text
stringlengths
3
16.2k
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MUNGUTI NAIROBI, KENYA RAIA wa Rwanda Desire Muhinyuza atasherehekea Mwaka Mpya 2024 akiwa na amani na utulivu moyoni, baada ya Serikali ya Kenya kuamuru arudishiwe Dola 2.6 milioni (sawa na Sh400 milioni) zilizokuwa zimetwaliwa na Polisi kufuatia mzozo wa umiliki wa kampuni ya biashara ya kimtandao kati yake na mfanyabiashara wa humu nchini Bw Kirimi Koome. Hatua hii ya serikali ni muhimu katika kuimarisha imani ya wawekezaji wanaotoroka nchini mara baada ya kulaghaiwa na baadhi ya Wakenya. Akiamuru Bw Muhinyuza akabidhiwe kitita hicho, hakimu mwandamizi katika mahakama ya Milimani, Nairobi Bi Dolphina Alego alisema Mahakama Kuu mnamo Desemba 27, 2023, ilimtambua mwekezaji huyo kuwa ndiye mwenye kampuni ya Stay Online Limited (SOL) aliyokuwa amenyang’anywa na Bw Koome kwa njia ya ujanja na ufisadi. Bi Alego alisema Jaji Alfred Mabeya, ambaye ni mkuu wa kitengo cha biashara katika Mahakama Kuu, alimtambua Bw Muhinyuza kuwa ndiye mmiliki wa SOL, aliyokuwa amelaghaiwa na Bw Koome mnamo Aprili 14, 2023. Jaji Mabeya alisema katika uamuzi huo wa kihistoria kwamba Bw Koome alitumia ukora na ulaghai kujisingizia na kujitambua kuwa mmiliki wa SOL ilhali alikuwa ameteuliwa na Bw Muhinyuza aiandikishe kwa niaba yake. “Bw Koome aliteuliwa na Bw Muhinyuza aandikishe SOL, Kenya kwa niaba yake, lakini akajisingizia kuwa yake na kupotosha idara ya usajili wa kampuni katika afisi ya Mwanasheria Mkuu,” Bi Alego alisema. Punde tu baada ya kuandikisha SOL, Kenya wafanyabiashara kutoka Canada, Estonia, Zambia, Tanzania, Uganda, na Kenya waliwekeza zaidi ya Dola 2.6 milioni (Sh400 milioni) katika biashara hiyo ya jukwa la mtandaoni. Kuona kwamba amepokonywa kampuni ya SOL, Bw Muhinyuza alilalamika kwa polisi kwamba ametapeliwa kampuni na pesa na Bw Koome ndipo, idara ya uchunguzi wa jinai (DCI) ikafika kortini na kupata agizo la kutwaa pesa hizo sizipotee. Na wakati huo huo Bw Muhinyuza akalalamikia idara ya usajili wa kampuni katika afisi ya mwanasheria mkuu kwamba Bw Koome alificha ukweli kuhusu umiliki wa SOL. Pia Bw Muhinyuza kupitia mawakili Danstan Omari, Shadrack Wambui, Sophie Nekesa, Ronald Momanyi na Aranga Omaiyo alimshtaki Bw Koome katika mahakama kuu akiomba ashurutishwe arudishe kampuni na pesa za wateja walioekeza katika SOL, Kenya. Baada ya kutathmini ushahidi uliowasilishwa na Bw Omari, Jaji Mabeya alifikia uamuzi kwamba SOL ni yake Bw Muhinyuza. Alisema mwekezaji huyo aliekeza USD ($)129,000 katika SOL na Bw Koome “hakutoa hata senti moja kufanikisha biashara na usajili wake.” Jaji huyo alimwagiza Bw Koome anayeshtakiwa mbele hakimu mkazi Bw Ben Mark Ekhubi kwa kula njama za kumlaghai Bw Muhinyuza kiasi cha Dola 2.6 milioni na wizi wa Dola 100,000 arudishe pesa hizo. Ijumaa ,viongozi wa mashtaka Bi Dorcus Rugut na James Gachoka walisema ijapokuwa Bw Koome anadai pesa hizo ni zake “hana mamlaka yoyote juu ya pesa hizo.” Bi Rugut alisema Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Renson Igonga ameamuru polisi wamrudishie Bw Muhinyuza kiasi hicho Dola 2.6 milioni. Bi Alego alisema serikali imeagiza pesa hizo zirudishwe kwa mwekezaji huyo aendelee na biashara na kubuni ajira kwa wakenya. Kabla ya polisi kuagizwa kurudisha pesa hizo Bw Koome alipinga ombi hilo akisema “apewe muda wa wiki mbili atafute wakili awasilishe ombi la kuzuia kutwaliwa kwa pesa hizo na Muhinyuza.” Bw Koome alisema : “nimewatimua kazini mawakili Cliff Ombeta, Jackson Omwanza na hivyo nahitaji muda wa kumtafuta wakili mwingine kwa vile sielewi ombi hili la DPP na madhara yake katika kesi hii inayonikabili.” Mahakama iliombwa na wakili Danstan Omari isitilie maanani ombi la Bw Koome kwa vile “pesa anazodai sio zake.” Bi Rugut alisema DPP hapingi pesa hizo zilizokuwa zimezuiliwa kama ushahidi katika kesi inayomkabili Bw Koome. Bi Rugut alisema Desemba 27, 2023, Bw Koome hajakata rufaa kupinga uamuzi wa kumng’oa katika kampuni ya SOL na agizo la kulipa fidia na kurudishia Muhinyuza Dola 100,000 alizomdanganya zilikuwa za kulipia kodi biashara ya SOL lakini “akazitia kibindoni.” Bi Alego alielezwa kesi inayomkabili Bw Koome ni kwamba alikula njama za kumlaghai Bw Muhinyuza kiasi Dola 2.6 milioni na wizi wa Dola 100,000. Mahakama ilikubalia ombi la DPP na kuagiza pesa hizo arudishiwe Muhinyuza. Sasa Bw Koome atapambana na hali yake na kesi ya ufisadi inayomkabili. Kesi inayomkabili Bw Koome itaanza kusikilizwa Februari 9, 2023. Alikana mashtaka manne ya ufisadi na wizi na yuko nje kwa dhamana ya pesa taslimu Sh500,000 You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MUNGUTI MASKWOTA wapatao 10,000 wamewasilisha upya kesi katika Mahakama ya Upeo wakiomba ibatilishe uamuzi kwamba wafukuzwe kutoka kwa shamba la ukubwa wa ekari 25,000 wanalong’ang’ania umiliki wake na familia ya mwanasiasa marehemu Mark Too. Maskwota hao wanaodai mababu zao ndio waliotimuliwa kutoka kwa shamba hilo enzi za ukoloni, wanasema walipewa shamba hilo rasmi na aliyekuwa Rais hayati Daniel arap Moi, kisha Kamishna wa Ardhi M Okundu akaratibisha uamuzi huo mwaka 2007. Katika ombi lililowasilishwa na wakili William Arusei chini ya sheria za dharura, kikundi cha maskwota hao–Sirikiwa Squatters Group–kimeomba mahakama ibatilishe uamuzi huo kwa vile ilitegemea ushahidi ambao haukuwa umewasilishwa katika kesi waliyoshtaki katika Mahakama ya kuamua kesi za mashamba (ELC), Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu. Pia wameeleza bayana Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaack Lenaola, na William Ouko walitegemea ushahidi wa Afisa wa Ugavi wa Mashamba R J Simiyu kutoa uamuzi wang’atuke shambani. Maskwota hao wamesema ushahidi wa Bw Simiyu uliowasilishwa mbele majaji hao saba kwa njia ya afidaviti ni mpya na kamwe “haukuwasilishwa mbele ya Jaji Antony Ombwayo aliposikiliza na kuamua kesi hiyo 2017.” Pia wanasema ushahidi huo haukuwasilishwa Mahakama ya Rufaa iliyosikiliza rufaa iliyowasilishwa na kampuni ya Fanikiwa, familia ya marehemu Mark Too, kampuni ya Lonrho Agribusiness (EA) Ltd, na Bw David K Korir. Hivyo basi, maskwota hao wanaeleza mahakama hii ya upeo kwamba ni kinyume cha sheria kutegemea ushahidi mpya kutoa uamuzi wa kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma. “Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu wa Desemba 15, 2023, hauna mashiko kisheria na kamwe hauna nguvu kisheria kuwatimua maskwota hawa kutoka kwa shamba lao,” asema Bw Arusei. Pia maskwota hawa wanadai kwamba badala ya Mahakama ya Juu kujadili masuala ya kikatiba jinsi ilivyo jukumu lake, majaji hao walianza kufafanua na kutafsiri ushahidi wa watu binafsi na kuelezea maana ya ‘skwota’. Mahakama hii imeombwa ikague upya uamuzi iliyotoa kwa vile ilidanganywa na walalamishi na pia kutendewa ujanja. Akinukuu maamuzi ya majaji wastahiki kama vile Lord Dening, Bw Arusei amesema, mahakama ikigundua ilipotoshwa au kudanganywa na upande mmoja, iko na mamlaka na uwezo wa kufutilia mbali uamuzi iliyotoa na kuandika mwingine. Maskwota hao wanaomba Mahakama ya Juu iwarudishe shambani kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Ombwayo na Mahakama ya Rufaa. Vile vile mahakama hiyo imekosolewa kwa kumshambulia hayati Moi katika uamuzi huo pasi kutoa agizo wasimamizi wa mali yake wafike mbele yao kutoa mwanga kuhusu suala la umiliki wa shamba hili lililorudishwa kwa serikali na kampuni iliyokuwa inakuza miti inayotumika katika viwanda vya ngozi. Naibu msajili wa Mahakama ya Juu Nelly Kariuki aliwaamuru maskwota hao wawakabidhi nakala za kesi hii yao mpya wahusika wote kabla ya Januari 31, 2024, kesi itakapotajwa tena kwa maagizo zaidi. Jaji aliyesikiliza kesi hii mpya hakuiratibisha kuwa ya dharura ila aliamuru pande zote ziwasilishe ushahidi katika muda wa siku 14 kuanzia Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
It looks like nothing was found at this location. Maybe try one of the links below or a search? Try looking in the monthly archives. 🙂 © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
It looks like nothing was found at this location. Maybe try one of the links below or a search? Try looking in the monthly archives. 🙂 © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na AFP na MARY WANGARI AFISI ya Rais Nigeria imefichua ujumbe uliotumwa kwa Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, na mjumbe maalum wa Rais Muhammadu Buhari, Bw Ahmed Rufai Abubakar, ambao umezingirwa na usiri. Ujumbe wa Rais ulionyesha kwamba, serikali ya Afrika Kusini ilikanusha dhana ya jumla kuwa mashambulizi ya hivi majuzi dhidi ya raia wa kigeni nchini humo, ni ya ubaguzi wa rangi huku duru kutoka THISDAY zikisema maafisa wake wakuu walitaja idadi ya vifo tangu Desemba 2017 kuwa 89. Abubakar, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Kitaifa ya Ujasusi (NIA), alitumwa Afrika Kusini wakati wa mashambulizi ya ubaguzi wa rangi yaliyotekelezwa na raia wa Afrika Kusini dhidi ya Waafrika wenzao, ikiwemo raia wa Nigeria. Mashambulizi hayo ambayo bado hayajakoma, yamefanya serikali ya Nigeria kuzidisha juhudi za kuwasafirisha raia wake wanaotaka kurejea nyumbani kutoka Afrika Kusini. Kufikia sasa, raia 640 wa Nigeria wamejisajilisha kurejea nchini kwao. Mipango ya usafirishaji inaendelea huku kukiwa na juhudi za kusuluhisha kwa njia ya amani tatizo hilo la kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili makuu Afrika. Kulingana na mamlaka ya Afrika Kusini, kuna makundi matatu ya raia wa Nigeria nchini Afrika Kusini. Kundi la kwanza ni wataalam wanaobobea katika nyanja za matibabu na elimu. La pili ni wafanyabiashara, ikiwemo wauza bidhaa halali. La tatu ni wanaohusika na mihadarati. “Hawa watu (walanguzi wa dawa za kulevya) ni wachache lakini wana sauti kubwa sana. Inasikitisha kuwa ndio wanaoonekana kama sura ya Nigeria nchini Afrika Kusini,” afisa mkuu mmoja alisema. Licha ya dhana ya jumla, duru za THISDAY zilisema Jumanne kuwa Ramaphosa na maafisa wakuu wa serikali yake walisisitiza kuwa mashambulizi hayo yaliyosambaa si ya ubaguzi wa rangi. Alifichua kuwa ingawa kati ya Desemba 2017 na Septemba 2019, raia 89 wa Nigeria waliuawa nchini humo, 39 miongoni mwao waliuawa na raia wenzao kutokana na migogoro inayohusu mihadarati. Hata hivyo, Afrika Kusini ilikiri kuwa vifo 19 vilitokana na ukatili wa polisi huku vingine vikitokana na sababu nyinginezo. Serikali ya Afrika Kusini pia ilisemekana kufichua kuwa kati ya raia 300,000 hadi 400,000 wa Nigeria wamo nchini Afrika Kusini. Kwa sasa, 10,860 miongoni mwao wamo gerezani wakihudumu vifungo mbalimbali lakini asilimia 60 ya wafungwa wamo gerezani kutokana na uhalifu unaohusu mihadarati. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MASHIRIKA KAMPALA, UGANDA SERIKALI imeidhinisha hoja ya kutaka kubuniwa kwa Baraza la Kitaifa la Kiswahili litakalotoa mwongozo kuhusu mchakato wa kufanya Kiswahili kuwa lugha rasmi nchini Uganda. Akihutubia wanahabari kuhusu uamuzi wa Baraza la Mawaziri katika Ikulu ya Rais mjini Entebbe, Msemaji wa Serikali Ofwono Opondo alisema, kubuniwa kwa baraza hilo kunaambatana na matakwa ya katiba. Alisema baraza hilo litahakikisha Kiswahili kinakuwa lugha rasmi ya pili nchini Uganda baada ya Kiingereza. “Katiba inahitaji kwamba tuwe na lugha mbili za kitaifa; Kiingereza na Kiswahili. Lakini hatujakuwa tukitumia Kiswahili. Baraza hilo litaajiri walimu watakaokuwa wakifundisha Kiswahili shuleni,” akasema. Alisema baraza hilo pia litasimamia kubuniwa kwa sera, mwongozo na kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili inafunzwa kwa ubora wa juu. Bw Opondo alisema baraza hilo pia litahakikisha kuwa Kiswahili kinatumika katika wizara na mashirika yote ya serikali na kutoa vifaa vinavyotakiwa kama vile vitabu na kamusi. Uganda imekuwa ikitumia Kiingereza kama lugha rasmi tangu nchi hiyo kupata uhuru wake mnamo 1962. Nchini Uganda, lugha ya Kiswahili ilianza kutumika katika Baraza la Kifalme la Buganda na Bunyoro, hata kabla ya ukoloni (1862). Kiswahili hutumika katika shughuli za biashara, dini na mila. Nchini Uganda Kiswahili hutumiwa zaidi na Polisi na Wanajeshi. Katika miaka ya 1980, raia wengi wa Uganda walikiona Kiswahili kama lugha ya wahalifu ikitumiwa na askari kuwadhulumu na kuwanyang’anya mali yao. Uganda ndiyo nchi ya hivi karibuni kuidhinisha Kiswahili kuwa lugha rasmi. Namibia, Rwanda na Afrika Kusini pia zimeidhinisha Kiswahili kufunzwa shuleni. Baraza la Mawaziri la Namibia liliidhinisha hoja ya kutaka Kiswahili kufunzwa shuleni Julai, mwaka huu. Serikali ya Namibia ilianza kujadili suala la kufundisha lugha ya Kiswahili baada ya kiongozi wa Tanzania John Magufuli kuzuru nchi hiyo Mei, mwaka huu. Wakati wa ziara yake, Rais Magufuli alitaka Namibia na Tanzania kudumisha ushirikiano ambao umekuwepo tangu 1991 kwa kufundisha Kiswahili. Magufuli alisisitiza kuwa kulikuwa na haja kwa mataifa hayo mawili kushirikiana katika sekta ya elimu. Kiswahili kitaanza kufunzwa katika shule nchini Afrika Kusini kuanzia mwaka 2020. Waziri wa elimu msingi, Angie Motshekga mnamo Septemba mwaka jana alisema kuwa, Kiswahili kitafunzwa kama lugha mbadala kwa wanafunzi nchini humo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

IBRAHIM ORUKO na NDUNGU GACHANE WABUNGE wa Chama cha Jubilee wanaoegemea mrengo wa Tangatanga, sasa wametishia kumwadhibu Inspekta Mkuu wa Polisi, Bw Hillary Mutyambai wakidai anatumia mamlaka yake kinyume cha kisheria. Wabunge hao wapatao 40 pia walirejelea wito wao kumtaka Katibu wa Wizara ya Usalama wa Nchi, Dkt Karanja Kibicho na Waziri wa Usalama wa Nchi, Dkt Fred Matiang’i wang’atuke mamlakani kwa madai kwamba wanawabagua kwa misingi ya kisiasa. Wakizungumza katika majengo ya bungejana, walidai Bw Mutyambai alishawishiwa na wakuu katika Afisi ya Rais kumhangaisha Mbunge wa Kiharu, Bw Ndindi Nyoro na hivyo basi wataanzisha mchakato wa kumwondoa mamlakani. Bw Nyoro alikamatwa na polisi usiku wa kuamkia jana baada ya kukwepa mtego wao tangu Jumapili alipodaiwa kuzua rabsha katika Kanisa Katoliki la Gitui, Kaunti ya Murang’a. Wakiongozwa na Mbunge wa Kikuyu, Bw Kimani Ichungwa na Seneta wa Kericho Aaron Cheruiyot, wabunge hao walidai Idara ya Polisi imegeuzwa kuwa chombo cha kukandamiza baadhi ya viongozi nchini. “Ukatili wa polisi na utumiaji wa idara hiyo kisiasa limekuwa jambo la kawaida tangu Bw Mutyambai alipochukua usukani kuwa Inspekta Mkuu. Tunakashifu mienendo hii kwa sababu ni kinyume cha matakwa ya kikatiba,” akadai Bw Cheruiyot. Kwa upande mwingine, Bw Ichungwa alitishia kwamba maafisa wa umma wanaoruhusu idara wanazosimamia zitumiwe kudhulumu wengine kisiasa, watachukuliwa hatua kibinafsi na wabunge kwani kile wanachofanya ni sawa na uharibifu wa mali za umma. “Tutafanya idara ya polisi iwe huru kutoka kwa afisi ya Rais ili kuzuia isitumiwe na watu kama Dkt Kibicho,” akasema. Lakini Bw Kibicho alipuuza madai ya wanasiasa hao akisema amekuwa akilaumiwa na viongozi kila wakijipata matatani na akawataka wasimuingize kwenye mizozo yao. “Watu wanapojikuta taabani, watatue shida zao bila kumhusisha Kibicho. Wananilaumu kwa sababu wanataka kugeuza suala la kihalifu liwe la kisiasa,” akasema. Huku hayo yakijiri, imefichuka wakuu serikalini waliamua kutoendeleza mashtaka dhidi ya Bw Nyoro baada ya kubaini kwamba hatua hiyo ingemzidishia umaarufu wa kisiasa. Usiku wa kuamkia jana, kulikuwa na maandamano Murang’a ambapo wafuasi wa mbunge huyo chipukizi waliziba barabara kwa kuwasha moto njiani, hali iliyolazimu polisi kuwatawanya kwa kutumia vitoa machozi. Duru zilisema suala hilo la kutaka kumkamata Bw Nyoro liliingizwa siasa tele na kama serikali ingeendeleza kesi dhidi yake, angezidi kugonga vichwa vya habari kila kukicha na kupata umaarufu mkubwa. “Tunaamini Mbunge huyo atashtakiwa baadaye, lakini kwa sasa kutokana na joto la kisiasa lililotokea, wakubwa wetu waliona ni busara kutumia mbinu nyingine kutatua suala hilo,” akasema afisa aliyeomba asitajwe jina kwani hana idhini kuzungumzia suala hilo kwa wanahabari. Viongozi wa Tangatanga vilevile, wamefufua wito wao wa kumtaka Rais Uhuru Kenyatta kuitisha mkutano wa wabunge wa chama hicho ili kumaliza mizozo na kuimarisha mazingira ya utawala. Wakiongozwa na mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro, Alice Wahome (Kandara) na Seneta wa Murang’a Irungu Kangata, viongozi hao walisema kukamatwa, kuhangaishwa na kutishwa kwa baadhi ya viongozi wa Mlima Kenya na polisi ni sehemu ya njama za kuvuruga Jubilee zinazoendelezwa na wanasiasa wenzao kupitia polisi. Bw Kangata alisema mashtaka ambayo polisi walitaka kumfungulia Bw Nyoro hayana msingi akidai hawakuwa na ushahidi wowote. Mbunge huyo aliachiliwa jana bila kushtakiwa. Seneta huyo alisema vinara wa chama cha Jubilee wanapaswa kukabiliana na masuala yanayozua mgawanyiko chamani akisema anataka chama hicho kuwa na amani na kuhakikisha Kenya inastawi. Bw Nyoro alimtaka Rais kuitisha mdahalo wa kuunganisha chama akilaumu kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga kwa kuvuruga chama tawala. Lakini mbunge wa Nyeri mjini Ngunjiri Wambugu alisema mzozo katika chama hicho hauwezi kutatuliwa na mkutano wa kundi la wabunge akisema ni tatizo la eneo la Mlima Kenya ambalo limesababishwa na Naibu Rais. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

CHARLES WASONGA na AFP RAIS wa Amerika Donald Trump amemfuta kazi mshauri wake kuhusu masuala ya Usalama wa Kitaifa John Bolton. Rais Trump kupitia akaunti yake ya Twitter alisema ni yeye alimshauri Bolton ajiuzulu. Alisema Bolton alizingatia ushauri wake na kujiuzulu mnamo Jumanne asubuhi. “Namshukuru John zaidi kwa huduma yake. Nitataja Mshauri wangu mpya wa Masuala ya Usalama wiki ijayo,” Trump akasema. Akaongeza: “Nilimweleza John Bolton kwamba huduma zake hazihitajiki tana katika Ikulu ya Whit House. Nilipiga vikali baadhi ya mawaidha yake, jinsi nilipopinga ushauri kutoka kwa wengine katika serikali yangu.” Lakini akijibu, Bolton alipinga kauli ya Trump akisema ni yeye aliyehiari kujiuzulu. “Niliamua kujiuzulu Jumatatu usiku na Rais Trump akasema: ‘Tuzungumzie suala hilo kesho (Jumanne),” Bolton akaandikia katika akaunti yake ya twitter. Hatua ya Trump kuamuru Bolton kujiuzulu inajiri huku mengi yakisemwa kuhusu msimamo wake kuhusu hatua ya Iran kutangaza kuwa ingeanza kuzalisha kawi ya nuklia. Bolton alikuwa ametuma ujumbe, kupitia twitter, alishutumu Iran katika kile alichotaja kuwa “rundo la uwongo” kuhusu suala la mzozo nchini Syria, suala ambalo Trump alitofautiana nalo. “Wakati huu ambapo zimesalia wiki mbili kabla ya kufanyika kwa Mkutano wa Mkuu wa Umoja wa Kimataifa (UNGA), fahamu kuwa Iran inafanya kila iwezalo kuhadaa,” Bolton akaandika “Huku tukikumbuka wiki hii mashambulio la kigaidi nchini Amerika mnamo Septemba 9, 2011, ni muhimu kukumbuka hatua ambayo tumepiga kukamilia na makundi ya kigaidi na pia kazi ambayo imesalia. Tunapinga serikali zinazofadhili ugaidi na mashauri,” Bolton akaongeza. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

Na LEONARD ONYANGO MGAWANYIKO ndani ya Chama cha Jubilee kuhusu ugombeaji wa ubunge Kibra ulizidi kudhihirika Jumanne wakati wakuu wa chama hicho walikosa kujitokeza kumkabidhi rasmi Bw McDonald Mariga vyeti vya uwaniaji, na kuchangia kufungiwa nje kwa mwaniaji huyo na Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC). Tofauti na vyama vingine vya kisiasa ambako wagombeaji walilakiwa na wakuu wa vyama baada ya kuteuliwa kuwania wadhifa huo, Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto, hawakuwepo katika makao makuu ya Jubilee Bw Mariga alipopewa vyeti. Badala yake, shughuli hiyo ilisimamiwa na Katibu Mkuu wa Jubilee, Bw Raphael Tuju akiandamana na wanasiasa wengine wa chama hicho hasa wa mrengo wa Tangatanga unaomuunga mkono Dkt Ruto. Tangu kuteuliwa kuwa mwaniaji wa Jubilee, Bw Mariga hajawahi kukutana na Rais Kenyatta ambaye ni kiongozi wa chama hicho. Duru zilisema, uamuzi wa kuwasilisha mwaniaji wa Jubilee katika uchaguzi mdogo wa Kibra ulifanywa na Dkt Ruto kwa lengo la kumpinga Bw Odinga. Ripoti zilisema Rais Kenyatta alikataa mwaliko wa naibu wake aliyemtaka aende kumkabidhi Bw Mariga cheti cha uteuzi katika makao makuu ya chama cha Jubilee. Viongozi wa Jubilee wanaoegemea mrengo wa Kieleweke unaopinga mienendo ya Tangatanga, wakiwemo Mbunge wa Cherangany Joshua Kutuny na Mbunge Maalumu Maina Kamanda wanadai kuna baadhi ya watu ndani ya Jubilee wanalenga kusambaratisha uhusiano mwema uliopo baina ya Rais Kenyatta na Bw Odinga kwa kusimamisha mwaniaji Kibra. “Naibu wa Rais anajua kwamba hatashinda kiti cha Kibra na lengo lake kuu ni kutaka kuzua uhasama kati ya Rais Kenyatta na Bw Odinga,” akasema Bw Kamanda. Wakati huo huo, Bw Tuju pia amethibitisha kuwa Rais Kenyatta hatashiriki katika kampeni za ubunge Kibra. Viongozi wa Vyama vya ODM, Ford-Kenya, na Amani National Congress ambavyo vina wagombeaji wanaomezea mate kiti hicho kilichoachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge, Ken Okoth, wamekuwa mstari wa mbele kutafutia umaarufu wagombeaji wao. Bw Odinga alimtangaza mbunge wa Suna Mashariki ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa ODM, kuwa kinara wa kampeni za Bw Okoth katika uchaguzi mdogo wa Kibra. Bw Odinga alifanya kikao cha faragha na wawaniaji wote waliopoteza katika uchaguzi wa kura za mchujo uliofanyika Jumamosi iliyopita ili kuwapatanisha baada ya malalamishi kuibuka miongoni mwa baadhi yao awali. Baada ya kikao hicho, wawaniaji hao walitangaza kumuunga mkono Bw Bernard Otieno Okoth, almaarufu Imran, aliyeibuka mshindi. “Hii ilikuwa mechi ya kirafiki, hivyo hakuna uhasama kati yetu. ODM ni chama kinachozingatia demokrasia na sasa tutaunga mkono Bw Imran Okoth na tutahakikisha chama chetu kinahifadhi kiti hicho,” akasema Bw Peter Orero ambaye awali alikuwa amelalamika kuhusu udanganyifu katika kura ya mchujo. Wawaniaji wengine ambao wamewasilisha stakabadhi zao kwa IEBC ni Eliud Owalo wa chama cha Amani National Congress (ANC), Khamisi Butichi wa Ford Kenya, Malaseh Hamida (United Green Movement) Editar Ochieng (Chama cha Ukweli chake mwanaharakati Boniface Mwangi) na Fridah Kerubo Kingara (mwaniaji wa kujitegemea). You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

Na NDUNGU GACHANE ASKOFU wa Kanisa Katoliki Dayosisi ya Murang’a, amepiga marufuku wanasiasa dhidi ya kuhudhuria ibada kwenye makanisa yake, kutokana na zogo lililotokea Jumapili kati ya wabunge Ndindi Nyoro na Maina Kamanda. Kulingana na ilani iliyotumwa na Askofu James Maria Wainaina, makasisi wote wameagizwa kufutilia mbali mialiko yote ya harambee kwa wanasiasa, akisema tukio la Jumapili limeaibisha kanisa hilo. Askofu Wainaina pia alishutumu ghasia katika kanisa la Gitui. “Habari za jioni ndugu makasisi. Wengi wenu mnafahamu kilichotokea katika parokia ya Gitui. Sisi sote tumeaibika ndiyo maana ningependa kuwajuza kwamba mfutilie mbali mialiko yote ya wanasiasa katika makanisa yenu,” akasema kwenye ujumbe huo. Kasisi huyo ambaye alizungumza na Taifa Leo kwa njia ya simu alisema kisa cha Jumapili hakikufaa kutokea japo akakiri kwamba hajajuzwa na kasisi wa kanisa hilo kuhusu tukio hilo. “Ni jambo la kusikitisha kwamba tukio hilo lilifanyika katika kanisa letu. Sikuwa na habari kwamba kulikuwa na wageni ambao walialikwa kwenye kanisa hilo na nilisikia tu kupitia vyombo vya habari kwamba ghasia zilikuwa zimetokea. Ni jambo la kutamausha na nimeanza uchunguzi kulihusu kabla ya kuchukua hatua,” akasema Askofu Wainaina. Mkuu wa kanisa hilo nchini Kadinali John Njue, amewatwika jukumu Maaskofu wa Parokia mbalimbali, kuamua iwapo viongozi wanaohudhuria ibada kwenye maeneo yao, wataruhusiwa kuwahutubia waumini au la kama njia ya kuzuia ghasia kati ya wanasiasa wa mirengo mbalimbali. Kadinali Njue alisema ni maaskofu hao ambao wanaelewa hali ya kisiasa katika parokia wanazosimamia kwa hivyo wao ndio wanafahamu njia ya kukabiliana na joto la kisiasa linalozidi kupanda kwenye maeneo hayo. Askofu huyo alitoa tangazo hilo baada ya tukio la Jumapili ambapo Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro na Mbunge Maalum Maina Kamanda, walikabiliana kanisani kuhusu nani alifaa kuwa mfawidhi kwenye hafla ya Harambee katika kanisa Katoliki la Gitui. “Maaskofu wanafaa kutoa ushauri ili kuepuka aibu inayosababishwa na vurugu kwenye makanisa yetu. Hii ni kwa sababu wao ndio wanaelewa parokia zao na wanafaa kutoa uamuzi wa mwisho,” akasema Kadinali Njue kwenye mahojiano na Taifa Leo. Akizungumza na wanahabari mjini Murang’a jana, Bw Nyoro ambaye wafuasi wake walikabiliana na wanaompinga alimlaumu Bw Kamanda kwa kujifanya mbunge wa eneo hilo na kumnyima nafasi ya kuongoza mchango wa Jumapili kanisani. “Siwezi kuwaruhusu watu kutoka Nairobi waje na kunifunza namna ya kuendesha masuala yangu hapa Kiharu. Mimi ndiye nilichaguliwa na kama mwenyeji nina jukumu la kuwaalika wageni kuhutubu hapa,” akasema Bw Nyoro. Vilevile, alisema kwamba anafahamu polisi wanapanga kumkamata japo akasisitiza kwamba hatishiki kwa sababu hajafanya kosa lolote. “Najua wananitafuta kwa sababu za kisiasa na hayo yanathibitishwa na matamshi ya Bw Kamanda kwamba nitakamatwa kutokana na msimamo wangu wa kisiasa. Mimi siogopi kwa sababu sijafanya chochote kibaya,” akaongeza. Hata hivyo, madiwani Isaac Kamote na Charles Mwangi pamoja na mwenyekiti wa Muungano wa Maaskofu wa Murang’a, Stephen Maina walimlamu Bw Nyoro kwa kusababisha ghasia za Jumapili. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MHARIRI
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini.
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na BENSON MATHEKA
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na MASHIRIKA
LONDON, Uingereza
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya... Na ELIZABETH MERAB
WANASAYANSI wanachunguza kuhusu mchipuko wa virusi vipya vya corona aina ya Delta, katika nchi za Amerika, Uingereza,... Na MAUREEN ONGALA
MASAIBU ambayo wagonjwa wa Covid-19 hupitia katika kaunti za Pwani, yameanikwa wazi baada ya kifo cha afisa mkuu wa... SIAGO CECE na ANTHONY KITIMO
UFISADI miongoni mwa baadhi ya maafisa wa serikali katika mpaka wa Kenya na Tanzania, umezidi kuwaweka... Na WAANDISHI WETU
WINGU la maangamizi limetanda kote nchini huku aina mpya ya corona maarufu kama 'Delta' ikiua watu kwa... Na WINNIE ONYANDO
HUENDA visa vya wasafiri kulazimishwa kupima upya corona mpakani mwa Kenya na Tanzania vikakoma baada ya serikali hizo... NA WANGU KANURI
AGIZO la serikali la kudhibiti mkurupuko wa ugonjwa wa corona mwaka jana limewashurutisha Wakenya wengi kufanyia kazi... Na Titus Ominde
VIONGOZI wa kidini Kaskazini mwa Rift Valley (North Rift) wameshutumu wanasiasa kwa kupepeta usambazaji wa virusi vya... Na WANTO WARUI
Huku wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiripoti katika shule zao mpya za sekondari hii leo, kuna uwezekano wa maambukizi... Na CHARLES WASONGA
NAKUBALIANA na kauli ya maafisa wa afya katika kaunti ya Nairobi kwamba wanasiasa ndio wanachochea ongezeko la visa... Na SAMMY WAWERU
DICKSON Muceri amekuwa mkazi wa Nairobi kwa muda wa miaka kadhaa ila sasa kitovu hicho cha jiji kuu la nchi hakikaliki... Na MARY WANGARI
WANASAYANSI wamethibitisha kuwa kuchelewesha upokeaji dozi ya pili ya chanjo ya Covid-19 kwa kiasi cha miezi 10 baada ya... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na KINYUA BIN KINGORI
WAKATI huu viongozi wa kisiasa wameanza mapema kampeni zao kwa kuzuru maeneo mbalimbali nchini, ili kushawishi... Na WANDERI KAMAU
KULINGANA na Ripoti ya Jaji Mstaafu Akilano Akiwumi (1997) kuhusu chimbuko la ghasia za kikabila nchini, wanasiasa ndio... Na WANTO WARUI
KWA mara nyingine tena tuzo inayoenziwa sana kote ulimwenguni imerudi katika eneo letu la Afrika Mashariki mara hii... Na DOUGLAS MUTUA
MWAFRIKA akiwajibishwa na Mzungu hupiga kamsa na kudai anaonewa, ati msingi wa maonevu ni ubaguzi wa rangi... Na WANDERI KAMAU
MOJA ya changamoto kuu zinazokikumba kizazi cha sasa nchini ni ukosefu wa ufahamu wa lugha zao asili.
Ingawa lugha... Na KINYUA BIN KINGORI
JUHUDI za kuhakikisha taifa limefanikiwa kupiga vita ufisadi lazima ziendeshwe kuambatana na Katiba, bila njama... Na WANDERI KAMAU
UFICHUZI wa sakata ambapo watu maarufu duniani wamekuwa wakificha mabilioni ya fedha katika akaunti za siri ng’ambo... Na FAUSTINE NGILA
NINA imani kuwa iwapo kufikia sasa hujawahi kuelewa teknolojia ya blokcheni, leo utaelewa kwa kuwa jana uliathirika... Na CHARLES WASONGA
NI jambo la kusikitisha kuwa ni wakati kama huu ambapo uchaguzi mkuu unakaribia ndipo wanasiasa wametambua umuhimu wa... Na MARY WANGARI
IDADI ya watu wanaoandaa hafla za uchangishaji pesa za kugharamia matibabu imeongezeka pakubwa katika siku za hivi... Na CECIL ODONGO
CHAMA cha Kanu bado kina safari ndefu kurejelea umaarufu wake wa enzi za utawala wa chama kimoja na miaka ya 90 hata... Na CHARLES WASONGA
UTEUZI wa waliokuwa maafisa wanne wa ngazi za juu katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kushikilia nyadhifa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Naomi Wamboi, 21, ndiye anatupambia yeye ni mwanamitindo aliyewahi kushinda tuzo za Miss Nakuru. Akipata muda anapenda kusafiri na... Winnie Miriam Nechesa 21, ni mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu Cha Maasai Mara kaunti ya Narok.Anapenda kuchora, na kujumuika na... Lilian Njeri mwenye umri wa miaka 21 ndiye anatupambia jarida letu leo.Yeye ni mwanamitindo na mkaazi wa Narok.Uraibu wake ni kusafiri na... Mary Njeri mwenye umri wa miaka 21 ni mkaazi wa mtaa wa Langalanga kaunti ya Nakuru.Yeye ni mwanafasheni wa mapambo na vipodozi.Uraibu wake... Marylene Watiri mwenye umri wa miaka 22 ni mtaalam wa Beauty Therapy jijini Nairobi, aidha yeye ni mwanamitindo na mlimbwende.Uraibu wake... Zaweria Njoki mwenye umri wa miaka 21 ni Video Vixen kutoka kaunti ya Nakuru.Uraibu wake ni kuandika makala ya kitaaluma na kujumuika na...
Malkia wetu leo ni  Babra Ingasiani mwenye umri wa miaka 21, yeye ni mzaliwa wa kaunti ya Kakamega.Uraibu wake ni kusakata densi ya... Pauline Kimani mwenye umri wa miaka 23 ndiye anatupambia jarida letu leo.Yeye ni mkaazi wa eneo la Lanet na mfanyikazi mjini Nakuru.Uraibu...
Sayfer Godez ni mkaazi wa Nakuru .Anapenda kushiriki kwenye majukwaa ya mapambo na urembo.Uraibu wake ni kusafiri na kujumuika na... Sylvia Wangeci 23 ni mzaliwa wa Molo, na mwanafunzi katika Chuo Kikuu Cha MKU tawi la Nakuru.Uraibu wake ni kusafiri na... Mical Abulatsia Imbukwa, 28, ni mwanahabari katika shirika moja jijini Nairobi. Uraibu wake ni kutazama filamu za Afro sinema na kujumuika... Faith Karungari mwenye umri wa miaka 22 ni mwanafasheni na mwanamitindo maarufu kutoka Nakuru.Uraibu wake ni kuogelea na kusikiliza muziki... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na RICHARD MUNGUTI
MAHAKAMA ya Juu jana ilianza kusikiza rufaa ya mpango wa kubadilisha katiba (BBI) huku Mwanasheria Mkuu Bw Paul... Na BENSON MATHEKA
RAIS Uhuru Kenyatta jana Jumapili alisema kuwa ndoto yake ya kubadilisha katiba ya Kenya iliyopitishwa 2010 kupitia... Na CHARLES WASONGA
KWA mara nyingine Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza kuwa mageuzi ya katiba yaliyopendekezwa katika Mswada wa Mpango wa... Na JOSEPH WANGUI
Mwanasheria Mkuu, Paul Kihara Kariuki hatimaye amewasilisha rasmi rufaa katika Mahakama ya Juu kupinga uamuzi wa... Na Gitonga Marete