text
stringlengths
3
16.2k
Na RICHARD MUNGUTI
ALIYEKUWA Gavana wa Nairobi Mike Sonko Mbuvi Ijumaa alizimwa na mahakama kupeperusha katika mitandao ya kijamii video... Na RICHARD MUNGUTI
KUNDI jipya la mawakili sita waliokuwa wanamwakilisha aliyekuwa gavana wa Nairobi Bw Mike Sonko Jumanne walijiondoa... Na RICHARD MUNGUTI
RIPOTI ya daktari wa tiba za akili imesema Alhamisi kuwa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko anaugua maradhi ya... Na RICHARD MUNGUTI
MAHAKAMA ilielezwa jana kuwa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko angali amelazwa katika Nairobi Hospital... Na RICHARD MUNGUTI
UFICHUZI wa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko kwamba mtu aliingia kwenye seli anamozuiliwa katika kituo cha... Na BENSON MATHEKA
Aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Bw Mike Sonko anajuta kwa vitendo alivyofanya akiwa mamlakani; akiepuka kuadhibiwa kwa... Na RICHARD MUNGUTI
KAMA kuna wakati wenye changamoto tele kwa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko ni sasa.
Maji yalizidi unga hata... Na RICHARD MUNGUTI
MASAIBU ya aliyekuwa gavana wa Nairobi, Bw Mike Sonko, yaliongezeka Jumatano ilipofichuka kuwa serikali inapanga... Na RICHARD MUNGUTI
ALIYEKUWA Gavana wa Nairobi, Mike Sonko aliangua kilio kortini Jumatano wakati wa kusikizwa kwa kesi ya ufisadi wa... Na CHARLES WASONGA
WANASIASA na watu ambao majina yao yatawekwa katika orodha ya aibu ya Tume ya Uwiano na Utangamano ya Kitaifa (NCIC)... BENSON MATHEKA na SIMON CIURI
Masaibu ya aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Mike Sonko yaliendelea kuongezeka jana alipozuiliwa rumande baada... Na RICHARD MUNGUTI
MASAIBU ya aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko Mbuvi Gidion Kioko yameongezeka baada ya  kusukumwa ndani hadi... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA SAMMY WAWERU MSANII tajika wa nyimbo Mugithi, Samuel Muchoki maarufu kama Samidoh huenda ametengana na mpenzi wake mwanasiasa Karen Nyamu. Hii ni kutokana na video iliyochipuka ambayo anaskika akisema “nilikuwa kwenye ndoa ya mitara, sasa niko singo”. Samidoh amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Seneta Maalum Karen Nyamu, na wamejaaliwa kupata watoto wawili. Msanii huyo wa nyimbo za Agikuyu, alifichua kuachana na Karen kupitia video ya mbashara ya Tiktok (live) ambapo alikuwa akijibu maswali ya mashabiki wake. Wakati wa mafichuzi hayo, alionekana kuwa kwenye eneo la burudani alikoandamana na msichana ambaye hakuweka wazi endapo ndiye mchumba wake mpya. “Ati hongera kwa kuwa na mpenzi mpya…” Samidoh akasoma mojawapo ya jumbe zilizotumwa na mashabiki wake. Alijibu, “Si wewe pekee ulishushwa madaraka kutoka kiwango cha hadhi hadi dereva wangu…Nilikuwa kwenye ndoa ya mitara ila sasa niko singo”. Mfuasi huyo aliendelea kumdadisi, akitaka kujua iwapo Samidoh anafahamu kuhusu ukurasa wa kimitandao unaohusishwa na mchumba wake – Karen Nyamu Fun Page. Kwa ucheshi, mwimbaji huyo wa kibao tajika cha Kairetu Gakwa (Binti yangu) na Ndiri Mutwe Mwega (Sina kichwa kizuri) alisema kwa sasa anajishughulisha na biashara. “Kwa sasa, ninajishughulisha na masuala biashara. Ikiwa si mradi au biashara, ishi na mama yako,” alielezea. Shabiki wake alimkejeli akitaka kujua aliko nina yake, isijulikane ikiwa alimaanisha mama yake mzazi au mpenzi wake. “Ameoleka na kwa sasa anafurahia fungate (honeymoon),” Samidoh alidokeza. Kidosho aliyeandamana naye alitambua shabiki huyo kama Shabaan, akisema kwamba yeye ni mchochezi. “Wee acha hiyo, unajua Shabaan wewe ni mchochezi sana… (Yuko hapa (akimaanisha Karen Nyamu),” mwanadada huyo alisema. Naye Samidoh aliendelea, “Tunataka Karen, naona hivo ndivo mchango safuni unasema…Naona, lakini sasa yuko online kweli?” Kipusa aliyeandamana naye, alijibu, “Yuko online, mjaribu”. Aidha, shabiki wa Samidoh alitaka Karen Nyamu ajumuishwe kwenye mazungumzo hayo ya mbashara Tiktok. Kilichoshangaza zaidi na kuashiria utengano wa Samidoh na Karen, ni kudai kwamba alimbloki mtandaoni na angeweza kushiriki endapo atamuondoa alikomuweka. “Yuko kwenye orodha ya kublokiwa, sasa hiyo ndio shida. Labda nisitishe mazungumzo haya ya moja kwa moja ili nimuondoa aweze kujumuika nasi,” Samidoh alifafanua. Mahusiano kati ya Samidoh na Karen, ndiyo yalichangia kuachana na mkewe, Edday Nderitu ambaye alihamia Amerika Mei 2023. Edday alikuwa ameonya msanii huyo mapema 2023, akisisitiza kwamba hakuwa tayari kuwa kwenye ndoa ya mitara. Samidoh na Edday wana watoto watatu pamoja. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MAOSI WAKAZI wa mtaa wa Mazembe viungani mwa mji wa Nakuru wamekiri kuhangaishwa na wezi ambao huwaibia na kuwasindikiza hadi nyumbani. Huwawekea ulinzi huo makusudi ili kuhakikisha kwamba wateja wao wanafika nyumbani salama salimini. Kwa kawaida, wahuni wamebuni mbinu mpya ya kutembea na mbwa wakubwa nyakati za usiku, ili kujiwekea ulinzi wa kibinafsi. Owen Shibala mwendeshaji bodaboda kati ya Nakuru mjini na Mazembe, anasema hajui walikotoa ujasiri walio nao kushika doria usiku utadhani ni polisi. Mazembe ni mojawapo ya mitaa ambayo hushuhudia visa vya kihalifu na utumiaji wa mihadarati mara kwa mara. “Ukikutana nao usiku ni lazima usalimishe kila kitu lau sivyo utaona cha mtema kuni. Watakucharaza viboko na kuiba kila kitu cha nguvu,”akasema. Hata hivyo, wanapoiba hujitwika jukuma la kuwasindikiza wakazi, wasije wakakutana na vibaka wengine barabarani. Aidha, wanalia sare za polisi jambo linalowafanya baadhi ya raia kuamini huenda wanashirikiana na maafisa wa polisi. Baadhi yao wanajifanya ni maafisa wa polisi ambao huwa wameshika doria, wakilenga kuhangaisha wapita njia wanaotoka kazini usiku. Agnes Wahome mfanyibiashara mtaani Rhonda anasema huwa wamejihami kwa visu, rungu na wako tayari kupigana. Kulingana na Bi Wahome, hii ni hali ya kawaida siku hizi katika mitaa ya Manyani, Bondeni na Freearea ambapo vijana wengi wamejiingiza kwenye uhalifu. Bi Wahome anasema wahalifu wengi wanajulikana, kwani ni vijana wadogo kutoka mitaa jirani ya Flamingo na Lakeview. Mkazi huyo angependa polisi kushika doria katika maeneo husika ili kuzuia kuzuka kwa magenge hatari yanayohangaisha wenyeji. Hili linajiri siku chache baada ya Taifa Leo Dijitali kufichua visa vya wizi ambapo baadhi ya wezi kutoka kwenye mtaa wa Gioto, Nakuru wamekuwa wakipika chakula katika kila nyumba wanamoingia kuiba. Mtaa wa Bondeni, Kaunti ya Nakuru ambapo wezi huwaibia wakazi na kuwasindikiza mpaka nyumbani. PICHA|RICHARD MAOSI
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L

You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MUNGUTI MASKWOTA wapatao 10,000 wamewasilisha upya kesi katika Mahakama ya Upeo wakiomba ibatilishe uamuzi kwamba wafukuzwe kutoka kwa shamba la ukubwa wa ekari 25,000 wanalong’ang’ania umiliki wake na familia ya mwanasiasa marehemu Mark Too. Maskwota hao wanaodai mababu zao ndio waliotimuliwa kutoka kwa shamba hilo enzi za ukoloni, wanasema walipewa shamba hilo rasmi na aliyekuwa Rais hayati Daniel arap Moi, kisha Kamishna wa Ardhi M Okundu akaratibisha uamuzi huo mwaka 2007. Katika ombi lililowasilishwa na wakili William Arusei chini ya sheria za dharura, kikundi cha maskwota hao–Sirikiwa Squatters Group–kimeomba mahakama ibatilishe uamuzi huo kwa vile ilitegemea ushahidi ambao haukuwa umewasilishwa katika kesi waliyoshtaki katika Mahakama ya kuamua kesi za mashamba (ELC), Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu. Pia wameeleza bayana Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaack Lenaola, na William Ouko walitegemea ushahidi wa Afisa wa Ugavi wa Mashamba R J Simiyu kutoa uamuzi wang’atuke shambani. Maskwota hao wamesema ushahidi wa Bw Simiyu uliowasilishwa mbele majaji hao saba kwa njia ya afidaviti ni mpya na kamwe “haukuwasilishwa mbele ya Jaji Antony Ombwayo aliposikiliza na kuamua kesi hiyo 2017.” Pia wanasema ushahidi huo haukuwasilishwa Mahakama ya Rufaa iliyosikiliza rufaa iliyowasilishwa na kampuni ya Fanikiwa, familia ya marehemu Mark Too, kampuni ya Lonrho Agribusiness (EA) Ltd, na Bw David K Korir. Hivyo basi, maskwota hao wanaeleza mahakama hii ya upeo kwamba ni kinyume cha sheria kutegemea ushahidi mpya kutoa uamuzi wa kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma. “Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu wa Desemba 15, 2023, hauna mashiko kisheria na kamwe hauna nguvu kisheria kuwatimua maskwota hawa kutoka kwa shamba lao,” asema Bw Arusei. Pia maskwota hawa wanadai kwamba badala ya Mahakama ya Juu kujadili masuala ya kikatiba jinsi ilivyo jukumu lake, majaji hao walianza kufafanua na kutafsiri ushahidi wa watu binafsi na kuelezea maana ya ‘skwota’. Mahakama hii imeombwa ikague upya uamuzi iliyotoa kwa vile ilidanganywa na walalamishi na pia kutendewa ujanja. Akinukuu maamuzi ya majaji wastahiki kama vile Lord Dening, Bw Arusei amesema, mahakama ikigundua ilipotoshwa au kudanganywa na upande mmoja, iko na mamlaka na uwezo wa kufutilia mbali uamuzi iliyotoa na kuandika mwingine. Maskwota hao wanaomba Mahakama ya Juu iwarudishe shambani kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Ombwayo na Mahakama ya Rufaa. Vile vile mahakama hiyo imekosolewa kwa kumshambulia hayati Moi katika uamuzi huo pasi kutoa agizo wasimamizi wa mali yake wafike mbele yao kutoa mwanga kuhusu suala la umiliki wa shamba hili lililorudishwa kwa serikali na kampuni iliyokuwa inakuza miti inayotumika katika viwanda vya ngozi. Naibu msajili wa Mahakama ya Juu Nelly Kariuki aliwaamuru maskwota hao wawakabidhi nakala za kesi hii yao mpya wahusika wote kabla ya Januari 31, 2024, kesi itakapotajwa tena kwa maagizo zaidi. Jaji aliyesikiliza kesi hii mpya hakuiratibisha kuwa ya dharura ila aliamuru pande zote ziwasilishe ushahidi katika muda wa siku 14 kuanzia Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti,  baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA WAZIRI wa Utumishi wa Umma Moses Kuria amejipalia makaa miongoni mwa maseneta kwa kumtetea Gavana wa Meru Kawira Mwangaza. Sasa maseneta wa mirengo ya Kenya Kwanza na Azimio wanashinikiza kutimuliwa kwa waziri huyo wakidai mienendo yake inaleta aibu kwa serikali na haswa Rais William Ruto. Wakiongozwa na Kiongozi wa Wengi katika Seneti Aaron Cheruiyot, maseneta hao Jumatano Novemba 8, 2023 walilalamikia kile walichokitaja kama hatua ya Bw Kuria kuingilia vikao vya kushughulikia kesi ya kumtimua afisini Gavana wa Meru Kawira Mwangaza. Walimsuta Bw Kuria, ambaye ni mbunge wa zamani wa Gatundu Kusini, kwa kutoa orodha ya maseneta 13 aliodai kuwa “wamepotoshwa” kuhakikisha kuwa Bi Mwangaza anaondolewa afisini. “Huyu waziri amekuwa na mwenendo mbaya wa kuaibisha Rais kupitia matamshi yake yasiyo ya heshima. Ama kwa hakika nakubaliana na maseneta wa bunge hili ambao awali waliwasilisha hoja ya kujadili mienendo ya Bw Moses Kuria. Kwa mfano, sasa waziri huyu anaibisha Rais wa nchi hii kwa kudai kuwa baadhi yetu tunapotoshwa kumwondoa afisini Gavana Mwangaza,” akasema Bw Cheruiyot. Seneta huyo wa Kericho alieleza kuwa waziri huyo amekuwa akiikosea heshima serikali ya Kenya Kwanza kupitia mienendo yake inayokwenda kinyume cha hitaji la Katiba kuhusu Maadili na Uongozi Bora. “Ama kwa hakika, Mheshimiwa Spika anapendekeza kuwa waziri Kuria avuliwe wadhifa huo ili kuokoa hadhi ya serikali hii na Rais William Ruto,” Bw Cheruiyot akaongeza. Maseneta wengine waliunga mkono pendekezo la Bw Cheruiyot wakisema mienendo ya Bw Kuria ni ya kutiliwa shaka na anafaa kupigwa kalamu. “Moses Kuria ni kielelezo cha aibu ya kitaifa. Mbona Rais anakubali aina kama hii. Ikiwa hatua yoyote haitachukuliwa dhidi ya Kuria huenda akaiabisha serikali hata zaidi,” akasema Seneta wa Homa Bay Moses Kajwang’. Seneta wa Homa Bay Moses Kajwang’ aliwashauri maseneta wa mrengo wa Kenya Kwanza wamshauri kumtimua waziri huyo wa Utumishi wa Umma. “Nendeni mkamwambie Mkubwa kwamba waziri Kuria analeta aibu sio tu kwa serikali bali kwa taifa hili na ukanda wa Afrika Mashariki kwa ujumla. Matendo na matamshi yake yanafanya Kenya kuonekana kama nchi isiyo zingatia sheria,” akasema seneta huyo aliyechaguliwa kwa tiketi ya chama cha ODM. Seneta wa Nandi Samson Cherargei aliunga mkono pendekezo la wenzake lakini akaongeza kuwa Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen pia anafaa kupigwa kalamu kwa “kudharau viongozi waliochaguliwa”. “Kuria hurusha matumisi kupitia mtandao wa Twitter lakini Murkomen huwarushia hutusi na kudunisha viongozi katika katika hafla ya mazishi,” akasema. Spika Amason Kingi alikatiza mjadala kuhusu Bw Kuria na kupendekeza kuwa maseneta waandae hoja ambayo itawasilishwa katika bunge la kitaifa. Hii ni kwa sababu kwa mujibu wa Katiba, kipengele cha 152 Bunge la Kitaifa ndilo lenye mamlaka ya kuanzisha hoja ya kuondoa afisini Waziri wa Serikali ya Kitaifa. “Kwa hivyo, waheshimiwa maseneta. Ikiwa mwahisi kuwa mienendo ya waziri Kuria si mizuri, mtumie mamlaka mliopewa na sheria za bunge hili,” Bw Kingi akasema. Akaongeza: “Hili ni bunge la vitendo. Mwandae hoja ya kumtimua waziri huyo afisini kisha muiwasilishe kwa Bunge la Kitaifa liweze kuanzisha mchakato huo.” Kulingana na kipengele hicho, hoja kama hiyo sharti iungwe mkono na angalau thuluthi mbili ya idadi jumla ya wabunge katika Bunge la Kitaifa. Kwa misingi ya idadi ya sasa ya wabunge 349, hoja ya kumtimua waziri sharti iungwe mkono na angalau wabunge 233. Mawaziri wa serikali ya kitaifa ambao wamewahi kukabiliwa na tishio la kuondolewa afisini ni aliyekuwa Waziri wa Ugatuzi Anne Waiguru (sasa Gavana wa Kirinyaga), aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi James Macharia na aliyekuwa Waziri wa Elimu Jacob Kaimenyi. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MWANDISHI WETU GAVANA wa Meru Kawira Mwangaza ambaye amekuwa na kibarua kigumu kujitetea mbele ya maseneta ana kila sababu ya kutabasamu baada ya kesi dhidi yake kuamuliwa saa sita usiku wa kuamkia Alhamisi ambapo maseneta walipiga kura, Bunge la Seneti likishindwa kumng’oa ofisini. Kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa Jumanne iliamuliwa baada ya maseneta kusikiliza ushahidi wa madiwani na kumpa nafasi Gavana Mwangaza kujitetea.  Spika wa Bunge la Seneti Amason Kingi alifafanua kabla ya shughuli ya upigaji kura, akisema maseneta wangepiga kura kwa kila mojawapo ya mashtata dhidi ya Gavana Mwangaza. Maseneta walipiga kura mara saba. Shtaka la kwanza lilikuwa ni ubadhirifu na matumizi mabaya ya rasilimali za kaunti. Maseneta 19 walipiga kura ya kukubaliana na madiwani huku maseneta 28 wakipiga kura ya ‘La’. Shtaka la pili lilikuwa upendeleo wa jamaa na ukiukaji mwingine wa maadili. Maseneta watano waliunga mkono ang’olewe huku 42 wakipinga. Katika shtaka la tatu la kuwadhalilisha viongozi wengine kura ilipigwa ambapo matokeo yalikuwa kwamba watatu walikubaliana na madiwani wa Meru huku 44 wakipinga. Kwenye shtaka la nne, Gavana Mwangaza alimulikwa na madiwani kwa kufanya uteuzi unaokiuka mchakato unaohitajika ambapo katika upigaji kura, maseneta 20 wamekubaliana na madai hayo huku 27 wakipinga. Nalo shtaka la tano likihusu kuidharau mahakama ambapo maseneta watatu wamekubaliana na madiwani lakini wakalemewa na 44 waliopinga. Aidha kiongozi huyo wa Kaunti ya Meru alikabiliwa na shtaka la sita la kuipa barabara jina la mume wake Bw Murega Baichu. Maseneta wanne wamepiga kura ya ‘Ndiyo’ ambapo tena walilemewa na 43 waliopinga. Shtaka la saba na la mwisho lilisema Gavana Mwangaza alidharau Bunge la Kaunti. Shtaka hilo limepata uungwaji mkono kutoka kwa maseneta 10 pekee, tena wakilemewa na 37 waliopinga. “Seneti haijathibitisha kosa lolote hivyo Gavana Kawira Mwangaza anaendelea kuongoza Kaunti ya Meru,” amesema spika Kingi. Ikiwa maseneta wangepitisha hata shtaka moja tu, basi Gavana Mwangaza angebanduliwa ofisini. Sasa cha kusubiriwa ni kuona namna atakavyojinyanyua tena na kutafuta njia ya kushirikiana na madiwani waliopitisha hoja ya kumbandua. Hii imekuwa mara ya pili kwa kesi dhidi ya Gavana Mwangaza kuwasilishwa na kujadiliwa katika Bunge la Seneti. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MWANDISHI WETU Mahakama Kuu imepiga breki utekelezwaji wa tangazo la Gazeti Rasmi la Serikali lililochapishwa Novemba 7, 2023 ambalo liliongeza ada katika huduma mbali mbali ikiwemo upataji kitambulisho cha kitaifa na paspoti. Hatua hiyo imejiri baada ya mkazi wa Nakuru, ambaye ni daktari kufika mahakamani kupinga nyongeza hizo ambazo zilipata Wakenya katika hali ya kutozitarajia. Kulingana na tangazo hilo lililotiwa saini na Waziri wa Usalama na Mambo ya Ndani Profesa Kithure Kindiki, kujipatia paspoti ya kawaida, ya kurasa 34 itakuwa Sh7,500 kutoka Sh4,500 ambayo Wakenya wamekuwa wakilipa kwa miaka mingi. Ile ya kurasa 66 nayo imetoka Sh7,500 hadi Sh12,500. Kujipatia kitambulisho cha kawaida ambapo Mkenya hajakuwa akitozwa ada yoyote, tangazo hilo lilisema mtu atakuwa anatozwa Sh1,000. Hii ilimaanisha kwamba Mkenya yeyote anayetimu umri wa miaka 18 atahitaji kutafuta Sh1,000 kujipatia kitambulisho cha kitaifa ambacho kinahitajika katika huduma zote ikiwemo kujipatia laini ya Mpesa na pia kupiga kura. Huduma zingine kama vile kujipatia kitambulisho baada ya kilichokuwepo kupotea, pia imeongezwa kutoka Sh100 hadi Sh2,000 huku kuandikisha mtoto aliyezaliwa ili apate cheti cha kuzaliwa, pamoja na kujipatia cheti cha kuaga dunia kwa mpendwa pia kukiongezwa ada. Haya yanajiri wakati ambapo serikali ya Rais William Ruto imeleta mabadiliko makubwa haswa katika ulipaji ushuru na uongezeaji ada katika huduma nyingi nchini. Yanajiri pia wakati ambapo mamilioni ya Wakenya wanalalamikia hali mbovu ya uchumi wanaosema umelemazwa zaidi na nyongeza kubwa ya ushuru ukiwemo ule wa bei ya mafuta ambao umefanya bidhaa nyingi za kimsingi kupanda mara dufu. Mengi zaidi kadiri yanavyojiri… You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA SIAGO CECE WAKAZI wa Kaunti ya Kwale wamebaki vinywa wazi baada ya kampuni ya uchimbaji madini ya Base Titanium kutangaza kuwa itafunga mtambo wao mwaka 2024. Baadhi ya wakazi waliisifu kampuni hiyo wakisema kuwa imekuwa ya manufaa kwa jamii kwa miaka ambayo imekuwa ikifanya uchimbaji, na kuondoka kwake kutakuwa pigo kubwa kwa jamii. Kando na jamii, wafanyakazi zaidi ya 1,400 pia ni miongoni mwa wanaosikitika kutokana na tangazo hilo la kumaanisha kuwa kila mmoja wao atapoteza kazi. “Base Titanium imenisaidia katika kuhifadhi mazingira kwa kupanda mikoko, na pia imeboresha hali ya afya. Base ikiondoka itakuwa mzigo mkubwa kwetu kwa sababu hii misaada ambayo wanafunzi wamekuwa wakipata haitakuwa na wazazi wataendelea kuishi maisha ya uchochole,” Bw Kondo Harun alisema. Kampuni hiyo wiki jana ilitangaza kuwa hakuna madini yenye thamani ya kutosha katika maeneo yaliyofanyiwa utafiti katika kaunti hiyo, na hii italazimisha kampuni hiyo kufunga shughuli mwaka wa 2024 wakati madini yote yatakuwa yameisha. Kulingana na meneja wa kampuni hiyo Simon Wall, wafanyikazi ambao asilimia kubwa ni wenyeji wa kaunti ya Kwale, watapokea ushauri nasaha ili kuwasaidia kimawazo wakati kampuni hiyo imeanza matayariho kabla kufunga. “Tunaelewa kuwa hili ni swala kubwa sana hasa kwa familia ambazo zimekuwa zikitegemea wapendwa wao wanaofanya kazi hapa Base Titanium. Lakini tunawapa fursa ya kupata ushauri ili kujitayarisha kwa jambo hilo. Mimi mwenyewe nimesikitika,” Bw Wall alisema. Aliongeza kuwa kampuni hiyo imetoa ombi la kufanya utafiti katika Kaunti ya Lamu na eneo la Kuranze lililo katika mpaka wa Kwale na Taita Taveta. Ikiwa serikali itakubali ombi hilo, kampuni hiyo itachukua zaidi ya miaka mitatu kabla kuhakikisha kuwa madini hayo yana thamani na kuanza uchimbaji upya katika maeneo hayo. Baadhi ya wakazi walikuwa wameipongeza Base kwa miradi yao ya kijamii katika kaunti za Kwale na Mombasa ambayo ni pamoja na zahanati, kumbi za kijamii, miradi ya maji, barabara na ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa shule za upili. Miradi hiyo sasa itakamilika mwaka 2024 wakati kampuni hiyo itafunga. Hata hivyo, swala tata limebaki kwa ardhi ambayo kampuni hiyo ilikuwa ikifanyia uchimbaji wao baada ya baadhi ya wakazi waliohamishwa hapo awali wakitaka waruhusiwe kurudi ili waishi hapo upya. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MUNGUTI MKURUGENZI wa Mashtaka ya Umma (DPP) Renson Ingonga ameiomba Mahakama Kuu kudumisha adhabu ya kifungo jela dhidi ya aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) James Oswago kwa kuhusika katika sakata ya Sh1.3 bilioni ya uagizaji wa vifaa vya uchaguzi mkuu wa mwaka 2013. Wakili wa serikali amemuomba Jaji Nixon Sifuna adumishe hukumu dhidi ya Oswago na aliyekuwa Naibu Katibu wa IEBC aliyehusika na Masuala ya Huduma Wilson Shollei akisema mahakama iliyowahukumu ilifuata sheria. Oswago na Shollei walitozwa faini ya Sh7.5 milioni au watumikie adhabu ya kukaa jela miaka mine kila mmoja kwa kukiuka sharia za uagizaji wa vifaa vya uchaguzi wa Machi 4, 2013. Oswago hata hivyo anapinga akisema adhabu hiyo ilikuwa kali sana kwa yeye ambaye alikuwa mkosaji wa kwanza. Wakikosoa hukumu iliyotolewa na hakimu Felix Kombo, Oswago na Shollei walisema alivuka mipaka yake  kwa sababu kwa mujibu wa sheria ya Kuzuia Ufisadi na Makosa ya Kiuchumi, mwenye hatia anafaa kutozwa faini ya Sh1 milioni, lakini hakimu alitoza faini ya Sh5 milioni na Sh2.5 milioni za ziada kwa mashtaka mawili. Jaji Sifuna ameratibu uamuzi kutolewa Februari 28, 2024. Oswago na Shollei walifungwa Desemba 2022 kwa kuidhinisha malipo ya Sh1,397,724,925.51 kwa Face Technologies Limited bila kukagua au kujali kwamba vifaa vilikubalika na vilikuwa vya teknolojia iliyohitajika kwa kurejelea mkataba. “Mahakama imezingatia changamoto za uchaguzi lakini imebaini kwamba dosari katika uagizaji wa vifaa vya kura ziliathiri matokeo kwa namna moja au nyingine,” akasema Bw Kombo wakati huo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA JOSEPH OPENDA FAMILIA zilizoathiriwa na mkasa wa bwawa la Solai mnamo Mei 9, 2018, zinatazamiwa kupokea fidia ya jumla ya Sh57.6 milioni baada ya kuafikiana na mmiliki wa bwawa, Bw Perry Mansukh nje ya mahakama. Bw Mansukh, mmiliki wa bwawa lililopasuka na kusababisha vifo vya watu 48, amekubali kuzifidia familia hizo Sh1.2 milioni kwa kila maisha yaliyokatizwa ya mtu mzima na Sh800,000 kwa kila mtoto aliyefariki. Mazungumzo yaliyofanyika Jumanne, Taifa Leo imebaini, yalihusisha wawakilishi kutoka familia 48, Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), mawakili wa wamiliki wa mabwawa, na wamiliki wenyewe. Wakili Boniface Masinde anayewakilisha mmiliki wa bwawa hilo, alithibitisha kwamba pande zote zilikutana Solai ili kukamilisha na kuafikiana huhusu mpango huo kufuatia mazungumzo. Bw Masinde alisema kuwa mahakama iliruhusu pande zote kujaribu kusuluhisha kesi hiyo nje ya mahakama. Kesi iliwasilishwa na waathiriwa. Vile vile, Tume ya Haki za Kibinadamu Nchini Kenya, inayowakilisha familia 29, ilithibitisha mpango huo kupitia kwa meneja wao wa mipango Bi Mary Kambo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

Na MASHIRIKA KIGALI, RWANDA AMERIKA kwa mara nyingine imejaribu kuleta upatanisho kati ya marais wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa lengo la kupunguza uhasama kati ya nchi hizo jirani. Waziri wa Masuala ya Kigeni wa Amerika Antony Blinken alizungumza na Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi mnamo Jumanne jioni, kulingana na taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na msemaji wa Wizara hiyo Mattthew Miller. “Kwenye mazungumzo yake na marais hao wawili, Waziri alijadili hali hiyo ya uhamasa na hali mbaya ya kibinadamu inayoshuhudiwa karibu na mpaka wa Rwanda na DRC. Waziri huyo alihimiza kwamba uhasama huo umalizwe kwa njia ya kidiplomasia na kila nchi iondoe wanajeshi wake katika maeneo ya mpaka,” akasema Miller. Baada ya mazungumzo kati ya Blinken na Kagame, kwa njia ya simu, Ikulu ya Rwanda ilisema inaunga mkono haja ya “kupunguza uhasama na kukumbatiwa kwa suluhu ya kisiasa kwa mapigano nchini DRC.” Ilisema Rais Kagame anaunga mkono juhudi za sasa za kuleta amani DRC zinazoendeshwa na mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki. Kuna michakato miwili inayolenga kupata suluhu kwa mzozo unaoshuhudiwa mashariki mwa DRC. Mchakato unaosimamiwa na Kenya unaendeshwa chini ya mwavuli wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa lengo la kukomesha vita kati ya mamia ya makundi ya wapiganaji yanayojulikana kama “mai mai” na kundi kubwa la waasi wa M23. Aidha, kuna mchakato unaosimamiwa na Angola na unaolenga kukomesha uhasama kati ya Rwanda na DRC. Ukosefu wa amani mashariki mwa DRC, haswa mkoa wa Kivu Kaskazini, unaweza kuathiri uendeshwaji wa uchaguzi mkuu ulioratibiwa kufanyika Desemba 20, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA SAMMY WAWERU SPIKA wa Seneti, Amason Kingi, ametoa onyo kwa Waziri wa Utumishi wa Umma, Moses Kuria, kuhusu ukosoaji wake kwa mchakato unaoendelea wa kumwondoa mamlakani Gavana wa Meru, Kawira Mwangaza. Gavana huyo ambaye anaandamwa na changamoto za kiutawala anatarajiwa kujua hatma yake leo, Jumatano, Novemba 8, 2023 baada ya kura ya kutokuwa na imani naye kupitishwa na madiwani (MCAs) wa Meru, maamuzi sasa yakiwa mikononi mwa Bunge la Seneti. Spika Kingi ameelezea wasiwasi wake kufuatia cheche za maneno zinazorushwa na Wakenya, hasa baadhi ya viongozi serikalini akilalamika kwamba hatua hiyo itaathiri mchakato wa kusikiliza malalamishi ya Bunge la Kaunti ya Meru. Kingi anasema Wakenya, pamoja na maafisa wa umma wa ngazi ya juu, wanapaswa kujiepusha na kutoa maoni, iwe kwa njia ya maandishi au kwa matamshi, kuhusu mdahalo wa kumuondoa Gavana Mwangaza. “Mnamo Jumanne (Novemba 7, 2023), niliwaonya maseneta dhidi ya kutoa maoni, iwe kwa njia ya maandishi au semi za matamshi, kuhusiana na pendekezo la kumwondoa mamlakani kwa njia ya kura ya kutokuwa na imani Mheshimiwa Kawira Mwangaza, Gavana wa Kaunti ya Meru, wakati suala hilo likiwa mbele ya Seneti. Nina wasiwasi kumekuwa na maoni ambayo huenda yakadhuru mchakato unaondelea katika Seneti, yanayosambazwa kwenye majukwaa mbalimbali ya kijamii, ikiwa ni pamoja na mtandao wa X (awali Twitter) na Wakenya wakiwemo maafisa wa ngazi ya juu serikalini.” Seneta Kingi aliongeza, “Hasa, Waziri wa Utumishi wa Umma, Utendaji, na Utoaji wa Huduma ametoa machapisho kadhaa yakikosoa mchakato unaondelea, kutisha, na kutoa shutuma kwa baadhi ya maseneta. Suala la kumuondoa Gavana ni mjadala wa umma. Mchakato huu unapeperushwa moja kwa moja katika vituo mbalimbali tajika vya televisheni, ikiwa ni pamoja na YouTube, na haupaswi kutumika kama njia kulenga seneta fulani na kutoa shutuma dhidi ya Seneti.” Kikao cha Seneti kusikiliza kesi ya kuondolewa kwa Gavana Mwangaza kilianza Jumanne, MCA wa Meru wakimtuhumu kwa matumizi mabaya ya ofisi, ufujaji na ubadhirifu wa mali ya umma. Isitoshe, madiwani hao wanalalamikia Gavana Mwangaza kutumia mamlaka yake kuajiri watu wa familia yake katika kaunti. Hali kadhalika, anatuhumiwa kwa kutoa vitisho, kudhalilisha na kukashifu viongozi wengine wa kaunti, uteuzi wa nyadhifa usio halali, na kukiuka sheria za uongozi. Waziri Kuria amekuwa akimuunga mkono Bi Mwangaza kusalia ofisini, akilaumu baadhi ya maafisa wakuu serikalini na viongozi waliochaguliwa kufuatia mahangaiko yanayoandama Gavana Mwangaza. Jaribio la sasa kumbandua ni la pili, chini ya kipindi cha mwaka mmoja. Mnamo Jumanne, Bw Kuria alichapisha kwenye akaunti yake ya X orodha ya maseneta ambao alidai wanatumika kumwondoa Gavana Mwangaza mamlakani. Baadhi ya maseneta waliotajwa ni pamoja na Aaron Cheruiyot wa Kericho, Jackson Mandago wa Uasin Gishu, Kamau Murango (Kirinyaga), na Wahome Wamatinga wa Nyeri, miongoni mwa wengine. “KOMENI HAYO. Ushahidi ni wazi kwamba mnatumika vibaya,” Kuria alihoji kupitia X. Chapisho hilo aidha limezua hisia mseto, huku likionekana kumkera Spika wa Seneti, Bw Amason Kingi, ambaye amemkosoa vikali Waziri huyo wa Utumishi wa Umma. “Hivyo basi nawaonya; Mheshimiwa Moses Kuria, Waziri wa Utumishi wa Umma, Utendaji, na Utoaji wa Huduma na watu wengine wote wasizungumze na kutoa maoni, iwe kwa maandishi au kwa njia ya matamshi, kuhusu mchakato wa kumuondoa mamlakani Gavana Kawira Mwangaza wa Meru. Yanaweza kuathiri uamuzi kupata haki,” Spika Kingi alionya. Ikiwa Waziri Kuria hatatii onyo hilo, Bunge la Seneti limetishia kumwita. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MUNGUTI MKURUGENZI wa Mashtaka ya Umma (DPP) Renson Ingonga amepewa siku 14 kukamilisha uchunguzi katika kesi ambapo Brian Mwenda ameshtakiwa kwa kujifanya wakili. Agizo hilo lilitolewa Jumanne na hakimu mkuu katika Mahakama ya Milimani Lucas Onyina kufuatia ufichuzi kwamba polisi wanawasaka mashahidi kutoka asasi tano za serikali kurekodi ushahidi. Akiwasilisha ombi kesi hiyo iahirishwe kwa siku 14, kiongozi wa mashtaka Bw Festus Njue alisema “ushahidi uliopo hautoshi kwa vile polisi wanaendelea na uchunguzi.” Akasema Bw Njue: “Naomba kesi hii iahirishwe kwa siku 14 kuwezesha polisi kukamilisha uchunguzi na kurekodi ushahidi kutoka kwa asasi tano za serikali.” Bw Njue aliongeza kueleza mahakama kuwa ombi lake lisichukuliwe kana kwamba “DPP hana ushahidi.” Hakimu aliombwa amkubalie DPP kusaka ushahidi ndipo kesi hiyo itengewe siku ya kusikilizwa. Lakini wakili Danstan Omari alipinga ombi hilo na kuomba hakimu amwachilie huru Mwenda akisema DPP ameungama kortini hana ushahidi. “Hatujakabidhiwa nakala za ushahidi na DPP. Ukweli ni kwamba DPP hana ushahidi. Kesi hii iliwasilishwa kwa sababu za siasa za Chama cha Mawakili nchini (LSK). Siku ile Mwenda alishtakiwa mahakama hii ilifurika mawakili na baraza kuu la LSK. Sasa mawakili hao wametoweka,” Bw Omari alimwelea hakimu. Akinukuu Kifungu nambari 50 cha Katiba, Bw Omari alisema kila mshukiwa anafaa kupata haki mahakamani kwa kukabidhiwa nakala za mashahidi ajiandae namna ya kujitetea. “Naomba umwachilie Mwenda kwa vile hakuna ushahidi. Ni siasa tu zilizofanya afikishwe kortini. Uchaguzi wa mwakilishi wa LSK katika Tume ya Kuajiri Watumishi wa Idara ya Mahakama ni Februari 2024,” Bw Omari alidokeza. Aliomba mahakama itengee kesi hii muda isikilizwe na kuamuliwa kabla ya Februari 2024. Bw Onyina aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 29, 2023. Mwenda amekana alijifanya wakili na kujipatia cheti cha uanachama wa LSK akidai kimeidhinishwa na  Msajili wa Idara ya Mahakama Bi Anne Amadi. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA BENSON MATHEKA MABUNGE mawili ya nchi za Afrika, Zambia na Kenya, yameomba mabunge barani kutambua Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA), kinacholeta pamoja mabunge katika nchi zinazostawi. Juhudi za mabunge ya Kenya na Zambia zinajiri wiki chache baada ya kongamano la CPA ambalo lilifanyika Ghana mnamo Oktoba. Shinikizo za “kutambuliwa ipasavyo” kwa CPA zilizidi baada ya Kamati za Biashara za Bunge ya nchi hizo mbili kukutana nchini Zambia. Ujumbe wa Kenya unaongozwa na Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula, ambaye pia alikutana na mwenzake wa Zambia Nelly B.K. Muti. Kamati hizo mbili zilibainisha kuwa kutambua CPA kutasaidia kuendeleza mchakato wa kutunga sheria barani Afrika. Huku zikisisitiza juu ya umuhimu wa utambuzi unaohitajika sana, timu hizo mbili zilisema hii itasaidia katika uanzishaji wa mfumo wa kisheria ulioainishwa vyema na hivyo kuifanya kuwa ya manufaa kwa nchi wanachama. Pia zilisema kuwa kutambuliwa kutahakikisha kwamba makoloni ya zamani ya Uingereza yatawakilishwa ipasavyo ndani ya Jumuiya ya Madola. Mkutano huu wa hadhi ya juu pia ulitoa jukwaa mwafaka la kubadilishana mawazo kuhusu taratibu za bunge za mataifa yote mawili. Washiriki walibadilishana maarifa muhimu katika muundo wa vyumba vyao vya kutunga sheria na kamati mbalimbali. Mkutano wa Maspika hao wawili Wetang’ula na Mutti pia uliangazia uhusiano thabiti wa kiuchumi kati ya Zambia na Kenya, ukiwa na msisitizo maalum juu ya athari chanya ya wawekezaji wa Kenya wanaoendesha shughuli zao nchini Zambia. Bw Wetang’ula alitumia fursa hiyo kumwalika Muti kuhudhuria maombi ya kitaifa mwaka ujao ambayo hufanyika kabla ya sherehe za Siku ya Madaraka. Harakati za kutaka kutambuliwa na mkoloni wa zamani zinakuja wakati ambapo Kenya iko katika harakati za kuanzisha Kituo cha Mafunzo ya Bunge (CPST) kitakachotumika kama nyenzo ya kuwafunza wafanyikazi na wajumbe wanaohudumu katika mabunge kote Afrika na kuna uwezekano kitawanufaisha watu wa Zambia. Wakati wa kikao hicho, Kamati ya Biashara ya Bunge la Zambia ilipongeza ufanisi wa Hazina ya Maendeleo ya Maeneobunge ya Kenya (CDF). Hapo awali, Bw Wetang’ula alikutana na kutangamana na Wakenya wanaoishi Zambia kutafuta fursa za ushirikiano na nchi hiyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MHARIRI
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini.
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na BENSON MATHEKA
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI