text
stringlengths 3
16.2k
|
---|
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti, baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA SAMMY WAWERU RAIS William Ruto amesuta vikali wanaomkosoa jinsi anavyoendesha nchi akisema alichaguliwa kubadilisha maisha ya Wakenya. Licha ya gharama ya maisha kuzidi kuongezeka na kulemea wananchi, Dkt Ruto amesema shabaha yake ni kuona Kenya imeimarika. Alisema hajalishwi na vitisho vya wapinzani wake “ambapo wanasema nitahudumu muhula mmoja pekee”. Akiwajibu Jumapili jioni, Desemba 17, 2023 kwenye mahojiano ya pamoja na vyombo vya habari, Dkt Ruto alisema hajalishwi endapo hatarejea tena. “Ninaskia watu wakisema, eti ukiendelea vile tunaona, hutapata muhula wa pili. Ninawaambia; Sikuchaguliwa ili nihudumu muhula wa pili,” Rais alisema. Mahojiano hayo yalipeperushwa moja kwa moja kupitia runinga kuu za habari nchini. Aliongeza, “Nilichaguliwa kubadilisha Kenya”. Kulingana na kiongozi wa nchi, serikali za awali zimekuwa zikiahirisha mambo na mikakati kukuza Kenya, ikiwa ni pamoja na kutathmini ushuru (VAT) na ada ya bidhaa kuongeza mapato ya serikali kuu ifanye maendeleo. Chini ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita – tangu atwae mamlaka Septemba 2022, gharama ya maisha imepanda mara dufu hasa baada ya nyongeza ya VAT kwa bidhaa za mafuta ya petroli. Serikali ya Kenya Kwanza, inayoongozwa na Ruto, ilipandisha ushuru wa petroli kutoka asilimia 8 hadi 16, hatua ambayo imechochea mfumko wa bei ya bidhaa muhimu za kimsingi. “Hatutaendelea kuahirisha mambo. Kenya, hadhi yake ni sawa na mataifa kama Afrika Kusini, Morocco na Tunisia,” Rais Ruto aliambia wanahabari waliomhoji. Akidai kwamba amesaidia kushusha gharama ya chakula kwa kiwango kikubwa, alipuuzilia mbali maombi ya viongozi wa kidini kumtaka asikilize kilio cha Wakenya na upinzani, akisema hatua aliochukua kuendesha nchi ina machungu ila baada ya muda, uchumi utaimarika. “Ninachofanya ninajua Wakenya watanituza vizuri,” akaelezea. Alitumia mfano wa uongozi wake kama ule wa Rais Mstaafu, Marehemu Mzee Mwai Kibaki, ambaye anaendelea kupigiwa upatu kutokana na jinsi aliboresha Kenya chini ya kipindi cha miaka kumi pekee. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA MWANDISHI WETU RAIS William Ruto anaonekana kutapatapa kutafuta jibu la matatizo ya Wakenya huku shinikizo zikizidi kwamba atimize ahadi alizotoa kwa wapigakura wakati wa kampeni. Japo anasisitiza kuwa ana mpango wa kutatua matatizo yanayokumba Wakenya, sera za serikali ya Kenya Kwanza zimekuwa zikiwaongezea raia mzigo wa gharama ya maisha, suala ambalo katika manifesto ya muungano wake wa Kenya Kwanza aliahidi kushughulikia kwa muda wa siku 100 baada ya kuingia mamlakani. Badala ya kutangaza mipango thabiti ya kuimarisha uchumi, Rais Ruto amekuwa akilaumu serikali ya mtangulizi wake Uhuru Kenyatta mwaka mmoja tangu aingie mamlakani. “Tuna mipango ya kurekebisha na kubadilisha uchumi kuanzia mashinani. Tumefanya uamuzi unaofaa. Wakati mwingine tumefanya maamuzi magumu mno na yenye uchungu ili kuepusha Kenya kutumbukia katika shimo la madeni na kuipa nchi yetu mwelekeo mpya,” Rais Ruto alisema kwenye hotuba yake katika maadhimisho ya Jamhuri Dei mnamo Desemba 12, 2023. Gharama ya maisha imeendelea kupanda huku akianzisha aina mpya za ushuru na ada zinazopunguza mapato ya raia na kupuuza ushauri unaoweza kusaidia kuwaletea raia afueni. Akiwa katika Kaunti ya Kisii mnamo Jumamosi, kiongozi wa nchi alisema hahitaji ushauri wowote wa kupunguza gharama ya maisha akisisitiza kwamba ana mpango wa kushughulikia matatizo yanayokumba raia. “Hawa wangwana (viongozi) wamenipa mawaidha mengi. Lakini nataka kuwaambia kwamba nilipotafuta hii kazi (urais) nilikuwa na mpango,” alisema. Ingawa Wakenya wanalia kulemewa na gharama ya maisha, rais alisema “hawana (raia) shida” na badala yake aliwanyooshea wanasiasa kidole cha lawama akidai kwamba ndio wanaochochea raia kukosa utulivu na kulalamika, “Hawa raia hawana shida, ni sisi viongozi tunaozozana na kuzua vurugu,” alisema. Rais Ruto alisema hana uwezo wa kupunguza bei ya mafuta ambayo imelaumiwa kwa kuongeza gharama ya maisha akilaumu kampuni za mafuta kimataifa kwa ongezeko la bei za bidhaa hiyo ulimwenguni. “Kuna kazi ambayo rais anaweza kufanya na hayo mafuta sina njia ya kupunguza bei yake,” alisema. Wadadisi wanasema kwamba matamshi ya Rais Ruto ya kuelezea kwa nini hajatimiza ahadi zake yamekosa kuridhisha Wakenya licha ya kuyarudia kila wakati. “Ni kinaya kwa rais kusema kwamba hana uwezo wa kupunguza matatizo ilhali anatazamwa na raia kama kiongozi wao na ambaye serikali yake iliondoa ruzuku na kuongeza ushuru wa thamani (VAT). Kwa ufupi, anaepuka ahadi aliyowapa wapigakura ili asilaumiwe moja kwa moja,” asema mtaalamu wa masuala ya utawala na uchumi James Waki. Aidha, japo aliahidi kuwa serikali yake ingeheshimu utawala wa sheria na kuhakikisha uhuru wa Mahakama, Rais Ruto amekuwa akitoa matamshi yanayochukuliwa kuwa tishio kwa uhuru huo. Akiwa Baringo kuhudhuria mnada wa mbuzi wa Kimalel, Rais Ruto aliwalaumu Wakenya wanaowasilisha kesi kupinga ajenda yake ya afya kwa wote akisema wanafadhiliwa na wanaofaidika na ufisadi katika sekta hiyo. Hii ilikuwa siku chache baada ya kuapa kuwa hakuna anayeweza kusitisha ushuru nyumba alioanzisha licha ya baadhi ya Wakenya kuupinga kortini na kupata agizo usitishwe kwa msingi kuwa unakiuka Katiba. “Kuna hisia kwamba Rais anakiuka Katiba huku akidai anaheshimu sheria na badala yake kutumia vitisho kushinikiza ajenda zake,” asema Bw Waki. Anataja Sheria ya Fedha ya 2023 ambapo kabla ya kupitishwa alionya wabunge ambao wangeipinga na baadaye baadhi ya vipengele vyake kikiwepo kile cha ushuru wa nyumba kuharamishwa na Mahakama na kisha akasisitiza haiendi popote. “Kwa rais aliyeahidi utawala wa sheria, ingekuwa bora iwapo angeacha kuzungumzia masuala yaliyo mbele ya korti na kuacha mkondo wa sheria ufuatwe kikamilifu,” asema mchanganuzi wa siasa Dkt David Gichuki. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA CHARLES WASONGA RAIS William Ruto ameshikilia kuwa serikali ya Kenya Kwanza haitawapunguzia Wakenya viwango vya ushuru licha ya kilio chao na shinikizo kutoka kwa viongozi wa upinzani. Kwenye kikao na wanahabari katika Ikulu ya Nairobi mnamo Jumapili kuangazia masuala kadha yanayoowaathiri Wakenya, Dkt Ruto alisema kuwa kufanya hivyo kutalemaza uchumi wa Kenya. “Nikiitikia wito ya watu wengine kwamba serikali ipunguze ushuru, tutashindwa kulipa madeni. Kwa mfano, wakati huu kwa kila Sh10 tunazokusanya, Sh7 zinaelekezwa kulipa madeni. Mnataka nipunguze ushuru ili tufeli kulipa madeni?” Dkt Ruto akauliza. Kiongozi wa taifa alisema Kenya inakabiliwa na wakati mgumu kiuchumi kutokana na mzigo mzito wa madeni ambayo umechangia kuongezwa kwa ushuru. “Ni kweli kwamba kesho ninaweza kusema tupunguze ushuru na pia ni kweli kwamba kati ya Sh10 tunazokusanya Sh7 huelekezwa kulipa ushuru,” Rais Ruto akakariri. Kiongozi wa taifa alisema njia ya pekee inayosalia ni kwa Wakenya kulipa ushuru ili uchumi uendelee kunawiri. “Ni pesa zinazokusanywa kutokana na ushuru ambazo hutumika kuendesha shughuli za kila siku za serikali,” Dkt Ruto akasema. Aliongeza ni ushuru huo unatumiwa kufadhili elimu na kulipa walimu miongoni mwa mahitaji mengine. “Sasa mwataka kuniambia niambie walimu kuwa hakuna pesa za kulipa mishahara yao kwa sababu Wakenya wameniambia nipunguze ushuru unaotozwa mafuta?” Dkt Ruto akauliza kwa mzaha. Alisema anafahamu kwamba maamuzi magumu anayofanya wakati huu yatamgharimu lakini akasema ni bora ayafanye kulika serikali kushindwa kulipa madeni. “Kuna nchi nyingi ambazo zimeshindwa kulipa madeni. Sitaki Kenya kuwa mojawapo ya nchi hizo,” Rais Ruto akasema. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA TITUS OMINDE SERIKALI ya Kenya haiko katika mgogoro wa kidiplomasia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Kinara wa Mawaziri na Waziri wa Mashauri ya Kigeni Musalia Mudavadi amesisitiza. Bw Mudavadi amesema kuwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili uko sawa. Akizungumza katika Kaunti ya Nandi mnamo Jumapili wakati wa mkutano wa kuchanga pesa kusaidia ujenzi wa ofisi ya uongozi wa makanisa ya Seventh Day Adventist (SDA) West Rift Valley eneo la Kapyagan, Bw Mudavadi alisema Kenya imejitolea kuhakikisha Afrika ina amani. “Rais wa Kenya anaendeleza kampeni ya amani, uhusiano mwema na anajali sana juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi duniani. Hivi sasa Rais William Ruto kupitia IGAD, anafanya kazi usiku kucha kuhakikisha kuna amani nchini Sudan ili kuokoa maisha zaidi na kurejesha amani katika nchi hiyo. Pia anafanya kila juhudi kuona Somalia inajiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki na sio kuleta vita katika nchi hizo,” akasema Bw Mudavadi. Bw Mudavadi alisema kumekuwa na baadhi ya watu wanaodai kuwa Kenya ina mzozo wa kidiplomasia na DRC kwa nia mbaya ya kuonyesha kana kwamba kuna shida kati ya nchi hizo. Alisema kuwa Kenya ina uhusiano mzuri na DRC na hawataingilia uchaguzi ujao nchini DRC. “Nataka kuwahakikishia Wakenya kwamba hakuna mzozo wa kidiplomasia kati ya Kenya na DRC kama inavyoonyeshwa na baadhi ya watu. Tunawatakia watu wa DRC uchaguzi wa amani na kama nchi, hatutaingilia kati uchaguzi huo,” akaeleza. Alisema Kenya inajitenga na matamshi au shughuli zozote zinazoweza kudhuru amani na usalama wa taifa rafiki, DRC. Kauli hiyo inakuja baada ya DRC mnamo Jumamosi kumuita nyumbani balozi wake nchini Kenya huku kukiwa na mvutano mkubwa kati ya nchi hizo mbili kufuatia kuzinduliwa kwa muungano mpya wa kijeshi wa DRC wakiwemo waasi jijini Nairobi. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA MARY WANGARI SHIRIKA la ndege la Kenya Airways (KQ) kwa mara nyingine tena limegonga vichwa vya habari baada ya ndege iliyokuwa ikielekea Kigali, Rwanda kushindwa kutua mara mbili na kulazimika kupiga abautani kurejea katika jiji kuu la Nairobi. Taarifa ya KQ iliyofikia Taifa Jumapili imesema kuwa ndege kwa jina KQ 478 ililazimika kurejea Nairobi baada ya kushindwa kutua nchini Rwanda kutokana na hali mbaya ya hali ya hewa. “Kampuni ya Kenya Airways (KQ) inathibitisha kuwa mnamo Desemba 17, 2023, karibu saa mbili kasorobo (Saa za Afrika Mashariki) KQ 478 iliyopangiwa safari kutoka Nairobi hadi Kigali, ilikumbana na ukungu na hali mbaya ya hewa ilipokuwa ikielekea kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali,” imesema KQ kupitia taarifa iliyotumwa Jumapili. Kulingana na Idara ya Mawasiliano, wahudumu wa KQ walikata kauli ya kurejea kutokana na sababu za kiusalama ambapo ndege hiyo ilitua salama jijini Nairobi saa nne kasoro dakika 10 (Saa za Afrika Mashariki). “Baada ya kujaribu kutua mara mbili bila mafanikio, marubani waliamua kurejea Nairobi kwa usalama wa abiria na wahudumu waliokuwemo kwenye ndege hiyo,” ilisema. Huku ikifafanua kwamba visa vya ndege kurejea ikiwa hewani ni mchakato unaoruhusiwa kwa sababu za kiusalama, KQ ilisema kuwa “abiria wamehamishwa kwenye ndege itakayofuata”. “Tunaomba radhi kwa dhati wageni wetu kwa usumbufu huo na kuwahakikishia wateja wetu kwamba tunapatia kipaumbele usalama wao.” Haya yamejiri huku wasiwasi ukizuka kuhusu KQ almaarufu kama ‘The Pride of Afrika’ yaani ‘Fahari ya Afrika’ kutokana na kuongezeka kwa matatizo yanayokumba shirika hilo katika siku za hivi majuzi yanayoonekana kuathiri taswira ya shirika hilo nchini na kimataifa. Mnamo Ijumaa, jamaa na familia za abiria waliokuwa wakisafiri kuelekea Dubai kutoka Nairobi walikumbwa na taharuki safari yao ilipokatizwa ghafla na ndege kurejea. Usimamizi wa KQ ulifafanua kuwa maafisa wake wa kudhibiti trafiki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), walikumbana na mabaki ya tairi walipokuwa wakikagua mkondo wa ndege mwendo wa saa tatu na dakika ishirini jioni. Mabaki hayo yaligunduliwa kuwa ya tairi ya ndege ya KQ 310 iliyokuwa imeondoka Nairobi kuelekea Dubai. “Timu ya operesheni ya KQ iliwasiliana na wahudumu wa ndege na kuafikiana kuhusu sababu za kiusalama kwa kurejea Nairobi kwa ukaguzi wa kina kiufundi,” ilisema KQ. Soma Pia: Jinsi aibu ndogondogo za Kenya Airways, JKIA zinavyochoma picha kwa nchi isiyohitaji stakabadhi ya viza You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA MHARIRI |
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI |
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI |
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI |
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI |
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI |
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI |
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI |
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI |
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI |
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini. |
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI |
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI |
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na BENSON MATHEKA |
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU |
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA |
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA |
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA |
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU |
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA |
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO |
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI |
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA |
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON |
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA |
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na MASHIRIKA |
LONDON, Uingereza |
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya... Na ELIZABETH MERAB |
WANASAYANSI wanachunguza kuhusu mchipuko wa virusi vipya vya corona aina ya Delta, katika nchi za Amerika, Uingereza,... Na MAUREEN ONGALA |
MASAIBU ambayo wagonjwa wa Covid-19 hupitia katika kaunti za Pwani, yameanikwa wazi baada ya kifo cha afisa mkuu wa... SIAGO CECE na ANTHONY KITIMO |
UFISADI miongoni mwa baadhi ya maafisa wa serikali katika mpaka wa Kenya na Tanzania, umezidi kuwaweka... Na WAANDISHI WETU |
WINGU la maangamizi limetanda kote nchini huku aina mpya ya corona maarufu kama 'Delta' ikiua watu kwa... Na WINNIE ONYANDO |
HUENDA visa vya wasafiri kulazimishwa kupima upya corona mpakani mwa Kenya na Tanzania vikakoma baada ya serikali hizo... NA WANGU KANURI |
AGIZO la serikali la kudhibiti mkurupuko wa ugonjwa wa corona mwaka jana limewashurutisha Wakenya wengi kufanyia kazi... Na Titus Ominde |
VIONGOZI wa kidini Kaskazini mwa Rift Valley (North Rift) wameshutumu wanasiasa kwa kupepeta usambazaji wa virusi vya... Na WANTO WARUI |
Huku wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiripoti katika shule zao mpya za sekondari hii leo, kuna uwezekano wa maambukizi... Na CHARLES WASONGA |
NAKUBALIANA na kauli ya maafisa wa afya katika kaunti ya Nairobi kwamba wanasiasa ndio wanachochea ongezeko la visa... Na SAMMY WAWERU |
DICKSON Muceri amekuwa mkazi wa Nairobi kwa muda wa miaka kadhaa ila sasa kitovu hicho cha jiji kuu la nchi hakikaliki... Na MARY WANGARI |
WANASAYANSI wamethibitisha kuwa kuchelewesha upokeaji dozi ya pili ya chanjo ya Covid-19 kwa kiasi cha miezi 10 baada ya... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na KINYUA BIN KINGORI |
WAKATI huu viongozi wa kisiasa wameanza mapema kampeni zao kwa kuzuru maeneo mbalimbali nchini, ili kushawishi... Na WANDERI KAMAU |
KULINGANA na Ripoti ya Jaji Mstaafu Akilano Akiwumi (1997) kuhusu chimbuko la ghasia za kikabila nchini, wanasiasa ndio... Na WANTO WARUI |
KWA mara nyingine tena tuzo inayoenziwa sana kote ulimwenguni imerudi katika eneo letu la Afrika Mashariki mara hii... Na DOUGLAS MUTUA |
MWAFRIKA akiwajibishwa na Mzungu hupiga kamsa na kudai anaonewa, ati msingi wa maonevu ni ubaguzi wa rangi... Na WANDERI KAMAU |
MOJA ya changamoto kuu zinazokikumba kizazi cha sasa nchini ni ukosefu wa ufahamu wa lugha zao asili. |
Ingawa lugha... Na KINYUA BIN KINGORI |
JUHUDI za kuhakikisha taifa limefanikiwa kupiga vita ufisadi lazima ziendeshwe kuambatana na Katiba, bila njama... Na WANDERI KAMAU |
UFICHUZI wa sakata ambapo watu maarufu duniani wamekuwa wakificha mabilioni ya fedha katika akaunti za siri ng’ambo... Na FAUSTINE NGILA |
NINA imani kuwa iwapo kufikia sasa hujawahi kuelewa teknolojia ya blokcheni, leo utaelewa kwa kuwa jana uliathirika... Na CHARLES WASONGA |
NI jambo la kusikitisha kuwa ni wakati kama huu ambapo uchaguzi mkuu unakaribia ndipo wanasiasa wametambua umuhimu wa... Na MARY WANGARI |
IDADI ya watu wanaoandaa hafla za uchangishaji pesa za kugharamia matibabu imeongezeka pakubwa katika siku za hivi... Na CECIL ODONGO |
CHAMA cha Kanu bado kina safari ndefu kurejelea umaarufu wake wa enzi za utawala wa chama kimoja na miaka ya 90 hata... Na CHARLES WASONGA |
UTEUZI wa waliokuwa maafisa wanne wa ngazi za juu katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kushikilia nyadhifa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Naomi Wamboi, 21, ndiye anatupambia yeye ni mwanamitindo aliyewahi kushinda tuzo za Miss Nakuru. Akipata muda anapenda kusafiri na... Winnie Miriam Nechesa 21, ni mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu Cha Maasai Mara kaunti ya Narok.Anapenda kuchora, na kujumuika na... Lilian Njeri mwenye umri wa miaka 21 ndiye anatupambia jarida letu leo.Yeye ni mwanamitindo na mkaazi wa Narok.Uraibu wake ni kusafiri na... Mary Njeri mwenye umri wa miaka 21 ni mkaazi wa mtaa wa Langalanga kaunti ya Nakuru.Yeye ni mwanafasheni wa mapambo na vipodozi.Uraibu wake... Marylene Watiri mwenye umri wa miaka 22 ni mtaalam wa Beauty Therapy jijini Nairobi, aidha yeye ni mwanamitindo na mlimbwende.Uraibu wake... Zaweria Njoki mwenye umri wa miaka 21 ni Video Vixen kutoka kaunti ya Nakuru.Uraibu wake ni kuandika makala ya kitaaluma na kujumuika na... |
Malkia wetu leo ni Babra Ingasiani mwenye umri wa miaka 21, yeye ni mzaliwa wa kaunti ya Kakamega.Uraibu wake ni kusakata densi ya... Pauline Kimani mwenye umri wa miaka 23 ndiye anatupambia jarida letu leo.Yeye ni mkaazi wa eneo la Lanet na mfanyikazi mjini Nakuru.Uraibu... |
Sayfer Godez ni mkaazi wa Nakuru .Anapenda kushiriki kwenye majukwaa ya mapambo na urembo.Uraibu wake ni kusafiri na kujumuika na... Sylvia Wangeci 23 ni mzaliwa wa Molo, na mwanafunzi katika Chuo Kikuu Cha MKU tawi la Nakuru.Uraibu wake ni kusafiri na... Mical Abulatsia Imbukwa, 28, ni mwanahabari katika shirika moja jijini Nairobi. Uraibu wake ni kutazama filamu za Afro sinema na kujumuika... Faith Karungari mwenye umri wa miaka 22 ni mwanafasheni na mwanamitindo maarufu kutoka Nakuru.Uraibu wake ni kuogelea na kusikiliza muziki... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na RICHARD MUNGUTI |
MAHAKAMA ya Juu jana ilianza kusikiza rufaa ya mpango wa kubadilisha katiba (BBI) huku Mwanasheria Mkuu Bw Paul... Na BENSON MATHEKA |
RAIS Uhuru Kenyatta jana Jumapili alisema kuwa ndoto yake ya kubadilisha katiba ya Kenya iliyopitishwa 2010 kupitia... Na CHARLES WASONGA |
KWA mara nyingine Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza kuwa mageuzi ya katiba yaliyopendekezwa katika Mswada wa Mpango wa... Na JOSEPH WANGUI |
Mwanasheria Mkuu, Paul Kihara Kariuki hatimaye amewasilisha rasmi rufaa katika Mahakama ya Juu kupinga uamuzi wa... Na Gitonga Marete |
KIONGOZI wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi amesisitiza kuwa Bunge linapaswa kurejelea Mpango... Na Leonard Onyango |
NAIBU wa Rais William Ruto amewataka wabunge kujadili masuala nyeti yanayoathiri Wakenya badala ya kujaribu kufufua... Na CHARLES WASONGA |
JUHUDI za wabunge wanaoegemea mrengo wa Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga kutumia bunge kupitisha... Na WALTER MENYA |
JUHUDI za kuokoa mchakato wa marekebisho ya katiba kupitia mpango wa maridhiano (BBI) zimefikishwa rasmi katika Mahakama... Na FRANCIS MUREITHI |
KUSAMBARATIKA kwa Mpango wa Kubadilisha Katiba (BBI) kumefifisha pakubwa ushawishi wa kisiasa wa mwenyekiti wa Kanu,... Na WANDERI KAMAU |
KUHARAMISHWA kwa Mpango wa Kubadilisha Katiba (BBI) na Mahakama ya Rufaa kunatarajiwa kutoa mwelekeo mpya kwa siasa za... Na WANDERI KAMAU |
NAIBU Rais William Ruto jana alimtaka Rais Uhuru Kenyatta kurejelea miradi ya maendeleo iliyoanzishwa na Jubilee, baada... Na Cecil Odongo |
BAADA ya Mahakama ya Rufaa kukubaliana na uamuzi wa mahakama kuu wa kuzima mswada wa Mpango wa Maridhiano (BBI) Ijumaa,... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA MAUREEN ONGALA |
SERIKALI ya kaunti ya Kilifi imeonya wamiliki wa maeneo ya burudani wanaocheza muziki kwa sauti ya juu bila kuwa na... NA PETER MBURU |
WAKENYA wanazidi kulishwa ahadi butu na wagombeaji wakuu wa urais, hasa Raila Odinga na William Ruto kuhusu jinsi maisha... Na LEONARD ONYANGO |
HOFU ya kuangushwa kwenye mchujo na wawaniaji chipukizi imesukuma baadhi ya wanasiasa kung’ang’ania wakuu wa... Na BENSON MATHEKA |
Maisha ya kisiasa ya kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga yamebadilika pakubwa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao... Na SAMMY WAWERU |
NI rasmi sasa kiongozi wa ODM, Raila Odinga atakuwa debeni kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao,... NA JUMA NAMLOLA |
WIKI hii hapa katika meza ya habari ya Taifa Leo tuliangazia mambo ambayo wanasiasa wote waliojitokeza kutamani uraia... NA WANDERI KAMAU |
JE, taswira ya urais wa kiongozi wa ODM, Raila Odinga, itakuwa vipi ikiwa ataibuka mshindi kwenye uchaguzi mkuu wa... NA BENSON MATHEKA |
Kila dalili zinaonyesha kuwa Naibu Rais William Ruto anahofia kwamba ataibiwa kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.... NA KIPKOECH CHEPKWONY |
NAIBU Rais Dkt William Ruto Jumatatu amewataka wapinzani wake, akiwemo kinara wa ODM Raila Odinga, kukataa kuungana... NA PAUL WAFULA |
AHADI za kuimarisha uchumi zinazotolewa na Naibu Rais William Ruto na Kiongozi wa ODM Raila Odinga zitaongeza matatizo ya... Na CHARLES WASONGA |
WAZIRI wa zamani wa Kilimo Mwangi Kiunjuri ameonyesha dalili za kuunga mkono ndoto ya kiongozi wa ODM Raila Odinga ya... Na LEONARD ONYANGO |
WANASIASA sasa wanatumia ahadi hewa kama chambo cha kunasa kura za vijana huku Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9, 2022... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na PATRICK KILAVUKA |
Subsets and Splits
No saved queries yet
Save your SQL queries to embed, download, and access them later. Queries will appear here once saved.