text
stringlengths 3
16.2k
|
---|
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti, baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

CONSTANT MUNDA NA FATUMA BARIKI Wizara ya Fedha imeanzisha mchakato wa kuuza tariban mashirika 10 ya serikali, katika juhudi za kutafuta na kuokoa pesa inazotumia kuendesha shughuli zao kila mwaka. Katika hatua hiyo ambayo ni miongoni mwa masharti ya Shirika la Kifedha la Kimataifa kwa utawala wa Ruto waliyoweka mapema mwaka huu, Waziri wa Fedha Njuguna Ndung’u ametangaza kuuza hisa za serikal kwenye mashirika 11 ya kiserikali. Prof Ndung’u alitangaza Jumatatu, Novemba 27, 2023 mpango huo wa kuuza mashirika hayo, mwezi mmoja baada ya sheria kuhusu mchakato huo kupitishwa. Chini ya Sheria ya Ubinafsishaji ya 2023, Wizara ya Fedha itakusanya maoni kutoka kwa wananchi kabla ya kupeleka orodha ya mwisho iidhinishwe na Baraza la Mawaziri. Orodha hiyo kisha itapelekwa Bungeni kupata idhini ya mwisho. Wakenya wana hadi Disemba 11 kutoa maoni yao kuhusu kubinafsishwa kwa mashirika hayo. Mpango huo wa ubinafsishaji unajumuisha mashirika matano ambayo yanaleta faida, na sita ambayo hayaleti pesa kabisa. Mashirika yaliyoorodheshwa ambayo yanaleta faida kwa sasa ni Kenya Pipeline (KPC), jumba la KICC, Kenya Literature Bureau, New KCC na Kenya Seed Company. Yale ambayo yamelemewa kifedha ni National Oil Corporation, Rivatex East Africa, Numerical Machining Complex (NMC), Kenya Vehicle Manufacturers (KVM), Mwea Rice Mills na Western Kenya Rice Mills. Rais William Ruto amekuwa akipangia kuuza hisa katika baadhi ya mashirika zaidi ya 100 kama njia mojawapo ya serikali yake kupata pesa za matumizi na kutamatisha ukame wa karibu ya miaka 10 ya kutokuwepo kwa mashirika yanayoorodheshwa katika soko la hisa. Wakati wa ziara yake ya kwanza katika Soko la Hisa la Nairobi (NSE) Oktoba 11, 2022, Dkt Ruto aliahidi kuuza hisa kwa watu binafsi kwa karibu mashirika 10 katika mwaka wake wa kwanza afisini. Alhamisi ya wiki jana, Rais aliambia kikao cha shirikisho la wafanyabiashara wa hisa kwamba Kenya imeshatenga mashirika 35 ya kiserikali kwa ajili ya kubinafsishwa. “Mojawapo ya sababu za kubinafsisha mashirika ni kuyawezesha yachochee shughuli za kibiashara,” akaambia kikao hicho akisisitiza kwamba kujipatia pesa kutokana na uuzwaji huo hakukuwa jambo la kimsingi kwake. “Mpango huu wa ubinafsishaji utachangiwa na jinsi kampuni inafanya vizuri kifedha. Kama shirika limekuwa likipata hasara, huwezi kulipeleka kwenye soko la hisa,” akasema Joseph Koskey, afisa mkuu wa Halmashauri ya Ubinafsishaji. “Lazima uwe umepata faida kwa muda ili uweze kuuza hisa za kampuni hiyo kwa wawekezaji.” Hiyo inamaanisha kwamba mashirika kama Nock, NMC, KVM, Mwea Rice Mills na Western Kenya Rice Mills huenda yauzwe kwa watu ambao washatambuliwa tayari. “Ikiwa shirika limekuwa likileta hasara, na unakisia kwamba chanzo cha hasara hiyo ni miundombinu iliyopitwa na wakati ambayo haijakuwa ikipata mgao wa pesa kutoka kwa serikali, inamaanisha kwamba tunahitaji kupata mwekezaji maalum,” akasema Bw Koskey. Sheria ya Ubinafsishaji ya 2023 inamhitaji Waziri Ndung’u kubainisha vigezo alivyotumia kutambua mashirika kwa ajili ya kuyauza. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA WINNIE ONYANDO WAZIRI wa Ardhi, Alice Wahome amethibitisha kwamba ni lazima waajiri wote waendelee kukatwa Ushuru wa Nyumba kutoka kwa mishahara ya jumla ya wafanyikazi na kuituma kwa Mamlaka ya Ushuru nchini (KRA) pamoja na mchango wa mwajiri. Katika taarifa, waziri huyo alisisitiza kuwa yeyote atakayekiuka sheria hiyo atatozwa faini. “Ni muhimu kutambua kwamba kulipa Ushuru wa Nyumba kunaamriwa chini ya Kifungu cha 15 cha Sheria ya Kodi ya Mapato. Mwajiri ambaye atakosa kufuata sheria atawajibika kulipa faini sawa na asilimia mbili ya madeni yote,” akasema waziri Wahome. Haya yanajiri siku moja tu baada ya Mahakama Kuu kuharamisha sheria ya ushuru wa nyumba ikisema ushuru huo ni kinyume cha katiba. Majaji David Majanja, Christine Meoli na Lawrence Mugambi walizima KRA kuendelea kupokea kodi hiyo wakisema kuwa haijulikani pesa hizo zinaenda wapi. Hata hivyo, muda mfupi baadaye mahakama hiyo iliruhusu Serikali kuendelea kutoza ushuru huo hadi January 10, 2024 ili kuruhusu rufaa dhidi ya uamuzi huo kuwasilishwa. Uamuzi huu ulijiri baada ya maombi kutoka kwa KRA na Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula kufuatia walalamishi wakiongozwa na Seneta Okiya Omtatah kutaka serikali ishurutishwe kurudishia wafanyakazi na waajiri pesa ambazo zimekantwa tangu Julai wakati sheria hiyo ilipoanza kutekelezwa. Katika uamuzi wa awali, mahakama ilitangaza kuwa ushuru wa nyumba ni kinyume na katiba, jambo ambalo huenda likaathiri mpango wa Rais William Ruto wa kujenga nyumba za bei nafuu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wah ametishia kufichua majina ya wabunge wawili wa kiume aliodai huwaingiza kisiri vimada wao bungeni. Mbunge huyo wa Kikuyu (UDA) anasema mienendo hiyo “ni tishio kwa usalama”, na inaingilia “usiri wa wabunge” kando na kukiuka kanuni za kualika wageni katika asasi hiyo. Akichangia mjadala kuhusu taaarifa ya Spika Moses Wetangula kuhusu mtindo wa mavazi bungeni, Bw Ichung’wah alitishia kutaja majina ya wabunge hao wanaume ikiwa hawatakomesha tabia hiyo. “Mara kadha, utawapata wabunge wamewaalika wageni katika sebule maalum ambayo sio eneo la wageni. Kuna maeneo yaliyotengewa wageni wala sio sebule (lounge), mahala maalum pa wabunge kukutana, kushawishiana kuhusu masuala mbalimbali yanayoshughulikiwa bungeni. Hatuwezi kufanya hivyo kwa njia huru ikiwa kuna wageni kando yako baadhi yake wakiwa wapenzi wa wabunge,” Ichung’wah akasema Akaongeza: “Nilishangaa Jumatano moja jioni, wakati vikao vya bunge huendelea hadi saa tatu usiku, nilipoingia kwenye baa ya wabunge nikawapata wabunge wawili wanaume wakiwa na wapenzi wao wa kike. Sitawataja majina wakati huu, lakini wakirudia tena, nitawasilisha majina yao afisini mwako ili uwachukulie hatua.” Bw Ichung’wah alisema baa iliyoko bungeni inafaa kuwahudumia wabunge pekee wala sio wageni. “Wageni wakialikwa eneo hilo huwa vigumu kwa wabunge kuingiliana miongoni mwao. Ni aibu kwamba unapotaka kutangamana na wenzako, unapata wageni wa kike kando yako,” akaeleza. Kulingana na Kanuni ya Spika kuhusu Mienendo Bungeni, mgeni hafai kusalia katika majengo ya bungeni baada ya saa mbili za usiku (8.00Pm). You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA CAROLINE WAFULA MAGAVANA watatu wamehimiza Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kuangazia ufisadi katika kiwango cha Serikali ya Kitaifa kwa kutumia ari sawia na inayotumika kulenga serikali za kaunti. Magavana Jonathan Chelilim Bii (Uasin Gishu), Profesa Anyang Nyongó (Kisumu), na Dkt Wilbur Ottichilo (Vihiga) Jumanne, Novemba 28, 2023 walishutumu Tume hiyo wakisema magavana katika kaunti zote 47 wanahisi kuwa vita dhidi ya ufisadi vinapendelea Serikali ya Kitaifa. Wakuu hao wa kaunti walisema haya kufuatia ripoti ya EACC, iliyotaja kaunti zinazoongoza kwa ufisadi huku ikifichua kuwa inachunguza kesi 67 za watu maarufu kuhusu ufisadi na ukiukaji wa sheria za ununuzi katika kaunti za Marsabit, Samburu, Wajir, na Mandera. Mkurugenzi Mkuu wa EACC Twalib Mbarak aliyewasilisha ripoti hiyo kwa Kamati ya Seneti kuhusu Haki na Masuala ya Sheria Septemba 2023 alisema kesi hizo ni sehemu ya kesi 231 kuhusu ufisadi zilizopokewa na kusajiliwa na Tume. Wakizungumza Eldoret, magavana Bii, Nyong’o, na Ottichilo, vilevile walikosoa mashirika ya kukusanya maoni huku wakiyashutumu kwa kusawiri, kwa njia isiyo ya haki, kaunti kama zilizo fisadi zaidi, kwa kutumia walichotaja kama mbinu zisizo za Kisayansi ambazo hazina ushahidi. Gavana Bii alisema kumekuwa na dhana kuwa kaunti na magavana ndio wafisadi zaidi, huku serikali za kitaifa zikidaiwa kuangaziwa kidogo tu. Alisema Tume hiyo aghalabu imelaumiwa kwa kuandama kaunti na magavana. Kulingana na Gavana wa Uasin Gishu, ufisadi mwingi hufanyika katika kiwango cha kitaifa hivyo basi EACC inapaswa kuonekana ikikabiliana na suala hilo kwa kutumia nguvu zizo hizo inazotumia kwa kaunti. “Mitandao sugu zaidi ya ufisadi ipo kwenye viwango vya kitaifa, inaonekana sisi ni vituo rahisi,” alisema katika Boma Hotel, Eldoret ambapo EACC ilikuwa na kikao na kaunti nne kwenye mpango wa uhamasishaji na mafunzo unaolenga kufafanua kazi yake. “Tafadhali mnapotuadhibu huku chini, tazameni juu vilevile. Tunataka kukuona kuanzia juu kwa sababu jambo hili limegatuliwa na linaanza katika Serikali Kuu,” alisema. Gavana wa Siaya James Orengo na naibu wake walisusia mafunzo hayo yaliyowaleta pamoja wafanyakazi wa kaunti na magavana kutoka kaunti za Siaya, Vihiga na Kisumu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

JUSTUS OCHIENG na RUHDIE OUDIA KIONGOZI wa Azimio la Umoja-One Kenya Raila Odinga anaonekana kubuni mikakati mipya ya kupambana na serikali ya Kenya Kwanza, tofauti na awali alipokuwa akiitisha maandamano. Kinara huyo wa upinzani anaonekana kuacha maandamano barabarani huku akiendeleza upinzani wake dhidi ya serikali ya Rais William Ruto. Duru ndani ya mrengo wa Bw Raila zinasema kuwa ingawa kiongozi huyo wa chama cha ODM anashikilia kuwa Kifungu cha 37 cha katiba kinaruhusu maandamano, serikali ya Dkt Ruto ilitumia maandamano hayo “kuwapiga risasi kiholela na kuwaua waandamanaji wasio na hatia. “Jumapili iliyopita, Bw Raila alimshutumu Rais Ruto kwa kuwaelekeza polisi kuwapiga risasi waandamanaji wakati wa maandamano ya Azimio. “Huu sio mwisho. Tutaendelea kupigania haki za Wakenya. Tulikuwa na maandamano ya amani lakini polisi walitumia nguvu kupita kiasi,” Bw Raila alisema. Mnamo Jumatatu, alimshutumu Rais Ruto kwa kuwaelekeza polisi kuwapiga risasi waandamanaji wakati wa maandamano ya Azimio, akisema kwamba upinzani umeishtaki serikali katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu jijini The Hague, Uholanzi kwa uhalifu dhidi ya binadamu. “Waliwapiga watu wetu na kuwaua wengine wakati wa maandamano ambayo ni haki yetu ya kimsingi. Tumefungua kesi dhidi yao katika ICC, The Hague ambayo tunafuatilia. Pia tumesema tulisimamisha maandamano ili kutoa nafasi ya mazungumzo wala si kwa sababu tunamuogopa yeyote,” akasema Bw Raila. Aliongeza: “Jumatano (leo) na Alhamisi (kesho), nitafanya mikutano muhimu na baadaye nitawapa njia ya kusonga mbele.”Jana, Taifa Leo iliarifiwa kwamba Bw Raila sasa anabadilisha mbinu katika kukabiliana na serikali ya Kenya Kwanza. “Maandamano ya barabarani yanatabirika, ni ya kawaida na yanaleta migawanyiko,” mmoja wa walio karibu wa Bw Raila alisema.Katika mpango wake, Bw Raila anataka kujiondoa kwenye maandamano na kufichua kashfa za ufisadi na kupinga serikali kupitia mahakama za sheria. Tayari kiongozi huyo wa ODM ametoa onyo kwa kufichua sakata ya ununuzi wa bidhaa za petroli chini ya mkataba kati ya Serikali na Serikali (G-to-G) ambao Kenya inasema ilitia saini na Saudi Arabia. “Hakukuwa na G-to-G. Kenya haikutia saini kandarasi zozote na Saudi Arabia au UAE. Ni Wizara ya Kawi na Petroli pekee iliyotia saini mkataba na kampuni zinazomilikiwa na serikali katika Mashariki ya Kati,” alifichua. Aliongeza: “Kwa Ruto kuchagua kutambulisha mpango huo kama G-to-G inaashiria ufisadi katika mpango huu.” Bw Rail kupitia kwa mshauri wake wa kisheria Paul Mwangi pia ameiandikia Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC), Mkaguzi Mkuu wa Hesabu na Mamlaka ya Kudhibiti Kawi na Petroli kuhusu suala hilo, akiomba uchunguzi kuhusu suala hilo. Katika mashambulizi yake mapya dhidi ya serikali, Bw Raila pia anatarajiwa “kuacha makabiliano ya moja kwa moja na Rais Ruto kuhusu gharama ya juu ya maisha na kumwachia yeye kushughulikia hali hiyo jinsi alivyoahidi kufanya.” Rais Ruto amekuwa akisema mara kwa mara kwamba ana mpango wa kukabiliana na kupanda kwa bei za bidhaa za kimsingi nchini na kuleta utulivu wa uchumi wa nchi. Jana, wandani wa Bw Odinga walifichua kwamba kuanzia sasa watamruhusu rais “kushughulikia makosa yake,” lakini wataendelea kutoa suluhu zinazowezekana ili kurahisisha maisha kwa Wakenya wa kawaida. “Tunamwachia Ruto gharama ya maisha ashughulikie jinsi alivyodai. Na kutakuwa na shida ikiwa hawatatoa pesa kamili za masomo kwa shule mnamo Januari, ” duru ndani ya Azimio ziliambia Taifa Leo. Bw Odinga anatazama korti kulazimisha serikali kutupilia mbali baadhi ya sera zake ili kurahisisha maisha ya Wakenya wa kawaida. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

Na RICHARD MUNGUTI SERIKALI ya Rais William Ruto imepata pigo kubwa baada ya Mahakama Kuu kuharamisha sheria ya kuwatoza wafanyakazi na waajiri kodi ya nyumba. Agizo hili la kuzima kodi hii ya asili mia moja nukta tano inayotozwa kila mfanyakazi na kiwango sawa na hicho kulipwa na waajiri ni afueni kubwa. Habari njema ni kwamba mamlaka ya ushuru nchini KRA italazimika kuwarudisha wafanyakazi na waajiri mabilioni ya pesa ilizokuwa imepokea kupitia utekelezaji wa sheria hii haramu. Majaji David Majanja, Christine Meoli na Lawrence Mugambi walisema bunge ilikosea kuidhinisha kodi hii ya nyumba bila kutunga sheria za kuidhibiti. “Inakinzana na katiba kuidhinisha kodi ya nyumba ilhali hakuna hazina maalum ya kuweka fedha hizo. Hii mahakama imefikia uamuzi sheria nambari 84 ya sheria za Fedha 2023 inakizana na Katiba na imeharamiashwa,” walisema Majaji Majanja, Meoli na Mugambi. Majaji hao walisema wabunge waliidhinisha kinyume cha sheria. Mahakama ilimkosoa Waziri wa Nyumba kwa kuamuru KRA kupokea pesa kutoka kwa wafanyakazi na waajiri kinyume cha sheria. “Mamlaka ya KRA imeruhusiwa kupokea kodi na wala sio ada ya nyumba kutoka kwa wananchi,” mahakama ilisema. Majaji Majanja, Meoli na Mugambi waliharamisha kodi hiyo ya nyumba walipotoa uamuzi katika kesi ambapo Seneta wa Busia Okoiti Okiya Omutatah alipinga Sheria ya Fedha 2023 akisema bunge la kitaifa ilikosea kuidhinisha wananchi watozwe ushuru. Punde tu majaji hao walipotoa uamuzi wao, mwanasheria mkuu aliomba agizo hilo lisitishwe kwa muda wa siku 45 kabla ya kukata rufaa. Bw Omutatah, Mbunge wa Rarieda Otieno Amollo na chama cha wanasheria nchini LSK kupitia wakili Eric Theuri walipinga wakisema “mahakama haiwezi kuidhinisha makosa kuendelea kufanyika.” You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA CAROLINE WAFULA MAGAVANA watatu wamehimiza Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kuangazia ufisadi katika kiwango cha Serikali ya Kitaifa kwa kutumia ari sawia na inayotumika kulenga serikali za kaunti. Magavana Jonathan Chelilim Bii (Uasin Gishu), Profesa Anyang Nyongó (Kisumu), na Dkt Wilbur Ottichilo (Vihiga) jana walishutumu Tume hiyo wakisema magavana katika kaunti zote 47 wanahisi kuwa vita dhidi ya ufisadi vinapendelea Serikali ya Kitaifa. Wakuu wa kaunti walisema haya kufuatia ripoti ya EACC, iliyotaja kaunti zinazoongoza kwa ufisadi huku ikifichua kuwa inachunguza kesi 67 za watu maarufu kuhusu ufisadi na ukiukaji wa sheria za ununuzi katika kaunti za Marsabit, Samburu, Wajir, na Mandera. Mkurugenzi Mkuu wa EACC Twalib Mbarak aliyewasilisha ripoti hiyo kwa Kamati ya Seneti kuhusu Haki na Masuala ya Sheria mnamo Septemba alisema kesi hizo ni sehemu ya kesi 231 kuhusu ufisadi zilizopokewa na kusajiliwa na Tume. Wakizungumza Eldoret, magavana Bii, Nyong’o, na Ottichilo, vilevile walikosoa mashirika ya kukusanya maoni huku wakiyashutumu kwa kusawiri, kwa njia isiyo ya haki, kaunti kama zilizo fisadi zaidi, kwa kutumia walichotaja kama mbinu zisizo za kisayansi ambazo hazina ushahidi. Gavana Bii alisema kumekuwa na dhana kuwa kaunti na magavana ndio wafisadi zaidi huku serikali za kitaifa zikidaiwa kuangaziwa kidogo tu. Alisema Tume hiyo aghalabu imelaumiwa kwa kuandama kaunti na magavana. Kulingana na Gavana wa Uasin Gishu, ufisadi mwingi hufanyika katika kiwango cha kitaifa hivyo basi EACC inapaswa kuonekana ikikabiliana na suala hilo kwa kutumia nguvu zizo hizo inazotumia kwa kaunti. “Mitandao sugu zaidi ya ufisadi ipo kwenye viwango vya kitaifa, inaonekana sisi ni vituo rahisi,” alisema katika Boma Hotel, Eldoret ambapo EACC ilikuwa na kikao na kaunti nne kwenye mpango wa uhamasishaji na mafunzo unaolenga kufafanua kazi yake. “Tafadhali mnapotuadhibu huku chini, tazameni juu vilevile. Tunataka kukuona kuanzia juu kwa sababu jambo hili limegatuliwa na linaanza katika Serikali Kuu,” alisema. Gavana wa Siaya James Orengo na manaibu wake walisusia mafunzo hayo yaliyowaleta pamoja wafanyakazi wa kaunti na magavana kutoka kaunti za Siaya, Vihiga na Kisumu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA MASHIRIKA JERUSALEM, ISRAELI PANDE hasimu za Israeli na kundi la Hamas zimekubali kurefusha muda wa kusitisha mapigano kwa siku mbili zaidi. Tangazo hilo ni afueni kwa waathiriwa wa mapigano hayo. Kulingana na maafisa wa Qatar, makubaliano hayo yatakuwa ya siku mbili na kuna matumaini yatajumuisha kuachiliwa huru kwa mateka wa Israeli waliokamatwa na kundi la Hamas. Msemaji wa wizara ya mambo ya Kigeni wa Qatar ni miongoni mwa maafisa walioeleza habari hizo kupitia mtandao wa kijamii wa X. Katika makubaliano ya hapo awali ambapo mapigano hayo yalisitishwaa kwa siku nne, kundi la Hamas lilikuwa likiwaachia mateka kadhaa wa Israeli kila siku. Hata hivyo, Israeli bado inasubiri idhini ya serikali yake kabla ya makubaliano yaliyotangazwa jana kuanza kutumika. Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, ameiomba serikali yake ikubali kurefusha mkataba wa kusitisha operesheni zake katika Ukanda wa Gaza ili mateka zaidi waachiliwe. Maafisa wa Qatar ambao wanashirikiana na Amerika kuratibu mashauriano kati ya Israeli na kundi la Hamas wamesema wana imani kubwa kwamba usitishaji mapigano kwa siku mbili zaidi utaidhinishwa nchini Israeli. Netanyahu alisema Rais wa Amerika, Joe Biden amesaidia sana kufanikisha makubaliano hayo ya sasa yatakayowezesha kuachiwa mateka zaidi bila upande wa Israeli kutimiza matakwa mengi ya kundi la Hamas. Hata hivyo, amesisitiza kwamba malengo ya Israeli kwenye vita vyake dhidi ya Hamas hayajabadilika. “Kuhusiana na suala la mateka, tunaendelea kutekeleza tulichokubaliana na pia tunaendelea na lengo letu kuu tulilolitaja – kuhakikisha mateka wetu wanarejea nyumbani, kulitokomeza kabisa kundi la Hamas, na bila shaka kuhakikisha kwamba tukio kama hilo halijitokezi tena,” akasema Netanyahu. Tangu awamu ya kwanza ya usitishaji mapigano ilipoanza Ijumaa iliyopita, jumla ya mateka 69 wameachiwa huru na kundi la Hamas huku Israeli ikiwaachilia huru wafunga 150 wa Kipalestina na msaada mkubwa wa kibinadamu kuruhusiwa kuingia Ukanda wa Gaza. Inaaminika zaidi ya mateka 200 walichukuliwa na kundi la Hamas. Hapo jana wengine zaidi waliachiwa huru ikiwemo vijana wawili raia wa Ujerumani. Hadi sasa mamlaka za Ukanda wa Gaza zinasema watu wapatao 14,000 wameuawa tangu Israeli ilipoanza kufanya mashambulizi yake ya kulipiza kisasi. Wakati uo huo, Waziri wa Mambo ya Nje Amerika, Antony Blinken, anatarajiwa kufanya ziara nyingine Mashariki ya Kati wiki hii ikiwa ni ya tatu tangu mapigano kuzuka Ukanda wa Gaza. Hayo yalielezwa na ofisi yake Jumatatu. Blinken anatarajiwa kukutana na Netanyahu na rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mamhoud Abbas mjini Ramallah. Ananuia kupigia debe usambazaji wa misaada ya kibinadamu kwenye Ukanda wa Gaza na kuachiliwa kwa mateka wote. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA SAMMY WAWERU MBUNGE wa Githunguri Gathoni Wamuchomba ametishia kuangusha Ripoti ya Kamati ya Mazungumzo ya Maridhiano (NADCO) itakapowasilishwa bungeni, endapo haitaangazia matakwa ya jamii ya Mlima Kenya. Mbunge huyo aliyechaguliwa kwa tikiti ya chama tawala cha United Democratic Alliance (UDA) japo anatofautiana na serikali ya Rais William Ruto, amesisitiza kwamba ripoti hiyo sharti iangazie masuala yanayohusu jamii anayotoka. Akizungumza kwenye hafla ya mazishi, mwanasiasa huyo jasiri alisisitiza kwamba ugavi wa raslimali za umma unapaswa kusambazwa kwa mujibu wa idadi ya watu. Alikuwa akirejelea kigezo cha ‘mtu mmoja-kura moja-shilingi moja’. Bi Wamuchomba alisema mkondo huo katika ugavi wa raslimali za umma, ndio utasaidia kuangazia changamoto zinazokumba maeneo. “Mazungumzo au majadiliano yoyote mezani, hoja yetu ni mtu mmoja, kura moja, shilingi moja. Nilizungumzia hilo, nikaambiwa ninyamaze. Mwaka mmoja sasa umepita. Tumegawa basari (ufadhili wa masomo unaotolewa kupitia Fedha za Hazina ya Kitaifa ya Ustawishaji Maeneobunge – NG-CDF) kwa mara ya kwanza, tunangojea raundi ya pili. Ni haki ninyamaze mkiteseka?” Wamuchomba akataka kujua. Mbunge huyo ambaye kati ya 2017 hadi 2022 alihudumu kama Mwakilishi wa Wanawake Kaunti ya Kiambu, alitahadharisha kwamba endapo NADCO haitaainisha hoja za Mlima Kenya, basi hatakuwa na budi ila kushawishi wabunge wenzake kuangusha ripoti hiyo itakapowalishwa bungeni kujadiliwa ili kupitishwa kuwa sheria au kuangushwa. Ripoti hiyo ya Mazungumzo ya Maridhaino kati ya Serikali ya Kenya Kwanza na muungano wa upinzani – Azimio la Umoja, iliandaliwa na mbunge wa Kikuyu, Kimani Ichung’wah (akiwakilisha Kenya Kwanza) na kiongozi wa Wiper, Kalonzo Musyoka (Azimio). NADCO, hata hivyo, haikuangazia jinsi ya kushusha gharama ya juu ya maisha inayozidi kulemea Wakenya. Suala la kupunguza ushuru (VAT) unaotozwa mafuta ya petroli kutoka asilimia 16 hadi 8, na kuondoa ada ya asilimia 3 inayotozwa mfanyakazi na mwajiri, liliachiwa Rais William Ruto na kinara wa Azimio, Raila Odinga. Wanachama wa kamati ya NADCO hawakukubaliana kuhusu hoja hizo. Dkt Ruto na Bw Raila walikabidhiwa ripoti hiyo kwa njia ya kielektroniki. “Hiyo ripoti ambayo Ichung’wah anataka kuleta kule bungeni…Hiyo ripoti ambayo ametengeneza akiwa na kina Kalonzo Musyoka, kama haitakuwa na maneno ya mtu mmoja, kura moja, shilingi moja, Wamuchomba anaomba ruhusa kutoka kwenu niiangushe asubuhi na mapema kama haina matakwa yetu,” Wamuchomba akasema. Mbunge huyo wa Githunguri, Kiambu anasema ugavi wa raslimali za umma lazima utolewe kwa mujibu wa idadi ya watu kwenye maeneobunge. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

BENSON MATHEKA Na FRIDAH OKACHI HATIMAYE serikali ya Kitaifa imetoa Sh10 billioni kwa serikali za Kaunti ili kukabiliana na athari za mvua ya El-Nino inayoendelea kunyesha nchini. Mkutano wa Baraza la Mawaziri (CoG) uliofanyika Jumatatu, Novemba 27, 2023 uliidhinisha Wizara ya Fedha kutoa pesa hizo kusaidia watu waliopoteza makao, kufurushwa makazini na kukumbwa na hatari ya milipuko ya magonjwa, kurekebisha uharibifu wa miundomsingi na mali. Taarifa kutoka Ikulu ilisema kaunti 38 kati ya 47 zinakumbwa na mafuriko ambayo yameangamiza watu 76 huku familia 35,000 zikihama makazi yao hasa katika maeneo ya Kaskazini Mashariki, Mashariki na Pwani. Serikali pia, kupitia Hazina Kuu imetenga Sh500 milioni kusaidia kampuni za maziwa nchini kununua maziwa ya ziada katika msimu huu wa mvua. Pia Sh180 milioni zitatumiwa kununua vifaa vya matibabu. Juma lililopita, Naibu wa Rais Bw Gachagua kwenye ziara yake Mombasa alisema magavana walikuwa wamepokea pesa za kukabiliana na El Nino. “Hatutaki kuona gavana yeyote akilaumu serikali ya kitaifa kwa kukosa kusambaza chakula. Kama serikali tulitoa Sh10 bilioni kwa shughuli hii,” alisema awali akiwa Mombasa. Baadaye akiwa Nairobi alisema: “Tunashangaa kuona magavana wakilalamika kwamba hawajapokea pesa za El Nino kutoka kwa serikali ya kitaifa. Hakuna pesa kama hizo watapata. Wanapaswa kutumia pesa za dharura wanazotenga katika bajeti za mwaka kusaidia watu wanaotawala.” Magavana wakiongozwa na mwenyekiti wa Baraza lao (CoG), Anne Waiguru, walimfunza Bw Gachagua mambo anayopaswa kujua vyema kwa kumjulisha kuwa pesa za El Nino hazikutumwa kwa kaunti na hawajapokea mgao wowote kutoka kwa serikali ya kitaifa wa kima cha Sh62 bilioni. “Kufikia sasa, tunataka kusema serikali za kaunti, hazijapokea mgao wowote kutoka kwa serikali ya kitaifa kutekeleza hatua za kukabiliana na El Nino. Kaunti zinadai mgao wa jumla ya Sh62.3 bilioni ambazo bado hazijatolewa. Tunachukulia matamshi hayo (ya Gachagua) kuwa dhidi ya moyo wa ushirikiano wa viwango viwili vya serikali inavyohitaji ibara ya 6(2) ya Katiba,” akaeleza Bi Waiguru kwa niaba ya magavana wote 47. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA MHARIRI |
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI |
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI |
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI |
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI |
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI |
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI |
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI |
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI |
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI |
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini. |
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI |
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI |
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na BENSON MATHEKA |
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU |
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA |
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA |
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA |
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU |
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA |
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO |
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI |
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA |
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON |
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA |
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na MASHIRIKA |
LONDON, Uingereza |
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya... Na ELIZABETH MERAB |
WANASAYANSI wanachunguza kuhusu mchipuko wa virusi vipya vya corona aina ya Delta, katika nchi za Amerika, Uingereza,... Na MAUREEN ONGALA |
MASAIBU ambayo wagonjwa wa Covid-19 hupitia katika kaunti za Pwani, yameanikwa wazi baada ya kifo cha afisa mkuu wa... SIAGO CECE na ANTHONY KITIMO |
UFISADI miongoni mwa baadhi ya maafisa wa serikali katika mpaka wa Kenya na Tanzania, umezidi kuwaweka... Na WAANDISHI WETU |
WINGU la maangamizi limetanda kote nchini huku aina mpya ya corona maarufu kama 'Delta' ikiua watu kwa... Na WINNIE ONYANDO |
HUENDA visa vya wasafiri kulazimishwa kupima upya corona mpakani mwa Kenya na Tanzania vikakoma baada ya serikali hizo... NA WANGU KANURI |
AGIZO la serikali la kudhibiti mkurupuko wa ugonjwa wa corona mwaka jana limewashurutisha Wakenya wengi kufanyia kazi... Na Titus Ominde |
VIONGOZI wa kidini Kaskazini mwa Rift Valley (North Rift) wameshutumu wanasiasa kwa kupepeta usambazaji wa virusi vya... Na WANTO WARUI |
Huku wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiripoti katika shule zao mpya za sekondari hii leo, kuna uwezekano wa maambukizi... Na CHARLES WASONGA |
NAKUBALIANA na kauli ya maafisa wa afya katika kaunti ya Nairobi kwamba wanasiasa ndio wanachochea ongezeko la visa... Na SAMMY WAWERU |
DICKSON Muceri amekuwa mkazi wa Nairobi kwa muda wa miaka kadhaa ila sasa kitovu hicho cha jiji kuu la nchi hakikaliki... Na MARY WANGARI |
WANASAYANSI wamethibitisha kuwa kuchelewesha upokeaji dozi ya pili ya chanjo ya Covid-19 kwa kiasi cha miezi 10 baada ya... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na KINYUA BIN KINGORI |
WAKATI huu viongozi wa kisiasa wameanza mapema kampeni zao kwa kuzuru maeneo mbalimbali nchini, ili kushawishi... Na WANDERI KAMAU |
KULINGANA na Ripoti ya Jaji Mstaafu Akilano Akiwumi (1997) kuhusu chimbuko la ghasia za kikabila nchini, wanasiasa ndio... Na WANTO WARUI |
KWA mara nyingine tena tuzo inayoenziwa sana kote ulimwenguni imerudi katika eneo letu la Afrika Mashariki mara hii... Na DOUGLAS MUTUA |
MWAFRIKA akiwajibishwa na Mzungu hupiga kamsa na kudai anaonewa, ati msingi wa maonevu ni ubaguzi wa rangi... Na WANDERI KAMAU |
MOJA ya changamoto kuu zinazokikumba kizazi cha sasa nchini ni ukosefu wa ufahamu wa lugha zao asili. |
Ingawa lugha... Na KINYUA BIN KINGORI |
JUHUDI za kuhakikisha taifa limefanikiwa kupiga vita ufisadi lazima ziendeshwe kuambatana na Katiba, bila njama... Na WANDERI KAMAU |
UFICHUZI wa sakata ambapo watu maarufu duniani wamekuwa wakificha mabilioni ya fedha katika akaunti za siri ng’ambo... Na FAUSTINE NGILA |
NINA imani kuwa iwapo kufikia sasa hujawahi kuelewa teknolojia ya blokcheni, leo utaelewa kwa kuwa jana uliathirika... Na CHARLES WASONGA |
NI jambo la kusikitisha kuwa ni wakati kama huu ambapo uchaguzi mkuu unakaribia ndipo wanasiasa wametambua umuhimu wa... Na MARY WANGARI |
IDADI ya watu wanaoandaa hafla za uchangishaji pesa za kugharamia matibabu imeongezeka pakubwa katika siku za hivi... Na CECIL ODONGO |
CHAMA cha Kanu bado kina safari ndefu kurejelea umaarufu wake wa enzi za utawala wa chama kimoja na miaka ya 90 hata... Na CHARLES WASONGA |
UTEUZI wa waliokuwa maafisa wanne wa ngazi za juu katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kushikilia nyadhifa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Naomi Wamboi, 21, ndiye anatupambia yeye ni mwanamitindo aliyewahi kushinda tuzo za Miss Nakuru. Akipata muda anapenda kusafiri na... Winnie Miriam Nechesa 21, ni mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu Cha Maasai Mara kaunti ya Narok.Anapenda kuchora, na kujumuika na... Lilian Njeri mwenye umri wa miaka 21 ndiye anatupambia jarida letu leo.Yeye ni mwanamitindo na mkaazi wa Narok.Uraibu wake ni kusafiri na... Mary Njeri mwenye umri wa miaka 21 ni mkaazi wa mtaa wa Langalanga kaunti ya Nakuru.Yeye ni mwanafasheni wa mapambo na vipodozi.Uraibu wake... Marylene Watiri mwenye umri wa miaka 22 ni mtaalam wa Beauty Therapy jijini Nairobi, aidha yeye ni mwanamitindo na mlimbwende.Uraibu wake... Zaweria Njoki mwenye umri wa miaka 21 ni Video Vixen kutoka kaunti ya Nakuru.Uraibu wake ni kuandika makala ya kitaaluma na kujumuika na... |
Malkia wetu leo ni Babra Ingasiani mwenye umri wa miaka 21, yeye ni mzaliwa wa kaunti ya Kakamega.Uraibu wake ni kusakata densi ya... Pauline Kimani mwenye umri wa miaka 23 ndiye anatupambia jarida letu leo.Yeye ni mkaazi wa eneo la Lanet na mfanyikazi mjini Nakuru.Uraibu... |
Sayfer Godez ni mkaazi wa Nakuru .Anapenda kushiriki kwenye majukwaa ya mapambo na urembo.Uraibu wake ni kusafiri na kujumuika na... Sylvia Wangeci 23 ni mzaliwa wa Molo, na mwanafunzi katika Chuo Kikuu Cha MKU tawi la Nakuru.Uraibu wake ni kusafiri na... Mical Abulatsia Imbukwa, 28, ni mwanahabari katika shirika moja jijini Nairobi. Uraibu wake ni kutazama filamu za Afro sinema na kujumuika... Faith Karungari mwenye umri wa miaka 22 ni mwanafasheni na mwanamitindo maarufu kutoka Nakuru.Uraibu wake ni kuogelea na kusikiliza muziki... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na RICHARD MUNGUTI |
MAHAKAMA ya Juu jana ilianza kusikiza rufaa ya mpango wa kubadilisha katiba (BBI) huku Mwanasheria Mkuu Bw Paul... Na BENSON MATHEKA |
RAIS Uhuru Kenyatta jana Jumapili alisema kuwa ndoto yake ya kubadilisha katiba ya Kenya iliyopitishwa 2010 kupitia... Na CHARLES WASONGA |
KWA mara nyingine Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza kuwa mageuzi ya katiba yaliyopendekezwa katika Mswada wa Mpango wa... Na JOSEPH WANGUI |
Mwanasheria Mkuu, Paul Kihara Kariuki hatimaye amewasilisha rasmi rufaa katika Mahakama ya Juu kupinga uamuzi wa... Na Gitonga Marete |
KIONGOZI wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi amesisitiza kuwa Bunge linapaswa kurejelea Mpango... Na Leonard Onyango |
NAIBU wa Rais William Ruto amewataka wabunge kujadili masuala nyeti yanayoathiri Wakenya badala ya kujaribu kufufua... Na CHARLES WASONGA |
JUHUDI za wabunge wanaoegemea mrengo wa Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga kutumia bunge kupitisha... Na WALTER MENYA |
JUHUDI za kuokoa mchakato wa marekebisho ya katiba kupitia mpango wa maridhiano (BBI) zimefikishwa rasmi katika Mahakama... Na FRANCIS MUREITHI |
KUSAMBARATIKA kwa Mpango wa Kubadilisha Katiba (BBI) kumefifisha pakubwa ushawishi wa kisiasa wa mwenyekiti wa Kanu,... Na WANDERI KAMAU |
KUHARAMISHWA kwa Mpango wa Kubadilisha Katiba (BBI) na Mahakama ya Rufaa kunatarajiwa kutoa mwelekeo mpya kwa siasa za... Na WANDERI KAMAU |
NAIBU Rais William Ruto jana alimtaka Rais Uhuru Kenyatta kurejelea miradi ya maendeleo iliyoanzishwa na Jubilee, baada... Na Cecil Odongo |
BAADA ya Mahakama ya Rufaa kukubaliana na uamuzi wa mahakama kuu wa kuzima mswada wa Mpango wa Maridhiano (BBI) Ijumaa,... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA MAUREEN ONGALA |
SERIKALI ya kaunti ya Kilifi imeonya wamiliki wa maeneo ya burudani wanaocheza muziki kwa sauti ya juu bila kuwa na... NA PETER MBURU |
Subsets and Splits
No saved queries yet
Save your SQL queries to embed, download, and access them later. Queries will appear here once saved.