanayotarajiwa kutoa suluhu kwa changamoto zinazokumba bara Afrika. Akitoa hotuba yake ya ufunguzi, Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi alilinganisha kongamano hilo na soko la hisa ambapo watu wanakutana kubadilishana mawazo yanayoweza kuleta manufaa. Aidha, alilitaja kama jukwaa la kutoa sera ambazo zinaweza kuzalisha mapato kwa manufaa ya nchi za Afrika. Mkutano huo, Rais Masisi alisema, ilipatia wadau muhimu nafasi ya kukadiria kiwango cha kujitolea kwao kutekeleza mpango wa kimaendeleo kwa Afrika na hivyo kuimarisha uwezo wa mataifa ya bara hili kufikia malengo ya Ajenda ya Maendeleo ya 2063. “Tumeshawishika kikamilifu kwamba mkutano huu unatoa nafasi kwa viongozi kutoka bara Afrika kuchanganua masuala mbalimbali na kuweka juhudi zetu za pamoja,” akasema. Rais Masisi aliongeza kuwa mada zitakazojadiliwa na wakuu wa serikali, sekta za kibinafsi, mashirika ya kijamii, wawekezaji na asasi mbalimbaili zitachangia maono ya pamoja ya kimaendeleo ya Afrika. Muhimu katika ufikiaji wa malengo hitajika itakuwa ni Afrika iliyoungana na inayoenda mbele kwa lengo moja huku ikiimarisha juhudi zake za kuendeleza ushirikiano wa kibiashara. “Ni nafasi yetu ya kutafakari kuhusu mianya ya ufanisi na changamoto kwa mipango ya maendeleo Afrika. Bila shaka sote tunachangamkia Mkataba wa Biashara Huru Kati ya Mataifa ya Afrika (ACFTA) ulioanza kutekelezwa 2021. Rais huyo wa Bostwana alionya wajumbe dhidi ya kudhani kuwa mwaka wa 2063 ni mbali akisema zimesalia miaka 40 kuufikia. “Watu wengi hapa ni wenye umri mdogo na wanashikilia nyadhifa za uongozi. Hii ndio maana mkutano huu unatoa jukwaa kwa watu kama hao kuratibu mustakabali wanaoutaka,” Bw Masisi akasema. Miongoni mwa masuala muhimu yanayojadiliwa katika kongamano la mwaka huu ni pamoja na kuligeuza bara la Afrika kuwa lenye ufanisi, linaloongozwa na mkataba wa kibiashara unaofanyakazi, uzingativu wa sheria na haki za kibinadamu na kuendelezwa kwa utawala bora na demokrasia. Aidha, kongamano hilo linajadili umuhimu wa kuwepo kwa amani Afrika na kuungwa mkono mwa juhudi za Umoja wa Afrika (AU) kurejesha amani katika nchi zinazokumbwa na vita. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirika la Habari la Nation (NMG) Dkt Wilfred Kiboro aliwataka Waafrika kujipa moyo kwamba wanao uwezo wa kuleta ufanisi katika bara hili. Alishangaa ni vipi watu wengi Ulaya, sehemu za bara Asia na Amerika wangali wanadhani Afrika ni nchi moja ilhali ina mataifa mengi. “Hii ina maana kuwa Afrika haijajinadi ipasavyo ulimwenguni,” akasema. Dkt Kiboro pia alisema Afrika inapasa kuwajibikia maendeleo yake na ikome kutizama enzi za ukoloni ambapo Waafrika walitendewa aina mbalimbali za unyama na watawala wa kigeni. “Naamini kuwa hatupasi kuendelea kulaumu nchini zilizotutawala kwa madhila yanayokumba Afrika. Nashawishika kuwa tuko na uwezo wa kukabiliana na changamoto zote zinazotukumba na kupata masuluhisho ya kutufaa. Mojawapo ya suala kuu ambalo ningetaka tujadili katika kongamano hili ni jinsi ya kuondoa fikra za kikoloni mawazoni mwetu ni tujiamini kama Waafrika wenye suluhu kwa changamoto zinazotukumba,” akasema. Shirika la NMG ni mwandalizi mwenza wa kongamano hilo. Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa aliwahimiza viongozi wa Afrika kuungana kwa lengo la kuwahudumia raia wao na wakome kufurahisha viongozi wa nchi zilizoendelea. “Kama Afrika twapaswa kuzungumza kwa sauti moja. Sharti tutambuliwe kama viongozi wazuri kwa watu wetu na tukome kujipendekeza au kufurahisha vingozi wa nchi za Magharibi,” akasema. Wengine waliohutubu ni Waziri Mkuu wa Rwanda Edouard Ngirente na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

Na RICHARD MUNGUTI SERIKALI imepata pigo tena baada ya mahakama kuu kusitisha kesi ya ulaghai wa Sh29 milioni aliyoshtakiwa Msimamizi wa Bajeti Margaret Nyakang’o Jumanne jijini Mombasa. Akisitisha kusikizwa kwa kesi hiyo, Jaji Enock Chacha Mwita alisema kesi aliyowasilisha Bi Nyakang’o iko na mashiko kisheria. Jaji Mwita alisitisha kusikizwa kwa kesi hiyo hadi Mei 21 2024 na kumwamuru wakili Danstan Omari aliyewasilisha kesi hiyo akabidhi Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) nakala za kesi hiyo katika muda wa siku 14. Jaji huyo aliratibisha kesi hiyo kuwa ya dharura na kuamuru DPP ajibu malalamishi ya Bi Nyakang’o katika muda wa siku 14. “Baada ya kusikiza mawasilisho ya mlalamishi Bw Stephen Mogaka (Mbunge wa Mugirango Magharibi) na  wakili Bw Omari nimefikia uamuzi kwamba haki za Bi Nyakang’o zimekandamizwa,” Jaji Mwita alisema. Jaji huyo alisema kuna masuala nyeti ya sheria anayozua pamoja na kudai haki zake zimekandamizwa. Katika mawasilisho yake, Bw Omari alisema kukamatwa na kushtakiwa kwa Bi Nyakang’o kunamfedhehesha. Msimamizi huyo wa bajeti alikamatwa na kushtakiwa mbele ya hakimu mkuu wa Mombasa kwa ufisadi wa Sh29 milioni. Alikana mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh500,000. Alishtakiwa kwamba alimlaghai Bi Claudia Mueni Mutungi Sh29 milioni kwa kughushi sahihi yake akidai atanufaika katika uwekezaji kwenye chama cha ushirika cha FEP Sacco Advantage (Mavuno) kati ya Novemba 1 2019 na  Mei 2020. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MHARIRI
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini.
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na BENSON MATHEKA
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na MASHIRIKA
LONDON, Uingereza
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya... Na ELIZABETH MERAB
WANASAYANSI wanachunguza kuhusu mchipuko wa virusi vipya vya corona aina ya Delta, katika nchi za Amerika, Uingereza,... Na MAUREEN ONGALA
MASAIBU ambayo wagonjwa wa Covid-19 hupitia katika kaunti za Pwani, yameanikwa wazi baada ya kifo cha afisa mkuu wa... SIAGO CECE na ANTHONY KITIMO
UFISADI miongoni mwa baadhi ya maafisa wa serikali katika mpaka wa Kenya na Tanzania, umezidi kuwaweka... Na WAANDISHI WETU