text
stringlengths 0
4.5k
|
---|
Baadhi ya vijana wakiwa wanaendelea kufanya usafi maeneo ya Uwanja wa Taifa wa Ifakara eneo ambapo Tamasha hilo la Msafara lilifanyika.
|
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero Bw. Yahya Naniya(aliyevaa miwani) akiwa katika ushiriki wa kufanya usafi kaika uwanja wa Taifa wa Ifakara
|
Baadhi ya wakazi wa Ifakara wakiendelea kusikiliza kinacho endelea
|
Mbunge wa Kilombero Mh.Peter Lijuakali akielezea Historia ya Maisha yake na mpaka amefanikiwa kuwa Mbunge, na kuwasihi vijana wengine wasikate tamaa kwa sababu kila jambo lina wakati wake
|
Baadhi ya watoto wa shule mbalimbali za Msingi katika mji wa Ifakara wakiwa katika Tamasha la Msafa
|
Bi. Nusura Salum akitoa ushuhuda wake wa namna alivyo anza maisha yake kwa kuuza maandazi , kuwa mkulima na sasa mfanyabiashara mkubwa na alivyopitia katika safari yake ya mafanikio
|
Ramadhani Lyasa akielezea kwa ufupi jinsi alivyopitia changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutokusoma na kuwa alianza na kilimo na sasa ni mfanyabiashara
|
Bi. Veronica Malwata mkazi wa Ifakara akieleza jinsi alivyotaka kukata tamaa ya maisha baada ya kushindwa endelea na shule na baadae kujiinua kwa kuanza kufanya kazi katika moja ya Zahanati kama muhudumu na baadae alipelekwa shule ya uuguzi na sasa ni muuguzi katika Hospitali ya Ifakara.
|
Baadhi ya waandaaji wa Msafara wakiwa wanatoa neno la Shukurani kwa wakazi wa Ifakara.
|
Vijana wengi wa Ifakara Wilayani Kilombero mkoani Morogoro wamepewa nasaha kutumia vipaji vyao kwa lengo la kutimiza ndoto zao ili maisha yao yaende sawa na kukuwa kiuchumi
|
Mwenyekiti wa Programu ya Msafara James Isdore akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya msafara wilayani Kilombero kata ya Ifakara alisema asilimia kubwa ya vijana wenye umri kati ya miaka 14-15 wamekuwa wakijirudisha nyuma kutumia vipaji vyao kutimiza ndoto zao kwa sababu mbalimbali.
|
"Tumeamua kuja Ifakara kwa lengo la kuja kuinua vijana kupitia programu hii ambapo programu hii kwa sasaa ipo katika majaribio inatarajia kuanza rasmi mwakani 2016 hadi sasa majaribio ya programu hii yameweza kufanyika katika mikoa miwili Dar es Salaam na Ifakara na matokeo yake tumeanza kuona ni makubwa mno katika kusaidia jamii ya vijana kutimiza ndoto zao na sio kukaa vijiweni kudidimiza ndoto zao"alisena Isdore
|
Ramadhani Lihapa ni mmoja wa vijana ambaye alifanikiwa kutimiza ndoto zake, alisema kijana anapaswa kujitambua ananafasi gani katika jamii na kuona ni namna gani anaweza kufikia ndoto yake aliyekuwa anaiwaza siku nyingi.
|
Wachezaji wa Singida United wakiwa katika gari lao lenye nembo ya mdhamini mpya
|
KLABU ya Singida United imeendelea kuneemeka baada ya kupata udhamini mnono wa milioni 250 kutoka katika Kampuni ya YARA.
|
Singida United ambayo imepanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu imepata udhamini huo mnono wa mwaka mmoja kutoka katika kampuni hiyo inayojishughulisha na kilimo cha nafaka.
|
akizungumza katika hafla ya kuingia mkataba iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Singida United, Festus Sanga amesema kuwa klabu yao imefurahia kuingia mkataba na YARA.
|
Alisema wameamua kuingia mkataba wa mwaka mmoja na kampuni hiyo kwa ajili ya kusaidia uendeeshaji wa timu hiyo.
|
Sanga alisema kuwa udhamini huo mpya ni habari njema za kiuchumi kwa klabu yao ambayo imefanya usajili wa 'kufa mtu' msimu huu.
|
“Tuna furaha kutangaza kuingia mkataba wa udhamini na YARA kwa mwaka mmoja, haya ni manufaa makubwa sana katika klabu yetu na hadi sasa tuna hekari 10 kwa ajili ya kilimo cha zao la alizeti chini ya usimamizi wa kampuni ya yara, itakayosimamia suala zima la kilimo,” alisema Sanga.
|
Naye mkurugenzi wa YARA, Alexandre Macedo, alisema kwamba wamefurahi kuwa sehemu ya Singida United na watayaboresha mahusiano hayo katika sekta ya kilimo.
|
Singida United imeendelea kuneemeka katika timu za ligi kuu hapa nchini baada ya kuingia mkataba wa udhamini kutoka katika kampuni nne ambazo ni Sportpesa, Puma, Oryx na sasa YARA.
|
Mkurugenzi wa Singida United, Festus Sanga kushoto akisaini mkataba pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya YARA Alexander Macedo katika hafla ya kuidhamini timu hiyo ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
|
MAAMUZI YA KAMATI YA SAA 72 YA UENDESHAJI NA USIMAMIZI WA LIGI - SUFIANIMAFOTO
|
Home Michezo MAAMUZI YA KAMATI YA SAA 72 YA UENDESHAJI NA USIMAMIZI WA LIGI
|
MAAMUZI YA KAMATI YA SAA 72 YA UENDESHAJI NA USIMAMIZI WA LIGI
|
Rais Magufuli amualika Rais wa Zambia kwa ziara ya siku 3 _ DUNIA KIGANJANI _ Ifanye Dunia Kuwa Yako
|
Home » Kitaifa » Rais Magufuli amualika Rais wa Zambia kwa ziara ya siku 3
|
Rais Magufuli amualika Rais wa Zambia kwa ziara ya siku 3
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, amesema Rais Edgar Lungu wa Zambia anatarajiwa kufanya ziara rasmi ya siku tatu nchini kuanzia Novemba 27 kwa mwaliko wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
|
Dkt. Mahiga amesema wakati wa ziara hiyo, Rais Lungu atasaini mikataba mbalimbali ya ushirikiano kati ya Zambia na Tanzania.
|
Miongoni mwa mikataba hiyo ni pamoja na ushirikiano wa masuala ya anga, ulinzi na usalama, ushirikiano katika masuala ya uhamiaji, na kuweka utaratibu wa kubadilishana wafungwa.
|
Kwa upande wake Mkurugenzi idara ya Afrika Balozi Samweli Shelukindo amesema utekelezaji wa mikataba hiyo utaleta maendeleo baina ya nchi hizi mbili.
|
Naibu Waziri wa afya atembelea kituo cha afya Miwani
|
Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Miwani, Wilaya ya Kati Unguja Fatma Keisi Ali akimtembeza Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo sehemu mbali mbali za Kituo hicho kuona changamoto zinazowakabili ikiwemo tatizo la umeme, maji na upungufu wa wafanyakazi kituoni hapo.
|
Kituo cha Afya cha Miwani ambacho Naibu Waziri ameahidi kukiboresha ikiwa pamoja na kuondosha tatizo la umeme, maji na kujenga nyumba ya wafanyakazi. Picha Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
|
Mmoja ya wananchi wa kijiji cha Miwani akimueleza Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo (hayupo pichani) matatizo wanayoyapata kutokana na upungufu wa huduma muhimu katika kituo hicho .
|
Naibu Waziri wa Afya Mhmoud Thabit Kombo akiwasilikiza wananchi wa Miwani wakati alipofanya viara ya kutembelea kituo cha Afya cha Kijiji hicho kujua matatizo yanayokikabili kituo hicho, (kushoto) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Mohammed Saleh Jidawi.
|
Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Miwani baada ya kusikiliza matatizo yanayokikabili kituo cha Afya cha Miwani.
|
Daktari dhamana Kanda ya Unguja Dkt. Fadhil Mohd Abdalla akitoa ufafanunuzi baadhi ya masuala yaliyoulizwa na wananchi wa kijiji cha Miwani wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afya katika kituo hicho.
|
Muuguzi wa Kituo cha Afya Miwani Fatma Keis Ali akielezea changamoto anazokabiliana nazo wakati wa kutoa huduma kituoni hapo ikiwemo upungufu wa wafanyakazi, tatizo la usafiri, maji na umeme.
|
Siku kadhaa baada ya utabiri wa TB Joshua kuwa Hillary Clinton angeshinda urais wa Marekani kuwa tofauti, hatimaye mhubiri huyo maarufu wa Nigeria ametoa ufafanuzi kuhusu kilichotokea.
|
Awali, TB Joshua aliwaambia waumini wake kuwa aliona ndotoni kuwa Rais wa Marekani atakayechaguliwa atakuwa mwanamke na kwamba atakumbwa na changamoto nyingi ikiwemo jaribio la kutaka kumuondoa madarakani kwa kura za kutokuwa na imani naye.
|
Mhubiri huyo ametumia ukurasa wake wa Facebook na Twitter kuutetea utabiri wake akidai kuwa Clinton alishinda kupitia kura za jumla, kwa kupata kura nyingi zaidi ya Donald Trump.
|
“Tumeona matokeo ya uchaguzi wa Marekani. Kwa kusoma, utagundua kuwa [utabiri]ule ulikuwa kuhusu kura za jumla (popular votes), kura za wamarekani wengi,” unasomeka ujumbe wa TB Joshua.
|
“Katika hali hii, tunahitaji roho ya kinabii kutambua au kujua unabii. Viwango vyetu ni tofauti. Hatuko kwenye viwango sawa. Tunaweza kuwa na makanisa makubwa, kengele kubwa, na shughuli zote ambazo ni nzuri kwa viwango vya kibidamu lakini uwezo wa binadamu una kikomo,” aliongeza.
|
Alitumia pia Biblia Takatifu kuupa nguvu utetezi wake, akitaja maandiko ya 1 Wakorinto 1: 25, “Maana kinachoonekana kuwa ni upumbavu wa Mungu, kina busara zaidi kuliko hekima ya binadamu; na kinachoonekana kuwa ni udhaifu wa Mungu, kina nguvu zaidi kuliko nguvu za binadamu.”
|
Clinton alishinda kwa kupata kura nyingi zaidi za Wamarekani (popular votes) lakini alishindwa katika kura za majimbo muhimu (electoral votes). Mgombea wa Republican ambaye tafiti nyingi hazikumpa nafasi, alishinda uchaguzi huo na kuishangaza dunia.
|
Trump anatarajiwa kuapishwa rasmi kuwa Rais wa Marekani, Januari mwakani.
|
IWAPO kiwango cha kufaulu watoto wanaotarajiwa kuingia kidato cha kwanza kinazidi kushuka kwa miaka mitatu mfululizo, na kile cha wanaotarajiwa kuingia ngazi ya juu ya sekondari nacho pia kinashuka, serikali imeshindwa.
|
Uozo wa matokeo shule za majina ya wakubwa [2,037]
|
Ya Tunisia, polisi na majeshi ya ulinzi Ndimara Tegambwage [1,521]
|
Akiwa amefuatana na wajumbe wa Kamati ya siasa ya mkoa wa kusini mwakilishi wa jimbo la makunduchi Mwalimu Haroun Ali Suleiman na viongozi wa jimbo Amesema chama kimeguswa na tukio hilo la ujasiri lililofanywa na Mohamed la kuamua kujitolea maisha yake kwa kumuokoa mwenzake.
|
Mapema mwalimu HarounAli Suleiman alitoa salaam za pongezi rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein kuwa anathamini juhudi zilizofanywa na ndugu Mohamed katika kuokoa uhai wa bi Mariam.
|
Aidha ujumbe huo kwa pamoja ulifika nyumbani kwa mama yake bi Mariam Hassan Vuai kwa ajili ya kumpa pole yeye na familia yake.
|
Bi Mariam alijitumbukiza kisimani kutokana na tatizo la ugonjwa wa akili katika shehia ya kiongoni jimbo la makumbusho tarehe 9 mwezi wa 10 mwaka huu
|
Serikali ya Libya imeanzisha mpango maalum wa kuwataka watu nchini humo kusamilisha silaha. Na sio hilo tu, bali serikali badala yake inawapa wananchi waliorejesha silaha zao tarakilishi aina ya Laptop, wanaweza kushinda magari na hata televisheni kubwa.
|
Je unadhani mpango huu utawashawishi watu kuachana na silaha wakati Libya ingali inakumbwa na hali mbaya ya usalama? silaha hizo zilizagaa miongoni mwa wananchi baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomng'oa mamlakani Muamar Gaddafi.
|
As salaam aleykum ndugu zangu katika ukumbi huu leo tupeane keys za windows 10 japo sio zote zinafanya kazi kwa asilimia mia, ila kama zote zitagoma nimekuwekea windows loader kwaajili ya windows 10 hivyo hii hainaga ushemeji inapita na windows yako makini kabisa hapa chini ni baadhi ya keys
|
04. kisha kwenye kwenye sehemu ya activation bonyeza ‘EZ-Activator’. subiri kidogo copy yako itakuwa activated.
|
Natumaini utakuwa umepata keys makini kwaajili ya windows 10 yako, lakini kama hujapata unaweza kuniachia maoni yako hapo chini ili nikupatie nyingine zaidi.
|
Home > Shahidi Kwa Ajili Ya Ubinadamu > Sura Ya 14: Msisitizo Wa Yazid Juu Ya Kiapo Cha Utii Cha Husein Na Kukataa Kwa Husein.
|
Ndoto ya Mchezaji wa Ghana, Kevin Prince Boateng, ni kucheza dhidi ya Ujerumani katika fainali ya michuano ya kombe dunia. Je ataitimiza ndoto yake?
|
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) ambapo alisema Serikali ya China pamoja na watu wake wamekuwa marafiki wa kweli kwa Tanzania na wamekuwa wakitoa misaada mingi bila kutoa masharti.
|
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) ambapo aliishukuru Serikali ya China pamoja na watu wake kwa msaada wa vitanda 60 vya kujifungulia ambavyo vitasaidia kuokoa maisha ya Mama na Mtoto katika mkoa wa lindi .
|
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiangalia vitanda hivyo vya kujifungulia wakina mama akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Taasisi ya kukuza Urafiki wa Tanzania na China Ndugu Joseph Kulwa Kahama.
|
Bi. Ziada Maulid akitoa shukrani zake mbele ya Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing mara baada ya ya Balozi huyo kukabidhi vitanda 60 vya kujifungulia wakina mama.
|
Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama wakiwasili katika kata ya Kiwalala, jimbo la Mtama tayari kwa kukabidhi vifaa vya matibabu katika Zahanati ya Mauhumbika.
|
Wakazi wa kijiji cha Mahumbika wakiwa wamejitokeza kwa wingi kushuhudia makabidhiano ya vifaa vya matibabu katika Zahanati yao.
|
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akitoa salaam za shukrani kwa Serikali ya China kwa msaada wa vifaa vya tiba vilivyogharimu zaidi ya milioni 20.
|
Mwanzo > HABARI ZA AFRIKA > TP MAZEMBE YAENDA NUSU FAINALI KWA KISHINDO
|
TIMU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jana imeibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Al-Hilal Al-Ubayyid katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi.
|
Mabao ya Mazembe jana yalifungwa na Jean Kasasula dakika ya 39, Adama Traore dakika ya 49, Malango Ngita dakika ya 55, Elia Meshack dakika ya 84 na Djos Issama dakika ya 90 na ushei na kwa matokeo hayo, timu hiyo ya Lubumbashi inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 7-1, baada ya kushinda ugenini pia wiki iliyopita 2-1.
|
Mabingwa hao wa zamani wa Afrika, sasa watakutana na FUS Rabat ya Morocco katika Nusu Fainali.
|
Nayo Club African ya Tunisia imefanikiwa pia kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya MC Alger 2-0 usiku wa jana Uwanja wa Olimpiki mjini Rades.
|
Ushindi huo, unamaanisha MC Alger inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya awali kufungwa 1-0 na Waalgeria hao kwenye mchezo wa kwanza.
|
Imetumwa: May 17th, 2018 Wananchi wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuchangamkia fursa za kiuchumi kwa kushiriki kwenye kilimo cha mazao ya biashara likiwemo zao la korosho ambalo limetambulishwa kwa mara ya kwan...
|
Imetumwa: May 18th, 2018 style="text-align: justify;">Wito umetolewa kwa wapanda pikipiki mkoa wa Kilimanjaro kuvaa kofia ngumu (Helmet) wanapotumia vyombo hivyo vya moto ili kujilinda na kufuata sheria za usalama barabarani....
|
Imetumwa: May 17th, 2018 >Katibu Tawala Wilaya ya Hai Upendo Wella (katikati mwenye miwani na skafu nyeusi) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Yohana Sintoo (mrefu aliyevaa suti ya kijivu), Diw...
|
TSHISHIMBI AMGARAGAZA OKWI TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI LIGI KUU - Zinazosomwa
|
Kiungo wa timu ya Yanga, Papy Tshishimbi Kabamba amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kwa mwezi Februari 2018. Tshishimbi ametwaa nafasi hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili alioingia nao katika kinyang'anyiro kwa mwezi Februari, katika uchambuzi uliofanywa na Kamati ya Tuzo iliyokutana Dar es Salaam wiki hii. Kiungo huyo alitoa mchango …
|
Mwanzo > SIMBA > WATU NA SIMBA YAO KWA RAHA ZAO, NA WANAPENDEZA 'MASHAALLAH'!
|
WATU NA SIMBA YAO KWA RAHA ZAO, NA WANAPENDEZA 'MASHAALLAH'!
|
Mashabiki wa Simba wakiwa Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons Aprili 16, Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Simba ilishinda 2-0.
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.