text
stringlengths
3
16.2k
UFICHUZI wa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko kwamba mtu aliingia kwenye seli anamozuiliwa katika kituo cha... Na BENSON MATHEKA
Aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Bw Mike Sonko anajuta kwa vitendo alivyofanya akiwa mamlakani; akiepuka kuadhibiwa kwa... Na RICHARD MUNGUTI
KAMA kuna wakati wenye changamoto tele kwa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko ni sasa.
Maji yalizidi unga hata... Na RICHARD MUNGUTI
MASAIBU ya aliyekuwa gavana wa Nairobi, Bw Mike Sonko, yaliongezeka Jumatano ilipofichuka kuwa serikali inapanga... Na RICHARD MUNGUTI
ALIYEKUWA Gavana wa Nairobi, Mike Sonko aliangua kilio kortini Jumatano wakati wa kusikizwa kwa kesi ya ufisadi wa... Na CHARLES WASONGA
WANASIASA na watu ambao majina yao yatawekwa katika orodha ya aibu ya Tume ya Uwiano na Utangamano ya Kitaifa (NCIC)... BENSON MATHEKA na SIMON CIURI
Masaibu ya aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Mike Sonko yaliendelea kuongezeka jana alipozuiliwa rumande baada... Na RICHARD MUNGUTI
MASAIBU ya aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko Mbuvi Gidion Kioko yameongezeka baada ya  kusukumwa ndani hadi... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA SAMMY WAWERU MSANII tajika wa nyimbo Mugithi, Samuel Muchoki maarufu kama Samidoh huenda ametengana na mpenzi wake mwanasiasa Karen Nyamu. Hii ni kutokana na video iliyochipuka ambayo anaskika akisema “nilikuwa kwenye ndoa ya mitara, sasa niko singo”. Samidoh amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Seneta Maalum Karen Nyamu, na wamejaaliwa kupata watoto wawili. Msanii huyo wa nyimbo za Agikuyu, alifichua kuachana na Karen kupitia video ya mbashara ya Tiktok (live) ambapo alikuwa akijibu maswali ya mashabiki wake. Wakati wa mafichuzi hayo, alionekana kuwa kwenye eneo la burudani alikoandamana na msichana ambaye hakuweka wazi endapo ndiye mchumba wake mpya. “Ati hongera kwa kuwa na mpenzi mpya…” Samidoh akasoma mojawapo ya jumbe zilizotumwa na mashabiki wake. Alijibu, “Si wewe pekee ulishushwa madaraka kutoka kiwango cha hadhi hadi dereva wangu…Nilikuwa kwenye ndoa ya mitara ila sasa niko singo”. Mfuasi huyo aliendelea kumdadisi, akitaka kujua iwapo Samidoh anafahamu kuhusu ukurasa wa kimitandao unaohusishwa na mchumba wake – Karen Nyamu Fun Page. Kwa ucheshi, mwimbaji huyo wa kibao tajika cha Kairetu Gakwa (Binti yangu) na Ndiri Mutwe Mwega (Sina kichwa kizuri) alisema kwa sasa anajishughulisha na biashara. “Kwa sasa, ninajishughulisha na masuala biashara. Ikiwa si mradi au biashara, ishi na mama yako,” alielezea. Shabiki wake alimkejeli akitaka kujua aliko nina yake, isijulikane ikiwa alimaanisha mama yake mzazi au mpenzi wake. “Ameoleka na kwa sasa anafurahia fungate (honeymoon),” Samidoh alidokeza. Kidosho aliyeandamana naye alitambua shabiki huyo kama Shabaan, akisema kwamba yeye ni mchochezi. “Wee acha hiyo, unajua Shabaan wewe ni mchochezi sana… (Yuko hapa (akimaanisha Karen Nyamu),” mwanadada huyo alisema. Naye Samidoh aliendelea, “Tunataka Karen, naona hivo ndivo mchango safuni unasema…Naona, lakini sasa yuko online kweli?” Kipusa aliyeandamana naye, alijibu, “Yuko online, mjaribu”. Aidha, shabiki wa Samidoh alitaka Karen Nyamu ajumuishwe kwenye mazungumzo hayo ya mbashara Tiktok. Kilichoshangaza zaidi na kuashiria utengano wa Samidoh na Karen, ni kudai kwamba alimbloki mtandaoni na angeweza kushiriki endapo atamuondoa alikomuweka. “Yuko kwenye orodha ya kublokiwa, sasa hiyo ndio shida. Labda nisitishe mazungumzo haya ya moja kwa moja ili nimuondoa aweze kujumuika nasi,” Samidoh alifafanua. Mahusiano kati ya Samidoh na Karen, ndiyo yalichangia kuachana na mkewe, Edday Nderitu ambaye alihamia Amerika Mei 2023. Edday alikuwa ameonya msanii huyo mapema 2023, akisisitiza kwamba hakuwa tayari kuwa kwenye ndoa ya mitara. Samidoh na Edday wana watoto watatu pamoja. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MAOSI WAKAZI wa mtaa wa Mazembe viungani mwa mji wa Nakuru wamekiri kuhangaishwa na wezi ambao huwaibia na kuwasindikiza hadi nyumbani. Huwawekea ulinzi huo makusudi ili kuhakikisha kwamba wateja wao wanafika nyumbani salama salimini. Kwa kawaida, wahuni wamebuni mbinu mpya ya kutembea na mbwa wakubwa nyakati za usiku, ili kujiwekea ulinzi wa kibinafsi. Owen Shibala mwendeshaji bodaboda kati ya Nakuru mjini na Mazembe, anasema hajui walikotoa ujasiri walio nao kushika doria usiku utadhani ni polisi. Mazembe ni mojawapo ya mitaa ambayo hushuhudia visa vya kihalifu na utumiaji wa mihadarati mara kwa mara. “Ukikutana nao usiku ni lazima usalimishe kila kitu lau sivyo utaona cha mtema kuni. Watakucharaza viboko na kuiba kila kitu cha nguvu,”akasema. Hata hivyo, wanapoiba hujitwika jukuma la kuwasindikiza wakazi, wasije wakakutana na vibaka wengine barabarani. Aidha, wanalia sare za polisi jambo linalowafanya baadhi ya raia kuamini huenda wanashirikiana na maafisa wa polisi. Baadhi yao wanajifanya ni maafisa wa polisi ambao huwa wameshika doria, wakilenga kuhangaisha wapita njia wanaotoka kazini usiku. Agnes Wahome mfanyibiashara mtaani Rhonda anasema huwa wamejihami kwa visu, rungu na wako tayari kupigana. Kulingana na Bi Wahome, hii ni hali ya kawaida siku hizi katika mitaa ya Manyani, Bondeni na Freearea ambapo vijana wengi wamejiingiza kwenye uhalifu. Bi Wahome anasema wahalifu wengi wanajulikana, kwani ni vijana wadogo kutoka mitaa jirani ya Flamingo na Lakeview. Mkazi huyo angependa polisi kushika doria katika maeneo husika ili kuzuia kuzuka kwa magenge hatari yanayohangaisha wenyeji. Hili linajiri siku chache baada ya Taifa Leo Dijitali kufichua visa vya wizi ambapo baadhi ya wezi kutoka kwenye mtaa wa Gioto, Nakuru wamekuwa wakipika chakula katika kila nyumba wanamoingia kuiba. Mtaa wa Bondeni, Kaunti ya Nakuru ambapo wezi huwaibia wakazi na kuwasindikiza mpaka nyumbani. PICHA|RICHARD MAOSI
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L

You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MUNGUTI MASKWOTA wapatao 10,000 wamewasilisha upya kesi katika Mahakama ya Upeo wakiomba ibatilishe uamuzi kwamba wafukuzwe kutoka kwa shamba la ukubwa wa ekari 25,000 wanalong’ang’ania umiliki wake na familia ya mwanasiasa marehemu Mark Too. Maskwota hao wanaodai mababu zao ndio waliotimuliwa kutoka kwa shamba hilo enzi za ukoloni, wanasema walipewa shamba hilo rasmi na aliyekuwa Rais hayati Daniel arap Moi, kisha Kamishna wa Ardhi M Okundu akaratibisha uamuzi huo mwaka 2007. Katika ombi lililowasilishwa na wakili William Arusei chini ya sheria za dharura, kikundi cha maskwota hao–Sirikiwa Squatters Group–kimeomba mahakama ibatilishe uamuzi huo kwa vile ilitegemea ushahidi ambao haukuwa umewasilishwa katika kesi waliyoshtaki katika Mahakama ya kuamua kesi za mashamba (ELC), Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu. Pia wameeleza bayana Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaack Lenaola, na William Ouko walitegemea ushahidi wa Afisa wa Ugavi wa Mashamba R J Simiyu kutoa uamuzi wang’atuke shambani. Maskwota hao wamesema ushahidi wa Bw Simiyu uliowasilishwa mbele majaji hao saba kwa njia ya afidaviti ni mpya na kamwe “haukuwasilishwa mbele ya Jaji Antony Ombwayo aliposikiliza na kuamua kesi hiyo 2017.” Pia wanasema ushahidi huo haukuwasilishwa Mahakama ya Rufaa iliyosikiliza rufaa iliyowasilishwa na kampuni ya Fanikiwa, familia ya marehemu Mark Too, kampuni ya Lonrho Agribusiness (EA) Ltd, na Bw David K Korir. Hivyo basi, maskwota hao wanaeleza mahakama hii ya upeo kwamba ni kinyume cha sheria kutegemea ushahidi mpya kutoa uamuzi wa kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma. “Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu wa Desemba 15, 2023, hauna mashiko kisheria na kamwe hauna nguvu kisheria kuwatimua maskwota hawa kutoka kwa shamba lao,” asema Bw Arusei. Pia maskwota hawa wanadai kwamba badala ya Mahakama ya Juu kujadili masuala ya kikatiba jinsi ilivyo jukumu lake, majaji hao walianza kufafanua na kutafsiri ushahidi wa watu binafsi na kuelezea maana ya ‘skwota’. Mahakama hii imeombwa ikague upya uamuzi iliyotoa kwa vile ilidanganywa na walalamishi na pia kutendewa ujanja. Akinukuu maamuzi ya majaji wastahiki kama vile Lord Dening, Bw Arusei amesema, mahakama ikigundua ilipotoshwa au kudanganywa na upande mmoja, iko na mamlaka na uwezo wa kufutilia mbali uamuzi iliyotoa na kuandika mwingine. Maskwota hao wanaomba Mahakama ya Juu iwarudishe shambani kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Ombwayo na Mahakama ya Rufaa. Vile vile mahakama hiyo imekosolewa kwa kumshambulia hayati Moi katika uamuzi huo pasi kutoa agizo wasimamizi wa mali yake wafike mbele yao kutoa mwanga kuhusu suala la umiliki wa shamba hili lililorudishwa kwa serikali na kampuni iliyokuwa inakuza miti inayotumika katika viwanda vya ngozi. Naibu msajili wa Mahakama ya Juu Nelly Kariuki aliwaamuru maskwota hao wawakabidhi nakala za kesi hii yao mpya wahusika wote kabla ya Januari 31, 2024, kesi itakapotajwa tena kwa maagizo zaidi. Jaji aliyesikiliza kesi hii mpya hakuiratibisha kuwa ya dharura ila aliamuru pande zote ziwasilishe ushahidi katika muda wa siku 14 kuanzia Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti,  baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MAOSI HALI mbaya ya soko katika kituo maarufu cha Kibiashara cha Mlolongo, Machakos imefanya eneo hilo kugeuka maficho ya wahalifu. Wahalifu wamevunja uzio, kuiba mabati, vyuma vikuukuu na kuuza mbao mitaani. Vibanda vilivyochanika na barabara zisizoweza kupitika, vimegeuka kuwa mojawapo ya changamoto kwa wafanyibiashara. Millicent Obonyo mkazi wa barabara ya Katani, anasema yeye ni mfanyibiashara na hulazimika kila siku kufika sokoni mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi (6Am) kuchukua bidhaa. Hata hivyo, anashauri kuzibwa vichochoro vyote vya kuingia au kutoka sokoni kwa sababu vinatumika kama maficho ya wahalifu wa simu. Mwaka 2022, aliwahi kuvamiwa na vijana waliokuwa wamejificha katika vibanda vinavyozunguka soko na wakampokonya pesa za mtaji wake. “Mbali na kurekebisha soko, ingekuwa vyema liwekewe kamera za siri (CCTV) ili iwe rahisi kufuatilia mienendo ya wanaoingia na kutoka sokoni hasa nyakati za usiku,” Millicent akapendekeza. Hali ni kama hiyo ukizuru soko la Kiamunyeki barabara ya Nakuru-Nairobi, Kaunti ya Nakuru. Erick Sule ambaye ni mchuuzi wa samaki katika soko hilo, anasema mwanzo anarushia lawama serikali za kaunti ambazo zilianzisha miradi kisha zikakwama. Anasema hakika hali mbaya ya soko haijawafaidi wale ambao walipaswa kufaidika na miradi yenyewe, kwani serikali za kaunti zimekuwa zikirushiana lawama utawala mpya unaposhika hatamu. Kulingana na Sule ni kama kila serikali ya kaunti huja na mipangilio yake na wala hawajatilia maanani suala la kurekebisha soko. Anasema kati ya 2017-2018 soko analohudumu lilistahili kukamilika, ila wenyeji hawakufaidika na mradi wenyewe kwa sababu shughuli zilichelewa. Akizungumza na Taifa Leo Dijitali anasema Nakuru ni mojawapo ya kaunti nchini ambazo zina idadi kubwa ya vijana ambao hawana ajira. Baadhi yao hutegemea vibarua vya uchukuzi, kwa kubebea wafanyibiashara mizigo kutoka sokoni ili wajikimu kimaisha. Licha ya kwamba soko la Kiamunyeki limewekewa uzio, baadhi ya maeneo hutumika kama kituo cha kutupa taka na vijana wanaorandaranda mitaani wamekuwa wakilala humo na kuvamia wapit njia nyakati za usiku. Aidha, muungano wa wafanyibiashara katika soko la Wakulima Market katikati mwa jiji la Nakuru wangependa kuchimbiwa kisima cha maji ili kuwarahisishia shughuli. Pia, wangependa kuongezewa walinzi wa usiku ili kuhakikisha bidhaa zao zinabakia salama.
Tags
You can share this post!
Previous article
Amenipachika mimba, ndio, lakini sitaki kabisa kuolewa na...
Next article
Mchungaji alia kushindwa kuelekeza wapenzi wanaofarakana,...

NA SAM KIPLAGAT MUUNGANO wa Azimio La Umoja One Kenya unamtaka Sabina Chege kulazimishwa kurejesha pesa alizolipwa akishikilia wadhifa wa Naibu Kiranja wa Wachache. Kando na hayo, muungano huo unaitaka Mahakama ya Juu kuufutilia mbali wadhifa huo. Katika uamuzi wake, Spika wa Bunge la Kitaifa Bw Moses Wetang’ula alitambua Jubilee kama chama kinachojisimamia bungeni na hata kumteua Bi Chege kuwa Naibu Kiranja wa Wachache. Hata hivyo, muungano wa Azimio unadai kuwa hatua ya kumpa Bi Chege wadhifa huo wakati akiwa mwanachama wa muungano huo ni utumizi mbaya wa fedha za umma na kwa hivyo, ni kinyume cha Katiba. “Mlalamishi anadai kwamba hatua ya mlalamikiwa kutambua Jubilee kama chama kinachojisimamia Bungeni inadhihirisha kuondolewa kwa chama hicho kutoka kwa muungano wa waliowasilisha maombi bila kufuata utaratibu uliowekwa,” Bw Wycliffe Oparanya, mwenyekiti wa baraza kuu la muungano wa kitaifa wa Azimio alisema. Azimio inadai kuwa utambuzi huo sio wa haki kiutaratibu, na kwamba unazuia upatikanaji wa haki na ni kinyume cha Katiba. Chama cha upinzani pia kinasema kuwa kutambuliwa kwa Jubilee kama chama kinachojisimamia bungeni na kutelekeza vyama vingine ni ubaguzi na kinyume cha Katiba. Aprili 13 2023, Azimio ilimwandikia Bw Wetang’ula kuwasilisha azimio lake kumwondoa Bi Chege kama Naibu Kinara wa Wachache. Bw Wetang’ula wakati uo huo alidokeza kuwa amepokea ombi kutoka kwa mrengo huo wa upinzani kutaka chama cha Jubilee kitambuliwe kama chama kinachojisimamia bungeni. Bw Oparanya alidokeza kuwa mizozo ndani ya chama cha Jubilee kuhusu mirengo tofauti inaweza tu kusuluhishwa na Kongamano la Kitaifa la Wajumbe wa chama hicho na kwa ufahamu wake, hakujakuwa na mkutano au kongamano kama hilo. “Kwa sababu hiyo, chama cha Jubilee hakijawahi kujiondoa kuwa mwanachama wa Muungano wa Azimio la Umoja,” akasema. Alisema katika hali hiyo, Chama cha Jubilee hakiwezi kutambuliwa kama chama kinachojisimamia bungeni kwani hiyo itakuwa sawa na kuhujumu makubaliano ya muungano kati ya vyama.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA SAMMY WAWERU RAIS William Ruto ametetea mfumo wake wa utozaji ushuru (VAT), akidai umeondolea Kenya hatari ya madeni na mikopo. Akihutubu Jumanne, Desemba 12 wakati wa maadhimisho ya Jamhuri Dei 2023, Dkt Ruto alisema nchi haipo katika hali iliyokuwa hapo awali ya mikopo. “Taifa sasa halipo kwenye hatari ya madeni na mikopo kama ilivyokuwa hapo awali,” Rais akasema. Rais Ruto aliongoza nchi kuadhimisha miaka 60 ya kujitawala, tangu Kenya ipate uhuru wa kujitawala Desemba 12, 2023. Alitumia jukwaa la sherehe za Jamhuri Dei 2023 kupigia upatu serikali yake – Kenya Kwanza, akihoji mikakati aliyoweka imesaidia kukwamua nchi kutoka kwenye hatari ya madeni na mikopo. Rais Ruto aidha aliashiria mfumo wa utozaji ushuru ambapo 2023 alipandisha VAT ya mafuta ya petroli kutoka asilimia 8 hadi 16. Nyongeza hiyo ya ushuru imechochea gharama ya maisha kuwa ngumu. Isitoshe, kuna ada za ushuru ambazo zimezinduliwa ikiwemo ile ya nyumba za bei nafuu. Kenya inadaiwa zaidi ya Sh10 trilioni, madeni hayo yakiwa ni ya kigeni. Kauli ya Rais Ruto inaonekana kama kinaya, ikizingatiwa kuwa serikali yake inaendelea kuchukua mikopo nje ya nchi. Alipotwaa uongozi 2022 kutoka kwa mtangulizi wake, Uhuru Kenyatta ambaye kwa sasa ni Rais Mstaafu, naibu wake, Bw Rigathi Gachagua alisema walirithi serikali iliyofilisika. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA SAMMY KIMATU MAKUNDI ya vijana na akina mama waliosajiliwa kwenye miradi ya mandeleo, wanamazingira na makundi mengine ya kijamii walisafirishwa kwa matatu kutoka mitaa ya mabanda ya Mukuru kujiunga na wengine katika sherehe ya Jamhuri, Uhuru Gardens, Nairobi. Hafla ya maadhimisho ya Jamhuri Dei 2023 inafanyika leo, Jumanne, Desemba 12. Wakizungumza na Taifa Leo Dijitali kwa sharti la kutotambuliwa walisema kila mmoja alipewa Sh500 kuhudhuria sherehe hizo. “Tuliambiwa na viongozi kwamba kila mmoja atapewa Sh500 endapo atajitolea kuenda Uhuru Gardens ili uwanja usionekane hauna watu wengi waliohudhuria,” mama mmoja mwanachama wa mradi wa afya ya jamii mtaani Mukuru akasema. Makundi hayo yalikusanyika katika mtaa wa mabanda wa Mukuru-Hazina, South B, Kaunti Ndogo ya Starehe. Walisafiri kwa kutumia matatu. Katika barabara ya Lusaka, Entreprise na Lunga Lunga zilizo kitovu cha Eneo la Viwandani shughuli za uchukuzi wa magari ya usafiri wa umma zilikuwa chini. “Sisi hutegemea wateja wetu hasa wafanyakazi katika eneo la Viwandani. Kampuni zimefungwa leo (Jumanne) kwa ajili ya Jamhuri ndiposa hatuna matatu nyingi barabarani leo,” dereva wa matatu ya Indimanje Sacco akaambia Taifa Leo Dijitali. Katika eneo la Juakali, eneobunge la Kamukunji, mafundi wa kutengeneza masanduku ya vyuma walikuwa na kazi nyingi wakiyaunda kwa wingi, wakilenga kuuzia wazazi watoto watakapojiunga na shule za upili mapema 2024. Machakos Country Bus, jijini Nairobi, shughuli hazikuwa nyingi kwani waliokuwa wakisafiri hawakuwa wengi. Hata hivyo, katikati mwa jiji, wachuuzi walitawala wakiendeleza biashara zao. Waliozungumza walisema walitumia fursa ya Sikukuu ya Jamhuri kusaka riziki kwa sababu maafisa wa serikali ya kaunti maarufu “kanjo” hawakuwa kazini. Wachuuzi hulumbana mara kwa mara na maafisa hao wa halmashauri ya jiji.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA BENSON MATHEKA WAKENYA Jumanne, Desemba 12, 2023 wameadhimisha miaka 60 ya kujitawala bila matumaini huku wakilemewa na gharama ya maisha, ukosefu wa ajira, kukabiliwa na njaa, maradhi na kushindwa kulipia karo watoto wao kutokana na hali ngumu ya kiuchumi. Kwa vijana kote nchini ambao ndio asilimia 75 ya raia wa Kenya, uhuru kwao ungali ndoto huku hata waliosoma hadi vyuo vikuu wakishindwa kupata riziki. Wataalamu wanasema kwamba Kenya haina uwezo wa kulisha raia wake kwa namna toshelevu miaka 60 baada ya kujikomboa kutoka ukoloni. Njaa ni mojawapo ya maadui watatu wakuu ambao rais mwanzilishi wa Kenya Mzee Jomo Kenyatta na serikali yake aliazimia kuangamiza. Maadui wengine wawili ni maradhi na kutojua kusoma na kuandika. Bw Timothy Njagi, mtafiti katika Tegemeo Institute of Agriculture Policy and Development anasema kwamba kuna watu wengi wanaolala njaa nchini Kenya hata katika maeneo ya mijini; idadi ambayo imeongezeka miaka michache iliyopita kwa sababu ya janga la Covid-19, ukame na hali ya sasa ya mfumko wa bei za vyakula huku mapato yakipungua. “Tatizo pia linatokana na ukweli kwamba watu wengi katika maeneo ya miji hawapandi chakula na kwa hivyo, wanapokosa mapato ya kununua, hulazimika kupunguza mlo,” asema Njagi. Ingawa ndoto ya Mzee Jomo Kenyatta ilikuwa kuwawezesha Wakenya maskini kupitia elimu, kupata elimu hiyo kumebaki kuwa ndoto huku wengi wakishindwa kumudu karo ya watoto wao. “Kama ilivyo katika Ripoti ya Ominde ya 1964, Rais wa zamani alitaka kutumia elimu kuwawezesha Wakenya kiuchumi, kuunganisha na kukuza umoja wa kitaifa. Miaka 60 baadaye, tumepiga hatua za ajabu kulingana na maono ya Ominde ikiwa ni pamoja na maendeleo ya teknolojia na ufahamu wa kimataifa,” akasema mhadhiri mkuu wa Chuo Kikuu cha Moi Dkt Julius Jwan. Hata hivyo, wanaosoma hadi vyuo vikuu hawapati ajira na wanaofanya vibarua wanalemewa na gharama ya juu ya maisha inayoshuhudiwa nchini kwa wakati huu. Sera za serikali ya sasa ya Kenya Kwanza zinaonekana kuenda kinyume na ndoto ya waanzilishi wa taifa la Kenya za kuwezesha raia kuwa na maisha bora kuliko waliyokuwa nayo chini ya utawala wa kikoloni. Serikali imekumbatia mikopo kutoka mashirika yanayodhibitiwa na nchi za Ulaya yanayotoa masharti makali yanayoumiza raia wa kawaida kwa kumbebesha mzigo mkubwa wa ushuru. “Kwa mujibu wa takwimu, Kenya inakabiliwa na tatizo la ongezeko la vijana, huku makadirio yakionyesha kuwa asilimia 75 ya wakazi wa Kenya wana umri wa chini ya miaka 35. Ukosefu wa ajira kwa vijana nchini unasemekana kuwa juu hadi asilimia 35 (takriban vijana na wanawake milioni 4.5 hawana ajira), ikilinganishwa na kiwango cha ukosefu wa ajira kitaifa cha asilimia 10. Katika mwaka mmoja uliopita, Wakenya kadhaa wamepoteza kazi. Shirikisho la Waajiri nchini (FKE) lilishutumu kuongezeka kwa gharama ya uzalishaji nchini, huku likionya kuwa maelfu ya Wakenya watakosa kazi iwapo sera za serikali kuhusu ushuru hazitabadilishwa.   You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

JOHN MUTUA NA MARY WANGARI KAMPUNI ya Kenya Power itaanza kusambaza umeme kwa vipimo, ikilenga eneo la Magharibi katika jitihada za kupunguza presha kwenye laini kuu ya umeme ambayo imekuwa ikishindwa kuhimili ongezeko la mahitaji. Waziri wa Kawi Davis Chirchir jana alisema kuwa wizara hiyo imetafuta suluhu ya muda mfupi kutokana na kukatika kwa umeme kote nchini ambako kulikumba taifa Jumapili jioni. Kenya ilikumbwa na hitilafu ya umeme kote nchini kuanzia saa moja na nusu Jumapili usiku, baada ya laini ya Kisumu-Muhoroni iliyotumika kupita kiasi kukwama. Mgao wa umeme katika nchi nyingi unasababishwa na uzalishaji duni wa umeme ambao unashindwa kukidhi mahitaji kama ilivyo nchini Afrika Kusini na mataifa jirani. Hatua ya Kenya Power itaudhi wawekezaji katika eneo la Magharibi kwa kuongeza gharama zao za kuendesha biashara huku ikifanya laini kuu ya kusambaza umeme ambayo haijafanyiwa marekebisho kwa miaka mingi kupigwa darubini. Alisema shinikizo kuu kupita kiasi kwenye laini ya kusambaza stima ya Kisumu- Muhoroni ndicho kiini cha stima kupotea kote nchini mnamo Jumapili. Laini hii husambaza umeme katika maeneo ya Magharibi, Nyanza Kusini na maeneo ya Kusini mwa Bonde la Ufa. Huku akifichua kwamba ukarabati wa mifumo ya umeme nchini haujafanyika kwa muda wa miaka sita iliyopita, Waziri alisema serikali kupitia ufadhili wa serikali ya Japan na Benki ya Maendeleo Afrika (ADB) inapanga kujenga mtandao mpya kati ya Narok na Bomet. Wakati uo huo, Seneta wa Nandi Samson Cherargei sasa anaitaka Kampuni ya Kusambaza Umeme (KPLC) kuwafidia Wakenya kwa hasara waliyopata kutokana na stima kupotea kila mara hivi majuzi. Akihutubia vyombo vya habari katika majengo ya Bunge, Seneta huyo amesema wakati umewadia kwa taifa kuwa na mdahalo kuhusu kumaliza ukiritimba wa KPLC ambayo imekuwa kero. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

Na MASHIRIKA MWANA wa kiume wa Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, Mohammed Hassan Sheikh Mohamud, aliyedaiwa kugonga na kumuua mwendeshaji pikipiki jijini hapa ametoroka Uturuki. Hii ni licha ya ilani ya kutolewa kwamba akamatwe akionekana popote ulimwenguni, vyombo vya habari vimesema. Polisi walikuwa wamemwachilia huru Mohammed Hassan Sheikh Mohamud bila dhamana baada ya uchunguzi kuhusu kisa hicho kufanywa, lilisema gazeti la Cumhuriyet. “Mshukiwa ameondoka Uturuki bila vikwazo vyovyote,” akasema meya wa Instanbul Ekrem Imamoglu. Soma pia: https://taifaleo.nation.co.ke/habari-mseto/mwanawe-rais-atupwa-rumande-baada-ya-kukanyaga-mtu-barabarani You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

Na SAMWEL OWINO MSWADA unatarajiwa kuwasilishwa katika Bunge la Kitaifa ili kufanya upashaji tohara wanaume kuwa lazima ukitekelezwa na wahudumu wa matibabu. Mbunge wa Mukurweini John Kaguchia amewasilisha Mswada wa Upashaji Tohara 2023 akisema kupitishwa kwake kuwa sheria kutachangia kupungua kwa magonjwa ya zinaa nchini (STDs). “Kuruhusu mswada wa upashaji tohara kufanyiwa uangalizi na mtaalamu wa matibabu kunalenga watoto baada ya kuzaliwa na wakifikisha miaka 18. Mswada huu utachangia afya njema na salama,” akasema Bw Kaguchia. Mswada huo unalenga kupiga marufuku tohara za kitamaduni ambazo huendelezwa na ngariba na sasa shughuli hiyo ya kuingia utu uzima itakuwa ikifanyika hospitalini chini ya mtaalamu wa masuala ya matibabu. Tohara kwa miaka mingi imekuwa ikichukuliwa kuwa suala la kitamaduni na sasa litakuwa la lazima iwapo mswada huo utapitishwa, japo unatarajiwa kuzua pingamizi tele. Hata hivyo, Bw Kaguchia anasema kuwa ukataji govi kama sehemu ya tohara utafanyika hospitalini huku mchakato mwingine wa kitamaduni ukiendelea baada ya hapo. “Hii ni hatua nzuri kwa wavulana kwa kuwa hawatakuwa wakipashwa tohara kwa njia ya kitamaduni ila kupitia mchakato unaoeleweka wa kimatibabu,” akasema Bw Kaguchia. Kwa mujibu wa mswada huo, baadhi ya watoto wameathiriwa kutokana na upashaji tohara kwa njia ya kitamaduni baada ya uume wao kukatwa vibaya. Hata hivyo, sasa shughuli hiyo itaendeshwa kitaaluma tena mahali ambapo kuna viwango vya juu vya usafi. “Wataalamu wa kimatibabu watakuwa wakitathmini hali ya kila mtoto na kuangalia afya yake kisha kumfuatilia iwapo tatizo lolote litatokea baada ya kupashwa tohara,” inasema sehemu ya mswada huo. Bw Kaguchia, ambaye ni mbunge wa UDA, anasema kuwa magonjwa ya zinaa ni hatari kwa afya ya umma na huchangia kupanda kwa gharama ya matibabu na kupotea kwa maisha. Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa ya Kuambukizana (CDC) kimetambua kuwa tohara ya wanaume inapunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa ukimwi kwa kati ya asilimia 50-60. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA SHIRIKA la ndege nchini Kenya Airways (KQ) limetangaza kuwa kutakuwa na hitilafu katika safari zake ndani ya wiki mbili kutokana na changamoto ya ukosefu wa vipuri kote ulimwenguni. Kupitia taarifa, Afisa Mkuu Mtendaji wa shirika hilo Alan Kilavuka, alisema kuna uhaba mkubwa wa vipuri vya ndege katika masoko ya ulimwengu. “Kutokana na hali hii, baadhi ya ndege zetu zitakaa kwa muda mrefu kwenye maegesho zikisubiri kuletwa kwa vipuri kutoka ng’ambo ndiposa zianze kazi,” akasema. “Tutalazimika kuchukua hatua hii, isiyoepukika kwa sababu ya kujitolea kwetu kuzingatia usalama na uaminifu katika shughuli zetu,” Bw Kilavuka akaongeza. Afisa huyo alisema KQ itakuwa ikitoa habari kila mara kwa wateja kuhusu hali hiyo. “Kwa hivyo, tunaomba wateja wetu na washirika wengine kutizama mitandao yetu ya habari kila mara ili kupata ufahamu kuhusu suala hili na masuala mengine yanayohusu shughuli zetu,” Bw Kilavuka akaongeza. Changamoto hiyo huenda ikaaathiri mapato ya shirika hilo wakati huu wa msimu wa sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya ambapo idadi ya wateja imeongezeka.     You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MAOSI  LICHA ya kukamilika kwa mfumo wa masomo wa 8 – 4 – 4, baadhi ya matapeli jijini Nairobi bado wanauza vitabu vya marudio ya Mitihani ya Kitaifa ya Darasa la Nane (KCPE).  Ni jambo linalowafanya wazazi wengi kukosa mwelekeo ufaao jinsi ya kutofautisha mfumo mpya wa elimu na ule wa zamani. Ikumbukwe mtaala wa CBC, yaani mfumo wa 2-6-3-3-3, ulianzishwa 2017 kuchukua nafasi ya 8-4-4, chini ya uongozi wa Rais Uhuru Kenyatta ambaye kwa sasa ni mstaafu. Sehemu ambazo zinaendesha biashara yenyewe ni River Road katikati mwa jiji la Nairobi, ambapo kila aina ya bidhaa huuzwa, kutokana na idadi kubwa ya wateja wanaoamini soko hilo la bidhaa za bei nafuu. Taifa Leo Dijitali imebaini hii ni akiba ya mtaji wa mauzo ya mwaka uliopita, 2022, na wafanyibiashara wengi hawapo tayari kupata hasara. Alice Yegon mzazi katika shule moja eneo la Syokimau, Kaunti ya Machakos anasikitika soko la sekta ya elimu kusheheni na kujaa vitabu bandia. Hata hivyo, anawalaumu baadhi ya wazazi kwa kutotilia maanani masomo ya watoto wao. “Kwanza wanatakiwa kuwa na utamaduni wa kushirikisha wataalam wa elimu ili kufahamu orodha ya vitabu vinavyohitajika shuleni,” akasema wakati wa mahojiano. Isitoshe, Bi yegon amewataka wazazi hasa wenye watoto katika shule za umma mitaani kuchunguza masomo ambayo yanatahiniwa katika mtaala wa CBC. Hili linajiri karibu mwezi mmoja tangu waziri wa elimu Ezekiel Machogu kutangaza matokeo ya KCPE 2023 kwa mara ya mwisho tangu mfumo wa 8 – 4 – 4 uanzishwe 1985. Katika hotuba yake, Waziri Machogu aliambia Wakenya 2023 ni mwaka wa mwisho kupokea matokea ya KCPE baada ya kupisha mtaala wa CBC. Mwaka huu, 2023, watahiniwa wa kwanza wa gredi ya 6 walifanya mtihani wa KPSEA ili kujiunga na Sekondari Msingi.         You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

STANLEY NGOTHO na CHARLES WASONGA
KIONGOZI wa Azimio la Umoja-One Kenya Raila Odinga, sasa anaitaka serikali ya Kenya Kwanza kupunguza bei ya mafuta ya magari kwa kima cha Sh50.
Akiongea Jumamosi, Desemba 9, 2023 katika Kaunti ya Kajiado, Bw Odinga alitaja kushuka kwa bei mafuta katika masoko ya ulimwengu kama sababu ya kuitaka serikali kushusha bei ili kuwapa raia afueni.
Kwa mara nyingi, alimsuta Rais William Ruto kwa kuendesha serikali isiyojali maslahi ya wananchi kwa kuwatoza ushuru wa juu na kudinda kupunguza gharama ya maisha.
“Tunafahamu fika kwamba bei ya mafuta katika masoko ya ulimwengu imepungua kwa kiwango kikubwa. Kwa hivyo, tunataka bei ya bidhaa hiyo nchini kushuka mara moja. Bei isipunguzwe kwa Sh5 tu kuwahadaa Wakenya, bali kwa kiwango cha kuanzia Sh48 hadi Sh50,” Bw Odinga akasema.
Alikuwa akizungumza katika kijiji cha Merrueshi, eneo bunge la Kajiado Mashariki, ambako alihudhuria hafla ya kutoa shukrani kwa heshima ya Mbunge wa eneo hilo Kakuta Maimai.
Mbunge huyo, anayehudumu bungeni kwa muhula wa kwanza, alichaguliwa kwa tikiti ya ODM.
Mamlaka ya Kusimamia Sekta ya Kawi na Petroli (EPRA) hutumia viwango vya bei ya mafuta katika masoko ya ulimwengu kukadiria bei mpya ya rejareja ya bidhaa hiyo tarehe 14 kila mwezi.
Mnamo Alhamisi, Desemba 7, 2023 bei ya bidhaa hiyo ilishuka hadi dola 69.6 (sawa na Sh10,676.28) kwa pipa – bareli katika masoko ya kimataifa.
Bei hiyo ya mafuta yasiyosafishwa kutoka kampuni ya Murban, ni ya chini zaidi kushuhudiwa tangu Julai mwaka huu, 2023, japo ilikuwa juu kidogo kuliko bei ya Jumatano, Desemba 6.
Juni 2023 bei hiyo ilishuka hadi dola 69.15 ya Amerika, sawa na Sh10,607.73 kwa pipa.
Novemba 14, EPRA iliweka bei ya mafuta aina ya petroli katika kiwango cha Sh217.36 kwa lita, huku dizeli ikiwa Sh203.47 jijini Nairobi.